BIBLIA NDIO KITABU PEKEE KINACHOZUNGUMZIA MAMBO YA NYAKATI ZOTE.

Na Mwl Peter Mabula 
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi 



Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe Ndugu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU wa Mbinguni.

◼️Biblia Takatifu ndio Kitabu pekee Cha MUNGU wa Mbinguni.

✓✓Biblia Ndio kitabu pekee kinachozungumzia Mambo ya nyakati zote.

◼️Hii Ina maana kwamba Biblia inazungumzia Mambo ya Nyakati zilizopita, inazungumzia pia Mambo ya Nyakati zilizopo sasa na inazungumzia pia Mambo ya Nyakati zijazo.

Ufunuo 1:19 '' Basi, uyaandike mambo hayo uliyoyaona, nayo yaliyopo, na yale yatakayokuwa baada ya hayo.''

✓✓Andika hili linaonyesha mambo yaliyopita, Mambo yaliyopo na mambo yajayo. Hayo yote yalitakiwa kuandikwa kama Malaika anavyoelekeza kwa Mtume Yohana.

◼️Hii maana yake Yako mambo ya zamani MUNGU anataka tuyajue ili tujifunze kitu Cha kutusaidia katika Wakati wetu huu wa Sasa, mambo ya zamani baadhi yamebeba mifano kwetu ili tusikosee katika Wakati wetu.

1 Kor 10:6-11 ''Basi mambo hayo yalikuwa mifano kwetu, kusudi sisi tusiwe watu wa kutamani mabaya, kama wale nao walivyotamani. Wala msiwe waabudu sanamu, kama wengine wao walivyokuwa; kama ilivyoandikwa, Watu waliketi kula na kunywa, kisha wakasimama wacheze. Wala msifanye uasherati, kama wengine wao walivyofanya, wakaanguka siku moja watu ishirini na tatu elfu. Wala tusimjaribu BWANA, kama wengine wao walivyomjaribu, wakaharibiwa na nyoka.
Wala msinung'unike, kama wengine wao walivyonung'unika, wakaharibiwa na mharabu. Basi mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa ili kutuonya sisi, tuliofikiliwa na miisho ya zamani. ''

✓✓Mambo ya Nyakati zilizopita yanatufundisha juu ya wenzetu walifanyaje ili kumpendeza MUNGU.

✓✓Mambo ya Nyakati zilizopita yanatufundisha pia juu ya makosa ya watu walioishi katika Nyakati hizo ila sasa sisi tusitembee katika makosa hayo.

✓✓Walioishi wakati uliopita makosa yao yameandikwa ili kutufanya sisi tusitembee katika makosa kama wao.

✓✓Biblia hapo kwa ufupi inataja baadhi ya makosa ya wakati uliopita ikisema, wapo waliotamani mabaya, walikuwa waabudu sanamu, walikuwepo waasherati na wapo waliomjaribu MUNGU na wote waliofanya makosa hayo waliadhibiwa na MUNGU hivyo tumejulishwa juu ya tabia zao mbaya ili sisi tusitembee katika ubaya kama huo.

◼️Biblia pia inazungumzia habari za siku zijazo,  siku za mwisho na siku ya mwisho.

Waebrania 10:27 '' bali kuna kuitazamia hukumu yenye kutisha, na ukali wa moto ulio tayari kuwala wao wapingao. ''

✓✓Biblia hapa inaposema "Kuna kuitazamia hukumu" maana huo muda wa hiyo hukumu bado haujafika ila wakati wake utafika.

✓✓ Hivyo katika  nyakati zijazo jambo kubwa ni Nyakati za mwisho na kisha kurudi kwa Bwana YESU mara ya pili na kisha siku ya hukumu.

✓✓Katika wakati huu hakika tuko katika siku za mwisho.

✓✓Na wakati huu wa siku za mwisho utaendelea hadi Bwana YESU KRISTO anarudi Kumlipa kila mwanadamu kama matendo yale yalivyokuwa alipokuwa anaishi duniani, ndio wakati huu wa siku za mwisho utafika mwisho.

Mithali 24:12 "Ukisema, Sisi hatukujua hayo; Je! Yeye aipimaye mioyo siye afahamuye? Naye ailindaye nafsi yako siye ajuaye? Je! Hatamlipa kila mtu sawasawa na kazi yake?"

✓✓Katika siku ya mwisho tukio kubwa ni Moja tu Bwana YESU KRISTO akija kuwahukumu Wanadamu wote.

Mathayo 25:31-33" Hapo atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu wake, na malaika watakatifu wote pamoja naye, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake;  na mataifa yote watakusanyika mbele zake; naye atawabagua kama vile mchungaji abaguavyo kondoo na mbuzi; atawaweka kondoo mkono wake wa kuume, na mbuzi mkono wake wa kushoto."

✓✓Tukio kubwa siku ya mwisho ni kila Mwanadamu aliyewahi kuishi Duniani ama Mwanadamu huyo aende uzima wa milele au aende jehanamu milele.

✓✓Katika wakati huu tulionao dalili zote za siku za mwisho zimeshatokea.

◼️ Nyakati nyingine inayozungumzwa na Biblia ni Nyakati iliyopo.

