![]() |
| Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu zangu wote.
Karibu sana tujifunze Neno la MUNGU la uzima.
✓✓Mimi naamini wewe ni muombaji na unamtarajia MUNGU siku zote kupitia maombi yako, ni sawa kabisa lakini leo nataka nizungumzie maombi ya mwana maombi makini na shujaa.
Biblia inasema '' Ombeni, nanyi mtapewa;....... -Mathayo 7:7'' ila haigizi kila mtu kuomba tu atakavyo bali aombe sawasawa na kanuni ya MUNGU inayoleta majibu ya maombi.
Leo wapo baadhi ya watu hufanya maombi sana lakini sio maombi yaliyo katika mpango wa MUNGU unaomfanya MUNGU ajibu maombi yao.
Kuna watu hadi husema kwamba MUNGU anajibu maombi hata ya mwizi anapoenda kuua, kwamba MUNGU anajibu hata maombi ya kahaba anayeomba ili apate mtu wa kuzini naye, wapo watu hata husema kwamba hata jambazi anapoenda kuua huomba MUNGU ili amfanikishe kuua, watu wote wanaodhani iko hivyo hawamjui MUNGU na njia zake za kujibu maombi.
✓✓Kwa kusoma kwangu Biblia kuanzia Kitabu cha Mwanzo hadi kitabu cha Ufunuo MUNGU hujibu ombi moja tu la Mtu mwenye dhambi, MUNGU katika KRISTO YESU husikia na kujibu maombi ya mtu mwovu anapotubu tu huku moyoni mwake akiachana na ubaya ambayo alikuwa anautenda, hivyo hata mwizi akitubu na kuacha wizi basi MUNGU katika KRISTO YESU anamsamehe.
Sio kudanganyana kwamba hata mtu anapoenda kufanya dhambi akimuomba MUNGU amfanikishe kutenda dhambi eti MUNGU anafanya hivyo, sio kweli milele.
Wengine hufanya dhambi na inakuwa ni salama kwa muda kwa sababu tu ya neema ya MUNGU iliyopo sasa na sio kwa sababu MUNGU amejibu maombi ya mtu huyo, neema ikikoma ndio utasikia mwizi amechomwa moto alipokuwa anaiba, mara utasikia jambazi kauliwa na polisi alipojaribu kupiga risasi. Mara fulani kavunjwa mkono alipokamatwa akizini na mume/mke wa mtu.
Hivyo kama wewe ni mwovu na huwa unaomba MUNGU akulinde katika uovu wako na kwa imani unadhani MUNGU hukujibu kwa sababu hujapata madhara tambua kwamba MUNGU hajawahi kujibu maombi yako, ipo siku unaweza kufa huku unajiona hivyo tubu na acha dhambi hiyo.
Wako watu pia hudhani kwamba MUNGU anajibu maombi yao wakati wamejitenga na Wokovu wa MUNGU ulio katika KRISTO YESU, jibu sio kweli.
Ok, inawezekana wewe ni muombaji mzuri lakini hupati matokeo ya maombi yako kutoka kwa MUNGU kwa sababu tu unaomba kwa jina la dini au jina la dhehebu au jina la nabii wako n.k, kama ni hivyo hakika na wewe sio muombaji makini.
◼️Ngoja nikujulishe juu ya muombaji manikini.
✓✓Maombi ya mwanamaombi makini ni haya;
1. Maombi ya mwana maombi makini ni maombi katika jina la YESU KRISTO.
Yohana 14:13-14 ''Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana. Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya.''
✓✓Ni Bwana YESU mwenyewe ndio anasema hapo juu kwenye maandiko kwamba tukitaka MUNGU atujibu basi tuombe katika jina lake YESU KRISTO.
◼️Hakuna jina lingine lolote nje na Jina la YESU KRISTO ambalo tunaweza kuomba kwa hilo na tukajibiwa maombi.
Siku moja Mimi Peter Mabula nilimsikia mtu mmoja anaomba akisema ''Katika jina la Mungu wa baba yangu(akimtaja mtumishi) naomba na nitapokea'', mtu kama huyo sio mwanamaombi makini maana anaomba kwa jina la mtu na sio kwa jina la YESU KRISTO ambalo ndilo pekee tunaweza kuomba na kupokea mahitaji yetu.
✓✓Ndugu, kama wewe huwa unaomba kwa jina la nabii au mtume au mchungaji wewe sio mwanamaombi makini.
