NJIA SABA (7) AMBAZO KWA PAMOJA HUTENGENEZA UHUSIANO MZURI KATI YAKO NA MUNGU.

Na Mwl Peter Mabula 
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi 



Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe Ndugu zangu wote.
Karibu sana tujifunze Neno la MUNGU wa Mbinguni.

◼️MUNGU anataka tuwe na uhusiano naye mzuri.
Katika andiko hili MUNGU anawashangaa makuhani maana wanafanya mambo yanayovunja uhusiano mzuri naye.

Malaki 1:6 "Mwana humheshimu baba yake, na mtumishi humcha bwana wake; basi, kama mimi ni baba yenu, heshima yangu iko wapi? Na kama mimi ni bwana wenu, kicho changu ki wapi? BWANA wa majeshi awauliza ninyi, enyi makuhani, mnaolidharau jina langu. Nanyi mwasema, Tumelidharau jina lako kwa jinsi gani?"

◼️Ukiwa na uhusiano mzuri na MUNGU katika KRISTO YESU utamwita kwa Maombi naye ataitika.

Isaya 58:9 "Ndipo utaita, na BWANA ataitika; utalia, naye atasema, Mimi hapa. Kama ukiiondoa nira; isiwepo kati yako, wala kunyosha kidole, wala kunena maovu;'

Kuna faida nyingi sana kama Mimi Peter Mabula na Wewe rafiki yangu unayesoma somo hili tukiwa na uhusiano mzuri na Baba yetu wa Mbinguni.

✓✓Ukiwa na uhusiano mzuri na MUNGU huwezi kuwaogopa wanadamu wala kuwahofu.

✓✓Ukiwa na mawasiliano mazuri na MUNGU huwezi kuwaogopa wachawi wala majini.

✓✓Ukiwa na YESU na unamtii lazima shetani na marafiki zake wakuogope na kukukimbia.

◼️Uhusiano wako na MUNGU ni jambo la muhimu sana kwako ili adui zako wakukimbie.


Njia saba(7) ambazo kwa pamoja hutengeneza uhusiano mzuri kati yako na MUNGU.

1. Kuokoka.

Yohana 3:16-18 " Kwa maana jinsi hii MUNGU aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana MUNGU hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa MUNGU."

◼️Kuokoka maana yake kumkubali YESU KRISTO kuwa Mwokozi wako Kisha unampokea kuwa Mwokozi wako.

Mambo hayo 2 yaani kumkubali YESU Kisha Kumpokea ndiyo hukamilisha Wokovu wako, baada ya hapo ni jukumu lako kuishi Maisha matakatifu ukiwa ndani ya Wokovu huo.

◼️Kuokoka ni Kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako Kisha unaanza kuishi Maisha matakatifu katika yeye.

◼️ Kuokoka ndio Mwanzo wa kumwabudu MUNGU wa Mbinguni katika kweli yake ya milele.

✓✓Kuokoka kutengeneza uhusiano wako na MUNGU wa Mbinguni.

2. Kuishi maisha matakatifu na ya haki.

1 Petro 1:14-15 " Kama watoto wa kutii msijifananishe na tamaa zenu za kwanza za ujinga wenu; bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote;"

◼️MUNGU ni mtakatifu hivyo Ukitaka uwe na uhusiano mzuri na MUNGU Hakikisha unakuwa mtakatifu.

Chagua kuishi Maisha matakatifu katika KRISTO YESU na kwa njia hiyo uhusiano kati Yako na MUNGU utakuwa imara.

Kuishi Maisha matakatifu katika KRISTO YESU hutengeneza uhusiano mzuri na MUNGU wa Mbinguni.

3. Kumwamini MUNGU na kuliamini Neno lake linalotolewa na watumishi wake.

2 Mambo ya Nyakati 20:20 "Wakaamka asubuhi na mapema, wakaenda nje katika jangwa la Tekoa; nao walipokuwa wakitoka, Yehoshafati akasimama, akasema, Nisikieni, enyi Yuda nanyi wenyeji wa Yerusalemu; MWAMININI BWANA, Mungu wenu, NDIVYO MTAKAVYOTHIBITIKA; WAAMININI  MANABII WAKE, NDIVYO MTAKAVYOFANIKIWA.''

Neno la MUNGU la kweli Lina wasemaji waje.
Wasemaji hao ni Watumishi wa Bwana YESU KRISTO wanaijua sauti ya ROHO MTAKATIFU ndani ya maandiko matakatifu na wakafanyia kazi.

