![]() |
| Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
Bwana YESU KRISTO atukuzwe Ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU wa Mbinguni.
✓✓Inawezekana Wewe ni Mtumishi wa MUNGU, ni jambo jema.
✓✓Inawezekana Wewe unatamani kuwa Mtumishi wa MUNGU, unatamani jambo jema.
◼️Kazi mojawapo ya MUNGU ni kuwa Askofu yaani Mwangalizi wa kazi ya MUNGU, na Biblia inasema ukitamani hivyo unatamani jambo jema.
1 Timotheo 3:1-2 " Ni neno la kuaminiwa; mtu akitaka kazi ya askofu, atamani kazi njema. Basi imempasa askofu awe mtu asiyelaumika, mume wa mke mmoja, mwenye kiasi na busara, mtu wa utaratibu, mkaribishaji, ajuaye kufundisha;"
✓✓Niko hapa leo kukuambia kazi za Mtumishi wa MUNGU ili uzifanyie kazi zote kama zilivyo na utafanikiwa sana.
1. Kumtumikia Bwana YESU kwa uaminifu.
1 Kor 4:1-2 ''Mtu na atuhesabu hivi, kuwa tu watumishi wa KRISTO, na mawakili wa siri za MUNGU. Hapo tena inayohitajiwa katika mawakili, ndiyo mtu aonekane kuwa mwaminifu. ''
2. Kuishi maisha matakatifu yanapasao walioitwa na KRISTO YESU kwa ajili ya Wokovu.
1 Petro 1:14-16 ''Kama watoto wa kutii msijifananishe na tamaa zenu za kwanza za ujinga wenu; bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote; kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu. ''
3. Kumtukuza MUNGU na kumwabudu katika Roho na kweli.
Zaburi 113:1-3 ''Haleluya. Enyi watumishi wa BWANA, sifuni, Lisifuni jina la BWANA. Jina la BWANA lihimidiwe Tangu leo na hata milele. Toka maawio ya jua hata machweo yake Jina la BWANA husifiwa. ''
✓✓Kumwabudu MUNGU katika Roho na kweli ni utaratibu wa lazima kwa watumishi wa MUNGU katika KRISTO YESU.
Yohana 4:23-24 '' Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba(MUNGU) katika roho na kweli. Kwa maana Baba(MUNGU) awatafuta watu kama hao wamwabudu. MUNGU ni ROHO, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.''
4. Kufanya kazi ya MUNGU na walio juu yako walioitwa na MUNGU.
2 Nyakati 20:20B ''mwaminini BWANA, Mungu wenu, ndivyo mtakavyothibitika; waaminini manabii wake, ndivyo mtakavyofanikiwa. ''
5. Kuwa kielelezo chema katika yote.
1 Timotheo 4:12 '' Mtu awaye yote asiudharau ujana wako, bali uwe kielelezo kwao waaminio, katika usemi na mwenendo, na katika upendo na imani na usafi. ''
✓✓Mtu aliye kielelezo chema ni mtu wa mfano mzuri na unaofaa kuiga.
◼️Ni muhimu sana wateule wa KRISTO wote tukawa kielelezo chema katika mema.
✓✓Kumbuka Bwana YESU Mwokozi wetu alitupa kielelezo na anatutaka tuwe vielelezo vyema.
Yohana 13:15 ''Kwa kuwa nimewapa kielelezo; ili kama mimi nilivyowatendea, nanyi mtende vivyo. ''
✓✓Kuwa kwako kielelezo kunaweza kuwafanya watu hata wakaokoka kama wewe au hata wakiokoka baadae watajifunza kwako wewe uliye kielelezo chema katika mema.
1 Timotheo 1:16 '' Lakini kwa ajili hii nalipata rehema, ili katika mimi wa kwanza, YESU KRISTO audhihirishe uvumilivu wake wote; niwe kielelezo kwa wale watakaomwamini baadaye, wapate uzima wa milele. ''
Je wewe ni Mtumishi wa MUNGU?
◼️Kama wewe ni Mtumishi wa MUNGU inakupasa sana kuwa kielelezo chema.
Kuna watu ni wa Kanisani lakini ni vielelezo vibaya ndio maana husababisha Injili inatukanwa.
✓✓Ndugu, Kama ni wewe ulikuwa kielelezo kibaya basi tubu na anza sasa kuwa kielelezo chema.
Zingatia na MUNGU atakubariki sana.
Mche MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi na utaitwa heri.
Kama pia unatumia Facebook ni follow maana itafika kipindi nitakuwa napost tu katika page yangu na profile yangu.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292(Ushauri, Maombezi, Whatsapp n.k)
Share ujumbe huu kwenye magroup ya Whatsapp uliyopo.
Ubarikiwe

Comments