USHUHUDA UNAJENGA.
Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe.
Hapa chini ni ujumbe ambao rafiki yangu mmoja alinitumia, usome yamkini ukajifunza kitu, Muhimu usiache kumtegemea Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
Nauleta ujumbe kama ulivyo.
"Mtumishi namshukuru Mungu kwa matendo yake makuu aliyonitendea, Sina cha kukupatia zaidi ya kusema asante kwa maombi yako na Mungu akubaliki, akuongoze, akutie nguvu ,uendelee na moyo huo,uendelee kutuombea bila kuchoka.
Mtumishi Peter Mimi nilikata tamaa ya maisha, niliwaza nihame eneo hili nikaambiwa utakufa wachawi hawakimbiwi, nikaamua kuacha kazi nikafuatwa nyumbani na ndugu na marafiki zangu nikagombezwa, hapo mtumishi nikiwa nimechoka vibaya Sana natembea nimeinamisha Mgongo.
Siku moja niliamua kuwa bora nife nipumzike ili wachawi wasinione. Wakati naelekea hospitali nikakutana na rafiki yangu tuliyesoma nae akiwa amenitangulia madarasa Mawili, nikiwa nalia huku barabarani akaniita jina na kusema !!!!umekuwaje?? Akachukua pikipiki tukarudi nae kwenda kwake, tulipofika tu pale akachukua maji akaninyunyia na akaanza kuomba, mimi wakati huo nalia tu, akaita tena jina langu akisema umekuwaje???? Akaniambia tamka neno "Mungu nisamehe" rudia tena na tena karibia kama mara 20 hivi.
Basi niliporudia ile hasira ikawa imetulia tukaanza kuongea, nikamweleza story ndefu, Naye sasa akaanza kulia tena yeye akalia kwa sauti mpaka watu wakaja, wakauliza kulikoni yeye aliwajibu matendo ya Mungu ni makubwa, watu wakaondoka, akaniambia kwamba unaelekea kufa kwa sababu ya wachawi akiwemo mama yako.
Akaendelea kusema kwamba nimetamka haya nami yalinikuta zaidi yako kutoka kwa mama yangu na dada zangu ila yote yanaisha kwa kumtegemea Yesu aliye kufa msalabani, hapo ndio kilio kilianza moja kwangu, akanifungia sebureni kwake akaenda kazini kuaga, Aliporudi tukaongea kisha nikamuaga naenda nyumbani tukaomba akanisindikiza mpaka kwangu tulipofika akaomba Rehema, akaniaga akasema kesho niende kwake saa moja jioni.
Mtumishi hapo ndio mwanzo wa kuuona mkono wa Mungu kupitia kwa mwanae Yesu Kristo, baadae majanga zaidi yalianza sasa yale yasio elezeka hadi kukosa chakula ndani kila mtu anakutemea mate story ni ndefu.
Namshukuru Mungu baada ya kukupigia simu uniombee na namshukuru Mungu baada ya mimi kuomba maombi ya kwenye masomo yako ya maombi.
Mtumishi baada ya kukutana na wewe katika maombi Kwa njia ya simu Mungu ni mkuu, kama hajapanga yeye watazunguka tu nawe hautadhurika.
Kwanza nimeanza kwenda kanisani,
Pili kila lililobaya mbele yangu Mungu ananiepusha.
Tatu mwili umeanza kurudi katika hali yake.
Nne kinanipa kuringa na kuruka ruka macho ya rohoni.
Tano nimeanza nami kuomba kwa sauti bila roho kuuma.
Maombi yako yanaupako ndani yake sala zako sijui nikuelezeje, kitabu chako kimenifaa sana tena sana Mpaka sasa nimeanza kulipa hadi wadeni wangu. nakurudisha Mali zangu zilizokuwa mikononi mwa watu, Usichoke kuniombee,
Mungu akubariki sana.
Ipo siku nitakutumia sadaka kidogo kwa ajili ya maombi.
Ubarikiwe sana."
Comments