![]() |
| Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu zangu wote.
Karibuni sana tujifunze Neno la MUNGU.
✓✓Leo nazungumzia Amani ya MUNGU ndani ya Mteule wa KRISTO.
◼️Amani ya MUNGU ni nini?
◾Amani ya MUNGU ni hali ya Uhuru na usalama rohoni anayokupa MUNGU ikiwa unamcha MUNGU.
✓✓Amani ya MUNGU hukaa tu kwa Wateule wa KRISTO.
✓✓Amani ya MUNGU kwetu Kanisa hai ni baraka ya MUNGU kwetu.
Zaburi 29:11 "BWANA atawapa watu wake nguvu; BWANA atawabariki watu wake kwa amani."
✓✓Amani ya MUNGU huja kwa sababu ya mtu husika analishika Neno la MUNGU na kulizingatia siku zote, Neno la MUNGU ndio chanzo cha amani ya MUNGU ndani ya Mteule wa KRISTO.
Zaburi 119:165 "Wana amani nyingi waipendao sheria yako, Wala hawana la kuwakwaza."
✓✓Unaweza kuwa na amani na mtu kwa sababu tu mtu huyo kakupa kitu fulani kizuri, lakini amani ya MUNGU haina mipaka.
◼️Ndio maana MUNGU wetu anaitwa MFALME WA AMANI(Isaya 9:6)
◼️Tena MUNGU wetu anaitwa MUNGU WA AMANI.
Warumi 15:33 "MUNGU wa amani na awe pamoja nanyi nyote. Amina. "
Je unaitaka amani ya MUNGU ndani yako?
◼️Okoka na mtegemee MUNGU na kumtumainia yeye na atakupa amani timilifu.
Isaya 26:3 "Utamlinda yeye ambaye moyo wake umekutegemea Katika amani kamilifu, kwa kuwa anakutumaini."
◼️Mtu mwenye amani ya MUNGU ni Mkristo yule aliyeokoka na anamjua MUNGU sana.
Ayubu 22:21 "Mjue sana MUNGU, ili uwe na amani; Ndivyo mema yatakavyokujia."
✓✓Amani ya MUNGU ndio hufanya maamuzi sahihi moyoni mwako Mteule wa KRISTO.
✓✓Amani ya MUNGU kwa jina lingine inaitwa amani ya KRISTO, na hiyo hutusaidia katika maamuzi.
Kazi za amani ya MUNGU ndani ya mtu.
1. Kumsaidia kuamua jambo jema.
Wakolosai 3:15″ Na amani ya KRISTO iamue mioyoni mwenu; ndiyo mliyoitiwa katika mwili mmoja tena iweni watu wa shukrani."
2. Amani ya MUNGU hutuondolea mfadhaiko na uoga.
Yohana 14: 27 "Amani yangu nawaachieni; amani yangu nawapa;niwapavyo mimi si kama ulimwengu utoavyo.Msifadhaike mioyoni mwenu wala msiwe na woga"
3. Amani ya MUNGU hutuhifadhi mioyo yetu na nia zetu katika KRISTO YESU Mwokozi wetu.
Wafilipi 4:7 " Na amani ya MUNGU , ipitayo akili zote , itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika KRISTO YESU."
4. Amani ya MUNGU inaweza kumuongoza mtu kuliendea jambo jema.
Isaya 55:12 "Maana mtatoka kwa furaha, Mtaongozwa kwa amani; Mbele yenu milima na vilima vitatoa nyimbo; Na miti yote ya kondeni itapiga makofi."
◼️Ndugu ihitaji sana amani ya MUNGU.
1. Kor 1:3 "Neema na iwe kwenu na amani, zitokazo kwa MUNGU Baba yetu, na kwa Bwana YESU KRISTO."
Zingatia na MUNGU atakubariki sana.
Mche MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi na utaitwa heri.
Kama pia unatumia Facebook ni follow maana itafika kipindi nitakuwa napost tu katika page yangu na profile yangu.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292.
Ubarikiwe sana

Comments