![]() |
| Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe Ndugu zangu wote.
Karibuni sana tujifunze Neno la MUNGU wa Mbinguni.
✓✓Inawezekana uko katika wakati mgumu sana na unahitaji msaada.
✓✓Inawezekana unaumwa sana na akili yako inawaza kwamba angetokea daktari fulani ningepona.
✓✓Inawezekana unaonewa sana kazini kwako au kwenye eneo lako na unawangoja wanadamu Fulani ili wakusaidie.
◼️Ndugu usiweke tegemeo na tumaini kwa wanadamu Bali weka tumaini lako kwa MUNGU Muumbaji wako.
✓✓Najua katika ulimwengu huu yapo mengi ya kuchukiza, makwazo ni mengi na watu wa kutukasilisha ni wengi lakini tunasonga mbele kwa Jina la YESU KRISTO.
✓✓Wako watu waliweka tumaini kwa MUNGU na Biblia inasema Watu hao kwa kumtumaini MUNGU wakawa Watu Bora kuliko waliowatangulia mfano hai ni Mfano Hezekia
2 Wafalme 18:5 "Alimtumaini BWANA, Mungu wa Israeli; hata baada yake hapakuwa na mfano wake katika wafalme wote wa Yuda, wala katika hao waliomtangulia."
◼️Weka tumaini kwa YESU KRISTO Mwokozi wako.
Waefeso 1:12 "Nasi katika huyo tupate kuwa sifa ya utukufu wake, sisi tuliotangulia kumwekea Kristo tumaini letu."
◼️Funga na kuomba ukimngoja BWANA.
✓✓MUNGU akiwa upande wako atakushindia, MUNGU akiwa ndio mlinzi wako unayemtegemea kwa maombi hakika atakulinda.
✓✓Kwanza ni baraka kubwa kumtegemea MUNGU na kumtegemea MUNGU huleta faida nyingi za kiroho.
Yeremia 17:7 " Amebarikiwa mtu yule anayemtegemea BWANA, Ambaye BWANA ni tumaini lake."
◼️YESU KRISTO akiwa ni Mwokozi wako hakika MUNGU Baba atakuokoa.
◼️ROHO MTAKATIFU akiwa ni kiongozi wako unayemtii hakika atakuongoza kukupeleka kwenye ushindi.
Yeye anasema " Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea; Nitakushauri, jicho langu likikutazama.-Zaburi 32:8"
✓✓Ndugu hakikisha tu MUNGU yuko upande wako na umtumaini Yeye.
✓✓Hakikisha YESU KRISTO yuko upande wako hata ukamilifu wa dahari.
✓✓Hakikisha ROHO MTAKATIFU yuko upande wako na anakuongoza.
◼️Fanya sehemu yako kwa maombi na utakatifu ili MUNGU akamilishe ahadi zake kwako.
2 Wakorintho 1:20 "Maana ahadi zote za MUNGU zilizopo katika yeye ni Ndiyo; tena kwa hiyo katika yeye ni Amin; MUNGU apate kutukuzwa kwa sisi."
✓✓Usiwangoje wanadamu bali mngoje MUNGU ili akushindie.
✓✓Ndugu usiwangoje wanadamu maana wao wana mwisho.
✓✓Usiwangoje wanadamu maana hao hubadilika, usiwangoje wanadamu maana hao hawana uwezo wote, mngoje Bwana YESU na sio wanadamu.
2 Petro 3:9 " BWANA hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu ,............"
✓✓Ndugu mngoje MUNGU Baba wa mbinguni unayemwabudu na kuomba mbele zake KRISTO KRISTO.
Usiwahusudu wanaokukatisha tamaa wakati wewe unamtegemea JEHOVAH aliye hai.
✓✓Ndugu, endelea kumngoja BWANA huku ukiomba na huku ukiishi maisha matakatifu ya Wokovu wa KRISTO YESU.
nasema tena mngoje MUNGU maana mawakala wa shetani hawatakuabisha kamwe.
✓✓Wewe unayesubiri kupata mchumba mngoje MUNGU huku ukiendelea na maombi na maombezi.
✓✓Wewe unayesubiri kupata kazi mngoje MUNGU huku ukiendelea na maombi na maombezi.
✓✓Wewe unayesubiri mtoto katika ndoa yako mngoje MUNGU huku ukiendelea na maombi na maombezi.
✓✓Wewe ambaye ni yatima au mjane mngoje MUNGU huku ukiendelea na maombi na maombezi.
