KAULI MBAYA KATIKA KUMZUIA MTU KUINGIA KATIKA NDOA

Na Mwl Peter Mabula 
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi 



Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe Ndugu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU wa Mbinguni.

◼️Kauli mbaya ni Moja ya vikwazo vinavyowazuia Wanaume au Wanawake wanaotaka wenzi wa kufunga nao Ndoa.

✓✓Binti au kijana kumbuka kwamba kauli mbaya zinaweza kukuponza hata ukakosa Mchumba sahihi, na kauli zako nzuri zinaweza kukupa Mchumba sahihi na ukaingia katika Ndoa safi.

◼️Hakikisha unakuwa na kauli nzuri na sio kauli mbaya, Neno la MUNGU linakushauri hivi hapa chini

Mithali 16:24 " Maneno yapendezayo ni kama sega la asali; Ni tamu nafsini, na afya mifupani."

✓✓Ni muhimu sana binti ukawa na lugha nzuri mbele za watu wote.

✓✓Unaweza kuwa na kauli mbaya mbele za majirani zako au wamama wa Kanisani kwetu na Mtu anayehitaji kufunga Ndoa na wewe atapitia kwa hao hao ili kuulizia tabia yako, atakutana na tabia yako mbaya ya kauli mbaya hivyo atadhani akikuoa basi siku moja unaweza hata kumjibu Mama yake mzazi kwa kauli mbaya hivyo anafuta mpango wa kukuoa wewe.

Mithali 11:16 "Mwanamke wa adabu huheshimiwa daima; ......"

✓✓Inakubidi uwe makini sana katika kauli maana ni kwa faida yako mwenyewe.

✓✓Wewe Kijana ambaye kwa siku lazima uongee matusi 20 na kuendelea chunga sana maana unaweza ukakosa Mke mwema.

Yakobo 3:13 "N'nani aliye na hekima na ufahamu kwenu? Na aonyeshe kazi zake kwa mwenendo wake mzuri, katika upole wa hekima."

✓✓Kwa mabinti hata kama atakujia Kijana anataka kukuoa na wewe hujampenda basi mkatalie na sio kumtukana na kumdhalilisha.

Biblia inasema kwamba maneno yapendezayo ni matamu kama Sega la asali.

✓✓Tena Biblia inasema "maneno yenu yawe na Neema "

Wakolosai 4:6 "Maneno yenu yawe na neema siku zote, yakikolea munyu, mpate kujua jinsi iwapasavyo kumjibu kila mtu."

Sasa kama wewe huwa unaongea maneno machungu yaani matusi na vitisho je maneno yako ni machungu kama nini?

✓✓Na kama maneno yako ni machungu ujue hakuna atakayetamani kuingia katika Ndoa na mtu wa maneno machungu.

◼️Baadhi ya mabinti hutoa kauli mbaya mbele za Wanaume wanaotaka kuwaoa kwa sababu tu mabinti hao wanataka tu kuolewa na matajiri.

✓✓Katika Kanisa Leo au katika jamii Leo mabinti wengi wanataka kufunga Ndoa na wanaume wenye hali nzuri kimaisha lakini wao hao mabinti wako katika hali mbaya kimaisha.

Wewe unayetaka tu kuolewa na Mwanaume mwenye hali nzuri jiulize, je hali yako na wewe ni nzuri?

Ukiwa tu na akili za kutaka kuolewa na mtu mwenye hali nzuri tambua kwamba wapo Wanawake wengi wenye akili kama zako waliangukia pua na sasa wanateseka maana waliwapata wenye pesa au wasomi na hao hao wenye hali nzuri ndio waliwatesa hao wanawake baada ya kuingia katika ndoa.

◼️Ndugu, Mume mwema au Mke mwema hatokani na utajiri bali hutoka kwa MUNGU.

✓✓Sasa kama kwa kauli unawadharau wanaokuijia wakiwa masikini basi unaweza hata kupishana na kusudi la MUNGU.

1 Petro 3:2 "wakiutazama mwenendo wenu safi, na wa hofu."

Nataka upate Mwenzi bora na nataka ufunge ndoa takatifu Kanisani yenye ushuhuda mzuri ndio maana nakufundisha haya.

◼️Kama ulikuwa na tabia mbaya kwa kauli zako mbaya Acha kuanzia Leo.

Waefeso 4:22-24 " mvue kwa habari ya mwenendo wa kwanza utu wa zamani, unaoharibika kwa kuzifuata tamaa zenye kudanganya; na mfanywe wapya katika roho ya nia zenu; mkavae utu mpya, ulioumbwa kwa namna ya Mungu katika haki na utakatifu wa kweli."
Zingatia  na MUNGU atakubariki sana.
Mche MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi na utaitwa heri.
Kama pia unatumia Facebook ni follow maana itafika kipindi nitakuwa napost tu katika page yangu na profile yangu.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter  Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292.
Ubarikiwe sana

Comments