| Na Peter M Mabula. Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU |
Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.
Kuna aina nyingi za watumishi hivyo uwe makini sana.
Sio kila anayejiita ni Mtumishi basi huyo ni Mtumishi wa MUNGU wa mbinguni.
Kuna watumishi waliojiita wenyewe wakiwa na ajenda zao mbaya za siri sana.
Hawa wana sifa nyingi tu mbaya na mojawapo ya sifa yao kuu ni kwamba wao kuhubiri utakatifu ni nadra sana sana.
Hawa wana lengo Lao lisilo la KRISTO YESU Mwokozi.
Wakolosai 2:4 '' Nasema neno hili, mtu asije akawadanganya kwa maneno ya kuwashawishi.''
Kuna watumishi waliotumwa na shetani ili kuwaondoa watu kwenye wokovu wa KRISTO.
Hawa ni mawakala wa shetani Kabisa.
1 Timotheo 4:1-3 '' Basi ROHO anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani; kwa unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe;''
Kuna watumishi wasiojua wanamtumikia nani.
Hawa huiga watumishi wengine wa MUNGU.
Hawa hujipa majina mazuri ili majina hayo yawafanye waonekane ni watumishi wa MUNGU kumbe wala sio.
Hawa wanaweza wakatunga hadithi za uongo ili kupumbaza watu ili watu hao wasiambatane na YESU KRISTO Mwokozi.
2 Timotheo 4:3-4 ''Maana utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia waalimu makundi makundi, kwa kuwa wana masikio ya utafiti; nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli, na kuzigeukia hadithi za uongo.''
Lakini pia kuna watumishi halisi wa MUNGU.
Hawa wanamhubiri KRISTO na injili yake ya Wokovu wa milele.
Matendo 10:42 '' Akatuagiza tuwahubiri watu na kushuhudia ya kuwa huyu ndiye aliyeamriwa na MUNGU awe Mhukumu wa walio hai na wafu. ''
Ukiona mahubiri yeyote ambayo hahubiriwi YESU KRISTO kama Mwokozi pekee ujue hapo unapotezwa.
Ukiona mahubiri ambayo yanawafanya watu kutegemea vitu na sio MUNGU ujue hapo unapotezwa.
Ukiona mahubiri yanaegemea kwenye mambo ya kidunia tu ujue hapo unapotezwa.
Roho ya mpinga Kristo ipo na wapo watumishi wengi tu wako upande wa mpingaKristo, hawa hawahubiri tena Wokovu, hawahubiri utakatifu, hawahubiri juu ya siku ya hukumu, hawahubiri kumtegemea MUNGU, Hawahubiri kumcha MUNGU, Hawahubiri kuhusu ROHO MTAKATIFU na hawamtaki kwao, msingi wa imani yao sio YESU KRISTO bali ni waanzilishi wa madhehebu yao, uwe makini sana ndugu maana unaweza kumtii sana mwanzilishi wa dhehebu lako hata kama yuko kinyume na YESU KRISTO. Kuna waanzilishi wa madhehebu wamepewa heshima kubwa kiasi kwamba Neno la MUNGU limeshamezwa na nasaha za mwanzilishi wa dhehebu, hiyo ni kazi ya shetani kuwafanya watu wawe mbali na YESU KRISTO.
2 petro 3:3 '' Mkijua kwanza neno hili ya kwamba katika siku za mwisho watakuja na dhihaka zao watu wenye kudhihaki, wafuatao tamaa zao wenyewe,''
Kumbuka kwamba katika masuala ya imani maroho wa kuzimu wanatenda kazi kwa siri sana hivyo watu wa MUNGU muwe makini sana. Roho ya mpinga Kristo imewavaa watumishi wengi sana na wengine walichobakiza kwa sasa ni kutoa tu mifano ya kumkejeli YESU, Ndugu ukiwa huko tambua kwamba unapotezwa.
Ukiona Mtumishi yeyote na popote pale anampinga YESU KRISTO kwa neno lolote ujue Mtumishi huo sio mtumishi wa MUNGU wa mbinguni, uwe makini sana maana roho ya mpinga Kristo imewavaa wengi.
1 Yohana 4:1-3" Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na MUNGU; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani. Katika hili mwamjua ROHO wa MUNGU; kila roho ikiriyo kwamba YESU KRISTO amekuja katika mwili yatokana na MUNGU. Na kila roho isiyomkiri YESU haitokani na MUNGU. Na hii ndiyo roho ya mpinga Kristo ambayo mmesikia kwamba yaja; na sasa imekwisha kuwako duniani."
Sasa katika wakati wa sasa watumishi wa MUNGU ni wengi, hilo ni jambo jema sana, lakini hata watumishi wa shetani ni wengi, hiyo ni hatari sana
Uwe makini na watumishi maana sio wote ni watumishi wa MUNGU katika KRISTO.
Jifunze mambo haya itakusaidia.
Alama za kudumu za Mtumishi wa kweli wa MUNGU.
1. Yeye mwenyewe awe ameokolewa na YESU KRISTO.
Waefeso 2:8 ''Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha MUNGU; ''
Kama yeye hajaokoka basi huyo hatimizi sifa za utumishi katika kazi ya MUNGU.
Mitume waliokolewa kwanza na YESU ndipo na wao wakatumwa kutumika.
