SHUHUDA MBALIMBALI

Ndoto muhimu.
BWANA YESU ASIFIWE MTUMISHI WA MUNGU, Niliota ndoto nikiwa nimelala ndani,nikaona kwenye ndoto nipo nje nimelala kwenye mkeka nikiwa nimetazama juu ghafla nikaona kitu kama radi juu, baada ya hiyo nikaona mbingu zinafunguka na ndani nikaona upinde wa mvua, baadae akashuka mtu mkubwa kutoka mbinguni akanipa kikombe, baada ya kupokea kile kikombe nikaanza kutetemeka,nikajikuta nakimbia huku na huku nikiwa naogopa sana nikiwaambia watu kwamba YESU anarudi, walikuwa ni wazungu wanakunywa pombe, wanafanya uzinzi wanaume kwa wanaume na wanawake kwa wanawake, nikiwaambia acheni jamaani dhambi YESU anarudi huku nikilia na kutetemeka, lakini wenyewe walikuwa wakinicheka Wanasema YESU toka kipindi hicho walisema atarudi hajarudi mpaka sasa ghafla nikashtuka nikiwa natetemeka na kuogopa sana huku mapigo ya moyo yakiwa yanapiga haraka sana.
Ujumbe huu alinitumia rafiki yangu mmoja.
Ukweli ni kwamba Bwana YESU KRISTO yu karibu sana.
Heri wanaokoka sasa, heri wanaoishi maisha matakatifu ya Wokovu sasa.
Ni wakati wa kutubu na kuacha dhambi.
Ni wakati wa kuuchagua uzima wa milele.
Bwana YESU mwenyewe anasema " Mwenye kudhulumu na azidi kudhulumu; na mwenye uchafu na azidi kuwa mchafu; na mwenye haki na azidi kufanya haki; na mtakatifu na azidi kutakaswa. Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo. Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho. Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake. -Ufunuo 22:11-14
MUNGU akubariki


Ushuhuda huu umenifurahisha.
Bwana Yesu asifiwe mtumishi Mabula.
Mimi niko Dar nilikuwa ninaota ndoto nafanya mapenzi na mtu nisiemjua . ni kama miezi mitatu tangu uniombee kwa simu baada ya kukueleza juu ya tatizo la kuteswa na majini mahaba. Mtumishi ilikuwa ni siri yangu tu ila ukweli nilikuwa naingiliwa na majini mahaba kila siku tangu ubinti wangu, yaani ni zaidi ya miaka 10 mfululizo. Mwanzoni nilidhani ni kawaida tu lakini baadae madhara yaliponifika ndipo nikajua ni jambo baya sana kuendelea kushiriki na majini. Kwanza niliachwa na mume baada ya kuzaa naye mtoto mmoja. Baadae nikapata Mwanaume mwingine ambaye nilipozaa tu alianza kunitesa, yaani kila siku alikuwa ananipiga kama ngoma, nilijaribu kuomba ila sikufanikiwa chochote maana hata kuomba nilikuwa sijui. Baadae nikagundua tatizo ni majini mahaba japokuwa hakuna mtu aliyekuwa anafahamu hata mmoja kwamba huwa nashiriki na majini. Siku moja nikaamua kusearch Google ndipo nikakutana na somo lako linalizungumzia maombi ya kuvunja ndoa na majini mahaba, nilijitambua sasa na matatizo uliyoyazungumzia ni kama ulinilenga Mimi tu, nilisoma somo hilo kisha nikaomba maombi ya ndani ya somo. Jambo la ajabu siku hiyo kwa Mara ya kwanza jini hakuja, na kesho yake nikaomba tena hakuja nilikaa siku chache ile hali ikarudi hivyo nikaona nikupigie Simu maana kichwa changu kilikuwa kizito hata kuomba yale maombi nikashindwa. Nilipokupigia Simu uliniombea kwa Simu na
Mungu kanisaidia. Maana ni miezi mitatu sasa hawajarudi tena wale majini ila kuna baadhi ya siku naona dalili kwamba wanakuja tena ila hawafanikiwi yaani tangu umeniombea hawajafanikiwa sasa mtumishi mimi najua nimeshinda ila naomba unisaidie maombi ili waangamie kabisa msaada wa Yesu.
Ni hayo mtumishi wa Mungu.



