![]() |
| Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO |
Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe Ndugu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU wa Mbinguni.
◼️Kuna sadaka zingine unaposikia msukumo wa MUNGU rohoni mwako ili kutoa basi usikawie kutoa.
Kutoka 22:29 " USIKAWIE KULETA malimbuko ya matunda yako na ya vinywaji vyako. Mzaliwa wa kwanza katika wanao waume utanipa mimi."
Hii Sadaka ya Malimbuko ni aina mojawapo ya Sadaka, Sasa Mimi Peter Mabula sipo hapa leo kuzungumzia Sadaka ya Malimbuko Ninachotaka uone ni kwanini MUNGU aseme "Usikawie kuleta Sadaka"
✓✓Kumbe tunajifunza kwamba Kuna Sadaka usichelewe kuitoa.
◼️ Unaweza ukasikia msukumo mkubwa rohoni mwako kwa ajili ya kutoa Sadaka fulani na kumbe ni ROHO MTAKATIFU amekupa msukumo huo kwa sababu ya mahitajio ya kiroho kwa ajili Yako.
2 Wakorintho 9:7 ''Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana MUNGU humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu."
✓✓Sadaka kama hiyo usipoitoa kwa Wakati hutapata Matokeo mazuri.
Kuna Sadaka MUNGU huwa anazitaka kwa kusudi lake ila kwa faida ya mtaji.
Kutoka 22:30 "Nawe utafanya vivyo katika ng'ombe zako, na kondoo zako; utamwacha siku saba pamoja na mama yake; siku ya nane utanipa mimi."
✓✓Inawezekana kabisa elfu 20 uliyoambiwa rohoni utoe leo kama sadaka ina thamani sana kuliko ukae miezi 6 kisha utoe laki mbili.
◼️ROHO MTAKATIFU akikupa msukumo wa utoaji leo fanya mapema kutoa maana hitajio la kiroho linalohitaji sadaka kwenye ulimwengu wa roho, hitajio hilo ni la leo.
◼️Mama wa Sarepta aliambiwa atoe sadaka kwa Eliya, sadaka hiyo ilihitajika muda ule ule ili afaidike yeye anayetoa, alipotoa tu ndipo Biblia inasema kuanzia siku hiyo chakula hakikupungua ndani ya nyumba hiyo.
1 Wafalme 17:13-16 " Eliya akamwambia, Usiogope; enenda ukafanye kama ulivyosema; lakini unifanyie kwanza mkate mdogo ukaniletee; kisha ujifanyie nafsi yako na mwanao. Kwa kuwa BWANA, Mungu wa Israeli, asema hivi, Lile pipa la unga halitapunguka, wala ile chupa ya mafuta haitaisha, hata siku ile BWANA atakapoleta mvua juu ya nchi. Basi akaenda, akafanya kama alivyosema Eliya; na yeye mwenyewe, na Eliya, na nyumba yake, wakala siku nyingi. Lile pipa la unga halikupunguka, wala ile chupa ya mafuta haikuisha, sawasawa na neno la BWANA alilolinena kwa kinywa cha Eliya."
◼️Kumbuka ni MUNGU ndio aliihitaji sadaka hiyo ya mama wa Sarepta na sio Eliya ndio alihitaji.
1 Wafalme 17:8-9 " Neno la BWANA likamjia, kusema, Ondoka, uende Sarepta, ulio mji wa Sidoni, ukae huko. Tazama, nimemwagiza mwanamke mjane wa huko akulishe."
✓✓Kumbe ni MUNGU ndio aliyekuwa anaihitaji hiyo sadaka ya Mama wa Sarepta hata kama huyo Mama aliona anampa Eliya.
Mama huyu alikuwa na uhuru wa kusema "Nitatoa mwezi ujao" lakini hiyo sadaka isingemletea faida kiroho wakati wa mwezi ujao maana majira yangekuwa yamepita.
◼️Kumbuka kuna baraka zimefungwa ndani ya majira fulani, mtu asipoyatumia majira husika anaweza kutumia nguvu nyingi mno kufanikiwa katika majira mengine baada ya majira sahihi kupita.
✓✓Hivyo vile vinavyohitajika katika majira ya sasa vya baraka ukividharau unakosa baraka, maana ziliamuriwa kwa majira haya.
✓✓Ndio maana MUNGU anasema usikawie kutoa.
Kutoka 22:29 "Usikawie kuleta malimbuko ya matunda yako na ya vinywaji vyako. Mzaliwa wa kwanza katika wanao waume utanipa mimi."
✓✓Ndugu, hakikisha Ukiwa na msukumo wa rohoni wa kukuambia kutoa, hakikisha unatoa.
◼️Anayeweza kukupa msukumo rohoni wa kutoa sadaka fulani ni ROHO MTAKATIFU, na hiyo ni kwa faida yako na sio vinginevyo.
Zingatia na MUNGU atakubariki sana.
Mche MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi na utaitwa heri.
Kama pia unatumia Facebook ni follow maana itafika kipindi nitakuwa napost tu katika page yangu na profile yangu.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292.
Ubarikiwe sana

Comments