Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe Ndugu zangu wote.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU wa Mbinguni.
◼️Leo namzungumzia "RAFIKI WA KWELI."
◾Rafiki ni nani?
✓✓Rafiki ni Mtu mnayeaminiana na kuthaminiana naye.
"Rafiki" sio tu Mtu ambaye yuko karibu na Wewe , bali ni Yule aliye kwa ajili yako.
Mithali 17:17 "Rafiki hupenda sikuzote; ......."
✓✓Rafiki ni Mtu ambaye unamwamini kwenye maisha yako ya kila siku.
✓✓Rafiki ni Mtu anayejulikana vizuri na mwingine na anayezingatiwa kwa kupenda, upendo, na uaminifu.
Mfano hai ni huu
Matendo 27:3 "Siku ya pili tukawasili Sidoni; Yulio akamfadhili sana Paulo akampa ruhusa kwenda kwa rafiki zake, apate kutunzwa."
◼️Tabia za marafiki wa kweli.
1. Marafiki wa kweli huongea/huzungumza.
2. Marafiki wa kweli husaidiana.
3. Marafiki wa kweli hushirikishana siri.
4. Marafiki wa kweli husameheana inapotokea kukosana.
5. Marafiki wa kweli huwa wawazi baina yao.
✓✓Inawezekana ndugu unaye rafiki wa kweli ambaye huwa unashirikiana naye Mara nyingi katika maisha, ni sawa lakini ukweli mmoja ni kwamba rafiki pekee wa kweli kuliko wote ni YESU KRISTO.
Yohana 15:14-15 " Ninyi mmekuwa rafiki zangu, mkitenda niwaamuruyo. Siwaiti tena watumwa; kwa maana mtumwa hajui atendalo bwana wake; lakini ninyi nimewaita rafiki; kwa kuwa yote niliyoyasikia kwa BABA yangu nimewaarifu."
◼️YESU KRISTO ndiye rafiki wa kweli.
✓✓Marafiki Wanadamu hubadilika.
Na Biblia inaonya juu ya marafiki Wanadamu ambao hubadilika na kutaka kuwabadilisha rafiki zao.
Kumbu 13:6-8 " Atakapokushawishi kwa siri ndugu yako, mwana wa mamaako, au mwana wako, au binti yako, au mke wa kifuani mwako, au rafiki yako aliye kama moyo wako, akikuambia, Twende tukaabudu miungu mingine usiyoijua wewe wala baba zako;
katika miungu ya mataifa yaliyo kando-kando yenu karibu nawe au mbali nawe, tokea ncha moja ya dunia hata ncha ya pili ya dunia; usimkubalie wala usimsikize; wala jicho lako lisimwonee huruma, wala usimwache, wala usimfiche;"
✓✓Marafiki Wanadamu hugeuka.
Ayubu 19:14 "Watu wa mbari yangu wamekoma, Na rafiki zangu niwapendao wamenisahau."
✓✓Marafiki Wanadamu hubadilika hata kuwa wauaji wako.
Mfano ni huu Yehu aliua hadi rafiki zake wote.
2 Wafalme 10:11 "Hivyo Yehu akawapiga wote waliosalia wa nyumba ya Ahabu katika Yezreeli, na hao wakuu wake wote, na rafiki zake, na makuhani wake, hata hakumwachia aliyesalia hata mmoja."
✓✓Rafiki Mwanadamu anaweza kuwa na tabia mbaya hata zikakuathiri na Wewe.
Mithali 22:24 "Usifanye urafiki na mtu mwenye hasira nyingi; Wala usiende na mtu wa ghadhabu nyingi;"
Ayubu 16:20 "Rafiki zangu hunidharau; Lakini jicho langu humwagia MUNGU machozi;"
Yohana 15:13 "Hakuna aliye na upendo mwingi kuliko huu, wa mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake."
◼️YESU KRISTO alitoa uhai wake kwa ajili Yako na yangu, huyo ndio rafiki wa kweli wa daima
Mfano hai ni huu ambapo Mtu aliyepooza alisamehewa dhambi na Bwana YESU KRISTO na baada ya kusamehewa alipona na ugonjwa wake.
Marko 2:5 "Naye YESU, alipoiona imani yao, akamwambia yule mwenye kupooza, Mwanangu, umesamehewa dhambi zako."
◼️YESU KRISTO ni rafiki pekee ambaye anaweza kusamehe dhambi na zikafutika zisiwepo Tena.
Marko 2:10 "Lakini mpate kujua ya kwamba Mwana wa Adamu anayo amri duniani ya kusamehe dhambi, (hapo amwambia yule mwenye kupooza),"
✓✓Ukimpokea YESU kama Mwokozi wako analiandika jina lako katika kitabu cha Uzima Mbinguni na hatalifuta kwenye kitabu Cha Uzima ukibaki kwake na kufanya Neno lake, hakuna rafiki wa kweli kama YESU KRISTO.
Ufunuo 3:5 "Yeye ashindaye atavikwa hivyo mavazi meupe, wala sitalifuta kamwe jina lake katika kitabu cha uzima, nami nitalikiri jina lake mbele za Baba yangu, na mbele ya malaika zake."
✓✓YESU hakuwazii mabaya na wala hakupangii mabaya.
✓✓Ukiamua kufanyika rafiki wa YESU hakika ni baraka kwako.
◼️Njia kuu za kudumisha urafiki na YESU KRISTO.
1. Zungumza na YESU KRISTO daima.
Yohana 14:14 "Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya.''
2. Ishi maisha matakatifu maana ni maisha hayo tu ndio ambayo YESU KRISTO ayapendayo.
1 Petro 1:15 'bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote;'
◼️YESU KRISTO ndio rafiki yangu Mkuu na wa kweli, vipi kwa upande wako?
✓✓MUNGU akubariki sana kama ukifanyika rafiki wa YESU KRISTO.
Zingatia na MUNGU atakubariki sana.
Mche MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi na utaitwa heri.
Kama pia unatumia Facebook ni follow maana itafika kipindi nitakuwa napost tu katika page yangu na profile yangu.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292.
Ubarikiwe sana

Comments