![]() |
| Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu zangu wote.
Karibu sana tujifunze matumizi sahihi ya Neno la MUNGU.
◼️Neno la MUNGU ndio sauti ya MUNGU, ndugu itii sauti ya MUNGU.
Isaya 40:8 "Majani yakauka, ua lanyauka; Bali neno la MUNGU wetu litasimama milele."
Mithali 30:5 "Kila neno la MUNGU limehakikishwa; Yeye ni ngao yao wamwaminio."
◼️Neno la MUNGU kwa jina lingine linaitwa Neno la KRISTO , lifanyie kazi katika maisha yako yote.
Wakolosai 3:16" Neno la KRISTO na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia MUNGU kwa neema mioyoni mwenu."
✓✓Ili ushinde dhidi ya nguvu za giza ni lazima uliamini Neno la KRISTO na likiri Neno hilo kwa kinywa chako.
Warumi 10:10" Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu."
Hatua 7 za matumizi sahihi ya Neno la MUNGU.
1. Omba YESU KRISTO akupe ufahamu wa kulielewa Neno la MUNGU.
Luka 24:45 "Ndipo akawafunulia akili zao wapate kuelewa na maandiko."
✓✓Hawa hawakuelewa maandiko ya Neno la MUNGU mpaka akili zao zilipofunuliwa kujua.
✓✓Kumbe unaweza ukasoma Biblia na usielewe MUNGU anazungumza Nini kuhusu Wewe, Unahitaji kufunuliwa akili Yako na Bwana YESU KRISTO ili uelewe.
✓✓Unaweza ukasoma Biblia na usielewe Neno la MUNGU hata ukizingatia ukaisamilisha roho Yako, mfano ni Wapinga KRISTO ambao husoma husoma Biblia kila mara lakini akili zao haijawahi kufunuliwa hata wakatambua kwamba bila YESU KRISTO hawawezi kuingia Uzima wa milele hivyo wanapata akili ya Kumpokea, wengi wanaishia kuisoma tu Biblia ila kuelewa hawajawahi kuelewa kusudi la MUNGU.
2. Taka sana maongozo ya ROHO MTAKATIFU.
Yohana 14:26" Lakini huyo Msaidizi, huyo ROHO MTAKATIFU, ambaye Baba(MUNGU) atampeleka kwa jina langu(YESU KRISTO), atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia."
✓✓Kazi mojawapo ya ROHO MTAKATIFU ni kutufundisha kwa Neno la MUNGU, kama humhitaji ROHO MTAKATIFU ujue huwezi kuelewa Neno la MUNGU kwa usahihi.
✓✓Kazi mojawapo ya ROHO MTAKATIFU ni kutukumbusha, anakukumbusha kutokea kwenye Neno lake.
Hivyo Ukitaka ujue Matumizi sahihi ya Neno la MUNGU Mhitaji sana ROHO MTAKATIFU akusaidie.
3. Tafuta kuelewa kwa usahihi maandiko unayosoma.
Matendo 8:30-31 " Basi Filipo akaenda mbio, akamsikia anasoma chuo cha nabii Isaya; akanena, Je! Yamekuelea haya unayosoma? Akasema, Nitawezaje kuelewa, mtu asiponiongoza? Akamsihi Filipo apande na kuketi pamoja naye."
✓✓Towashi wa Ethiopia alikuwa anasoma Maandiko ila haelewi kwa Neema ya MUNGU Filipo akatokea ili kumsaidia.
✓✓Hii hata kwako leo kwa sehemu ya maandiko ambayo huielewi shirikisha Watumishi waaminifu wa Bwana YESU watakusaidia hivyo utajua Matumizi sahihi ya Neno la MUNGU.
4. Iache Biblia ionyeshe msimamo wa ki MUNGU, usipotoe maandiko.
2 Petro 3:15-17 " Nanyi uhesabuni uvumilivu wa Bwana wetu kuwa ni wokovu, kama vile na ndugu yetu mpenzi Paulo alivyowaandikia kwa hekima aliyopewa; vile vile kama katika nyaraka zake zote pia, akitoa humo habari za mambo hayo; katika nyaraka hizo yamo mambo ambayo ni vigumu kuelewa nayo; na mambo hayo watu wasio na elimu, wasio imara, huyapotoa, kama vile wayapotoavyo na maandiko mengine, kwa uvunjifu wao wenyewe. Basi, wapenzi mkitangulia kujua hayo, jilindeni nafsi zenu, msije mkachukuliwa na kosa la hao wahalifu mkaanguka na kuuacha uthibitifu wenu."
