![]()  | 
| Na Mwl Peter Mabula  Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi  | 
Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe Ndugu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.
◼️Kuna vifungo vya kipepo vinaweza kumtesa Mtu muda mrefu na vifungo vimeletwa na ndugu zake.
◾Jifunze somo ili kama Kuna kifungo Cha kiroho kinakutesa kinachotokana na ndugu zako kiharibu Leo hicho kwa Maombi katika Jina la YESU KRISTO na utakuwa huru kabisa.
✓✓Kuna ndugu zako wa aina nyingi.
✓✓Kuna ndugu wa kuzaliwa, mnaotoka familia moja, mnaotoka ukoo mmoja, mnaotoka eneo moja, wazazi wako na mababu zako.
✓✓Hata mnaosali nao ni ndugu zako, hata wafanyakazi wenzako hao ni kama ndugu zako.
✓✓Hakuna mtu duniani amewahi kuishi pekeyake tangu kuzaliwa kwake.
✓✓Kumbuka ulimi unaumba na wako watu ulimi wa baadhi ya ndugu zao ulinena mabaya na kuwafunga vifungo vinavyowatesa sasa.
◼️Kumbuka katika ulimi yaani maneno yake kunaweza kutoka uzima au mauti.
Mithali 18:21 "Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; Na wao waupendao watakula matunda yake."
◾Je ndugu zako walikunenea mauti ya nini?
✓✓Je walikunenea mauti ya uchumba wako au biashara yako?
✓✓Je walikunenea mauti ya uzao au akili?
✓✓Je walikunenea mauti ya ndoa ili ndoa yako ivunjike?
✓✓Je walikunenea mauti ya nini?
✓✓Je mauti walizokunenea huwa unazifuta kwa Maombi?
✓✓Je ni mauti ipi
 walikunenea na hujaifuta ndio maana inakutesa?
✓✓Je unadhani ndugu yako au watu wako wa karibu walikuwa wanakunenea mema tu?
◼️Ona mfano huu, huyu ni Daudi aliyekuwa ameokoka wakati mwingine kuliko wewe lakini anasema " Kwa maana aliyetukana si adui; Kama ndivyo, ningevumilia. Aliyejitukuza juu yangu siye anichukiaye; Kama ndivyo, ningejificha asinione. Bali ni wewe, mtu mwenzangu, Rafiki yangu, niliyejuana nawe sana.
Tulipeana shauri tamu; na kutembea Nyumbani mwa MUNGU pamoja na mkutano.-Zaburi 55:12-14
✓✓Ndugu, mtu wako wa karibu sana anaweza kuwa ndio chanzo cha mateso yako na vifungo vya kiroho kwako.
Ngoja nikupe mifano hai.
1. Yusufu aliuzwa na ndugu zake ili awe mtumwa.
Mwanzo 37:27-28 " Haya, na tumwuze kwa hawa Waishmaeli, wala mikono yetu isimdhuru, maana yeye ni ndugu yetu, na damu yetu. Ndugu zake wakakubali. Wakapita wafanya biashara Wamidiani; basi wakamtoa Yusufu, wakampandisha kumtoa katika birika, wakamwuza Yusufu kwa Waishmaeli kwa vipande vya fedha ishirini; nao wakamchukua Yusufu mpaka Misri."
✓✓Je ndugu zako kwa laana zao na maneno yao wamekuuza ili uwe nani?
✓✓Je walikunenea maneno mabaya ili usitulie katika ndoa yako au usizae?
✓✓Je walikunenea maneno mabaya ili usifanikiwe kimaisha au ukipata kazi ufukuzwe?
◼️Ndugu Leo unayo nafasi ya maombi ili kujivua katika laana na vifungo ulivyofungwa na watu wako wa karibu.
Bwana YESU yuko tayari kukusaidia kuanzia sasa.
2. Reubeni aliondolewa ukuu na mzazi wake kwa makosa yake.
Mwanzo 49:3-4 " Reubeni, u mzaliwa wangu wa kwanza, Nguvu zangu, na malimbuko ya uwezo wangu. Umewapita wengine kwa ukuu na kwa nguvu. Umeruka mpaka kama maji, basi usiwe na ukuu, Kwa sababu ulikipanda kitanda cha baba yako, Ukakitia unajisi; alikipandia kitanda changu."
✓✓Inawezekana ulimkosea mzazi wako na akakulaani, laana hiyo inakutesa, je nani akusaidie?
◼️Ndugu mkimbilie YESU KRISTO ili akukomboe na laana zote.
✓✓Inawezekana ulipokuwa Mtoto mdogo tu ulichelewa kufika nyumbani tu lakini ulitamkiwa maneno mabaya sana na yamekuwa laana inayokushikilia, ndugu unamhitaji Bwana YESU KRISTO ili upone.
Nini ufanye kwenye maombi ya kufuta vifungo vya giza vilivyokupata kwa kusababishiwa na ndugu au watu wako wa karibu ulioishi nao?
1. Tubu kwa ajili ya aliyekufunga.
Matendo 3:19 "Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake BWANA;"
2. Ita ukamilifu wa MUNGU ule ulioumbwa nao.
Mwanzo 1:31 "MUNGU akaona kila kitu alichokifanya, na tazama, ni chema sana. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya sita."
✓✓Inawezekana maneno yao mabaya ndio yamekufanya uwe kituko uliyekataliwa.
 ✓✓Kumbuka MUNGU hakukuumba na roho ya kukataliwa wala hakukuumba na vifungo vya giza, ukirudisha kwa Maombi uumbaji wa MUNGU kwako vifungo vinaondoka.
3. Futa vifungo vya giza ulivyofungwa na ndugu zako au watu wako wa karibu ulioishi nao.
Yohana 14:13 "Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba(MUNGU) atukuzwe ndani ya Mwana(YESU KRISTO).
4. Jibarikie mema kimaombi.
Hesabu 6:24-26 "BWANA akubarikie, na kukulinda; BWANA akuangazie nuru za uso wake, na kukufadhili; BWANA akuinulie uso wake, na kukupa amani."
5. Haribu na kufuta madhabahu za giza za familia au ukoo au eneo ulikofungwa kipepo.
Kumbu 7:5 "Lakini watendeni hivi; zivunjeni madhabahu zao zibomosheni nguzo zao, yakateni maashera yao, ziteketezeni kwa moto sanamu zao za kuchonga."
Zingatia  na MUNGU atakubariki sana.
Mche MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi na utaitwa heri.
Kama pia unatumia Facebook ni follow maana itafika kipindi nitakuwa napost tu katika page yangu na profile yangu.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter  Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292.
Ubarikiwe sana 

Comments