✓✓Wewe uliyesingiziwa mngoje MUNGU huku ukiendelea na maombi na maombezi.
✓✓Wewe unayeshindana na wenye nguvu mngoje MUNGU huku ukiendelea na maombi na maombezi.
◼️Kila uliye katika adha na umeokoka mngoje MUNGU huku ukiendelea na maombi na maombezi.
✓✓Mngoje MUNGU kwa hatua nyingine.
✓✓Mngoje Bwana YESU kwa viwango vingine.
◼️Jipe moyo na songa mbele maana saa itakuja ambapo wanadamu watakuita heri maana unamtegemea na kumtumaini Bwana YESU.
✓✓Hata kama marafiki zako wamekusaliti, hata kama ndugu zako wamekutenga, hata kama uliowapa siri zako wamegeuka na kuwa mwiba kwako, hata kama mchumba wako amedanganywa na kukuacha wewe kwa hila, hata kama mwenzi wako wa Ndoa ametekwa kipepo na mtu wa nje, wewe endelea mbele na YESU KRISTO, omba mbele za MUNGU na mngoje yeye kukushindia.
Mimi Peter Mabula nasukumwa sana kukuambia wewe uliyekusudiwa kwamba mngoje MUNGU huku ukiishi maisha matakatifu ya Wokovu.
✓✓Nasema tena mngoje YAHWEH MUNGU wa pekee wa kweli.
Zaburi 27:10-14 " Baba yangu na mama yangu wameniacha, Bali BWANA atanikaribisha kwake. Ee BWANA, unifundishe njia yako, Na kuniongoza katika njia iliyonyoka; Kwa sababu yao wanaoniotea; Usinitie katika nia ya watesi wangu; Maana mashahidi wa uongo wameniondokea, Nao watoao jeuri kama pumzi. Naamini ya kuwa nitauona wema wa BWANA Katika nchi ya walio hai. Umngoje BWANA, uwe hodari, Upige moyo konde, naam, umngoje BWANA."
◼️Kumbuka haya;.
✓✓Tumekombolewa kwa damu ya YESU KRISTO ya agano.
✓✓Tumenunuliwa kwa damu ya YESU KRISTO ya agano.
✓✓Tumeokolewa kwa damu ya YESU KRISTO ya agano.
✓✓Tumeinuliwa kwa damu ya YESU KRISTO ya agano.
✓✓Tumefunguliwa kwa damu ya YESU KRISTO ya agano.
◼️Tutafufuliwa pamoja na KRISTO Mwokozi wetu.
◼️Hao ni sisi tuliompokea YESU Kama Bwana na Mwokozi wetu na tunaishi maisha matakatifu katika yeye.
✓✓Damu ya YESU KRISTO ni ya thamani kuliko vyote duniani.
✓✓Tumenunuliwa na MUNGU kwa damu ya YESU KRISTO na sasa Kazi yetu ni kumtukuza MUNGU Muumbaji wetu.
1 Wakorintho 6:20 "maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni MUNGU katika miili yenu."
✓✓Sisi sio watumishi tena wa dhambi, sio sio watumwa tena, tuko huru kwa damu ya YESU KRISTO.
1 Wakorintho 7:23 " Mlinunuliwa kwa thamani; msiwe watumwa wa wanadamu."
◼️Baada ya duniani kitakachofuata kwetu ni uzima wa milele, hilo ndilo tumaini Leo la kudumu.
Ndugu ambaye hujampokea YESU nakuomba mpokee Leo.
◼️Sisi ni wateule wa MUNGU.
hata kama wakati mwingine duniani tutaonekana kama ni wajinga au wasio na maana(Isaya 35:8) lakini aliyeianzia kazi ndani yetu ni MUNGU wa mbinguni hivyo hatutapotea kamwe.
✓✓Aliko YESU na sisi tutakuwa hapo uzima wa milele.
◼️Kazi aliyotupa Bwana YESU sasa ni kuwaita watu wote waje kwake ili waupate uzima wa milele.
◼️Ndugu unayesoma Ujumbe huu naomba hakikisha KRISTO ni Bwana na Mwokozi wako.
Zingatia na MUNGU atakubariki sana.
Mche MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi na utaitwa heri.
Kama pia unatumia Facebook ni follow maana itafika kipindi nitakuwa napost tu katika page yangu na profile yangu.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292.
Ubarikiwe sana

Comments