![]() |
| Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe Ndugu zangu wote.
Nawakaribisha tujifunze Neno la MUNGU wa Mbinguni.
◼️Nafasi ya Wokovu uliyopewa na MUNGU ishikilie.
Waebrania 2:3-4 " sisi je! Tutapataje kupona, tusipojali wokovu mkuu namna hii? Ambao kwanza ulinenwa na Bwana(YESU), kisha ukathibitika kwetu na wale waliosikia; MUNGU naye akishuhudu pamoja nao kwa ishara na ajabu na nguvu za namna nyingi, na kwa magawanyo ya ROHO MTAKATIFU, kama alivyopenda mwenyewe."
✓✓Wokovu ni mpango wa MUNGU kuwaokoa wanadamu ili hao wanadamu wasiende jehanamu.
◼️Wokovu wa MUNGU una njia moja tu ambayo ni YESU KRISTO.
Yuda 1:3 "Wapenzi, nilipokuwa nikifanya bidii sana kuwaandikia habari ya wokovu ambao ni wetu sisi sote, naliona imenilazimu kuwaandikia, ili niwaonye kwamba mwishindanie imani waliyokabidhiwa watakatifu mara moja tu."
◼️Sasa kwa wewe ambaye umeshaokoka itunze sana nafasi hiyo aliyokupa MUNGU kwa Neema yake.
✓✓MUNGU alikutoa kwa shetani na akakupeleka katika nafasi ya maisha ya Wokovu kwa sababu alipendezwa na wewe, ukiwa sasa katika nafasi hiyo hakikisha unaishi maisha matakatifu ya huo Wokovu wa KRISTO kwako.
2 Samweli 22:20-22 " Akanitoa akanipeleka panapo nafasi; Aliniponya kwa kuwa alipendezwa nami. BWANA alinitendea sawasawa na haki yangu; Sawasawa na usafi wa mikono yangu akanilipa. Maana nimezishika njia za BWANA, Wala sikumwasi MUNGU wangu."
◼️Zishike njia ya MUNGU na usimwasi MUNGU kamwe.
◾Nini nataka kusema?
◼️Ni kwamba hakikisha kazi yako haikuondolei nafasi yako kwa MUNGU.
◼️Hakikisha mafanikio yako hayakuondolei nafasi yako kwa MUNGU.
Usiwe kama Yeshuruni ambaye aliponenepa kiuchumi akamwacha MUNGU na akaanza kumdharau MUNGU, ni mbaya sana.
Kumbu 32:15 Lakini Yeshuruni alinenepa, akapiga teke; Umenenepa, umekuwa mnene, umewanda; Ndipo akamwacha MUNGU aliyemfanya, Akamdharau Mwamba wa wokovu wake.
◼️Hakikisha uchumi wako haikuondolei nafasi yako kwa MUNGU.
Jitunze usije ukamsahau Bwana YESU maana alikutoa kwa shetani akakuokoa na kuliandika Jina lako katika kitabu Cha Uzima, usije ukamsahau kwa sababu ya mafanikio ya kimwili.
Kumbu 6:12-14 " ndipo ujitunze, usije ukamsahau BWANA aliyekutoa nchi ya Misri, nyumba ya utumwa. Mche Bwana, MUNGU wako; ndiye utakayemtumikia, na kuapa kwa jina lake. Msifuate miungu mingine katika miungu ya mataifa wawazungukao;"
✓✓Ni hatari sana ukimwacha YESU KRISTO Mwokozi.
Kumbu 8:19 "Lakini itakuwa, kama ukimsahau BWANA, Mungu wako, na kuiandama miungu mingine, na kuitumikia na kuiabudu, nawashuhudia leo ya kuwa mtaangamia bila shaka."
✓✓Nafasi yako ya kiroho uliyopewa na MUNGU kwa Wokovu ni ya thamani kuliko uchumi, biashara na chochote chako.
Neno la MUNGU linasema,
Zaburi 119:4 " Wewe umetuamuru mausia yako, Ili sisi tuyatii sana."
◼️MUNGU ametupa Neno lake ili tulizingatie na kulitii sana.
◼️Itunze nafasi yako ya kiroho uliyopewa na MUNGU Baba baada ya kuokolewa na YESU KRISTO Mwokozi.
✓✓Hakikisha unaitunza nafasi ya Wokovu wa KRISTO ambayo MUNGU alikupa.
◼️ Baadhi ya Umuhimu wa Wokovu wa KRISTO.
