![]() |
| Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
Bwana YESU KRISTO atukuzwe.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU wa Mbinguni.
◾Je uko kwenye magumu sana?
Matendo 8:1 "Siku ile kukatukia adha kuu ya Kanisa lililokuwa katika Yerusalemu; wote wakatawanyika katika nchi ya Uyahudi na Samaria, isipokuwa hao mitume."
◾Ni jambo gani limeleta Dhiki kubwa kwako?
Warumi 12:12 kwa tumaini, mkifurahi; katika dhiki, mkisubiri; katika kusali, mkidumu;
◼️Nimekuandalia kanuni 7 muhimu za kukusaidia ukiwa kwenye Wakati mgumu.
1. Ukiwa kwenye magumu usiwe mtu wa manung'uniko.
1 Wakorintho 10:10 "Wala msinung'unike, kama wengine wao walivyonung'unika, wakaharibiwa na mharabu."
✓✓Kunung'unika ni dhambi.
2. Waheshimu na kuwasikiliza viongozi wako wa kiroho ambao MUNGU amekupa wakati huo, maana wakati mwingine hao wanaweza kubeba hatima njema ya kufanikiwa kwako.
Mfano hai ni hii.
A. Eliya alibeba hatima ya kufanikiwa kwa Mama wa sarepta aliyekuwa kwenye wakati mgumu.
(1 Wafalme 17:9-16) Utasoma yote ila nakuletea maandiko machache kutokea hapo.
1 Wafalme 17:12 "Naye akasema, Kama BWANA, Mungu wako, aishivyo, sina mkate, ila konzi ya unga katika pipa, na mafuta kidogo katika chupa; nami ninaokota kuni mbili ili niingie nijipikie nafsi yangu na mwanangu, tuule tukafe."
✓✓Ulikuwa Wakati wa njaa kali katika Taifa Wakati huu, Mama huyu Alikuwa katika Wakati mgumu sana na alijua kinachofuata ni kifo, lakini Eliya kama Kiongozi wa kiroho akatokea na kuwa msaada.
Na kwa kutamka Neno tu MUNGU alitenda Muujiza kwa familia ya mama yule na ule wakati mgumu ukaisha.
1 Wafalme 17:16" Lile pipa la unga halikupunguka, wala ile chupa ya mafuta haikuisha, sawasawa na neno la BWANA alilolinena kwa kinywa cha Eliya."
◼️Inawezekana na Wewe uko katika Wakati mgumu kiuchumi, Bwana YESU KRISTO anao Watumishi wake waaminifu ambao ukihusika nao wanaweza kukuombea katika Jina lake ukafanikiwa.
B. Elisha alibeba uponyaji wa Naamani(2 Wafalme 5:9-15)
2 Wafalme 5:1 "Basi Naamani, jemadari wa jeshi la mfalme wa Shamu, alikuwa mtu mkubwa mbele ya bwana wake, na mwenye kuheshimiwa, kwa sababu kwa mkono wake BWANA alikuwa amewapa Washami kushinda; tena alikuwa mtu hodari wa vita; lakini alikuwa mwenye ukoma."
✓✓Naamani alikuwa katika Wakati mgumu kwa sababu ya ugonjwa wa ukoma.
Lakini alimwendea Mtumishi wa MUNGU Elisha na MUNGU akamponya.
2 Wafalme 5:14 "Ndipo akashuka, akajichovya mara saba katika Yordani, sawasawa na neno lake yule mtu wa MUNGU; nayo nyama ya mwili wake ikarudi ikawa kama nyama ya mwili wa mtoto mchanga, akawa safi."
◼️ Inawezekana unapitia Wakati mgumu sana kwa ajili ya ugonjwa.
Ndugu Watumishi waaminifu wa Bwana YESU KRISTO wamebeba Majibu ya uponyaji Wako, waendee kawaeleze watakuombea utapona katika Jina la YESU KRISTO.
Haijalishi ni ugonjwa gani lakini YESU KRISTO anaweza kuhamisha ugonjwa huo utoke katika Mwili wako.
Kumbu 7:15 "Na BWANA atakuondolea ugonjwa wote; wala hatatia juu yako maradhi yo yote mabaya uyajuayo ya Misri, lakini atayaweka juu ya wote wakuchukiao."
