![]() |
| Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.
◼️Katika huduma nne za kiutendaji kibiblia ambazo ni Mitume, Manabii, Wainjilisti, Wachungaji na Walimu, Biblia imezungumzia huduma itakayovamiwa na waongo wengi ya kwanza ni huduma ya kinabii, yaani mawakala wa shetani watakaojiingiza kwa siri katika huduma wengi wataingia katika huduma ya Kinabii.
2 Petro 2:1-3 '' Lakini kuliondokea manabii wa uongo katika wale watu, kama vile kwenu kutakavyokuwako waalimu wa uongo, watakaoingiza kwa werevu uzushi wa kupoteza, wakimkana hata Bwana(YESU) aliyewanunua, wakijiletea uharibifu usiokawia. Na wengi watafuata ufisadi wao; na kwa hao njia ya kweli itatukanwa. Na katika kutamani watajipatia faida kwenu kwa maneno yaliyotungwa; ambao hukumu yao tangu zamani haikawii, wala uvunjifu wao hausinzii.''
◼️Baada ya huduma ya Kinabii kuvamiwa na Mawakala wa shetani huduma inayofuata kuingiliwa na wapambe wa shetani ni huduma ya kitume.
Bwana YESU anasema '' Nayajua matendo yako, na taabu yako, na subira yako, na ya kuwa huwezi kuchukuliana na watu wabaya, tena umewajaribu wale wajiitao mitume, nao sio, ukawaona kuwa waongo; tena ulikuwa na subira na kuvumilia kwa ajili ya jina langu, wala hukuchoka. -Ufunuo 2:2-3 ''
◾Najiuliza sana kwanini huduma ya Kinabii ndio inaongoza kwa kuvamiwa na mawakala wa shetani kuliko huduma nyingine na sasa kila anayekua kiroho kidogo anataka ajiite nabii?
Mathayo 24:23-26. " Kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, kama yamkini, hata walio wateule. "
◾Je Baadhi wanatimiza maandiko ambayo yanasema kutakuwa na manabii wa uongo wengi?
Mathayo 24:11 '' Na manabii wengi wa uongo watatokea, na kudanganya wengi.''
◾Mtu hajawahi kuitwa na MUNGU ili amtumikie katika unabii, kwanini mtu huyo ajiite nabii?
✓[Ndugu zangu tukumbuke vyema kwamba maandiko mengi zaidi yanayozungumzia watakaojiingiza kwa siri katika huduma wengi ni manabii wa uongo.
◾Unajisikije kwamba ni wewe Nabii wa uongo?
Maana MUNGU hajawahi kukuambia uwe Nabii, unadanganya watu, humhubiri YESU KRISTO anayeokoa.
Wakati mwingine mimi nikiona mtandaoni mtu anajiita Nabii huwa naangalia post zake 10 na walio wengi kwenye post zao kuona neno ''YESU KRISTO Mwokozi'' ni nadra sana sana.
Na hata akimtaja YESU KRISTO ni katika mifano dhaifu au katika kama ushahidi tu kwamba na yeye ni Mkristo lakini hamjui mwenye Injili ambaye ni YESU KRISTO na hafuati kweli ya MUNGU zaidi sana mtu huyo anajihubiri yeye na sio kumhubiri YESU KRISTO.
2 Kor 4:5-6 '' Kwa maana hatujihubiri wenyewe, bali KRISTO YESU ya kuwa ni Bwana; na sisi wenyewe kuwa tu watumishi wenu kwa ajili ya YESU. Kwa kuwa MUNGU, aliyesema, Nuru itang'aa toka gizani, ndiye aliyeng'aa mioyoni mwetu, atupe nuru ya elimu ya utukufu wa Mungu katika uso wa YESU KRISTO.''
✓✓Ninayemkwaza yeyote naomba anisamehe ila kama wewe huwa unachunguza maandiko utagundua kwamba maandiko yanayowazungumzia manabii wa uongo ni mengi kuliko maandiko yanayowazungumzia mitume wa uongo, walimu wa uongo, wachungaji wa uongo au wainjilisti wa uongo, japokuwa na wao walio wa uongo wapo pia.
✓✓Wachungaji wa uongo wapo, kama ni wewe acha mara moja.
✓✓Walimu wa uongo wapo, kama ni wewe acha mara moja kuwa mwalimu wa uongo.
✓✓Wainjilisti wa uongo wapo japokuwa ni wachache sana, kama ni wewe acha mara moja.
✓✓Mitume wa uongo wapo wengi, kama ni wewe acha mara moja.
✓✓Manabii wa uongo ndio wengi zaidi sana, kama ni wewe acha mara moja.
◼️Ngoja nilitahadhalishe Kanisa.
✓✓Wakati mwingine ni vigumu kumjua Nabii wa uongo, maana shetani hufanya pia kazi kwa siri, lakini zingatia injπili ya KRISTO vyema utawajua, wakala wa shetani kazi yake ya kwanza ni kuwa kinyume na kweli ya MUNGU ambayo ni KRISTO.
Wakolosai 2:2b '' wapate kujua kabisa siri ya MUNGU, yaani, Kristo; ''
◼️Kazi ya kwanza ya shetani ni kumpinga YESU KRISTO, hivyo ukiona mtu anahusika zaidi na mambo mengine asiyo yaagiza YESU KRISTO ujue huyo kama sio mchanga kiroho basi ni nabii wa uongo.
Kusema tu Bwana haisaidii maana YESU Mwenyewe alisema sio wote wamwitao Bwana wataingia uzima wa milele.
