![]() |
| Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe Ndugu!.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU wa Mbinguni.
◼️Shetani anao muda mchache tu maana anasubiria jehanamu.
Ufunuo 12:12 " Kwa hiyo shangilieni, enyi mbingu, nanyi mkaao humo. Ole wa nchi na bahari! Kwa maana yule Ibilisi ameshuka kwenu mwenye ghadhabu nyingi, akijua ya kuwa ana wakati mchache tu."
✓✓Shetani anajua anao muda mchache tu kabla hajatupwa ziwa la moto usiozimika, kwa kulijua hilo ndio maana anajaribu kuwakamata baadhi ya watu ili wasiokolewe na YESU KRISTO hata wakaiepuka jehanamu.
✓✓Ndio maana Leo kuna watu ukiwahubiria Injili wanakutukana kwa sababu shetani yuko ndani yao kuhakikisha hawakosekani jehanamu.
✓✓Kuna watu wakikuona unahubiri Injili au unamtaja YESU KRISTO Mwokozi wanakuona kana umekosa kazi au umepungukiwa sana, kumbe ndani yao shetani amewakamata wao ili Neema ya Wokovu wa KRISTO YESU usiwazukie.
2 Wakorintho 4:4 "ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake KRISTO aliye sura yake MUNGU."
◼️Ndugu ukiyempokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako hakikisha unang'ang'ania Wokovu hadi mwisho.
✓✓Uongo wa shetani ni mwingi sana lakini wewe ng'ng'ana na YESU anayeokoa.
✓✓Usikubali shetani akutawale hata na wewe uwe mwenda jehanamu.
Shetani anao muda mchache ili kutafuta waenda jehanamu.
Ndugu, wewe usikubali kushawishiwa na shetani au maajenti wake.
◼️Kataa dhambi zote maana dhambi na kumkataa YESU KRISTO kama Mwokozi ndizo silaha kuu za shetani ili kupata watu wa kwenda naye jehanamu.
Ndugu, ili shetani asikuhusu kwa lolote lile basi mhitaji sana Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
1 Yohana 3:8-10 " atendaye dhambi ni wa Ibilisi; kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa MUNGU alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi. Kila mtu aliyezaliwa na MUNGU hatendi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na MUNGU. Katika hili watoto wa MUNGU ni dhahiri, na watoto wa Ibilisi nao. Mtu ye yote asiyetenda haki hatokani na MUNGU, wala yeye asiyempenda ndugu yake."
◼️Ndugu mkimbilie YESU KRISTO kwa ajili ya Wokovu.
✓✓Mkatae shetani na kazi zake zote.
✓✓Kataa dhambi, iepuke dhambi, ipinge dhambi, jitenge mbali na dhambi na usifanye dhambi tena.
Wakati huu ulionao unaweza kuutumia kuishi maisha matakatifu katika KRISTO YESU na ukapata uzima wa milele.
◼️Wakati huu ulionao unaweza kuutumia kulitii Neno la MUNGU na ukafanikiwa kiroho na kimwili.
◼️Wakati huu ulionao unaweza ukautumia kusamehe na kusahau hata ukampendeza MUNGU naye akakubariki.
◼️ Wakati huu ulionao unaweza ukautumia kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako na jina lako likaandikwa mbinguni kwenye Kitabu cha Uzima.
◼️Wakati huu ulionao unaweza ukautumia kuwaleta watu kwa YESU hata watu wengi kupitia wewe wakaiepuka jehanamu.
Yuda 1:23 "na wengine waokoeni kwa kuwanyakua katika moto; na wengine wahurumieni kwa hofu, mkilichukia hata vazi lililotiwa uchafu na mwili."
✓✓Wakati huu ulionao unaweza ukautumia kufanya maombi ya kina na vitu vibaya vikazuiliwa kuja kwako.
◼️Wakati huu ulionao usiudharau bali utumie kwa mema ili iwe faida kwako kiroho na kimwili.
Waefeso 5:15-17 " Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima; mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu. Kwa sababu hiyo msiwe wajinga, bali mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya BWANA."
MUNGU akubariki Sana ukiutumia vizuri wakati wako.
Zingatia na MUNGU atakubariki sana.
Mche MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi na utaitwa heri.
Kama pia unatumia Facebook ni follow maana itafika kipindi nitakuwa napost tu katika page yangu na profile yangu.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292.
Ubarikiwe sana

Comments