![]() |
| Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu zangu wote.
Karibu sana tujifunze Neno la MUNGU la maombi kisha tuombe maombi ya ushindi kupitia jina kuu la YESU KRISTO Mwokozi wetu.
Vita yetu siku zote ni juu ya falme za giza, mammlaka za giza, wakuu wa giza na majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho, ndivyo inavyosema Waefeso 6:12.
Na maadui hao hutumia wanadamu wanaoitwa wachawi, washirikina, wanga, waganga wa kienyeji n.k ili tu kutimiza waliyokusudia.
Kwa sababu ni vita ya kiroho ni muhimu kujua kwamba vita ni vita tu, na vita ya kiroho kuna kushinda kama una nguvu za kiroho kuliko adui yako, na kuna kushindwa kama adui yako atakuzidi ujanja na nguvu.
Ashukuriwe MUNGU maana kupitia Wokovu wa KRISTO kwetu tumepewa nguvu kuliko nguvu za giza zote, haijalishi ni nguvu za giza kiasi gani, ndivyo inavyosema Luka 10:19 '' Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru.''
Yaani nguvu zote zote zoteeeee za yule shetani Biblia inasema tuna nguvu kuliko hizo na tuna mamlaka ya kuziharibu.
Sasa kwa sababu ni vita ya kiroho maadui zako wanaweza kufanya mitego ili tu wewe usiwe na uwezo wa kuwashinda.
Neno mtego wa giza lina maana mbili;
✓✓Maana ya kwanza ni kwamba mtego wa kipepo ni chombo kitumiwacho na mawakala wa shetani ili kunasa kinachohitajika.
✓✓Maana ya pili ya mtego wa kipepo ni ni tendo linalofanywa kwa siri na kwa ujanja na akili nyingi na mawakala wa shetani ili wapate wanachokihitaji.
Mawakala wa shetani wana mitego yao ambayo wanaweza kumtegea mtu ili wamnase na kumtesa kama walivyokusudia.
Ndugu, kama iko hivyo na kwako hakikisha unaomba MUNGU na kushinda kila mitego ya kipepo.
Zaburi 124:7-8 '' Nafsi yetu imeokoka kama ndege Katika mtego wa wawindaji, Mtego umevunjika, nasi tumeokoka. Msaada wetu u katika jina la BWANA, Aliyezifanya mbingu na nchi. ''
Ngoja nikupe mifano hai ili unielewe vyema.
Wanandoa fulani(ninawafamu) walikuwa wanaishi vizuri katika familia yao ya Kikristo, baadae wakahitaji msichana wa kazi na wakaagiza kutoka mkoa wa mbali, kumbe yule Msichana wa kazi alikuwa mchawi na alifundishwa uchawi na babu yake tangu utotoni, Binti yule alikuwa ni mtego wa shetani ili kuharibu familia ile maana alifanya uchawi wake taratibu taratibu, kwa kutumia vitu vingi vikiwemo vyakula na maneno ya kinywa, matokeo yake yalikuwa nini?
Mtego wa shetani ulifanikiwa maana ndoa ile ilikufa, na mama wa familia ile alifukuzwa akiwa mimba ya miezi 8.
Msichana yule alitumika kama nyavu au mtego wa kichawi.
1 Timotheo 3:7b inaonyesha kwamba mitego ya ibilisi ipo hivyo tunatakiwa kuishinda, Biblia inasema katika andiko hilo kwamba '' ili asianguke katika lawama na mtego wa Ibilisi. ''
Mchungaji mmoja aliletewa zawadi ya suti kutoka ulaya, alifurahi sana na aliwaamini waliomletea maana ni watu wa MUNGU waliofahamiana naye kwa muda mrefu, ajabu ni kwamba kila siku mchungaji huyo akivaa suti hiyo aliwaka tamaa ya ngono kupita kawaida, ujumbe uliyeyuka na kila mwanamke aliyemuona mbele yake alitamani amvulishe nguo na kuzini naye kwa nguvu. Mtumishi yule ni Mtumishi safi na mwaminifu wa Bwana YESU hivyo alijikuta analia tu na hata kushindwa kuhubiri huku akishangaa tamaa hiyo inatoka wapi? maana ana mke na hajawahi kuisaliti ndoa yake, alishangaa sana hali ile maana mwili ulisisimka na alihisi kuchanganyikiwa sana lakini akivua tu suti ile anarudi kwenye hali ya kawaida na hata anaanza kujishangaa kwanini alipatwa na tamaa hizo chafu. Siku moja hali ile ilimpata na aliomba na kulia sana bila mafanikio, aliamua kumshirikisha Mchungaji ambaye ni rafiki yake ambaye alipoomba aliona kwenye ulimwengu wa roho aliona ile suti. Alimwambia na suti ile wakaichoma moto, na tangu siku hiyo tamaa ile chafu haikumfuata tena.