✓✓Wakati mwingine miujiza huwaficha manabii wa uongo hata wasijulikane kama ni manabii wa uongo.
◼️Ndugu, kumbuka mfano huu kwamba Musa alikuwa ni Mtumishi safi wa MUNGU aliye hai, Musa alitupa fimbo yake ikageuka nyoka lakini na wachawi wa Misri nao walitupa fimbo zao zikawa nyoka.
Kutoka 7:10-12 '' Basi Musa na Haruni wakaingia kwa Farao, wakafanya vivyo kama BWANA alivyowaambia; Haruni akaibwaga fimbo yake chini mbele ya Farao, mbele ya watumishi wake, ikawa nyoka. Ndipo Farao naye akawaita wenye akili na wachawi; na hao waganga wa Misri wakafanya vivyo kwa uganga wao. Wakabwaga chini kila mtu fimbo yake, nazo zikawa nyoka; lakini fimbo ya Haruni ikazimeza fimbo zao ''
✓✓Hapa tunajifunza kwamba Musa na Haruni walifanya muujiza na mawakala wa shetani nao walifanya muujiza.
◼️Hivyo watumishi wa MUNGU katika KRISTO YESU hufanya miujiza lakini hata Mawakala wa shetani waliojiingiza kwa siri katika Kanisa hufanya miujiza vilevile.
◼️Kama kipimo chako cha kumtambua Mtumishi sahihi ni miujiza basi hata shetani hufanya miujiza hivyo chunga usiangukie katika mikono ya shetani na sio mikono ya YESU KRISTO.
2 Yohana 1:7 '' Kwa maana wadanganyifu wengi wametokea duniani, wasiokiri ya kuwa YESU KRISTO yuaja katika mwili. Huyo ndiye yule mdanganyifu na mpinga KRISTO.''
✓✓Kulikuwa na tofauti kidogo sana kati ya muujiza wa MUNGU alioufanya Musa na Haruni na muujiza wa shetani walioufanya wachawi na waganga wa Misri, nyoka wa Musa aliwameza nyoka wote wa Wachawi wa Misri, yaani tofauti ya miujiza hiyo ilikuwa kidogo sana, ndivyo ilivyo kwa Nabii wa kweli na nabii wa uongo, tofauti ya utendaji kazi au miujiza inaweza kuwa kidogo sana lakini mmoja ni Nabii wa MUNGU na mwingine ni mpambe wa shetani anayehadaa watu.
✓✓Uwe makini sana ndugu mana manabii wa uongo Kibiblia kabisa watakuwa wengi sana, uwe makini sana.
'' Mkijua kwanza neno hili ya kwamba katika siku za mwisho watakuja na dhihaka zao watu wenye kudhihaki, wafuatao tamaa zao wenyewe,-2 petro 3:3''
◼️Ninaposema haya sio kwamba Manabii wa kweli hawapo bali wapo wengi ila Biblia pia inasema kwamba manabii wa uongo pia ni wengi sana hivyo unahitajika umakini sana.
Sasa watu wengi zaidi hukimbilia kwa manabii wa uongo.
✓✓Manabii wa uongo huwafanya watu kudumaa kiroho.
✓✓Manabii wa uongo huwafanya watu wasimtii YESU KRISTO Mwokozi.
Manabii wa uongo huwafanya watu waipende dunia na machukizo yake na sio kumpenda MUNGU.
1 Yohana 2:15-17 '' Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba(MUNGU) hakumo ndani yake. Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba(MUNGU), bali vyatokana na dunia. Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya MUNGU adumu hata milele.''
✓✓Manabii wa uongo husema uongo ili kuwadanganya watu.
✓✓Manabii wa uongo wanaweza kuwa na ishara na miujiza mingi ila ni miujiza ya kishetani maana ni shetani ndiye aliyewatuma ili kuhakikisha watu hawamtii KRISTO an akupata uzima wa milele.
Kumbu 13:1-3 '' Kukizuka katikati yako nabii, au mwotaji wa ndoto, akikutolea ishara au ajabu, ikatukia hiyo ishara au hiyo ajabu aliyokuambia akisema, Na tuifuate miungu mingine usiyoijua, tuitumikie hiyo; wewe usiyasikize maneno ya nabii yule, au yule mwotaji wa ndoto, kwa kuwa BWANA, Mungu wenu, yuawajaribu, apate kujua kwamba mwampenda BWANA, Mungu wenu, kwa mioyo yenu yote na roho zenu zote. ''
◾Kwa njia gani manabii wa uongo huhakikisha watu hawamtii KRISTO?
✓✓Kwa kuwafanya watu wawaamini wao na sio kumwamini MUNGU.
✓✓Kuwafanya watu wategemee maji ya upako, mafuta ya upako, maji ya baraka, chumvi ya upako n.k na sio kumtegemea YESU KRISTO tena.
✓✓Ndio maana leo kuna makanisa watu wameenda hapo wengi sana ili watabiriwe gari, kiwanja, nyumba n.k
✓✓Watu wale hawajaenda pale ili watubu dhambi na kuziacha, hawajaenda pale ili waokoke na wabadilike mienendo kutoka mienendo mibaya kuwa mienendo misafi iwapasao waliookoka.
◼️Ndugu yangu, unamhitaji YESU KRISTO kwa ajili ya uzima wa milele kwanza.
Zingatia na MUNGU atakubariki sana.
Mche MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi na utaitwa heri.
Kama pia unatumia Facebook ni follow maana itafika kipindi nitakuwa napost tu katika page yangu na profile yangu.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292.
Ubarikiwe sana

Comments