![]() |
| Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
Bwana YESU KRISTO atukuzwe sana ndugu.
Karibu sana tujifunze Neno la MUNGU.
✓✓Uharibifu ni vifungo mbalimbali.
Shimo la uharibifu ni vifungo vya shetani vilivyomshikilia mtu, inawezekana ni wewe.
Zaburi 40:1-2 " Nalimngoja BWANA kwa saburi, Akaniinamia akakisikia kilio changu. Akanipandisha toka shimo la uharibifu, Toka udongo wa utelezi; Akaisimamisha miguu yangu mwambani, Akaziimarisha hatua zangu."
✓✓Ukihusika na MUNGU katika KRISTO YESU anaweza kukutoa ndani ya shimo la uharibifu na sasa ukawa huru bila kuteswa na vifungo vya giza.
✓✓MUNGU ana uwezo wa kukutoa katika mashimo ya uharibifu ulikowekwa na mawakala wa shetani, ilikowekwa ndoa yako au uchumba wako, ilikowekwa afya yako au uchumi wako au kibali chako.
✓✓MUNGU anaweza kukutoa katika vifungo vyote vya kiroho, Bwana YESU anaweza kukutoa katika magereza ya kichawi na anaweza kukutoa katika mashimo yote ya uharibifu.
Inawezakana uko sasa kiroho katika mashimo ya kipepo, magereza ya laana au uchawi n.k
Isaya 42:22 "Lakini watu hawa ni watu walioibiwa na kutekwa; wote wamenaswa katika mashimo, wamefichwa katika magereza; wamekuwa mawindo, wala hapana aokoaye; wamekuwa mateka, wala hapana asemaye, Rudisha."
Mimi sijui uko katika kifungo gani cha kipepo ila ninachojua ni kwamba MUNGU katika KRISTO YESU anaweza kukutoa katika kifungo hicho cha giza.
Je unataka MUNGU akutoe katika shimo la uharibifu ulikowekwa na mawakala wa shetani?
Fanya haya haraka sana.
1. Mpokee YESU KRISTO kama Mwokozi wako kisha tubu dhambi zako zote na kuziacha, tena tubu pia kwa kilichosababisha ukaingia katika shimo la uharibifu.
1 Yohana 1:8-9 " Tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo mwetu. Tukiziungama dhambi zetu, Yeye(MUNGU katika KRISTO YESU) ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote."
2. Baada ya kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako anza kuwa muombaji anayeomba kwa imani huku ukitumia mamlaka iliyo ndani ya YESU KRISTO ili utoke katika shimo la uharibifu.
Luka 10:19 "Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru."
Isaya 55:6-7 " Mtafuteni BWANA, maadamu anapatikana, Mwiteni, maadamu yu karibu; Mtu mbaya na aache njia yake, Na mtu asiye haki aache mawazo yake; Na amrudie BWANA, Naye atamrehemu; Na arejee kwa MUNGU wetu, Naye atamsamehe kabisa."
3. Fuata kanuni za MUNGU za baraka huku ukiishi maisha matakatifu ya Wokovu wa KRISTO.
Kumbukumbu la Torati 28:1-8 " Itakuwa utakaposikia sauti ya BWANA, Mungu wako, kwa bidii, kutunza kuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo leo, ndipo BWANA, Mungu wako, atakapokutukuza juu ya mataifa yote ya duniani; na baraka hizi zote zitakujilia na kukupata usikiapo sauti ya BWANA, Mungu wako. Utabarikiwa mjini, utabarikiwa na mashambani.
Utabarikiwa uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, na uzao wa wanyama wako wa mifugo, maongeo ya ng'ombe wako, na wadogo wa kondoo zako. Litabarikiwa kapu lako, na chombo chako cha kukandia unga. Utabarikiwa uingiapo, utabarikiwa na utokapo. BWANA atawafanya adui zako wainukao juu yako kupigwa mbele yako; watakutokea kwa njia moja, lakini watakimbia mbele yako kwa njia saba. BWANA ataiamuru baraka ije juu yako katika ghala zako, na mambo yote utakayotia mkono wako; naye atakubarikia katika nchi akupayo BWANA, Mungu wako."
Hiki ni kipengele muhimu sana ambacho hata baadhi ya watu waliookoka kimewashinda hivyo kujikuta uharibifu fulani unawafuata.
Ni lazima sana kuzifuata Kanuni za MUNGU za baraka.
Kanuni za MUNGU ni kama kuwa mwaminifu kutoa fungu la kumi na sadaka.
Kanuni za Kibiblia za ndoa au jinsi ya kupata mwezi n.k
Kufuata maelekezo yote anayakupa MUNGU ndio kufuata Kanuni zake za baraka.
4. Mwambie MUNGU apigane na waliokufunga.
Zaburi 35:1-3 " Ee BWANA, utete nao wanaoteta nami, Upigane nao wanaopigana nami. Uishike ngao na kigao, Usimame unisaidie. Uutoe na mkuki uwapinge wanaonifuatia, Uiambie nafsi yangu, Mimi ni wokovu wako."
5. Liamini Neno la MUNGU na ni ROHO MTAKATIFU hulituma kwako na litumie siku zote Neno hilo ili kupata ushindi.
Zaburi 107:20 "Hulituma neno lake, huwaponya, Huwatoa katika maangamizo yao."
6. Vunja kila patano lako na mawakala wa shetani, na sasa baki daima kwenye agano lako na YESU KRISTO Mwokozi.
1 Wakorintho 6:15 "Je! Hamjui ya kuwa miili yenu ni viungo vya KRISTO? Basi nivitwae viungo vya KRISTO na kuvifanya viungo vya kahaba? Hasha!"
7. Msikilize ROHO MTAKATIFU na mtii siku zote.
Yohana 14:26 "Lakini huyo Msaidizi, huyo ROHO MTAKATIFU, ambaye Baba(MUNGU) atampeleka kwa jina langu(YESU KRISTO), atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia."
Ndugu fuata kanuni hizo zote na utatoka kwenye kila vifungo vya giza.
Zingatia vipengele vyote ili utoke kwenye shimo la uharibifu.
MUNGU akubariki sana.
By Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292
Ubarikiwe

Comments