MAMBO MUHIMU YA KIJANA KUZINGATIA ANAPOIENDEA NDOA TAKATIFU.

Na Mwl Peter Mabula 
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi 


Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe Ndugu zangu wote.
Karibuni tujifunze Neno la MUNGU wa Mbinguni.

◼️Maisha ya Mwanadamu yana phases Nne(4).

Ayubu 14:1-2 " Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke Siku zake za kuishi si nyingi, naye hujaa taabu. Yeye huchanua kama vile ua, kisha hukatwa; Hukimbia kama kivuli, wala hakai kamwe."

✓✓Phase ya Kwanza ni Wakati wa Utoto.
Hiki ni kipindi Cha kuzaliwa hadi pale Utoto unaisha unaingia Ujana.

✓✓Phase ya pili ni Wakati wa Ujana

Huu Kwa mujibu wangu kwenye andiko ni wakati wa KUCHANUA.

✓✓Phase ya tatu ni wakati wa Utu Uzima.
Huu ni wakati wa kuchanua ila haufai sana kwa baadhi ya mambo.
Mfano Mtu mzima Mwanaume mwenye Miaka 45 na kuendelea akioa Kisha azae Watoto 4 Mtoto wa mwisho atamzaa akiwa na zaidi ya Miaka 50, Mtoto hadi anamaliza chuo ama Baba hayupo au Baba ni Mkongwe Mwenye umri zaidi ya 70, yaani wakati huo Mtoto anahitaji msaada na Baba anahitaji msaada kwa sababu ya Uzee.

Mtu mzima Mwanamke wa miaka 45 akitaka kuingia katika Ndoa na akataka kuzaa Watoto 4 ni vigumu sana sana.

◼️Hivyo Wakati wa Kuchanua katika Utu Uzima ni tofauti na wakati wa kuchanua wakati wa Ujana.

✓✓Phase ya nne ni Uzee.
Hapa Biblia Iko wazi sana kwamba katika phase hii ya Maisha kinachofuata ni "hukatwa; Hukimbia kama kivuli, wala hakai kamwe."

Tunafahamu mambo ambayo hufanyika wakati wa Utoto, wakati wa Ujana, wakati wa Utu Uzima na Wakati wa Uzee.

✓✓Katika Wakati wa Ujana yapo mengi yanayapaswa kufanyika mfano Elimu na kuanza kujitegemea lakini Muhimu kuliko yote ni Ndoa.
Ndio maana kauli za "Kosea yote usikosee Kuoa au Kuolewa" huwa zinachukua nafasi wakati huu wa Ujana.

◼️Sasa kwa habari ya Ndoa, Kuna mambo mengi ya kujifunza.

◼️Nini Kijana wa Kike au wa Kiume afanye anapoiendea Ndoa Takatifu?

✓✓Yapo mambo mengi sana ya kufanya, Mimi nimekuandalia baadhi tu ili yakusaidie.

1. Mtumikie Bwana YESU KRISTO kwa bidii.

Kumtumikia Bwana YESU kunaleta neema kuu sana juu yako.

Kumtumikia MUNGU kunaleta heshima, ulinzi na baraka.

1 Wakorintho 15:58 "Basi, ndugu zangu wapendwa, mwimarike, msitikisike, mkazidi sana kutenda kazi ya BWANA sikuzote, kwa kuwa mwajua ya kwamba taabu yenu siyo bure katika BWANA."

2. Kubali kuelekezwa kuelekezwa na waliokutangulia.

Esta 2:20 "Esta alikuwa hajadhihirisha jamaa yake wala kabila yake, kama vile Mordekai alivyomwagiza; kwa maana Esta alikuwa akiyashika maagizo ya Mordekai, vile vile kama wakati alipolelewa naye."

✓✓Esta alikuwa ni Binti aliyetakiwa kuolewa, Esta alikuwa anayashika maagizo ya Mordekai na ndio maana katika kundi la mabinti waliotakiwa kuolewa alishinda na kuolewa na mfalme huku mabinti wengine wakiachwa .

Nini nataka niseme? 

Elekezwa katika utakatifu na elewa.

 Kubali kuelekezwa kiroho ndipo utajua hekima na busara.

3. Uwe Mtu unayejituma.

1 Petro 3:13 " Naye ni nani atakayewadhuru, mkiwa wenye juhudi katika mema?"

Jitume katika mambo mema. 

