MWONGOZO WA MAOMBI YA KIFAMILIA YA SIKU 12.

Mchungaji Elly Botto 




Bwana YESU atukuzwe ndugu yangu.

Kanisani kwetu wakati fulani mwaka 2018  tulianza Maombi ya kuomba kifamilia kila siku kwa siku 12. 

Huu ulikuwa ni Ufunuo wa Mchungaji Elly Botto.

✓✓Tulimuona MUNGU kupitia Maombi Yale, 
Mimi Peter Mabula Leo Napata msukumo Leo wa kukushirikisha na wewe maana najua utamuona MUNGU kipekee sana.

✓✓Huwa Nina tabia ya kutunza Ufunuo ambao MUNGU amenipa ndio maana nakuletea Leo maana Neno la MUNGU li hai daima.

◼️Maombi haya ni ya Ibada ya familia yaani Familia nzima mnaingia katika Maombi pamoja kwa muda hata dakika 10 au zaidi mkiwa pamoja kabla ya kwenda kwenye majukumu ya kila siku.

◼️Au mnaingia  mnaweza mkajipangia ratiba muda ambao kila mmoja wa familia hiyo atakuwepo mfano kabla ya kulala usiku.

◼️Sio maombi ya kufunga ingawa mkipenda mnaweza Kufunga Kulingana na Ratiba zetu kama familia ila mnaweza kuomba kama familia na najua Bwana YESU KRISTO atatenda jambo jipya la ushindi.

Maombi ni haya na mnaweza mkaomba kwa siku 12  kila siku mkihusika na kipengele kimoja kama nilivyokuandikia na MUNGU katika KRISTO YESU atawaonekania.

1. Kutubu kwa ajili ya familia na ukoo.

Yeremia 14:20-21 " Ee BWANA, tunakiri uovu wetu, na ubaya wa baba zetu; maana tumekutenda dhambi. Usituchukie, kwa ajili ya jina lako; usikifedheheshe kiti cha enzi cha utukufu wako, kumbuka, usilivunje agano ulilofanya nasi.

2. Kuvunja laana za familia kutoka kwa mababu na vizazi.

✓✓Familia ya Abimeleki kipindi fulani ilipitia adhabu ya MUNGU kwa sababu ya dhambi za Baba wa familia.

Mwanzo 20:18 ''Maana BWANA alikuwa ameyafunga matumbo ya watu wa nyumbani mwa Abimeleki, wasizae, kwa ajili ya Sara mkewe Ibrahimu."

✓✓Watu wa familia ya farao kipindi fulani walikutana na mapigo ya MUNGU kwa sababu ya makosa ya Kiongozi wa ukoo wao.

Mwanzo 12:17 "Lakini BWANA akampiga Farao na nyumba yake mapigo makuu, kwa ajili ya Sarai, mkewe Abramu."

✓✓Hii Ina maana makosa ya wazazi wakati Mwingine yanaweza kuwagharimu hadi Watoto.

Kwenye Maombi Yako.
◼️Katika Jina la YESU KRISTO vunja laana za familia kutoka kwa mababu na vizazi.

3. Kuvunja roho za matambiko na kufuta nguvu ya kafara iliyowahi kufanyika kuhusu familia yenu au ukoo.

Ukisoma Waamuzi 6:25 unagundua kwamba Madhabahu ya shetani ilikuwa katika familia na katika ukoo na katika Nyumba ya Yoashi.

Waamuzi 6:25" Ikawa usiku uo huo Bw5ana akamwambia, Mtwae ng'ombe wa baba yako, yaani ng'ombe wa pili, wa miaka saba, ukaiangushe madhabahu ya Baali, aliyo nayo baba yako, ukaikate Ashera ile iliyo karibu nayo;"

◼️ Madhabahu ya shetani  ya familia au ukoo hukusika na matambiko kafara, mizimu na Kila Nguvu za giza katika ukoo husika au familia husika, Sasa kwa Maombi katika Jina la YESU KRISTO vunja roho za matambiko na kufuta nguvu ya kafara iliyowahi kufanyika kuhusu familia yenu au ukoo.

4. Kufuta maagano ya giza ya kila namna ambayo yaliwahi kufanyika ili kuwafunga.

◼️Maagano yeyote ya kishetani yana madhara.

Isaya 28:15 "Kwa sababu mmesema, Tumefanya agano na mauti, tumepatana na kuzimu; pigo lifurikalo litakapopita, halitatufikia sisi; kwa maana tumefanya maneno ya uongo kuwa kimbilio letu, tumejificha chini ya maneno yasiyo kweli;"

◼️Hivyo kwa Jina la YESU KRISTO futa maagano ya giza ya kila namna ambayo yaliwahi kufanyika ili kuwafunga

5. Kuharibu na kuzivunja madhabahu zote za giza zilizowafunga.

Kumbu  12:3 "nanyi zivunjeni madhabahu zao, zibomoeni nguzo zao, na maashera yao yateketezeni kwa moto, na sanamu za kuchonga za miungu yao zikateni; na jina lao lifutilieni mbali na mahali hapo."

