Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu zangu wote.
Karibuni sana tujifunze Neno la MUNGU la uzima wetu.
◾Tuko katika siku za mwisho ambapo Biblia inasema mambo kadhaa kuhusu hizi ziku za Mwisho, baadhi tu ya mambo hayo ni;
a. Maarifa kuongezeka na baadhi ya maarifa hayo yatawapotosha baadhi ya wanadamu
Danieli 12:4 '' ........hata wakati wa mwisho; wengi wataenda mbio huko na huko, na maarifa yataongezeka. ''
b. Watumishi wengi wa uongo nao watakuwepo wengi ili kudanganya wengi
Mathayo 24:11 '' Na manabii wengi wa uongo watatokea, na kudanganya wengi. ''
c. Mafundisho ya mashetani nayo yatakuwepo mengi tu
1 Timotheo 4:1 ''Basi ROHO anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani; ''
d. shetani atakuwa anatafuta nafasi ya kuabudiwa.
2 Thesalonike 2:4 ''yule mpingamizi(shetani), ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu ama kuabudiwa; hata yeye mwenyewe kuketi katika hekalu la MUNGU, akijionyesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu.''
e. Watu wengi watajitenga na imani ya Wokovu wa YESU KRISTO.
1 Timotheo 4:1 ''Basi ROHO anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani ..........''
f. Wapinga Kristo watakuwepo
1 Yohana 2:18 ''Watoto, ni wakati wa mwisho; na kama vile mlivyosikia kwamba mpinga Kristo yuaja, hata sasa wapinga Kristo wengi wamekwisha kuwapo. Kwa sababu hiyo twajua ya kuwa ni wakati wa mwisho. ''
g. Waabudu sanamu watakuwepo.
1 Kor 5:10 '' Sisemi msichangamane kabisa na wazinzi wa dunia hii, au na wenye kutamani, au na wanyang'anyi, au na wenye kuabudu sanamu; maana hapo ingewalazimu kutoka katika dunia. ''
h. Watumishi wanaoongozwa na mapepo watakuwepo, mapepo ni roho zidanganyazo.
1 Timotheo 4:1 ''Basi ROHO anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo ...........''
Nimekujulisha kwa ufupi mambo nane(8) tu ambayo yataambatana na siku za mwisho japokuwa yapo zaidi ya nane.
◼️Japokuwa katika nyakati hizi kutakuwa na watumishi wa uongo lakini hata watumishi wa kweli wa MUNGU katika KRISTO YESU nao watakuwepo wengi lakini wakati mwingine kuwajua inahitaji ufunuo wa MUNGU, ndio maana unamhitaji sana ROHO MTAKATIFU.
◼️Ashukuriwe MUNGU katika KRISTO YESU maana tangu mapema sana MUNGU alijua haya ya siku za mwisho ndio maana akatupa neema yake kwa ROHO wake kuja kwetu.
◼️Ni mapema kabisa MUNGU alisema kwamba atamleta ROHO MTAKATIFU kwa wateule wa KRISTO ili tu atusaidie kujitenga na kila mambo ya kishetani ambayo ni mengi sana.
◼️MUNGU alisema zamani kuhusu ROHO MTAKATIFU kwamba ''Hata itakuwa, baada ya hayo, ya kwamba nitamimina roho yangu juu ya wote wenye mwili; na wana wenu, waume kwa wake, watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono; -Yoeli 2:28''
◼️Nguvu za ROHO MTAKATIFU sasa zimeshamiminwa kwa wateule wa KRISTO wote ili tushinde maana bila ROHO MTAKATIFU Kanisa haliwezi kuwa Kanisa la MUNGU aliye hai.
◼️Tuko sasa katika wakati wa siku za mwisho na wakati huu pia Kibiblia unaitwa wakati wa ROHO MTAKATIFU kwa Kanisa hai la MUNGU.
◾Katika wakati huu wa mwisho ujanja ni mwingi mno, uongo ni mwingi mno,utapeli wa kiroho ni mwingi mno na ushawishi wa kipepo ni mwingi mno hivyo hakika wakati huu washindi kiroho ni wale tu walio na ROHO MATAKATIFU na wamekubali kuongozwa na yeye.
