![]() |
Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO |
"Shalom Mtumishi! Hivi muumini akisha okoka akabatizwa nini kinabaki kutimizwa?"
Kinachobaki baada ya Kuokoka na kubatizwa ni.
1. Ni kuendelea kuishi maisha matakatifu ya Wokovu wa Bwana YESU.
1 Petro 1:15 "bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote;"
Mithali 23:12 "Elekeza moyo wako kusikiliza mafundisho; Tega masikio yako kusikia maneno ya maarifa."
3. Kuwa mtu wa maombi.
1 Wathesalonike 5:17 "ombeni bila kukoma;"
4. Kumtumikia MUNGU kwa kuwaleta watu kwa YESU.
1 Wakorintho 15:58 " Basi, ndugu zangu wapendwa, mwimarike, msitikisike, mkazidi sana kutenda kazi ya BWANA sikuzote, kwa kuwa mwajua ya kwamba taabu yenu siyo bure katika BWANA."
5. Kuenenda katika ROHO MTAKATIFU ukifanyia kazi maelekezo yake yote.
Warumi 8:14 " Kwa kuwa wote wanaoongozwa na ROHO wa MUNGU, hao ndio wana wa MUNGU."
6. Kutokuipenda dunia na machukizo yake.
1 Yohana 2:15-17 " Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba(MUNGU) hakumo ndani yake. Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba(MUNGU), bali vyatokana na dunia. Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya MUNGU adumu hata milele."
7. Kujitenga na mabaya yote.
1 Wathesalonike 5:22 " jitengeni na ubaya wa kila namna."
2. Swali la pili.
Ni kwamba Wanajeshi hutambulika kwa mavazi yao ya kijeshi.
Polisi hutambulika kwa mavazi yao.
Majaji mahakamani hutambulika kwa mavazi yao.
Madaktari hutambulika kwa mavazi.
Wanafunzi hutambulika kwa mavazi yao.
✓✓Ni kwa sababu mavazi yanaweza kumtambulisha mtu.
Hayo ni mavazi mema, lakini pia yapo na mavazi mabaya, nayo yanaweza kumtambulisha mhusika tofauti.
Mfano hao ni kwamba
Makahaba/Machangudoa hutambulika kwa mavazi yao.
✓✓Sasa wako watu makanisani huvaa kikahaba na hiyo ni kama wanatambulisha ukahaba na sio utakatifu.
Kwanini baadhi ya watu wa kanisani mavazi yao huwatambulisha kama makahaba sio watu wa Kanisani?
Leo makanisani wapo baadhi ya wanawake wanavaa nguo matiti yakiwa nje.
Wapo mabinti Leo makanisani hufunika nyonyo na sio matiti, yaani badala ya kufunika matiti yao wao hufunika nyonyo tu na sio matiti, ni hatari sana, yaani mtu matiti yake yote nje ila ameziba nyonyo tu kwa nguo laini.
Wako watu makanisani tena ibadani huvaa kikahaba na kulifanya Kanisa kutukanwa.
Ole wako wewe mtu wa Kanisani lakini Kanisa kila siku linatukanwa kwa sababu yako kwa sababu ya nguo zako za kikahaba.
Unaimba kwaya huku mgongo wote uko nje, wewe unaita mtindo, na kumbe ni ushetani.
Unavaa nguo fupi na kumbe umevaa kwa agizo la shetani.
Kama ingetokea utolewe Kanisani muda huo na kupelekwa kuchanganywa na makahaba watu wangesema "Huyu ni kahaba mzoefu maana amevaa kikahaba kuliko wenzake"
✓✓Ndugu, kama kweli YESU KRISTO ni Mwokozi wako badilika na acha kuanzia Leo kuvaa kikahaba.
1 Wathesalonike 5:22-23 "jitengeni na ubaya wa kila namna. MUNGU wa amani mwenyewe awatakase kabisa; nanyi nafsi zenu na roho zenu na miili yenu mhifadhiwe mwe kamili, bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu YESU KRISTO."
✓✓Kanisa la MUNGU lazima tujitenge na kila ubaya, ukiwemo wanawake kuvaa kikahaba.
✓✓Kanisa la MUNGU
lazima likae salama bila lawama.
✓✓Kuna watu hakika wanalidhalilisha sana Kanisa kwa mavazi yao ya kikahaba.
