![]() |
| Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
Bwana YESU nifungue macho na nionyeshe njia yako siku zote, nishike mkono siku zote ili nikufuate maisha yangu yote.
Katika utumishi wakati mwingine kuna kusongwa, kutukana, kudharauliwa, kudhihakiwa na kuonewa.
Neno lako bado linaniambia kwamba "Majani yakauka, ua lanyauka; Bali neno la MUNGU wetu litasimama milele. Wewe uuhubiriye Sayuni habari njema, Panda juu ya mlima mrefu; Wewe uuhubiriye Yerusalemu habari njema, Paza sauti kwa nguvu; Paza sauti yako, usiogope; Iambie miji ya Yuda, Tazameni, MUNGU wenu. Tazameni, BWANA Mungu atakuja kama shujaa, Na mkono wake ndio utakaomtawalia; Tazameni, thawabu yake i pamoja naye, Na ijara yake i mbele zake.-Isaya 40:8-10"
Wakati mwingine kuna milima na mabonde, wakati mwingine Wateule wako tunaonekana mbele ya watu wa dunia kama waliochanganyikiwa, wakati mwingine njia ya utakatifu inaonekana kama ya wanyonge tu na wasio na akili mbele ya ulimwengu lakini Neno lako la milele linasema hata kama tutaonekana wajinga duniani lakini hatutapotea na tuendako ni uzima wa milele.
Isaya 35:8 "Na hapo patakuwa na njia kuu, na njia, nayo itaitwa, Njia ya utakatifu; wasio safi hawatapita juu yake; bali itakuwa kwa ajili ya watu hao; wasafirio, wajapokuwa wajinga, hawatapotea katika njia hiyo."
Haijalishi maadui ni wengi sana lakini bado wewe YAHWEH uliyeumba mbingu na dunia upo pamoja nami.
Hata kama maadui zangu ni wengi kuliko nywele za kichwa changu na mipango yao yote ni kutafuta njia ya kunionea, hata hapo najua nitashinda.
Zaburi 69:4 " Wanaonichukia bure ni wengi Kuliko nywele za kichwa changu. Watakao kunikatilia mbali wamekuwa hodari, Adui zangu kwa sababu isiyo kweli. Hata mimi nalilipishwa kwa nguvu Vitu nisivyovichukua."
Haijalishi kuna wachawi na majini.
Haijalishi kuna wanadamu wabaya na maroho ya kuzimu, bado katika Jina la YESU KRISTO nitashinda.
Haijalishi kuna vingunge na wakuu wa giza lakini ninakushukuru MUNGU wangu maana unaniambia kwa uhakika kwamba
" usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni MUNGU wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu. Tazama, wote walioona hasira juu yako watatahayarika na kufadhaika; watu washindanao nawe watakuwa si kitu, na kuangamia. Utawatafuta wala hutawaona wale wapiganao nawe; watakuwa si kitu; watakuwa kama kitu kisichokuwa, wale waliofanya vita juu yako. Kwa maana mimi, BWANA, Mungu wako, nitakushika mkono wako wa kuume, nikikuambia, Usiogope; mimi nitakusaidia.-Isaya 41:10-13.
Ninakushukuru MUNGU muumba wangu maana wewe u pamoja nami.
Sitaogopa chochote maana Mimi najua katikati ya maadui wengi Mimi nitakuwa mshindi.
Asante Bwana YESU KRISTO kwa wema wako, kwa kuja kuniokoa Mimi Peter Mabula
Nalitukuza jina lako maana wewe YESU KRISTO Mwokozi wangu u mwema.
Nakushukuru JEHOVAH MUNGU wangu maana unaniwazia mema daima, nakushukuru wewe peke yako maana ushirika kati yangu na ROHO wako MTAKATIFU unanipa kushinda kila iitwapo Leo.
Katika jina la YESU KRISTO nimeomba na sasa ninashukuru kwa MUNGU wangu.
Amen Amen Amen.
✓✓Ndugu unayesoma ujumbe huu, Mimi nilikuwa nazungumzia na MUNGU wangu wa Mbinguni, hata wewe hakikisha kila Mara una muda wa kuzungumza na MUNGU wa mbinguni huku ukiishi maisha matakatifu ya Wokovu wa KRISTO YESU ulio wa thamani sana.
◼️MUNGU akubariki na kwa maombi natarajia ushindi mkuu, hata wewe kama umeokoka omba, kama hujaokoka okoka kwanza na usisahau kuwa mtu wa maombi.
Zingatia na MUNGU atakubariki sana.
Mche MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi na utaitwa heri.
Kama pia unatumia Facebook ni follow maana itafika kipindi nitakuwa napost tu katika page yangu na profile yangu.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292.
Ubarikiwe sana

Comments