USHUHUDA.
Bwana YESU asifiwe Mtumishi Mabula.
Mimi ninamshukuru sana MUNGU wangu wa mbinguni, hakika namtukuza yeye. nakushukuru sana na wewe kwa maombi yako naamini kuna Nguvu ya ajabu uliyopewa na MUNGU . mie nilianza kuumwa kwenye tarehe za mwanzoni mwezi Wa 5 mwaka huu sikua najua tarehe rasmi niliyoanza kuumwa lakini nakumbuka ni mwezi Wa 5 siku moja niliamka nikakuta upande Wa titi la kulia kuna maumivu kwa ndani,sikua na hofu nilijua huenda nililala vibaya hivyo badae ningekua sawa! Ile hali iliendelea mpaka tarehe za mwishoni za mwezi ule ikabidi niende hospitali, Dr akaniambia kama nanyonyesha nami nikamjibu sinyonyeshi,akasema je kwenye chuchu kuna vitu vinatoka nikajibu hapana wakati ukweli nilikua nikijibinya naona vitu kama maziwa na nimeachisha mtoto muda Wa kama miez 6 umepita,unajisikia homa nikajibu hapana na kweli sikua na homa,miguu inavimba hapana (haikua inavimba) akashauri nipewe dawa nitumie basi nikaanza dozi ya dawa kwa muda Wa siku 5 kwakweli dawa zilivyoisha maumivu yakaanza upya ikabidi nimuelezee tena akanipa dawa zingine za siku 5 tena dawa tofauti na zile za mwanzo, nikatumia zilivyoisha tu maumivu yakarudi upya! Nakumbuka kipindi hicho nilianza maombi nikawa nakupigia simu jioni ya saa moja unaniombea kuna siku nilikutafuta sana nakuta simu inatumika kwa muda mrefu lakini sikukata tamaa. ikabidi nifunge safari nikaja hospital nyingne iliyopo mkoa mwingne Dr akanipa tena dawa, nilivyomaliza sawa maumivu yakaanza tena. ikumbukwe nikiwa natumia dawa maumivu yanapungua kiasi, ikabidi nibadilishe tena hospital nikaonana na Dr mwingne akanipa dawa za kutumia kwa siku 15 nikatumia nilivyomaliza maumivu yakarudi ikabidi nikamuone tena safari hii hakusema neno alinipa rufaa ya kwenda kufanya kipimo sehemu nyingne cha kupima saratan ya titi. kiukweli hiyo siku nililia sana maana dalili zote zilionyesha nina ugonjwa huo mbaya, nilijua huko Hospital kubwa naenda kuaibishwa na shetani sasa, maana hata nguvu ya kusali ilipungua ila nilikupigia simu nikaomba uniombee sana ukasema sawa utaniombea na ukaniombea na ukanipa shuhuda nikakueleza je niende hospital kuchunguzwa au nikazane na maombi ukasema nifanye yote niombe na nichunguzwe ukasema una hakika majibu yatakua mazuri. nilikubali lakini moyoni nilikosa kabisa Amani na kuna muda nilikua najiona kabisa sina hata nguvu ya kusali. kipimo ilikua nipime jumatatu lakini ulisema utaniombea hivyo nitajiamulia nipimwe jumatano. kweli siku ilipofika nikaenda kupima ila nikawa Nina hofu kuu ikabidi nitoroke majibu hospital, jioni ya siku hiyo ukaniombea tena kwa simu basi alhamisi asubuhi nikasema ntaenda kufuata majibu ya hospital nikafuata na nikayarudisha kule waliponiandikia rufaa nikampa Dr alivyonisomea akasema maumivu yako ni ya kawaida vipimo vyako vinaonyesha huna dalili wala ugonjwa wenyewe wa Saratani na kipimo hicho huwa hakikosei. jamani nilivyotoka hapo nilitafuta sehemu nitumie zaka maana niliahidi MUNGU akiniponya basi zaka itakua sehemu ya maisha yangu.
Hakika namshukuru sana MUNGU na namtukuza sana sana.
Mtumishi uzidi kubarikiwa sana.
USHUHUDA WA AJABU.
Bwana Yesu asifiwe mtumishi Peter Mabula. Tuliongea na ukaniombea ilikuwa mwezi wa pili mwaka huu. Namshkuru Mungu amenisaidia kunikinga na mawakala wa shetani nilioingia mikononi mwao bila ya kujua wakaniumiza sana.
Nimekupigia simu hii nakuomba kama utaona vyema fedha yangu ya fungu la kumi mwezi huu niitume kwako kama shukrani kwa Mungu wangu ili unitumie kitabu chako cha MAOMBI YA KINA.
Siwezi kueleza sana ila kila cha kipepo ulichokifukuza maishani mwangu kwa maombi yako kimeondoka, Mungu wetu kweli anaishi
Nakumbuka
Uliniunganisha na mtu hapa Tabora mjini nilipompigia akasema Vitabu vimeisha labda aniuzie chake. Kama utaona vyema naomba nikipate moja kwa moja toka kwako. Utanitumia kwenye anuani nitakayokutumia. Barikiwa mtumishi.
USHUHUDA.
Hakika MUNGU ni wa ajabu sana na Matendo yake ni makuu. Mama mmoja alinipigia simu Leo ili nimuombee maana alikuwa hoi, hata kutembea hawezi. Alisema mwili ulikuwa unaumwa na siku ugonjwa ulivyoanza ilikuwa ghafla tu, Leo Kanipigia simu maana alipewa namba na mtoto wake ambaye siku moja alisoma somo langu mtandaoni na kuchukua namba yangu. Mama huyu aliponipigia simu nilimuombea kisha nikamwambia Bwana YESU anakuponya. Nusu saa baadae akanipigia simu na kuniambia kwamba hakika amepona. Hata Mimi nilimtukuza MUNGU kwa muujiza huu. Kisha akaniandikia ujumbe huu.
"Mtumishi Mabula atukuzwe MUNGU wa mbinguni sifa na utukufu una yeye
ameniponya. ubarikiwe mtumishi wa MUNGU, damu ya YESU ikutakase, mkono
wa MUNGU ukuinue zaidi, MUNGU akupe afya na nguvu na mamlaka uendelee
kutenda kazi katika Bwana YESU ukifungua walio kifungoni mwa shetani.
ninaomba na kushukuru ni katika jina laYESU KRISTO AMEEN!"
Comments