Mtego wa shetani hapa ulikuwa ndani ya nguo, ni neema ya MUNGU hakunaswa na nguvu za giza hizo.
Je Kama wewe ni Mwanamke na amenasa katika mtego kama huo si atakuletea hadi magonjwa mabaya?
Je kama mtego kama huo umemnasa Baba yenu si mnaweza kulala njaa kila siku na shule mnafukuzwa kwa sababu ya karo wakati Baba yenu ana kazi nzuri na mshahara mzuri ila kwa sasa anachowaza ni ngono tu kwa sababu ya mtego wa shetani uliomnasa.
Ndugu, ipo mitego mingi ya giza inaweza kuwekwa kwenye eneo lako la biashara, kiwanja chako,kwenye kazi yako, kwenye kiti chako ofisini, kwenye nguo zako, kwenye pesa zako, kwenye ngozi yako n.k
Leo tunategua mitego yote ya kichawi na kuiondoa.
Kwanini labda mawakala wa shetani wakutegee mitego?
1. Ili wakunase na kukudhuru.
Zaburi 57:6 '' Wameweka wavu ili kuninasa miguu; Nafsi yangu imeinama; Wamechimba shimo mbele yangu; Wametumbukia ndani yake!''
Ndugu, leo kataa kunaswa na mitego ya mawakala wa shetani.
2. Ili usiendelee mbele katika mipango yako ya maisha.
Zaburi 56:5-6 '' Mchana kutwa wanapotosha maneno yangu, Mawazo yao yote ni juu yangu kunitakia mabaya. Hukutanika, hujificha, huziangalia nyayo zangu, Kwa kuwa wameniotea nafsi yangu.''
Wanaweza kukutegea miguu yako kiroho ili usifanikiwe, wanaweza wakaiotea nafsi yako ili wainase, usikubali kamwe kukwamishwa na mitego ya kipepo.
3. Ili uabike na kufedheheka.
Mithali 29:5 '' Mwenye kujipendekeza kwa jirani yake, Hutandika wavu ili kuitega miguu yake. ''
Usikubali kuabishwa na wakuu wa giza.
4. Ili kuchelewesha baraka zako.
Ayubu 18:10 '' Amefichiwa tanzi chini, Na mtego amewekewa njiani.''
Katika mitego ya njia zako za baraka kama umewekewa mitego ya giza hakikisha unaiharibu mitego hiyo na kuitowesha.
5. Ili kukuondolea uwezo wa kufanikiwa.
Zaburi 140:5 '' Wenye kiburi wamenifichia mtego na kamba; Wametandika wavu kando ya njia; Wameniwekea matanzi. ''
Mitego ya kipepo iko mingi sana lakini unaweza kuiharibu kwa maombi na ukafanikiwa wewe huku wao wakiabika.
✓Inawezekana wewe una mchumba na mnakaribia kufunga ndoa, lakini kuna mtu anaweza kutumika kama mtego wa giza ili kuharibu uchumba wako kabla ya ndoa.
✓✓Inawezekana unataka kazi na kuna mtu anafanya mipango ya siri ili usipate kazi.
✓✓Inawezekana unafanya biashara na kuna jirani yako ni wakala wa shetani na anafanya mbinu kila muda ili tu usifanikiwe kibiashara.
Kuna mitego mingi ya giza lakini ukisimama katika nafasi yako kama Mkristo mwombaji hakika utashinda huku waliotega mitego hiyo wakipata madhara wao.
Jinsi ya kujinasua katika mitego ya kipepo.