Kuna kazi 4 tu ambazo MUNGU anataka tuzifanye juu ya Madhabahu za kichawi.
Kazi hizo 4 ni;

✓✓Kuvunja Madhabahu za kichawi.

✓✓kubomoa Madhabahu za giza.

✓✓Kuteketeza kwa moto wa Damu ya YESU KRISTO kila vitu vinavyotumika na Madhabahu za kishetani.

✓✓ Kufuta Jina la Miungu katika maeneo yetu.
Omba mambo hayo 4 katika Maombi Yako kupitia Jina la YESU KRISTO Mwokozi wetu aliye hai milele.

6. Pasua na kufuta vifungo vya giza vyote. 

Zaburi 2:3 "Na tuvipasue vifungo vyao, Na kuzitupia mbali nasi kamba zao."

kama vifungo vya magonjwa, umasikini, laana n.k
◼️Leo kwa Mamlaka ya Jina la YESU KRISTO Pasua na kufuta vifungo vya giza vyote. 

7. Kurejesha mahusiano mazuri katika familia yenu.

Zaburi 133:1" Tazama, jinsi ilivyo vema, na kupendeza, Ndugu wakae pamoja, kwa umoja.''

◼️Ni kusudi la MUNGU wa Mbinguni kwamba Ndugu katika familia au Ukoo mkae kwa pamoja na kwa umoja.

✓✓Ombea umoja na mahusiano mazuri katika familia yenu 

8. Kurejesha baraka za MUNGU, ambazo MUNGU aliahidi.

Zaburi 128:3 "Mkeo atakuwa kama mzabibu uzaao, Vyumbani mwa nyumba yako. Wanao kama miche ya mizeituni Wakiizunguka meza yako."

◼️Omba katika Jina la YESU KRISTO  urejesho wa  baraka za MUNGU, ambazo MUNGU aliahidi.

9. Kurejesha mafanikio ya kiroho na kimwili.

3 Yohana 1:2 "Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo."

◼️Ni kusudi la MUNGU mfanikiwe katika mambo yote.

 ◼️Kwa Jina la YESU KRISTO ombea mafanikio ya kiroho na kimwili kwa familia yenu au ukoo wenu kama mnaombea Ukoo.

10. Kuombea neema ya Wokovu wa KRISTO kwa familia yenu yote na ukoo.

2 Wakorintho 13:14 "Neema ya Bwana YESU KRISTO, na pendo la MUNGU, na ushirika wa ROHO MTAKATIFU ukae nanyi nyote."

◼️ Neema ya Wokovu wa KRISTO YESU kwa familia yenu na Ukoo wenu ni Muhimu sana, omba Neema ya Wokovu wa Bwana YESU kwa watu w familia ambao hawajampokea YESU KRISTO kama Mwokozi ili wafanye hivyo.

11. Kuombea uzao, Kuirejesha familia ya Ki MUNGU ndani ya Kanisa.

Kutoka 23:26 "Hapatakuwa na mwenye kuharibu mimba, wala aliye tasa, katika nchi yako; na hesabu ya siku zako nitaitimiza."

◼️Sio kusudi la MUNGU watu kuwa tasa hivyo ombea Uzao wa ki MUNGU katika familia yenu, ukoo na Kanisa.

12. Kuomba ili ROHO MTAKATIFU awe Mwalimu katika familia yenu ya Ki MUNGU.

Yohana 14:26 "Lakini huyo Msaidizi, huyo ROHO MTAKATIFU, ambaye BABA atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia."

◼️Baada ya Kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi jambo la Muhimu zaidi kwa kila Mkristo baada ya hapo ni kumhitaji ROHO MTAKATIFU.

◼️ ROHO MTAKATIFU ni wa Muhimu sana kwa kila Mkristo, vivyo omba ROHO MTAKATIFU awe Mwalimu na Kiongozi wa familia yenu.

Ombeni katika jina la YESU KRISTO na MUNGU awabariki sana.
Zingatia  na MUNGU atakubariki sana.
Mche MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi na utaitwa heri.
Kama pia unatumia Facebook ni follow maana itafika kipindi nitakuwa napost tu katika page yangu na profile yangu.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter  Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292(Sadaka ya kuipeleka Injili, Ushauri, Whatsapp n.k)
Ubarikiwe sana.

Comments