✓✓Ukitaka uwe na uhusiano mzuri na MUNGU basi mwamini MUNGU na waamini Watumishi wake waaminifu Katika KRISTO YESU.

✓✓Ukimwamini MUNGU na ukawaamini Watumishi wake katika KRISTO Matokeo yake utathibitika na utafanikiwa katika mambo Yako mema.

◼️Ukitaka uwe na uhusiano mzuri na MUNGU wa Mbinguni basi mwamini yeye na waamini Watumishi waaminifu wa Bwana YESU KRISTO. 


4. Kuwa mtu wa maombi.

1 Wathesalonike 5:17 "ombeni bila kukoma;"

✓✓Maombi ndio njia rahisi zaidi ya kuboresha uhusiano mzuri kati Yako na MUNGU wa Mbinguni.

Kwanza Maombi huonyesha unamtegemea MUNGU, unamwamini na ndio njia Yako pekee ya ushindi.

Katika Maombi ROHO MTAKATIFU atazungumza na Wewe, utapata Ufunuo n.k yote hayo huonyesha uhusiano kati ya MUNGU na watu wake.

◼️Ukitaka uwe na uhusiano mzuri na MUNGU wa Mbinguni basi uwe Mtu wa Maombi.


5. Kuwa mtoaji wa matoleo sahihi.

Zaburi 50:5 "Nikusanyieni wacha MUNGU wangu Waliofanya agano nami kwa dhabihu."

Kuna matoleo ya aina 3 ambayo yanaweza kutengeneza uhusiano mzuri kati Yako na MUNGU wa Mbinguni.

✓✓Matoleo hayo ni Zaka au fungu la kumi kwa Jina lingine, Sadaka na Dhabihu.

◼️Zaka MUNGU ameagiza Wateule wake watoe, ukiwa hutoi maana yake unampinga MUNGU aliyeagiza hivyo ni vigumu MUNGU kuwa na uhusiano mzuri na Mtu anayempinga.

◼️Sadaka ni matoleo yote ya hiari unayoyatoa Kanisani, kwa Watumishi wa MUNGU, kwa yatima, kwa wajane na kokote ambako ROHO MTAKATIFU atakupa msukumo rohoni kutoa.

◼️Dhabihu ni sadaka ya hiari ambayo Mtu bila kuambiwa bila kushurutishwa hutoa kuiongeza katika zaka yake.
Mfano zaka ni milioni Moja yeye anatoa zaka milioni Moja na laki Moja, hiyo laki Moja ni Dhabihu.

Matoleo huonyesha unamtii MUNGU maana ameagiza hivyo ni njia ya kuongeza uhusiano mzuri kati Yako na MUNGU wa Mbinguni.


6. Kukaa kwenye kusudi la MUNGU la wito wa utumishi katika KRISTO.

Wafilipi 2:13 "Kwa maana ndiye MUNGU atendaye kazi ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa kulitimiza kusudi lake jema."

✓✓MUNGU hutenda kazi yake na Wateule wake katika KRISTO.

Ikiwa unamtumikia MUNGU lazima uwe na uhusiano naye.

Ukiwa unamtumikia Bwana YESU KRISTO hakika utakuwa unafaida kwenye ufalme wa MUNGU.

1 Wakorintho 15:58 "Basi, ndugu zangu wapendwa, mwimarike, msitikisike, mkazidi sana kutenda kazi ya BWANA sikuzote, kwa kuwa mwajua ya kwamba taabu yenu siyo bure katika BWANA."

✓✓Kumtumikia Bwana YESU KRISTO hutengeneza uhusiano mzuri na MUNGU wa Mbinguni.


7. Acha na Kataa dhambi, uovu na machukizo yote.


Zaburi 34:14 "Uache mabaya ukatende mema, Utafute amani ukaifuatie."

✓✓Dhambi, uovu na makosa ni vitu ambavyo huvuruga uhusiano mzuri kati Mtu na MUNGU wa Mbinguni.
 ✓✓Ukitaka uwe na uhusiano mzuri na MUNGU wa Mbinguni basi Acha Dhambi, maovu na makosa yanayokatazwa na Biblia Takatifu.

1 Yohana 2:15 "Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda BABA hakumo ndani yake."
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter  Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU.
+255714252292(Sadaka ya kuipeleka Injili,whatsapp, ushauri n.k).
Ubarikiwe 

Comments