Baadhi ya shuhuda.

Na Mwl Peter Mabula 
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi 



Baadhi ya shuhuda.

1. Bwana Yesu asifiwe Mtumishi wa Mungu nabarikiwa sana na mafundisho yako Mungu akiniwezesha nitakutafuta nifike kanisani kwako.
Pia ninao ushuhuda kidogo kuna siku nilikushirikisha hitaji Langu kuhusu kuolewa na jinsi ilivyokuwa ikitokea kila Mara uchumba unakatika pia nikaona ndoto ambayo ilionesha mtihani ambao si kumaliza ndipo nikakushirikisha ukaniambia nimsikilize sana Roho mtakatifu na kuishi maisha matakatifu, nilifanya hivyo na namshukuru Mungu ule mtihani ambao kwenye ndoto sikuumaliza Mungu alitumia muhubiri alipokuwa anafundisha nikawa napokea majibu. Kumbe tatizo ilikuwa ni mimi sitaki kuolewa na watumishi wa MUNGU na kweli nilikuwa siwapendi kabisa nikatambua kuwa ndo tatizo nilipotengua nikaona njia ingawa sijamuona kimwili ila Mungu ameishanijulisha na akanionesha ni mtumishi.
Namshukuru MUNGU sana na
MUNGU akubariki sana Mtumishi.

2. Bwana YESU asifiwe Mtumishi.
Namshukuru MUNGU kwa muujiza ariotenda kwa mwanangu sana ivi hasumbui usiku tena tangu siku ile umeniombea. Na Mimi kwa sasa naendelea vyema na nimeshaanza kujua kuomba kwani usiku nalala ikifika usiku sana naomba maombi yako uliyoelekeza YA KUOMBEA FAMIRIA UKOO NA NYUMBA. UBARIKIWE SANA KWA MAFUNDISHO YAKO NA MAOMBI

3. BWANA YESU ATUKUZWE NA KUPEWA SIFA MILELE, MTUMISHI WA MUNGU KATIKA KRISTO YESU BWANA WETU. Namshukuru MUNGU sana kwa maajabu aliyonitendea jana, kwa kumponya mke wangu. baada ya maombi ambayo ulimuombea ndipo nikampigia simu akasema hasikii maumivu ya kichwa wala mgongo wala miguu kuwaka moto. namtukuza KRISTO kwa hilo Mtumishi maana wakati ukiwa unaomba nikawa nasikia furaha sana moyoni mwangu hata mimi nilikuwa nikimuwaza tu mke wangu nasikia maumivu moyoni lakini baada ya maombi yako tulipokea uponyaji mimi na mke wangu. Kwa kweli MUNGU AENDELEE KUKUTUMIA KWA VIWANGO ALIVYOVIKUSUDIAAKUTUMIE.
UBARIKIWE SANA.

4. Bwana asifiwe mtumishi Peter, Shikamoo,
samahan kwa huu usumbufu mtumishi, Mimi ndo yule kijana uliye niombeaga katika simu siku za nyuma kidogo kama mwezi mzima na wiki mbili zimepita lile tatizo la kujichua halinisumbui tena kwa sababu nikuwa nikisoma biblia na kupenda uwepo wa MUNGU Kwangu muda mwingi, na pia mimi ni mfatiliaji wa masomo yako uyafundishayo fb, "sasa nakumbuka ulifundsha kuhusu ndoto mbaya za kuota unafanya mapenzi na mtu alafu kushtuka unakuta kumbe ni ndoto, SASA HIYO HALI TOKEA NIMEKATAA NGUVU ZA GIZA ZILIZOPELEKEA HADI NAJICHUA, NA HIZO NDOTO MBAYA ZIMETOWEKA.

Hizi no baadhi ya shuhuda za marafiki zangu ambao walisoma masomo yangu mtandaoni na wengine walinipigia simu niwaombee pale nafasi ilipopatikana ya maombi.
Nimepost kama walivyonitumia.
Namrudishia sifa, utukufu na adhama MUNGU Baba wa mbinguni.
Ndugu, nakushauri endelea na YESU Mwokozi, endelea na maombi na ishi maisha matakatifu ya Wokovu siku zote.
Ubarikiwe sana.
By Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la MUNGU.

Comments