1. Omba MUNGU akutoe katika mitego ya kipepo.
Zaburi 91:3 ''Maana Yeye(MUNGU) atakuokoa na mtego wa mwindaji, Na katika tauni iharibuyo.''
2. Enenda kwa ROHO MTAKATIFU.
1 Kor 2:10 '' Lakini MUNGU ametufunulia sisi kwa ROHO. Maana ROHO huchunguza yote, hata mafumbo ya MUNGU. ''
ROHO MTAKATIFU huchunguza kila kitu kutoka hata kwa maadui zako na anakujulisha, hivyo ukimtii ROHO MTAKATIFU na kuenenda katika yeye huwezi kamwe kunaswa katika mitego ya kipepo.
3. Vunja uhusiano na mawakala wa shetani.
Zaburi 1:1 '' Heri mtu yule asiyekwenda Katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wakosaji; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha.''
4. Omba MUNGU akuokoe na nguvu za giza.
Hosea 13:14 '' Nitawakomboa na nguvu za kaburi; nitawaokoa na mauti; ewe mauti, ya wapi mapigo yako? Ewe kaburi, ku wapi kuharibu kwako? Kujuta kutafichwa na macho yangu. ''
5. Omba MUNGU akulinde dhidi ya kila hila za giza.
Zaburi 141:9-10 '' Unilinde na mtego walionitegea, Na matanzi yao watendao maovu. Wabaya na waanguke katika nyavu zao wenyewe, Pindi mimi ninapopita salama.''
Natamani niseme mengi mno lakini naamini mwenye kuelewa ameelewa na somo hili kuna wakati nitalifafanua zaidi ndani ya kitabu.
MUNGU akubariki kwa kujifunza somo hili muhimu
Hapa chini ni MAOMBI YA KUTEGUA NA KUONDOA MITEGO YA WANAOTUMIKA KIPEPO DHIDI YAKO.
Maombi haya naomba yamsaidie mtu yule ambaye hajui kuomba ili katika kuomba kwa kutumia hayo basi atakumbuka mahitaji yake na kuyataja katika maombi yake. Haya hapa chini ni maombi ya kuanzia tu katika maombi yako ili uendelee zaidi kuomba
Kwa waombaji wazoefu naamini baada tu ya kulisoma somo na kulielewa basi anajua aombee nini maana alikuwa anaandika points za kuombea. Kumbuka pia fundisho ni muhimu kuliko maombi hivyo wewe ambaye huwa unahusika na maombi tu hakikisha unajifunza kwanza somo lote ndipo utapata nguvu za kuomba na kushinda.
MAOMBI YA KUTEGUA NA KUONDOA MITEGO YA WANAOTUMIKA KIPEPO DHIDI YAKO.
Baba katika jina la YESU KRISTO ninakushukuru na kukutukuza siku zote za maisha yangu.
Nashukuru maana ni kwa neema yako tu ndio maana mimi niko hai leo na ninaendelea mbele katika wewe MUNGU Muumba wangu.
Niko mbele zako BWANA ninaomba unisamehe kwa makosa yangu, maovu yangu na dhambi zangu zote, Nakuomba MUNGU wangu unitakase jina langu, nafsi yangu, mwili wangu na roho yangu, nitakase Eee MUNGU wangu kwa damu ya YESU KRISTO ya agano jipya.
Katika jina la YESU KRISTO ninaharibu kila mitego ya kipepo iliyotegwa mchana au usiku.
Ninaiharibu na kuitoweshwa kila mitego ya kipepo iliyotengenezwa na mwanaume au mwanamke.
Kila mtego wa kipepo nauvunja na kuuharibu kwa jina la YESU KRISTO.
Eee Bwana YESU ninakushukuru Mwokozi wangu kwa kuja kuniokoa mimi na kunipa neema yako ya Wokovu.
Ninaomba Bwana YESU nitetee katika maisha yangu ya wokovu na nitetee siku zote za maisha yangu ili nimpendeza MUNGU Muumbaji wangu siku zote.
Eee MUNGU wangu niko hapa leo ninaomba nikiwa kinyume na kila mitego ya giza niliyotegewa popote.
Kwa Mamlaka ya jina la YESU KRISTO kama ilivyoandikwa katika Yohana 14:14 niko hapa ninafuta kila mitego ya kipepo niliyotegewa.