Warumi 8:14 '' Kwa kuwa wote wanaoongozwa na ROHO wa MUNGU, hao ndio wana wa MUNGU.''
✓✓Katika nyakati hizi za mwisho ni ROHO MTAKATIFU pekee ndiye Mwalimu wa kweli wa Kanisa la kweli la YESU KRISTO, na yeye ROHO wa MUNGU anawatumia watumishi wa MUNGU waaminifu.
◾Kama wewe uliye Kanisa lakini humtaki ROHO MTAKATIFU ujue wewe sasa ni kanisa hewa na ni mtu wa mataifa maana watu wa mataifa ndio huchukuliwa kufuata sanamu(shetani) kama wanavyojiongoza wenyewe maana hawana ROHO MTAKATIFU.
1 Kor 12:2-3 '' Mwajua ya kuwa mlipokuwa watu wa Mataifa, mlichukuliwa kufuata sanamu zisizonena, kama mlivyoongozwa. Kwa hiyo nawaarifu, ya kwamba hakuna mtu anenaye katika ROHO wa MUNGU, kusema, YESU amelaaniwa; wala hawezi mtu kusema, YESU ni Bwana, isipokuwa katika ROHO MTAKATIFU.''
Mambo ya kujua kuhusu ROHO MTAKATIFU kwetu.
1. Kama unauhitaji uzima wa milele basi mhitaji sana pia ROHO MTAKATIFU maana ni yeye tu ndiye anayeweza kumfunua YESU KRISTO Mwokozi kwetu na MUNGU Baba Mwenyezi.
✓✓Hakika wewe uliye kanisa unamhitaji sana ROHO MTAKATIFU maana ni katika YESU KRISTO tu na kwa njia ya ROHO MTAKATIFU ndipo tunaweza kumkaribia MUNGU.
Waefeso 2:18 '' Kwa maana kwa yeye(YESU) sisi sote tumepata njia ya kumkaribia Baba(MUNGU) katika ROHO mmoja. ''
2. Tunapookolewa na YESU KRISTO tunatiwa muhuri na ROHO MTAKATIFU ili tuwe wa MUNGU.
Waefeso 1:13-14 ''Nanyi pia katika huyo mmekwisha kulisikia neno la kweli, habari njema za wokovu wenu; tena mmekwisha kumwamini yeye, na kutiwa muhuri na ROHO yule wa ahadi aliye Mtakatifu. Ndiye aliye arabuni ya urithi wetu, ili kuleta ukombozi wa milki yake, kuwa sifa ya utukufu wake.''
✓✓Ni jukumu letu tu kama Kanisa hai la MUNGU kuhakikisha tunaongozwa na ROHO MTAKATIFU na kukubaliana na ushauri wake kwetu maana ndio katika yeye tulitiwa muhuri hadi siku ya kuja kwa Bwana YESU mara ya pili.
Waefeso 4:30 ''Wala msimhuzunishe yule ROHO MTAKATIFU wa MUNGU; ambaye kwa yeye mlitiwa muhuri hata siku ya ukombozi.''
3. MUNGU anaishi ndani yetu kwa njia ya ROHO MTAKATIFU.
Waefeso 2:22 '' Katika yeye(YESU) ninyi nanyi mnajengwa pamoja kuwa maskani ya MUNGU katika ROHO.''
✓✓Hivyo unapompinga ROHO MTAKATIFU ujue umempinga MUNGU aliyeumba mbingu na nchi.
✓✓Unapompinga ROHO MTAKATIFU ujue unampinga Bwana YESU Mwokozi pekee kwa wanadamu.
◼️Uzuri ni kwamba ROHO MTAKATIFU hajipingi na Neno lake hivyo kama kuna watumishi wanaenda kinyume na Biblia na kudai ni ROHO MTAKATIFU amewajulisha ujue hao sio watumishi wa MUNGU na hawana ROHO MTAKATIFU hata kama wanaigiza kunena kwa lugha.
✓✓Watumishi wanaolipotoa Neno la MUNGU hiyo ndio njia yetu ya kuwajua hao kwamba sio watumishi wa MUNGU na ROHO MTAKATIFU hayuko kwao.