USHUHUDA.
Bwana Yesu asifiwe mtumishi Mabula, nashukuru sana kwa maombi ya muda mrefu kwangu.
Naomba nikushirikishe jambo moja la ajabu sana,Yesu Kristo alivyonitendea ni ushuhuda mkubwa sana!Siku ya jumatatu ,wakati wa mchana tulienda kumtembelea mtoto wa kaka yangu alikuwa anaumwa, yule mtoto zamani tulikuwa naye hapo home kwetu, tulipoenda tulimkuta hali mbaya sana,anaitwa Joyce ,anaishi kwa mama yake, mama yake ana watoto wawili, mmoja wa kike alikuwa hapo home kwao,utamwona ktk picha.
Tulipofika mazingira ni magumu mno na Joyce anaumwa , wakawa wanasema ugonjwa huu wa sasa ni mbaya na typhoid ikaingia ndani na alikuwa dhaifu ,wanasema aliacha na dawa za kutumia.
Sasa kufika pale ,nikaanza kutoa ushauri kwamba ni vema akate shauri la kumtumikia Mungu,Mungu anaponya,Daktari anatibu.
Mungu wetu ni tajiri,sio maskini,amtegemee Mungu,ndiye rafiki yetu mkuu!nikamshauri yeye na mama yake waokoke,wamtumikie Mungu,waende kanisa linalohubiri wokovu,Mungu atawaelekeza! katika kimalizia,nikawaomba wote tusimame,tushikane mikono,nikaongoza maombi ya rehema na baraka,kabla nilimkaribisha Roho mtakatifu atumie kinywa changu na nikawaambia kila mtu atafakari na kuomba Mungu uponyaji kwa Joyce! Baada ya hapo tukaanza kuomba,dakika mbili,mapepo yakalipuka,Joyce akaanza kukoroma sana,mama yake akaanza kulia,mimi sikumgusa nilimnyoshea mkono kwa mbali,nikakemea pepo ,likatoka!!!!sijawaho fanya hivyo maishani!!!!alikuwa kadondoka!!!baada ya hapo ,nikaona kumbe sio mpaka kanisani aende,kumbe naweza kuomba!!!nikamwambia upo tayari kumpokea Bwana Yesu awe Mwokozi wa Maisha yako?akasema ndio!!!nikamwambia anyoshe mikono juu!!!nikamwambia Afuatishe sala ya toba akafanya mpaka mwisho!!!baada ya hapo Nikamkabidhi Mwenyezi Mungu ampokee,Joyce,kwani amekiri mbele ya kinywa chake,ambariki,huku nimemgusa kichwa,Mchungaji pepo lingine likalipuka upya, ni mtoto mwingine alikuwa karibu akaanguka, nikalihoji likasema ni li shetani limekuja kumtesa, nikakemea kwa jina la Yesu likatoka!!!
Baada ya hapo tukamshukuru Mungu kwa uponyaji,tukawashauri wampeleke kanisani siku hiyo hiyo wakatoe ushuhuda kwa mchungaji jinsi Mungu alivyomponya na kwa mafundisho zaidi!!!Yesu ni Mwamba Imara!!!!mimi sikujua kama nina karama hiyo,sasa mie sijaombewa na mtumishi ili niweze kuombea wagonjwa!!!ninafikiri Mengi,Mungu anahitaji nifanye kazi hiyo au aliniinua kwa vile kulikuwa hakuna mchungaji ili nimwombee mgonjwa?sijaelewa!Naomba unifafanulie!!!!!
Nakushukuru sana pia kwa maombi yako ambayo umekuwa unaniombea kwa Simu.
Yaani huu ni muujiza mkubwa na nimeshangaa sana.
Mungu akubariki mtumishi