C. Musa alibeba hatima ya Waisraeli(Kutoka 3:9-10)
Kutoka 3:9-10 " Basi, tazama, kilio cha wana wa Israeli kimenifikilia; tena nimeyaona hayo mateso ambayo Wamisri wanawatesa. Haya, basi, nitakutuma sasa kwa Farao, ili upate kuwatoa watu wangu, hao wana wa Israeli, katika Misri."
✓✓Waisraeli walikuwa kwenye wakati mgumu sana wa mateso ya Wamisri ila MUNGU akamleta Mtumishi wake Musa ili kuwatoa Waisraeli katika mateso na wakatoka.
◼️ Ingawa Waisraeli walikuwa kwenye wakati mgumu sana lakini katika Wakati huo mgumu MUNGU hakushughulika kwanza na wao Bali alishughulika na Musa maana MUNGU alikuwa amembebesha Musa Majibu ya Waisraeli.
◼️Unaweza ukawa katika mateso labda ya Ndoa, kazi, magonjwa n.k ukawa unaomba na kufunga, ila wakati huo MUNGU akawa anashughulika na Mtumishi wake mwaminifu aliyembebesha Majibu Yako, usipomdharau huyo Mtumishi bali ukajihusisha naye kwa Maombi au Sadaka au Ibada lazima utoke katika mateso maana huyo Mtumishi mwaminifu wa KRISTO ndio mwenye Majibu Yako.
D. Petro na Yohana walibeba uponyaji wa Kiwete aliyekuwa pembeni ya hekalu(Matendo 3:1-10)
Matendo 3:2 "Na mtu mmoja aliyekuwa kiwete toka tumboni mwa mamaye alichukuliwa na watu, ambaye walimweka kila siku katika mlango wa hekalu uitwao Mzuri, ili aombe sadaka kwa watu waingiao ndani ya hekalu."
✓✓Mtu huyu Alikuwa kwenye Wakati mgumu sana kwa ajili ya ukilema aliokuwa nao, maana alikuwa kilema asiyeweza kutembea.
◼️Kilema akatafuta namna ya kujiunganisha na Watumishi waaminifu wa Bwana YESU KRISTO na hiyo ikapelekea kupona kwake.
Matendo 3:6 "Lakini Petro akasema, Mimi sina fedha, wala dhahabu, lakini nilicho nacho ndicho nikupacho. Kwa jina la YESU KRISTO wa Nazareti, simama uende."
◼️Hata kwako inaweza kuwa hivyo hivyo tafuta namna ya kujiunganisha na Watumishi waaminifu wa Bwana YESU KRISTO utapona.
Matendo 3:9-10 " Watu wote wakamwona akienda, akimsifu MUNGU. Wakamtambua, ya kuwa yeye ndiye aliyekuwa akiketi na kuomba sadaka penye mlango Mzuri wa hekalu; wakajaa ushangao wakastaajabia mambo yale yaliyompata."
3. Tamka Neno la kinabii kulingana na hali tete uliyonayo.
◼️Mfano sema ''Sitakufa bali nitaishi, Nami nitayasimulia matendo ya BWANA.-Zaburi 118:17"
◼️Mfano mwingine '' BWANA ataniokoa na kila neno baya, na kunihifadhi hata nifike ufalme wake wa mbinguni. Utukufu una Yeye milele na milele. Amina. -2 Timotheo 4:18''
◼️Mfano mwingine '' Naamini ya kuwa nitauona wema wa BWANA Katika nchi ya walio hai.-Zaburi 27:13 ''
✓✓Mifano hai ni mingi sana ndani ya Biblia, jifunze sana kusoma sana Biblia na kutafakari maandiko maana wakati mwingine ROHO MTAKATIFU hutumia Neno la MUNGU lililoko ndani yako ili kkusaidia, hivyo kama huna Neno la MUNGU ndani yako ujue wakati mwingine hutaisikia sauti ya ROHO MTAKATIFU.
4, Tambua kwamba hakuna tatizo la kudumu.
1 Wakorintho 10:13 "Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila MUNGU ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili."
◼️Hivyo hata kwako tatizo lako halitakuwa la kudumu kama ukimtegemea MUNGU katika KRISTO YESU.