4. Ni ROHO MTAKATIFU tu katika KRISTO YESU kwa njia ya injili ya Wokovu hufunua siri zote.
Waefeso 3:4-5 '' Kwa hayo, myasomapo, mtaweza kuutambua ufahamu wangu katika siri yake KRISTO. Siri hiyo hawakujulishwa wanadamu katika vizazi vingine; kama walivyofunuliwa mitume wake watakatifu na manabii zamani hizi katika ROHO;''
◼️Siri za kweli zote hufunuliwa na ROHO MTAKATIFU tu, hivyo kama unataka kujua mambo mengi ya MUNGU basi unamhitaji ROHO MTAKATIFU sana.
✓✓Katika maandiko hapo tu tunajifunza kwamba Waisraeli hawakujua kama Wokovu wa KRISTO utawahusu watu wote kutoka mataifa yote waliomtii KRISTO, Lakini ROHO MTAKATIFU ndiyo alifunua siri hii ambayo kwa muda mrefu haikujulikana.
◼️Nampenda sana ROHO MTAKATIFU maana hufunua mafumbo yote.
1 Kor 2:10 '' Lakini MUNGU ametufunulia sisi kwa ROHO. Maana ROHO huchunguza yote, hata mafumbo ya MUNGU.''
◼️Ndugu, kwa sababu hizo 4 tu je huoni kwamba unamhitaji sana sana ROHO MTAKATIFU?
Ziko sababu nyingi sana za kuonyesha unamhitaji sana ROHO MTAKATIFU.
✓✓Leo wako watu wamedanganywa na nguvu za giza kwa sababu tu hawana ROHO MTAKATIFU wa kuwafunulia kweli pekee ya MUNGU iliyo katika KRISTO pekee.
✓✓Katika ziku hizi za mwisho vikao vya kipepo ili kujadili jinsi ya kuwakosesha mbingu wateule vipo vingi sana, ndugu unamhitaji sana ROHO MTAKATIFU na Neno la KRISTO ili ushinde.
✓✓MUNGU alijua roho ya mpinga Kristo itafanya kazi katika siku hizi hivyo ili kutusaidia akatuletea ROHO MTAKATIFU ili tumshinde shetani na mawakala zake wote siku zote.
◼️ROHO MTAKATIFU ukiwa naye atakukumbusha nini kikupasacho kutenda
Yohana 14:26 "Lakini huyo Msaidizi, huyo ROHO MTAKATIFU, ambaye Baba(MUNGU) atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia. "
◼️ROHO MTAKATIFU ukiwa naye atakufundisha na atakuwa na wewe ili usinaswe na shetani
◼️ROHO MTAKATIFU ukiwa naye atakufundisha na atakuwa na wewe ili usinaswe na shetani
Zaburi32:8, "Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea; Nitakushauri, jicho langu likikutazama."
✓✓Ni muhimu sana kumhitaji ROHO MTAKATIFU.
✓✓Ni muhimu sana kumhitaji ROHO MTAKATIFU.
◼️Kama hujampokea YESU KRISTO kwanza mpokee YESU KRISTO kama Mwokozi wako, na kama ulishampokea YESU KRISTO anza kujifunza mafundisho ya Neno la MUNGU kuhusu ROHO MTAKATIFU kazi zake kwetu na kisha kwa maombi na maombezi fanya juhudi za kimaombi ili ujazwe nguvu za ROHO MTAKATIFU, maana ROHO MTAKATIFU ni kwa ajili yako Kanisa.
✓✓Watu wengi na watumishi wengi wasio na ROHO MTAKATIFU basi wana roho zidanganyazo ambazo ni roho za kuzimu.
◼️Ndugu mhitaji sana sana ROHO MTAKATIFU kama unataka kuwa Mkristo unayeishi maisha ya ushindi dhidi ya dhambi na dhidi ya nguvu za giza.
Zingatia na MUNGU atakubariki sana.
Mche MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi na utaitwa heri.
Kama pia unatumia Facebook ni follow maana itafika kipindi nitakuwa napost tu katika page yangu na profile yangu.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292.
Ubarikiwe sana.
Comments