✓✓Kama wewe huwa unaomba ukisema ''Kwa jina la Yesu wa nabii fulani'' wewe sio muombaji makini maana kwanza hujui kama huyo nabii ana YESU KRISTO au ana Baryesu, uwe makini sana maana maana unaweza hata kujiunganisha na kuzimu kwa sababu wewe sio mwanamaombi makini.
◼️Kwanini usiseme tu ''Kwa jina la YESU KRISTO wa Nazareti'' au ''kwa jina la YESU KRISTO Mwana wa MUNGU aliye hai'' ili ukubaliwe na MUNGU kuhusu maombi yako?
✓✓Ndugu, jifunze Kwa Petro ambaye aliomba hivi na kiwete akapona muda huo huo.
Matendo 3:6-8 '' Lakini Petro akasema, Mimi sina fedha, wala dhahabu, lakini nilicho nacho ndicho nikupacho. Kwa jina la YESU KRISTO wa Nazareti, simama uende. Akamshika mkono wa kuume, akamwinua, mara nyayo zake na vifundo vya miguu yake vikatiwa nguvu. Akaondoka upesi akasimama, akaanza kwenda; akaingia ndani ya hekalu pamoja nao, akienda, akiruka-ruka, na kumsifu MUNGU.''
✓✓Ndugu usiige kila kitu, wapo watumishi ni wasanii, badala ya kusema kwa jina la YESU KRISTO wao husema husema kwa haraka haraka kwa kwa jina la ''esu'' na sio sio kwa jina la YESU KRISTO.
◼️Tumia jina la YESU KRISTO kwenye maombi na sio kutumia jina la mwingine yeyote.
✓✓Hata usiseme ''Kwa Jina la Mungu'' maana Mungu sio jina ila ni cheo, hivyo hata shetani kuna mahali huitwa ''mungu'' wapo akina mungu wengi tu hivyo tumia jina la YESU KRISTO maana ndio hilo liliamuriwa na MUNGU aliyeziumba mbingu na dunia.
◼️Jina la YESU KRISTO ndilo jina lipitalo majina yote.
✓✓Vitu vyote kwenye ulimwengu wa roho hutii jina la YESU KRISTO tu na sio jina lingine lolote.
Wafilipi 2:10-11 '' ili kwa jina la YESU kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI Bwana, kwa utukufu wa MUNGU Baba. ''
2. Maombi ya mwana maombi makini ni maombi yanayoambatana na utakatifu.
Waebrania 12:14 ''Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona BWANA asipokuwa nao;''
✓✓Maombi ya mwana maombi makini ni maombi kupitia jina la YESU KRISTO huku maombi hayo yakiambatana na utakatifu.
Biblia inasema huwezi kumwona MUNGU akikutetea kama maombi yako hayaambatani na Utakatifu.
Wapo waliojaribu kuomba sana lakini Biblia lisema kwamba MUNGU hakuwapa mahitaji yao kwa sababu ya dhambi.
Isaya 59:1-2 ''Tazama, mkono wa BWANA haukupunguka, hata usiweze kuokoa wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia; lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na MUNGU wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia.''
◼️Dhambi zinaweza kuuficha uso wa MUNGU hata asisikie maombi yako, hivyo maombi yako lazima yaambatane na utakatifu ndipo utakuwa mwana maombi makini.
✓✓Kama unaomba tu bila kubadilika rohoni juu ya tabia chafu ufanyazo basi wewe sio mwana maombi makini.
Ndugu anza leo kuwa mwana maombi makini.
3. Maombi ya mwana maombi makini ni maombi katika ROHO MTAKATIFU.
Yuda 1: 20 '' Bali ninyi, wapenzi, mkijijenga juu ya imani yenu iliyo takatifu sana, na kuomba katika ROHO MTAKATIFU,''
◼️Maombi ya mwana maombi makini ni maombi kupitia jina la YESU KRISTO huku ukiongozwa na ROHO MTAKATIFU.
✓✓Maombi katika jina la YESU KRISTO yanaweza kutengeneza nguvu za MUNGU hadi mtu akanena kwa lugha katika ROHO MTAKATIFU.
✓✓Maombi ya mwana maombi makini ni maombi kupitia jina la YESU KRISTO huku mtu huyo akifanyia kazi maelekezo ya ROHO MTAKATIFU katika maombi yake.
✓✓Maombi ya mwana maombi makini ni maombi kupitia jina la YESU KRISTO huku akifundishwa na ROHO MTAKATIFU nini cha kufanya katika maombi hayo.