Watu wengi Leo huvaa kwa adabu msibani tu na ukweni lakini sio Kanisani.
Baadhi ya wachungaji nao huogopa kuwakemea washirika wao maana wanadhani wakiwakemea watahama Kanisa.
✓✓Ndugu zangu, jitahidi sana watu wasikuone kama kahaba kwa sababu ya mavazi yako.
✓✓Jitahidi sana watu wasikuone kama Malaya asie na akili kwa sababu ya mavazi ya kikahaba.
Biblia inajulisha juu ya makahaba na mavazi yao ya kikahaba ila Biblia haijawahi kumwelekeza mtu yeyote popote kuvaa kikahaba.
Mithali 7:10" Na tazama, mwanamke akamkuta, Ana mavazi ya kikahaba, mwerevu wa moyo;"
Je ni wewe huvaa mavazi ya kikahaba?
Kama ni wewe acha kuanzia Leo.
Kumbuka kama wewe ni mtu wa Kanisani na unavaa kikahaba utakufanya Kanisa kutukanwa na wewe utaambulia laana.
Ndugu uliye mtu wa Kanisa usikubali kamwe kuvaa kikahaba.
MUNGU akubariki sana.
By Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la MUNGU
3. Swali la tatu
Ni kwamba kuna Mtumishi wa MUNGU mmoja alinifundisha miaka 17 iliyopita kwa njia ya redio kwamba neno Suruali ndani ya Biblia linapatikana mara mbili tu na ni katika kitabu cha Danieli tu.
Kwa sababu ndio nilikuwa nimeokoka basi nilikariri hivyo na hata kuwaambia watu hivyo.
Kwa kutokuchunguza vyema hata Mimi niliwahi kumwambia watu hivyo kwamba Biblia nzima neno Suruali lipo sehemu mbili tu.
Pia nimewahi kukutana na masomo ya baadhi ya watumishi wakifundisha huku mtandaoni wakisema kwamba neno hilo Suruali ndani ya Biblia lipo katika maandiko mawili tu, hivyo nikajua iko hivyo.
Sasa kwa sababu huwa nataka kuchunguza ndani ya Biblia kile ninachofundishwa basi nikagundua jambo hilo kwamba ni maandiko saba yaliyoandikwa neno Suruali.
Hiyo ni kwa mujibu wa Mimi yaani kwa uchunguzi wangu.
Maandiko hayo ni Kutoka 39:28, Walawi 16:4, Ezekieli 44:18, Danieli 3:21, Kutoka 28:42, Danieli 3:27, na Walawi 6:10
Maoni yangu.
1. Jifunza Neno la MUNGU kwa watumishi mbalimbali lakini uwe unahakiki ndani ya Biblia vile ambavyo huna uhakika, uhakika wetu ni Biblia hivyo uwe na muda binafsi wa kusoma Biblia na kuchunguza na kutafakari ili uelewe kwa usahihi.
2. Tenga muda wa kusoma Biblia na tafakari Neno la MUNGU wewe Binafsi.
3. Hata watumishi sio wote wanajua vyote hivyo usiwaamini kiasi ambacho huhitaji kusoma Biblia mwenyewe kuthibitisha walichosema.
4. Kwa wahubiri: ni muhimu kufundisha kitu ulicho na uhakika nacho na sio kufundisha tu ulichosikia kwa Mtumishi fulani.
Najua jambo hili la neno Suruali kuwa Mara 7 ndani ya Biblia ya kiswahili ni jambo dogo tu lakini kama unafundisha watu ujue watachukua kwako ulichowafundisha na wao wataenda kuwafundisha wengine hayo hayo makosa, vipi kama umewapotosha kwa jambo kubwa? Ni hatari sana.
Wakala wa shetani mmoja alijiita Mungu na waumini wake wakaanza kumwita Mungu wa pili.
Hayo ndio madhara ya kipofu kumwelekeza njia kipofu mwenzake.
Watu wahubiri walihubiri kwamba YESU KRISTO ni mtu tu na hawezi kuokoa, na watu waliosikia hivyo wakashika upotofu huo na kuusambaza duniani kiasi kwamba dhehebu lao wanajiita Kanisa au Wakristo lakini ni wapinga KRISTO, ni hatari sana.