1. Wokovu wa KRISTO una Kinga za kiroho ndani yake.
2 Samweli 22:36 "Nawe umenipa ngao ya wokovu wako; Na unyenyekevu wako umenikuza."
◼️Unaweza ukashangaa Kuna matatizo ya kiroho yanawapa walio ndani ya Wokovu lakini Wewe hayakupati kwa sababu uko ndani Ya Wokovu, mfano laana, kurogwa, kuchezewa na nguvu za giza n.k
Ukiwa vizuri katika Wokovu wa KRISTO hayo hayatakupata maana huwa Kuna "Ngao ya Wokovu " inaambatana na walio ndani ya Wokovu.
Ngao ni Kinga inayomzuia adui kufanya uharibifu.
2. Wokovu wa KRISTO hubeba kusamehewa Dhambi kwa waliotubu.
Luka 1:77 "Uwajulishe watu wake wokovu, Katika kusamehewa dhambi zao."
◼️Uliupokea Wokovu wa KRISTO kwa Sala ya Toba hivyo ulisamehewa dhambi zako zote hata kama zilikuwa dhambi mbaya na kubwa kiasi gani.
Warumi 10:10 "Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu."
3. Hakuna Wokovu nje na Bwana YESU KRISTO.
Matendo 4:12 "Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo."
◼️Hivyo kila Mwanadamu anayeutaka uzima wa milele aingie kwanza katika Wokovu wa KRISTO.
4. Injili ya KRISTO ndio huuleta Wokovu.
Warumi 1:16 "Kwa maana siionei haya Injili; kwa sababu ni uweza wa MUNGU uuletao wokovu, kwa kila aaminiye, kwa Myahudi kwanza, na kwa Myunani pia."
◼️Hivyo ni Muhimu sana kuambatana na Injili ya KRISTO kama unauhitaji Wokovu wa MUNGU juu ya Maisha Yako milele.
◼️Ni Muhimu sana kuizingatia Injili ya KRISTO inapohubiriwa kwa njia yeyote maana Injili imebeba Wokovu.
5. Wokovu ni Sasa.
2 Wakorintho 6:2 (Kwa maana asema, Wakati uliokubalika nalikusikia, Siku ya wokovu nalikusaidia;tazama,wakati uliokubalika ndiyo sasa; tazama siku ya wokovu ni sasa)
◼️Hivyo Hakikisha Wokovu haukupiti kama hujaupokea na hakikisha hauwapiti watu wanaokuhusu.
2 Timotheo 2:10 "Kwa ajili ya hilo nastahimili mambo yote, kwa ajili ya wateule, ili wao nao waupate wokovu ule ulio katika KRISTO YESU, pamoja na utukufu wa milele."
6. Malaika huwahudumia Watu wanakaourithi Wokovu wa KRISTO.
Waebrania 1:14 "Je! Hao wote si roho watumikao, wakitumwa kuwahudumu wale watakaourithi wokovu?"
◼️Sio kila Mtu ana sifa ya kuhudumiwa na Malaika wa MUNGU ila Wateule wa KRISTO wote walioupokea Wokovu wake hao wana sifa za kuhudumiwa na Malaika wa MUNGU.
7. YESU KRISTO ndio Sababu ya Wokovu wetu na Ndiye Chanzo Cha Wokovu wetu.
Waebrania 5:9 "naye alipokwisha kukamilishwa, akawa sababu ya wokovu wa milele kwa watu wote wanaomtii;"
◼️ Hakikisha katika Maisha Yako inaambatana na sababu ya Wokovu wako ambaye ni YESU KRISTO.
◼️ Katika dini Yako au dhehebu lako Hakikisha unambatana na Chanzo Cha Wokovu wako, chanzo ni YESU peke kama Biblia inavyosema hapo juu.
✓✓Kuna watu wamefundishwa kuambatana na dini au dhehebu lao huku YESU KRISTO wamemwacha, hao wako nje na Wokovu wake.
✓✓Kuna watu wamefundishwa kuambatana na Kiongozi wao wa kiroho asiye YESU KRISTO, huyo Kiongozi atawapoteza hata wakose Wokovu.
◼️Ndugu ambatana na YESU KRISTO hata kama Kiongozi wako wa kiroho hataki maana ni YESU KRISTO tu ndiye mwenye uzima wako wa milele.
Zingatia na MUNGU atakubariki sana.
Mche MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi na utaitwa heri.
Kama pia unatumia Facebook ni follow maana itafika kipindi nitakuwa napost tu katika page yangu na profile yangu.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292.
Ubarikiwe sana

Comments