KWA JINSI GANI MAWAKALA WA SHETANI WATAPIGANA NA WEWE BILA KUKUSHINDA.

Na Mwl Peter Mabula 
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi 


Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe Ndugu yangu.
Karibu sana tujifunze Neno la MUNGU wa Mbinguni 

✓✓Kwa jinsi gani mawakala wa shetani watapigana na wewe bila kukushinda?

Yeremia 1:19 "Nao watapigana nawe; lakini hawatakushinda; maana mimi nipo pamoja nawe, asema BWANA, ili nikuokoe."

Mimi Peter Mabula natamani Wewe rafiki yangu unayesoma masomo yangu uwe mshindi daima dhidi ya Wachawi, wakuu wa giza, mapepo, na Kila Nguvu za giza, kazi yangu ni kukuletea Kanuni za ki MUNGU za kukufanya kuwa mshindi ukizifuata kwa ukamilifu.

◼️Sasa kwa jinsi gani mawakala wa shetani watapigana na wewe bila kukushinda?

Zingatia mambo haya 7 kama unataka kupigana na Mawakala wa Shetani bila wao kukushinda Wewe.
Utakuwa mshindi daima katika Jina la YESU KRISTO.

1. Mawakala wa shetani watapigana na wewe bila kukushinda kama una imani thabiti ya Wokovu katika KRISTO YESU Mwokozi.

1 Wakorintho 16:13 " Kesheni, simameni imara katika Imani, fanyeni kiume, mkawe hodari."

2. Mawakala wa shetani watapigana na wewe bila kukushinda kama tu MUNGU Baba wa Mbinguni yuko pamoja na wewe.

Isaya 41:10-13 " usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni MUNGU wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu. Tazama, wote walioona hasira juu yako watatahayarika na kufadhaika; watu washindanao nawe watakuwa si kitu, na kuangamia.Utawatafuta wala hutawaona wale wapiganao nawe; watakuwa si kitu; watakuwa kama kitu kisichokuwa, wale waliofanya vita juu yako. Kwa maana mimi, BWANA, Mungu wako, nitakushika mkono wako wa kuume, nikikuambia, Usiogope; mimi nitakusaidia."

3. Mawakala wa shetani watapigana na wewe bila kukushinda kama wewe una ROHO MTAKATIFU na unamsikiliza na kumtii.

1 Yohana 4:4 " Ninyi, watoto wadogo, mwatokana na MUNGU nanyi mmewashinda, kwa sababu yeye aliye ndani yenu(ROHO MTAKATIFU) ni mkuu kuliko yeye aliye katika dunia."

4. Mawakala wa shetani watapigana na wewe bila kukushinda kama tu wewe unalitii na kulifanyia kazi Neno la MUNGU.

Kumbu 28:1,7 " Itakuwa utakaposikia sauti ya BWANA, Mungu wako, kwa bidii, kutunza kuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo leo, ndipo BWANA, Mungu wako, atakapokutukuza juu ya mataifa yote ya duniani; ........ BWANA atawafanya adui zako wainukao juu yako kupigwa mbele yako; watakutokea kwa njia moja, lakini watakimbia mbele yako kwa njia saba."

5. Mawakala wa shetani watapigana na wewe bila kukushinda kama utakuwa Mtu wa maombi.

Mathayo 7:7-8 " Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa; kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa."

6. Mawakala wa shetani watapigana na wewe bila kukushinda kama wewe umejengwa juu ya msingi wa Neno la MUNGU na maombi

Waefeso 2:20 "Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye KRISTO YESU mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni."

✓✓Kujengwa juu ya msingi wa mitume na manabii maana yake tumejengwa juu ya Neno la MUNGU waliofundisha mitume na manabii ndani ya Biblia.

✓✓Msingi wa mitume na manabii ni Neno la KRISTO ambalo hilo hutujenga hata tunakuwa jengo imara ambalo haliwezi kutikiswa na kazi za shetani.

✓✓Mawakala wa shetani watapigana na wewe bila kukushinda kama wewe umejengwa juu ya msingi wa Neno la MUNGU na maombi.

7. Mawakala wa shetani watapigana na wewe bila kukushinda kama Umeokolewa na Bwana YESU KRISTO na umejitenga mbali na dhambi zote.

Isaya 59:1-2 " Tazama, mkono wa BWANA haukupunguka, hata usiweze kuokoa wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia; lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na MUNGU wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia."

✓✓Kujitenga mbali na maovu ni kukaribisha ushindi wa MUNGU kwako.

◼️Kuishi maisha matakatifu na maombi ni njia kuu ya kumshinda shetani na mawakala zake wote.

1 Petro 1:15 "bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote;"
Zingatia  na MUNGU atakubariki sana.
Mche MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi na utaitwa heri.
Kama pia unatumia Facebook ni follow maana itafika kipindi nitakuwa napost tu katika page yangu na profile yangu.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter  Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292.
Ubarikiwe sana.

Comments