Atukuzwe MUNGU aliyeziumba mbingu na dunia.
USHUHUDA kutoka kwa Mchungaji anayeanza huduma.
Mchungaji huyu ni Mwanamke na wana waumini 15, ndio wamepata eneo la kujenga Kanisa na wamekuwa wanafunzi wa YESU KRISTO wazuri na walinijulisha juu ya masomo yangu yalivyowasaidia hivyo nikamshukuru MUNGU sana.
USHUHUDA wa Mchungaji huyo jana ni huu.

Shalom Mtumishi Mabula jana asubuhi tulienda kukata mti kwa ajili yakuchoma matofali, sasa mume wangu akawa anaukata mti ule kama unavojua mti unakatwa kuangalia vile unavoelekea, basi Mimi nikawa nimekaa chini upande ambako mtu haujalalia, mti ni mkubwa sana ilikua ukatwe na mashine tukakosa hela basi mume wangu akawa anakata kuelekea mti unakoelekea. chakushangaza mti wakati unakatwa ukageuka kuelekea nilipo mimi, kuna kijana alisimama hapo MUNGU alimleta pale anaitwa Musa, alikuja kutuulizia tumuuzie kuku, sasa yeye akauona ule mti unaangukia niliko alichosema ni kwamba " Mchungaji mti huo ondoka" nikwambie Mtumishi niliita" YESU wangu" cha ajabu kwa sababu ya mshituko nilijikuta nakimbilia kulekule unakoangukia, yaani ilikuwa ni ajabu sana. Wakati wa tukio hilo watu walikuwa wanapiga kelele kwa ajili yangu wanaangalia, mume wangu anatetemeka, basi mara mti ule ukashikiliwa juu na mti mwingine. MUNGU akaniokoa kwa njia hiyo, nilitetemeka kwa hofu kubwa, mti ungeniangukia basi ningesagika vipande, yote haya ni nini? nimeanza kufuta maagano yangu ya damu yangu mwenyewe vita vimeanza vikali sanaa ila nataka kusema mimi ni mshindi ,niombee sana. nilisikiliza kwanza maombi yale uliyoniombea yalinisaidia sana, utukufu heshima namrudishia MUNGU wangu. asante mtumishi nimewiwa kukupa ushuhuda huu.


MUNGU wetu yu mwema na ametenda mema.
USHUHUDA.
Bwana Yesu Kristo asifiwe mtumishi
Kwa hakika Mungu yu mwema na sasa amejibu maombi na kilio changu cha miaka mingi. Kwasasa kati ya wachache waliochaguliwa kuripoti kazini na Mimi nimo. Nmepata kazi serikalini mtumishi na sasa najisikia furaha sana na namshukuru Mungu sana na atukuzwe milele yote. Nashukuru kwa jinsi Mungu anavyokutumia na akuwezeshe zaidi na zaidi na uifanye kazi yake kama apendavyo yeye na kadri ya maagizo yake na azidi kukufunulia mengi zaidi kwa njia ya Roho wake.
Asante kwa maombi yako maana Mungu ametenda.



Yuko MUNGU wa Israeli yeye anaweza yote.
USHUHUDA.
Shalom Mtumishi wa MUNGU. Mtumishi baada ya kuliona lile somo lako linalosema "NINI UFANYE KUHUSU MADHABAHU ZA GIZA? Niliamua kufanyia kazi kimaombi.
Nilikuwa kijijini kwetu yaani nyumbani nilikozaliwa, nilianza hayo maombi ya kuvunja madhabahu za giza tarehe 19.08.2018 usiku saa tisa usiku. Nilianza kwa kuomba toba kama Daniel alivyoomba juu ya wana wa Israeli. Mimi kama lango la familia niliomba toba binafsi na juu ya ukoo na familia yetu kwa ujumla kuanzia kizazi cha kwanza hadi cha nne... Daniel: 9: 4-19.