◼️Maelekezo ya ROHO MTAKATIFU ni ya lazima sana ukitaka kuwa mwana maombi makini.
ROHO MTAKATIFU ndiye anayeujua ulimwengu wa roho hivyo anaweza kukufunulia ili ujue namna ya kuomba.
1 Kor 2:10 '' Lakini MUNGU ametufunulia sisi kwa ROHO. Maana ROHO huchunguza yote, hata mafumbo ya MUNGU. ''
✓✓ROHO MTAKATIFU anaweza kukufunulia kwa kukupa tu msukumo rohoni juu ya kuombea kitu fulani, anaweza kukufunulia live ukaona kinachoendelea rohoni.
✓✓ROHO MTAKATIFU anaweza kukuondolea mzigo wa kuombea jambo fulani kwa sababu jambo gilo sio la wakati huu au halikuhusu wewe japokuwa unalihitaji.
✓✓ROHO MTAKATIFU hutusaidia mengi sana katika maombi, anaweza kukupa andiko, anaweza kukupa msukumo umshirikishe Mtumishi ili akuombee pia huku na wewe ukiendelea kuomba n.k
◼️Ndugu hakikisha unakuwa mwana maombi makini maana mwana maombi makini huomba kupitia jina la YESU KRISTO huku akiongozwa na ROHO MTAKATIFU.
4. Ni maombi ya kudumu hadi apokee hitaji lake.
1 Thesalonike 5:17 ''ombeni bila kukoma;''
✓✓Kuomba bila kukoma maana yake ni kuomba hadi upokee.
✓✓Kuuomba bila kukoma ni kuomba siku zote maana maombi ni maisha ya Mkristo makini.
◼️Maombi ya mwana maombi makini ni maombi kupitia jina la YESU KRISTO huku akiomba bila kukataa tamaa.
✓✓Maombi ya mwana maombi makini ni maombi kupitia jina la YESU KRISTO huku akiomba bila kukoma.
Kuna watu akiomba mara moja akatoa sadaka mara moja akiona hajibiwi anaweza hata kutangaza mitaani kwamba mbona MUNGU anapendelea kumbe ni yeye hajui kanuni ya maombi.
Kuna mahitaji mengine ukiomba au ukiombewa mara moja tu inakuwa lakini yapo maombi mengine kulingana na mbingu sio kwa wakati huo hivyo inakupasa kutokulalamika bali endelea na maombi hadi muda sahihi ukifika utapata.
Maombi ya mwana maombi makini ni maombi kupitia jina la YESU KRISTO huku ukiomba bila kukoma.
◼️Ndugu hakikisha unakuwa mwana maombi makini maana mwana maombi makini huomba kupitia jina la YESU KRISTO huku ukidumu katika maombi siku zote.
Wakolosai 4:2 '' Dumuni sana katika kuomba, mkikesha katika kuomba huku na shukrani; ''
✓✓Omba kupitia jina la YESU KRISTO huku ukidumu katika kuwa muombaji, tena maombi yako yaambatanishe na shukrani kwa MUNGU.
◼️Uwe mtu wa kumshukuru MUNGU.
✓✓Ndugu hakikisha unakuwa mwana maombi makini maana mwana maombi makini huomba kupitia jina la YESU KRISTO huku akiomba bila kukoma.
Kama wewe umeomba mara moja au mara mbili au mara kumi na umeshaanza lawama hadi kwa watumishi ni kwa sababu wewe sio mwana maombi makini.
Ndugu, hakikisha unakuwa mwana maombi makini.
5. Ni maombi ya Imani.
Yakobo 5:15 ''Na kule kuomba kwa imani kutamwokoa mgonjwa yule, na BWANA atamwinua; hata ikiwa amefanya dhambi, atasamehewa. ''
◼️Maombi ya mwana maombi makini ni maombi kupitia jina la YESU KRISTO huku muombaji akiomba kwa imani.
◼️Kitu kimoja ambacho huwezi kukitenganisha na maombi sahihi ni imani katika KRISTO YESU.
✓✓Mwana maombi makini huomba kwa imani katika Jina la YESU KRISTO Mwokozi wetu aliye hai milele.
✓✓Wapo pia waombaji ambao wana imani ya kuomba tu ila hawana imani ya kupokea, hao sio waombaji makini, yaani mtu ana imani wakati tu akiomba lakini baada ya hapo akiulizwa ''Je unadhani utapata Mchumba'' anasema hata sijui yaani hata sijui kama naweza kupata mchumba, anajibu hivyo wakati katika maombi yake aliomba kwa imani huku akilia kwamba apate Mchumba, huyo sio mwana maombi makini maana anaomba kwa imani ila hana imani ya kupokea.