2. Awe kielelezo chema cha kuishi maisha matakatifu na maisha ya haki.
1 Petro 1:15-16 '' bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote; kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu. ''
Ni lazima awe anaishi maisha matakatifu.
Kama hawezi kuishi maisha matakatifu basi hawezi kutumika vyema katika injili.
3. Awe analitumia Neno la MUNGU kwa haki na kweli ya KRISTO.
2 Timotheo 2:15-16 '' Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na MUNGU, mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli. Jiepushe na maneno yasiyo na maana, ambayo si ya dini; ......... ''
4. Awe anaenenda kwa ROHO MTAKATIFU na kuongozwa na ROHO MTAKATIFU katika kufanya kazi ya MUNGU.
Warumi 8:14 '' Kwa kuwa wote wanaoongozwa na ROHO wa MUNGU, hao ndio wana wa MUNGU.''
ROHO MTAKATIFU huisimamia Biblia katika kusudi la MUNGU.
Mtumishi halisi wa KRISTO ni lazima awe anaenenda kwa ROHO MTAKATIFU na anamtii ROHO MTAKATIFU.
5. Awe mtii na mnyenyekevu kwa MUNGU na kwa YESU KRISTO.
1 Petro 5:6-9 '' Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa MUNGU ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake; huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu. Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze. Nanyi mpingeni huyo, mkiwa thabiti katika imani, ...... ''
Mtumishi lazima ajue yeye sio Mwokozi Bali Mwokozi ni Bwana YESU.
Awe chini ya Neno la MUNGU na kulitii.
Mtumishi wa MUNGU kabla hajaanza kumtumikia MUNGU katika injili ya KRISTO anatakiwa awe amefaulu utii huu:1 Petro 1:15-16 '' bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote; kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu. ''
Ni lazima awe anaishi maisha matakatifu.
Kama hawezi kuishi maisha matakatifu basi hawezi kutumika vyema katika injili.
3. Awe analitumia Neno la MUNGU kwa haki na kweli ya KRISTO.
2 Timotheo 2:15-16 '' Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na MUNGU, mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli. Jiepushe na maneno yasiyo na maana, ambayo si ya dini; ......... ''
4. Awe anaenenda kwa ROHO MTAKATIFU na kuongozwa na ROHO MTAKATIFU katika kufanya kazi ya MUNGU.
Warumi 8:14 '' Kwa kuwa wote wanaoongozwa na ROHO wa MUNGU, hao ndio wana wa MUNGU.''
ROHO MTAKATIFU huisimamia Biblia katika kusudi la MUNGU.
Mtumishi halisi wa KRISTO ni lazima awe anaenenda kwa ROHO MTAKATIFU na anamtii ROHO MTAKATIFU.
5. Awe mtii na mnyenyekevu kwa MUNGU na kwa YESU KRISTO.
1 Petro 5:6-9 '' Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa MUNGU ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake; huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu. Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze. Nanyi mpingeni huyo, mkiwa thabiti katika imani, ...... ''
Mtumishi lazima ajue yeye sio Mwokozi Bali Mwokozi ni Bwana YESU.
Awe chini ya Neno la MUNGU na kulitii.
1. Awe amefaulu katika kumtii MUNGU.
Yakobo 4:7-10 '' Basi mtiini MUNGU. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia. Mkaribieni MUNGU, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu, enyi wenye nia mbili. Huzunikeni na kuomboleza na kulia. Kucheka kwenu na kugeuzwe kuwa kuomboleza, na furaha yenu kuwa hamu. Jidhilini mbele za BWANA, naye atawakuza. ''
2. Awe amefaulu katika kumtii YESU KRISTO .
Yohana 15:14 '' Ninyi mmekuwa rafiki zangu, mkitenda niwaamuruyo. ''
3. Awe amefaulu katika kumtii ROHO MTAKATIFU.
Zaburi 32:8 '' Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea; Nitakushauri, jicho langu likikutazama.''
Kumtii ROHO MTAKATIFU ni pamoja na kukubali kuongozwa naye na kuenenda katika yeye.
4. Awe amefaulu katika kulitii Neno la MUNGU na ajue kwamba atatakiwa kulitii Neno la MUNGU siku zote.
Kumb 28:1 '' Itakuwa utakaposikia sauti ya BWANA, Mungu wako, kwa bidii, kutunza kuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo leo, ndipo BWANA, Mungu wako, atakapokutukuza juu ya mataifa yote ya duniani; ''
Mtumishi wa MUNGU akifaulu katika utii huo hakika huyo atakuwa mtumishi mzuri wa MUNGU na atalitumikia kusudi la MUNGU kwa usahihi.
''
Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo ROHO ayaambia
makanisa. Yeye ashindaye hatapatikana na madhara ya mauti ya pili.
-Ufunuo 2:11''
Natamani niseme mengi mno lakini naamini mwenye kuelewa ameelewa.
MUNGU
akubariki kwa kujifunza somo hili muhimu pia kitabu changu cha MAOMBI
YA KINA kinapatikana, tuwasiliane nitakujulisha jinsi ya kukipata.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je,
Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika
Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima
Wa Milele?
Majibu
Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea
Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU.
+255714252292(Hadi whatsapp).
Nakuomba share kwa marafiki zako ujumbe huu.
Comments