✓✓Watu wengi husoma Biblia kwa mtazamo wa dhehebu lao au itikadi zao, kwa njia hiyo huwezi kuelewa Biblia na hutaweza kujua kusudi la MUNGU hata utembee kwenye kusudi hilo
Mfano hai Kuna Mtu Kuna Mtu Kanisani kwao wamekatazwa kujazwa ROHO MTAKATIFU na Kunena kwa lugha, Mtu kama huyo akisoma Biblia sehemu inayoonyesha umuhimu wa Kunena kwa lugha hataelewa maana Msimamo wa dhehebu lake unakataa, Mtu kama huyo anaweza hata kuruka maandiko yanayozungumzia ROHO MTAKATIFU hivyo hataelewa kwa usahihi Neno la MUNGU wa Mbinguni.
✓✓Kuna misimamo ya dhehebu sio ya MUNGU Bali ya adui, hivyo usisome Biblia Ukiwa na Msimamo wako binafsi, soma Neno la MUNGU Ukiwa huna Msimamo wa watu Wala dhehebu.
✓✓Mfano Kuna Mtu dhehebu lake linakataa Wokovu wa KRISTO, huyu hatasoma habari za Wokovu wa KRISTO hivyo anaweza kujikuta anakosa ufalme wa MUNGU kwa sababu alifuata misimamo ya kishetani iliyoingia kwa Siri katika dhehebu lake.
5. Chunguza maisha yako ikiwa umeasi agizo lolote la MUNGU la jinsi ya KRISTO tubu na rudi kwenye maagizo ya MUNGU.
Ufunuo 2:5 " Basi, kumbuka ni wapi ulikoanguka; ukatubu, ukayafanye matendo ya kwanza. Lakini, usipofanya hivyo, naja kwako, nami nitakiondoa kinara chako katika mahali pake, usipotubu."
✓✓Neno la MUNGU ndio taa inayotumulikia hata tujitambue, Ukisoma Neno la MUNGU likakupa kujua kosa lako tubia kosa hilo na kukiacha haraka.
✓✓Matumizi sahihi ya Neno la MUNGU ni pamoja na Kufuata maonyo ya Neno la MUNGU.
6. Tembea katika imani ya KRISTO YESU daima.
Waefeso 2:8-10 " Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha MUNGU; wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu. Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika KRISTO YESU, tutende matendo mema, ambayo tokea awali MUNGU aliyatengeneza ili tuenende nayo."
✓✓Kiini Cha Neno la MUNGU ambalo ni Biblia ni Mwanadamu ampokee YESU KRISTO kama Mwokozi na Kuokoka.
Hivyo Matumizi sahihi ya Neno la MUNGU ni pamoja na Mtu kulisoma na kujua inampasa Kuokoka Kisha anaamua Kumpokea YESU KRISTO na Kuokoka.
7. Rudia rudia kila mara kulisoma Neno la MUNGU hata ambalo ulishalisoma ili ROHO MTAKATIFU akusaidie kuelewa zaidi.
Yoshua 1:8 "Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana."
✓✓Anayefaulu katika Neno la MUNGU kulielewa na kukufanyia kazi ni Mtu yule anayelisoma mara kwa mara katika jinsi ya KRISTO na kuongozwa na ROHO MTAKATIFU katika Maisha yake.
Ndugu, Usiwe unasoma Neno la MUNGU kwa miezi mara Moja Bali soma kila siku ndio utaelewa sana na ukifanyia kazi Neno la MUNGU utafanikiwa sana.
◼️Tafakari Neno la MUNGU usiku na mchana.
Zingatia na MUNGU atakubariki sana.
Mche MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi na utaitwa heri.
Kama pia unatumia Facebook ni follow maana itafika kipindi nitakuwa napost tu katika page yangu na profile yangu.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292.
Ubarikiwe sana

Comments