Usiwe mzembe wala mlegevu.

4. Heshimu Ndoa za wengine.

Waebrania 13:4" Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi MUNGU atawahukumia adhabu."

Kama kweli unataka kuwa na Ndoa njema basi kumbuka wewe kuziheshimu Ndoa za wengine ambao wapo tayari katika Ndoa.

Wanadamu wote Neno la MUNGU linawataka kuziheshimu Ndoa za wengine, hakuna anayeweza kukwepa, hivyo hata mafanikio mazuri ya Ndoa yako mwenyewe wakati mwingine yanaweza pia kuja kutokana na wewe kuheshimu Ndoa za wengine.

◼️Usikubali uhusiano wa kimapenzi na Mke wa Mtu au Mume wa mtu.

◼️Usikubali kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Binti yeyote maana huyo atakuja kuwa Mke wa Mtu.

◼️Usikubali kuwa na uhusiano na Kijana yeyote maana huyo atakuja kuwa Mume wa Mtu.

◼️Usikubali kuwa katika uhusiano wa kimapenzi na mtu yeyote hata kama ni mchumba wako maana huo ni uasherati na waasherati mwisho ni jehanamu.

Waefeso 5:5 ''Maana neno hili mnalijua hakika, ya kwamba hakuna mwasherati wala mchafu wala mwenye tamaa, ndiye mwabudu sanamu, aliye na urithi katika ufalme wa KRISTO na MUNGU.''

✓✓Usikubali kamwe kuwa mwasherati.


5. Uwe na upendo wa ki MUNGU.

Warumi 12:9 " Pendo na lisiwe na unafiki lichukieni lililo ovu, mkiambatana na lililo jema."

✓✓Upendo wa ki MUNGU ni upendo usio na hila.

✓✓Upendo wa ki MUNGU ni Upendo usio na dhambi ndani yake.

◼️Kama kweli unaitazamia Ndoa njema basi ambatana na Upendo wa ki MUNGU.

6. Heshimu wazazi wako.

Waefeso 6:1-3 " Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika BWANA, maana hii ndiyo haki. Waheshimu baba yako na mama yako; amri hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi, Upate heri, ukae siku nyingi katika dunia."

✓✓Vijana wengi wanaishia katika Ndoa mbaya kwa sababu ya kukosa heshima mbele za wazazi.

✓✓Unao wazazi wa aina mbili. Una wazazi wa kukuzaa kimwili na una wazazi wa kukuzaa kiroho yaani wazazi wa kiroho.

◼️Una wajibu wa kuwaheshimu kama unahitaji kuingia katika ndoa safi na ya furaha na amani.

✓✓Kuna baraka za MUNGU katika kuwaheshimu wazazi, hivyo wewe Kijana au Binti unayetarajia ndoa takatifu basi zingatia kuwaheshimu wazazi wako.

◾Kwanini nimesema unatakiwa kuwaheshimu wazazi wako?

✓✓Ni kwa sababu wakati wa ujana ndipo binadamu wengi huwa na  kiburi.

Ndugu zingatia sana Kanuni hii kama unatarajia Ndoa Takatifu iliyo safi.

◼️Kumbuka ni agizo la MUNGU kwamba kuishi miaka mingi yenye heri kunaweza pia kutokana na kuwatii wazazi wako.

✓✓ Ndugu wakumbuke wazazi wako wa kimwili yaani waliokuzaa na wakumbuke wazazi wako wa kiroho yaani waliokufundisha Neno la MUNGU, ukaokoka na wakakulea kiroho hata sasa uko imara katika imani ya Wokovu wa KRISTO YESU Mwokozi.

7. Zitambue nyakati za Kuoa au Kuolewa.

Mhubiri 3:1 "Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu."

✓✓Vijana wengi hawaujui wakati sahihi ya kufunga ndoa.

Kila jambo lina majira yake.

◼️Majira mengine yakipita inaweza kuwa ngumu kupata baadhi ya baraka kwenye majira yanayofuata.

Mfano unaweza ukakuta Mwanamke ana miaka 40 na hataki kuolewa, akisema muda bado, sasa akiolewa akiwa na miaka 42 kisha uzao ukasumbua miaka 5 je ataweza kubeba mimba akiwa na miaka 48?
Hapo inahitajika Neema tu ya MUNGU maana ukomo wa kuzaa kidaktari ni miaka 45.