✓✓Maombi ya mwana maombi makini ni maombi kupitia jina la YESU KRISTO huku na imani kubwa ya muombaji.
◼️Bila imani thabiti katika KRISTO huwezi kumpendeza MUNGU.
Waebrania 11:6 '' Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.''
✓✓Ndugu hakikisha unakuwa mwana maombi makini maana mwana maombi makini huomba kupitia jina la YESU KRISTO huku akiomba kwa imani.
Muombaji lazima uwe unaomba kwa imani.
◼️Kwa wanaoomba kwa imani Kupitia jina la YESU KRISTO leo nina ujumbe huu mfupi kwao, ukiweza husika nao.
Ujumbe huo unatoka Yoshua 23:10 ambapo Biblia inasema '' Mtu mmoja miongoni mwenu atafukuza watu elfu; maana BWANA, Mungu wenu, ndiye anayewapigania, kama alivyowaambia.''
✓✓Kama unaishi maisha matakatifu ya Wokovu wa KRISTO amini hakika unayo mamlaka ya kufukuza maadui zako 1000 kwenye ulimwengu wa roho, utawafukuza kwa njia ya maombi ya vita.
[✓Sasa kama una imani ya kuomba na kupokea naomba uombe maombi ya kufukuza maadui zako wote kwenye ulimwengu wa roho.
1. Fukuza maadui zako wote ili waiachie afya yako.
2. Fukuza maadui zako wote ili waiachie ndoa yako.
3. Fukuza maadui zako wote ili wauachie uchumi wako.
4. Fukuza maadui zako wote ili wauachie uzao wako.
5. Fukuza maadui zako wote ili watoke katika mamlaka yako ya kumiliki katika ulimwengu wa roho.
◾Kwanini nimetaja mambo hayo matano tu?
◼️Ni kwa sababu baraka za MUNGU zote ziko ndani ya makundi hayo matano tu.
✓✓Yaani kuna baraka za Ndoa, Afya, Uchumi, Uzao na Kutamalaki(Kumiliki na kutawala)
Zingatia na MUNGU atakubariki sana.
Mche MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi na utaitwa heri.
Kama pia unatumia Facebook ni follow maana itafika kipindi nitakuwa napost tu katika page yangu na profile yangu.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292(Sadaka ya kuipeleka Injili, Ushauri, Whatsapp n.k)
Ubarikiwe sana.

Comments
Baada ya baba yangu mdogo kuniacha kwa miezi saba mirefu, nilikuwa nimevunjika moyo kabisa. Alinizuia kwenye mitandao yote ya kijamii, akaondoka, na hakukuwa na njia ya kumfikia. Karibu nikate tamaa, lakini ndani kabisa nilijua singeweza kupata mtu yeyote ambaye angenipenda na kunitendea jinsi alivyonitendea.
Siku moja, bosi wangu kazini aligundua jinsi nilivyokuwa na huzuni na akanitambulisha kwa Dkt. Dawn. Dkt. Dawn alisikiliza hadithi yangu na akaahidi kwamba mpenzi wangu angerudi kwangu ndani ya siku tatu. Kwa kweli, sikuamini mwanzoni—lakini kwa mshangao wangu mkubwa, siku ya tatu simu yangu iliita. Ilikuwa yeye! Alikuwa akilia na kuomba msamaha, akisema hataniacha tena.
Tangu siku hiyo, uhusiano wetu umekuwa na nguvu na uzuri zaidi kuliko hapo awali. Amekuwa akipenda na kunijali mimi na mtoto wetu, na sasa tunafunga ndoa katika miezi miwili tu! ❤️
Shukrani zote kwa Dkt. Dawn, ambaye kwa kweli alifanya jambo lisilowezekana liwezekane. Ninampendekeza kwa moyo wote kwa yeyote anayekabiliwa na changamoto katika:
Masuala ya uhusiano au ndoa
Ugonjwa au magonjwa
Matatizo ya utasa au bahati nasibu
Kesi za mahakamani au urejeshaji wa mali
Dkt. Dawn kweli hutatua matatizo kwa ufanisi na hurudisha furaha katika maisha ya watu.
Wasiliana na Dr. Dawn kwenye WhatsApp: +2349046229159
Barua pepe: dawnacuna314@gmail.com