Mitego ya kichawi iliyotegwa kwenye afya yangu au uchumi wangu, ninaifuta mitego hiyo kwa jina la YESU KRISTO.
Kila mitego ya maneno na mitego ya laana inayowinda maisha yangu, ninaifuta mitego hiyo kwa jina la YESU KRISTO.
Mitego ya madawa ya kichawi na mitego ya sumu za kichawi inayoelekezwa katika maisha yangu, ninaifuta mitego hiyo kwa jina la YESU KRISTO.
Kila mtego wa kishirikina ulioandaliwa ili unikamate, naamuru kwa mamlaka ya jina la YESU KRISTO kwamba mtego huo wa giza uharibike na hautanipata mimi kamwe.
Eee MUNGU Baba ninakuomba unitoe katika kila mitego ya kipepo niliyotegewa, Eee MUNGU wangu naomba unitoe katika mitego niliyotegewa kazini kwangu, kwenye njia yangu, kwenye Kanisa au mitego iliyotegwa na majirani wasionipenda, Eee Bwana YESU nakuomba unitoe katika mitego hiyo yote.
Kwa sababu mawakala wa shetani ndio hupanga mitego ili inipate, sasa kwa mamlaka ya jina la YESU KRISTO ninavunja kila uhusiano na mawakala wa shetani wa kila namna.
Ninavunja kila muunganiko uliyo kwenye ulimwengu wa roho kati yangu na majinim mahaba, mizimu, waganga, wachawi na wakuu wa giza.
Kuanzia sasa sina uhusiano tena na wakala wa shetani yeyote.
Ewe Wakala wa shetani nakuamuru sasa achia afya yangu na uchumi wangu, katika jina la YESU KRISTO na uachie sasa afya yangu na uchumi wangu.
Achia kibali changu na ndoa yangu, achia uchumba na uzao wangu, achia kila baraka yangu kwa jina la YESU KRISTO Mwokozi aliye hai achiaaaaaaa.
Nakushukuru MUNGU Baba maana unasema katika Hosea 13:14 kwamba '' Nitawakomboa na nguvu za kaburi; nitawaokoa na mauti; ewe mauti, ya wapi mapigo yako? Ewe kaburi, ku wapi kuharibu kwako? Kujuta kutafichwa na macho yangu. ''
Eee MUNGU wangu naomba unikomboe afya yangu dhidi ya nguvu za kaburi.
MUNGU wangu komboa ndoa yangu na uzao wangu dhidi ya kila nguvu za kaburi.
Katika jina la YESU KRISTO Ndoa yangu haitakufa, uchumba wangu hautavunjika, biashara yangu haitafilisika wala uchumi wangu hautapotea.
Ninakushuru MUNGU wa mbinguni maana katika wewe kuna ushindi.
Ninaomba MUNGU wangu unipe neema ya kushinda kila mipango ya giza, Eee ROHO MTAKATIFU ninakukaribisha ndani yangu Bwana na ninaomba uniongoze na kunifundisha kila eneo la maisha yangu ili usiwepo mtego wa kipepo wa kuninasa.
Najua kuna wakati kuna mitego ya kipepo dhidi yangu lakini ninakushukuru MUNGU Baba maana ninaomba '' Unilinde na mtego walionitegea, Na matanzi yao watendao maovu. Wabaya na waanguke katika nyavu zao wenyewe, Pindi mimi ninapopita salama.'' kama Zaburi 141:9-10 inavyosema.
Ninakushuru sana MUNGU wangu maana najua hakuna mtego wa kipepo utanipata.
Katika jina la YESU KRISRTO nimeomba na sasa ninashukuru.
Amen Amen Ameeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeen.
Hakika umeshinda. Ukiweza hata kuwa na maombi ya kufunga unaweza, pia baada ya maombi yako unaweza kufanya tendo la imani kwa MUNGU kwa kutoa sadaka itakayoambatana na maombi juu ya ukomo wa kuteswa na maadui zako katika ulimwengu wa roho, huo ni utashi wako na sio agizo.
Nawaonya pia wanaotumia masomo yangu vibaya na kwa manufaa yao waache tabia hiyo.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU.
+255714252292( whatsap, sadaka ya kuipeleka Injili mbele, Maombezi na Ushauri).

Comments