 Hivyo wanaoweza kuzaa wakiwa na miaka zaidi ya hiyo ni wale tu ambao MUNGU amewapa Neema hiyo.

 Sasa kama majira ya kuoa au kuolewa yakikupita unaweza kujikuta kuna baadhi ya baraka unakosa baadae.

✓✓Kama kwa kila jambo kuna majira yake hivyo ni muhimu kujua kwamba majira yakipita unaweza kujikuta katika ugumu sana pale utakapoanza kufanya mipango ya majira yaliyopita zamani.

◼️Ndugu, utambue wakati wako wa kuoa au kuolewa na utumie kwa utakatifu na kusudi la MUNGU ili uingie katika ndoa.

8. Omba Maombi kwa MUNGU ili akusaidie.

Mathayo 7:7 " Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa;"

◼️Kama kuna kitu muhimu unakihitaji katika kuiendea Ndoa Takatifu basi ni msaada wa MUNGU kwako, na msaada wa MUNGU unapatikana kwa maombi, Biblia inasema ombeni nanyi mtapewa.
Usipojua kumtafuta MUNGU kwa maombi katika kipindi hili unaweza kusumbuka sana.

✓✓Hata kama unajiona umejitosheleza lakini ukweli ni kwamba hakuna kijana aliyejitosheleza hata mmoja bali MUNGU ndio pekee anayeweza kukutosheleza.

◼️Kumbuka unamhitaji Mke au Mume kutoka kwa MUNGU ndio huyo atakuwa Mke mwema au Mume mwema.

Kumbuka unahitaji kibali na Neema ndipo utakubaliwa na Mchumba, tena unahitaji kuwa na kibali na Neema ndipo ukubalike ukweni na kwa Kanisa la MUNGU, kibali na Neema hupatikana kwa maombi, hivyo lazima uwe muombaji.

✓✓Kumbuka inahitajika mahari ili uoe au uolewe, kunahitajika afya njema ili uweze kufunga ndoa, kunahitajika watu kukusaidia ndipo utafunga Ndoa, hata kama una pesa nyingi lakini unahitaji Wachungaji, waimbaji, wapiga vigelegele, wenye hoteli, madereva, wahudhuliaji n.k, hao wote kuwapata unahitaji kuomba Maombi mbele za MUNGU.

◼️Maombi ni jambo la lazima kwa Mkristo anayetarajia kuingia katika Ndoa Takatifu.

9. Jielewa kwamba wewe ni mtu wa thamani na tembea kwenye uthamani.

◼️Waliookolewa na YESU KRISTO ni watu wa thamani sana hivyo hakikisha unakuwa wa thamani.

1 Wakorintho 6:20 "maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni MUNGU katika miili yenu."

✓✓Mtu wa thamani hawezi kamwe kuwa mzinzi au mwasherati.

✓✓Biblia inasema tumenunuliwa na MUNGU kwa damu ya YESU KRISTO, na hiyo damu ya YESU KRISTO imetufanya kuwa wa thamani sana, hivyo inatupasa kumtukuza MUNGU hata katika miili yetu yaani tujitenge na dhambi zote ambazo huuchafua mwili na roho.

✓✓Ni muhimu sana binti au kijana ujitambue kwamba wewe ni wa thamani.

✓✓Kumbuka kwamba usipojitambua wewe kwamba ni wa thamani ujue kwamba hakuna atakayekuona wa thamani.

Narudia tena "Usipojitambua kwamba wewe ni wa thamani hakuna mwanadamu atakayekuona wewe kuwa wa thamani"

Nyongeza za mambo ya kufanya unapoiendea ndoa takatifu ni pamoja na 

 shughulikia matatizo yako kama yapo.

Yaani elewana na watu, kubali kurekebishwa.

. Jenga mazingira ya kupata mwenzi.

✓✓Kama ni kijana jitegemee na sio kuishi kwa wazazi.

Mwenye sikio la kusikia naamini amesikia na kuelewa na atazingatia.
Zingatia  na MUNGU atakubariki sana.
Mche MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi na utaitwa heri.
Kama pia unatumia Facebook ni follow maana itafika kipindi nitakuwa napost tu katika page yangu na profile yangu.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter  Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292.
Ubarikiwe sana

Comments