Baada ya toba niliendelea na maombi ya vita ya kuvunja madhabahu zote za giza kama ulivyoelekeza kwenye somo. Maombi nilifanya kwa kuzunguka nyumba mara saba asubuhi na jioni. siku ya tatu mchana Mzee alianguka na kupoteza fahamu. nilikuwa bafuni nikasikia kelele, nikagongewa nikaambiwa toka haraka dada Mzee anakufa! Huyo aliyeniita nilimwambia mwacheni YESU afanye kazi yake.
Nilipotoka kwa kweli hali ilikuwa mbaya. nikaanza kuomba Kwa Jina la YESU na kwa Damu ya YESU mwisho nikimalizia kwa kusema mapenzi yake BWANA YESU yatimie. alitapika sana!. pia akawa hataki kulala kwenye chumba chake mpaka alipopelekwa kwa lazima. Huyo amefunguliwa na Nimeona mkono wa MUNGU ukifanya kazi.
Jamii yangu ilikuwa imefungwa sana na nguvu za giza isitoshe kuanzia Baba na ndugu zangu sio wakristo hivyo kuna vifungo vingi vimeletwa na ngugu za giza, Namshukuru MUNGU maana mimi nimeanza kuuona ushindi wake hadi kwenye familia yangu.
Sifa, Heshima na Utukufu wote ni kwa MUNGU katika KRISTO YESU. Barikiwa Mtumishi wa MUNGU.


 Kuna ufunuo wa ghafla wakati mwingine unaweza kukujia na ukakusaidia.
USHUHUDA.
Shalom mtenda kazi katika Shamba la BWANA.
Usiku huu niliota ndoto moja Mbaya saana.
nilipo shtuka nikatambua ni Vita!.
Nikaingia maombi ya Kutumia Mamlaka ya Jina la YESU KRISTO kuteketeza kila roho chafu.
Nilipomaliza ,nikachukua cm yangu na kuingia Web site ili nijifunze zaidi ,Mbinu za maombi haya ya vita.
Nimekutana na mafundisho yako Mengi na yamenisaidia sana.
Ubarikiwa sana
Mtenda kazi shambani Mwake BWANA.


Kuna watu hupata Neema ya MUNGU.
USHUHUDA.
Bwana YESU asifiwe Mtumishi Mabula.
Namshukuru sana MUNGU kwa muujiza huu, na
Nashukuru mtumishi baada ya sala ya toba uliyoniongoza maisha yangu ya wokovu yamerudi, nimeweza kuomba kutoka rohoni na kunena kwa lugha jambo nililokuwa naumia mno kulikosa.
MUNGU akubariki sana na uzidi kuniombea nizidi kupanda viwango kiroho.
Amen.



USHUHUDA MZURI.
Nuru yake BWANA wetu YESU KRISTO iendelee kukuangazia kwani mengi nimejifunza kutoka masomo yako, ninajisikia ni mtu wa maana sana, ninajihisi mimi ni mtumishi mwaminifu anaye lisha na kuvusha kondoo wake palipo shindikana, kwa sababu nimemuona ROHO wa MUNGU siku hadi siku akiniambia habari njema ya ufalme wa MUNGU na watu wote matokeo yake. kila mara ninapo Ninapoingia mtandaoni nakutana na ujumbe au somo kutoka kwako mteule wa MUNGU Peter Mabula, nilicho kuwa nakipigania katika maisha yangu na wateule wa MUNGU tayari nimepata nguvu nyingi my power my GOD kila kitu kinawezekana in the name of JESUS!! Nataka kukutana na watumishi na walimu kama wewe mtu wa MUNGU ili niweze kupata masomo zaidi! Nina mengi lakini nikupe nafasi ya masomo mengine tena, amina sana mtu wa MUNGU kwa furaha niliyo nayo ya ajabu kwa sababu kwanini MUNGU amenipendelea mimi??

Comments