✔️✔️Katika Nyakati hii iliyopo Mambo makuu Muhimu 4 Muhimu haya.

1. Kuokoka.

2 Wakorintho 6:2 (Kwa maana asema, Wakati uliokubalika nalikusikia, Siku ya wokovu nalikusaidia;tazama,wakati uliokubalika ndiyo sasa; tazama siku ya wokovu ni sasa)

2. Kuishi katika ROHO MTAKATIFU.

Wagalatia 5:16 "Basi nasema, Enendeni kwa ROHO, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili."

3. Kumwabudu MUNGU katika Roho na kweli.

Yohana 4:23-24 " Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu BABA katika roho na kweli. Kwa maana BABA awatafuta watu kama hao wamwabudu. MUNGU ni ROHO, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli."

✓✓Wakati wetu huu kiroho unaitwa wakati wa Ibada yaani wakati wa kumwabudu MUNGU Baba katika kweli yake. Na kweli yake ni Kumpokea YESU KRISTO na kuishi katika ROHO MTAKATIFU.

4. Kujihadhari na waongo ili wasitutoe katika Wokovu wa KRISTO YESU Mwokozi wetu.

Mathayo 24:25 "Tazama, nimekwisha kuwaonya mbele."

✓✓Aliposema  "nimekwisha kuwaonya mbele." Maana yake anatutahadharisha ili katika Wakati wetu tusinaswe na waongo ambao sharti waje.

◼️Waongo hawa ni akina nani ili tujihadhari nao.

Baadhi ya waongo ni hawa hapa.

1. Wanaofundisha mafundisho ya shetani.

1 Timotheo 4:1 "Basi ROHO anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani;"

✓✓Wanaofundisha mafundisho ya mashetani ni wale wote walioanzisha dini zote zilizo kinyume na Wokovu wa KRISTO.
✓✓Wanaofundisha mafundisho ya mashetani ni wale wote waliotumwa na shetani kuwatoa watu katika Wokovu wa KRISTO kwa mafundisho yao ya uongo.

✓✓Hawa kwa Jina lingine wanaitwa wapinga KRISTO.

1 Yohana 2:18 ''Watoto, ni wakati wa mwisho; na kama vile mlivyosikia kwamba mpinga Kristo yuaja, hata sasa wapinga Kristo wengi wamekwisha kuwapo. Kwa sababu hiyo twajua ya kuwa ni wakati wa mwisho.''

Biblia katika Wakati wetu inatutaka sana tujihadhari na watu wa aina hii.

2. Manabii wa uongo.

Mathayo 24:11 "Na manabii wengi wa uongo watatokea, na kudanganya wengi."

✓✓Kazi ya Nabii wa uongo ni kudanganya.
Hawa Manabii wa uongo YESU anatutaka tujihadhari nao sana.

◼️Bwana YESU KRISTO katika Wakati uliopita alisema juu ya wakati wetu kwamba tujihadhari na waongo ili wasitutoe katika Wokovu wake.

◼️Huu pia  kibiblia unaitwa wakati wa neema, kwamba ni wakati wa  maamuzi binafsi ya mtu kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi au kukataa.

✔️✔️Biblia iko wazi sana juu yao wanaompokea Bwana YESU kama Mwokozi wao na pia Biblia ipo wazi sana juu ya wanaomkataa YESU kuwa Mwokozi wao.

Yohana 3;16-18 '' Kwa maana jinsi hii MUNGU aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana MUNGU hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa MUNGU.''

✓✓Ndugu, ukiwa unaishi katika wakati huu naomba utambue kwamba kama ilivyokuwa kuzaliwa mara moja basi kuna kufa mara moja tu.

✓✓Wanaompinga YESU KRISTO na Wokovu wake wanasubiri hukumu ya kutisha, ni hatari sana.

Mtu akifa hakuna anayeweza kumuombea ili atoke kuzimu na aende paradiso, bali baada tu ya kifo kuna hukumu yaani kila mmoja anaenda kunakomstahili, kama ni Mbinguni anaenda na kama ni jehanamu ataenda, jalada lake linafungwa na halitafunguliwa kamwe.

Waebrania 9:27 '' Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu; ''

✓✓Baada ya kifo ni ama itafuata kwako mbingu mpya yenye uzima wa milele katika KRISTO YESU ama itafuata jehanamu ya moto.

◼️Naomba usitembee kwenye makosa ya watu wa zamani bali jifunze Biblia ili utembee tu kwenye yale yanayompendeza MUNGU.

✓✓Usipompokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako na ukaanza kuishi maisha matakatifu ya Wokovu ni  kwamba uzima wa milele hautakuhusu kamwe, ndugu nafasi bado ipo hivyo mpokee YESU KRISTO kama Mwokozi wako na kisha jiunge na Kanisa la kiroho ili uukulie Wokovu na kuanzia sasa anza kuishi maisha matakatifu.
Zingatia  na MUNGU atakubariki sana.
Mche MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi na utaitwa heri.
Kama pia unatumia Facebook ni follow maana itafika kipindi nitakuwa napost tu katika page yangu na profile yangu.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter  Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292(Ushauri, Maombezi, Whatsapp n.k)
Share ujumbe huu kwenye magroup ya Whatsapp uliyopo.
Ubarikiwe

Comments