5. Fanyia kazi kila atakachosema MUNGU wakati wa magumu yako.
Ayubu 42:10 'Kisha BWANA akaugeuza uteka wa Ayubu, hapo alipowaombea rafiki zake; BWANA naye akampa Ayubu mara mbili kuliko hayo aliyokuwa nayo kwanza."
✓✓Ayubu alikuwa katika Wakati mgumu sana kwa sababu ya magonjwa yaliyompata ghafla, kufilisika ghafla, kufiwa na Watoto wake wote kumi Kwa siku Moja. Sidhani kama Kuna wakati mgumu kupita huu katika Maisha ya Mwanadamu lakini licha ya wakati huo mgumu MUNGU alisema na Rafiki zake Ayubu kwamba waende Ayubu awaombee, Baada tu ya Ayubu kuwaombea akafunguliwa kwanza yeye Kisha rafiki zake, ni kama MUNGU alitaka Ayubu afute maneno yake ya kujifunga aliyokuwa amejitamkia kabla, alipotii Neno la MUNGU la Maombi Biblia inasema MUNGU akambariki mara mbili zaidi kuliko alivyokuwa Mwanzo.
◼️ Hata wewe chukua hatua katika kile ambacho ROHO MTAKATIFU atasema na wewe wakati ukiwa katika magumu.
6. Mwamini MUNGU ataenda kufanya njia ya ushindi katika hali yako.
Isaya 26:3-4 "Utamlinda yeye ambaye moyo wake umekutegemea Katika amani kamilifu, kwa kuwa anakutumaini. Mtumainini BWANA siku zote Maana Bwana YEHOVA ni mwamba wa milele."
7. Hakikisha unaishi maisha matakatifu ya Wokovu wa KRISTO.
1 Petro 1:15 '' bali kama yeye(YESU) aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote; ''
◼️Kama magumu yako umesababisha wewe basi tubu sana.
◼️Kama unapata ushawishi wa kishetani ukiwa kwenye magumu kataa ushawishi huo.
✓✓Mche MUNGU na endelea mbele na Wokovu wa KRISTO ulio wa thamani sana.
◾Ushauri wangu ni huu "Usijilinganishe na watu ambao hawako katika magumu wakati huo.
Zingatia na MUNGU atakubariki sana.
Mche MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi na utaitwa heri.
Kama pia unatumia Facebook ni follow maana itafika kipindi nitakuwa napost tu katika page yangu na profile yangu.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292(Sadaka ya kuipeleka Injili, Ushauri, Whatsapp n.k)
Ubarikiwe sana.

Comments
Baada ya baba yangu mdogo kuniacha kwa miezi saba mirefu, nilikuwa nimevunjika moyo kabisa. Alinizuia kwenye mitandao yote ya kijamii, akaondoka, na hakukuwa na njia ya kumfikia. Karibu nikate tamaa, lakini ndani kabisa nilijua singeweza kupata mtu yeyote ambaye angenipenda na kunitendea jinsi alivyonitendea.
Siku moja, bosi wangu kazini aligundua jinsi nilivyokuwa na huzuni na akanitambulisha kwa Dkt. Dawn. Dkt. Dawn alisikiliza hadithi yangu na akaahidi kwamba mpenzi wangu angerudi kwangu ndani ya siku tatu. Kwa kweli, sikuamini mwanzoni—lakini kwa mshangao wangu mkubwa, siku ya tatu simu yangu iliita. Ilikuwa yeye! Alikuwa akilia na kuomba msamaha, akisema hataniacha tena.
Tangu siku hiyo, uhusiano wetu umekuwa na nguvu na uzuri zaidi kuliko hapo awali. Amekuwa akipenda na kunijali mimi na mtoto wetu, na sasa tunafunga ndoa katika miezi miwili tu! ❤️
Shukrani zote kwa Dkt. Dawn, ambaye kwa kweli alifanya jambo lisilowezekana liwezekane. Ninampendekeza kwa moyo wote kwa yeyote anayekabiliwa na changamoto katika:
Masuala ya uhusiano au ndoa
Ugonjwa au magonjwa
Matatizo ya utasa au bahati nasibu
Kesi za mahakamani au urejeshaji wa mali
Dkt. Dawn kweli hutatua matatizo kwa ufanisi na hurudisha furaha katika maisha ya watu.
Wasiliana na Dr. Dawn kwenye WhatsApp: +2349046229159
Barua pepe: dawnacuna314@gmail.com