KAZI ZA MLINZI WA KIROHO.

Na Mwl Peter Mabula 
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi 




Bwana YESU KRISTO Atukuzwe ndugu zangu.
Karibu nikujuze jambo muhimu.

◼️Wateule wa KRISTO walio waombaji ni walinzi wa kiroho.

✓✓Waalimu wa Neno la kweli la MUNGU katika KRISTO YESU nao ni walinzi wa kiroho.

Ezekieli 33:7 "Basi wewe, mwanadamu, nimekuweka kuwa mlinzi kwa nyumba ya Israeli; basi ulisikie
neno hili kinywani mwangu, ukawape maonyo yangu."

◼️Ulinzi wa kiroho unafanywa kwa maombi na kwa fundisho la Neno la MUNGU.

Kazi za mlinzi wa kiroho.

1. Kumjua na kumfunua adui na kupambana naye kimaombi.

Waefeso 6:12" Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho."

✓✓Hao ndio maadui wa Kanisa la MUNGU.

2. Kuwapiga mawakala wa shetani kimaombi ili wasiwadhuru watu wa MUNGU.

2 Samweli 8:1 Ikawa baadaye, Daudi akawapiga Wafilisti, akawashinda; Daudi akautwaa Gathi na vijiji vyake mikononi mwa hao Wafilisti."

✓✓Wakati huu Kanisa la MUNGU hupigana na maadui kimaombi.

3. Kuwajulisha watu wa MUNGU juu ya hatari iliyopo inayotoka ulimwengu wa roho wa giza.

Ezekieli 33:6 "Bali mlinzi akiona upanga unakuja, kama hapigi tarumbeta, wala watu hawakuonywa,
na upanga ukaja ukamwondoa mtu awaye yote miongoni mwao; ameondolewa huyo katika uovu
wake, lakini damu yake nitaitaka mkononi mwa mlinzi huyo."

✓✓Neno la MUNGU likiwaonya watu na kuwapa watu akili maarifa na ufahamu huyo aliyewafundisha hilo Neno la MUNGU atakuwa amawasaidia wao kushinda vita ya kiroho, mlinzi ni wa muhimu sana.

4. Kuwaonya anaowalinda kiroho ili wasiangukie mikononi mwa mawakala wa shetani.

Ezekieli 3:17 "Mwanadamu, nimekuweka kuwa mlinzi wa nyumba ya Israeli; basi, sikia neno hili litokalo katika kinywa changu, ukawape maonyo haya yatokayo kwangu."

✓✓Watumishi wa MUNGU ni walinzi wa kiroho hivyo mafundisho yao kuwaonya watu ili wasiangukie mikononi mwa mawakala wa shetani.

✓✓Mlinzi wa kiroho kwenye familia, Kanisa, ukoo au eneo hakikisha unasimama katika nafasi yako ya ulinzi wa kiroho.

5. Kuvaa silaha za kiroho siku zote ambapo kwa hizo silaha atampinga adui wa kiroho.

Waefeso 6:11 "Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani."

6. Nguvu ya ushindi ya mlinzi wa kiroho hutoka kwa MUNGU hivyo inampasa mlinzi kumtii sana MUNGU kupitia ROHO MTAKATIFU ambaye ndiye hutusimamia Kanisa hai la YESU KRISTO.

Kutoka 15:2 "BWANA ni nguvu zangu, na wimbo wangu; Naye amekuwa wokovu wangu. Yeye ni MUNGU wangu, nami nitamsifu; Ni MUNGU wa baba yangu, nami nitamtukuza."

7. Utakatifu katika KRISTO ndio hutengeneza ujasiri,hivyo kushinda vita kirahisi, hivyo inampasa sana mlinzi wa kiroho kuishi maisha matakatifu ya Wokovu wa KRISTO YESU siku zote ili awe jasiri na mshindi dhidi ya nguvu za giza.

Mithali 28:1 "Waovu hukimbia wasipofuatiwa na mtu; Bali wenye haki ni wajasiri kama simba."

✓✓Wenye haki ndio majasiri.

◼️Bwana YESU KRISTO ndio kiini cha ujasiri wa Mkristo muombaji.

Waefeso 3:12 "Katika yeye tunao ujasiri na uwezo wa kukaribia katika tumaini kwa njia ya kumwamini."


✓✓MUNGU hana furaha na Mkristo vuguvugu wa kiroho.
Mkristo vuguvugu ni mtu asiyeeleweka yuko upande gani.

Ufunuo 3:15-16 " Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto. Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu."

✓✓Mkristo vuguvugu ni mkristo ambaye ana jina la kuwa hai kiroho ila amekufa.

✓✓Ni mtu mwenye dhambi lakini anajiona hana dhambi.

✓✓Ni mtu anayesali na kuomba lakini kuna mtu hajamsamehe na anajiona yuko sawa tu.

✓✓Ni mkristo mwenye chuki na baadhi ya watu ila anajiona ni sawa tu.

✓✓Ni mtu asiye na moyo wa toba ila anajiita mtakatifu.

✓✓Anafanya uzinzi au uasherati kwa siri akiwaogopa watumishi wasimjue lakini MUNGU anamuona.

✓✓Kama ni Mama Kanisani yuko tayari kuwazushia uongo wamama wenzake na anajiona yuko sawa tu.

✓✓Kama ni binti au kijana anafanya uasherati kwa siri huku akiendelea na huduma, anadhani kwamba ataenda mbinguni kwa sababu ya utumishi, kumbe mbinguni watu wanaenda kwa sababu ya utakatifu katika KRISTO.

Yako mambo mengi yanaweza kumfanya mkristo kuwa vuguvugu haijalishi anajielewa au haelewi.

◼️Ndugu, MUNGU hatakati wateule vuguvugu.

◼️Bwana YESU KRISTO hahitaji wateule vuguvugu maana hao wasipobadilika wanaweza kutapikwa.

◼️Ndugu, usiwe mkristo vuguvugu na mwambie na mtu aliye karibu yako kwamba haimpasi kuwa mkristo vuguvugu.

✓✓Ukitaka kuwa mlinzi safi wa kiroho kataa uvuguvugu wa kiroho.
Zingatia  na MUNGU atakubariki sana.
Mche MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi na utaitwa heri.
Kama pia unatumia Facebook ni follow maana itafika kipindi nitakuwa napost tu katika page yangu na profile yangu.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter  Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292(Ushauri, Maombezi, Whatsapp n.k)
Share ujumbe huu kwenye magroup ya Whatsapp uliyopo.
Ubarikiwe



Comments