Ni muhimu sana kuijaribu kila roho ya mhubiri na kuipima ili ujue kama inatokana na MUNGU aliyeziumba mbingu na nchi.
Ni vyema sana kumchunguza kila mhubiri ila kama haleti injili ya KRISTO YESU ya Wokovu umkatae Mtumishi huyo, injili yetu ni YESU KRISTO anayeokoa hivyo anayemtambulisha Mwokozi mwingine ujue huyo hatokani na MUNGU.
Wengine kwa kudanganya watu wamefikia hatua wanadhani dhehebu leo tu ndilo linaokoa na sio YESU KRISTO ndio anayeokoa, ni hatari sana.
Kuna mpaka makanisa leo ni wapinga KRISTO kwa sababu wakala wa shetani ndio aliwafundisha na wao wakashika hivyo bila kuchunguza maandiko kwa usahihi wake.
YESU KRISTO yu karibu kuja na atamlipa kila mtu sawasawa na matendo yake.
MUNGU akubariki Sana.
By Peter Mabula.
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
◾Majibu ya Mtumishi Peter Mabula.

2. Kujifunza sana Neno la MUNGU.

Mtumishi Mabula mbona watu husakama sana Wanawake kwa mavazi, tufanyeje? Yaani Kanisani ndio tunasakamwa zaidi, tufanyeje sisi Wanawake?
◾Majibu ya Mtumishi Peter Mabula.
◼️Wanawake nisikilizeni.
Ni kwamba Wanajeshi hutambulika kwa mavazi yao ya kijeshi.
Polisi hutambulika kwa mavazi yao.
Majaji mahakamani hutambulika kwa mavazi yao.
Madaktari hutambulika kwa mavazi.
Wanafunzi hutambulika kwa mavazi yao.
Kwanini nimesema hivyo?
✓✓Ni kwa sababu mavazi yanaweza kumtambulisha mtu.
Hayo ni mavazi mema, lakini pia yapo na mavazi mabaya, nayo yanaweza kumtambulisha mhusika tofauti.
Mfano hao ni kwamba
Makahaba/Machangudoa hutambulika kwa mavazi yao.
✓✓Sasa wako watu makanisani huvaa kikahaba na hiyo ni kama wanatambulisha ukahaba na sio utakatifu.
Kwanini baadhi ya watu wa kanisani mavazi yao huwatambulisha kama makahaba sio watu wa Kanisani?
Leo makanisani wapo baadhi ya wanawake wanavaa nguo matiti yakiwa nje.
Wapo mabinti Leo makanisani hufunika nyonyo na sio matiti, yaani badala ya kufunika matiti yao wao hufunika nyonyo tu na sio matiti, ni hatari sana, yaani mtu matiti yake yote nje ila ameziba nyonyo tu kwa nguo laini.
Wako watu makanisani tena ibadani huvaa kikahaba na kulifanya Kanisa kutukanwa.
Ole wako wewe mtu wa Kanisani lakini Kanisa kila siku linatukanwa kwa sababu yako kwa sababu ya nguo zako za kikahaba.
Unaimba kwaya huku mgongo wote uko nje, wewe unaita mtindo, na kumbe ni ushetani.
Unavaa nguo fupi na kumbe umevaa kwa agizo la shetani.
Kama ingetokea utolewe Kanisani muda huo na kupelekwa kuchanganywa na makahaba watu wangesema "Huyu ni kahaba mzoefu maana amevaa kikahaba kuliko wenzake"
✓✓Ndugu, kama kweli YESU KRISTO ni Mwokozi wako badilika na acha kuanzia Leo kuvaa kikahaba.
1 Wathesalonike 5:22-23 "jitengeni na ubaya wa kila namna. MUNGU wa amani mwenyewe awatakase kabisa; nanyi nafsi zenu na roho zenu na miili yenu mhifadhiwe mwe kamili, bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu YESU KRISTO."
✓✓Kanisa la MUNGU lazima tujitenge na kila ubaya, ukiwemo wanawake kuvaa kikahaba.
✓✓Kanisa la MUNGU
lazima likae salama bila lawama.
✓✓Kuna watu hakika wanalidhalilisha sana Kanisa kwa mavazi yao ya kikahaba.
Watu wengi Leo huvaa kwa adabu msibani tu na ukweni lakini sio Kanisani.
Baadhi ya wachungaji nao huogopa kuwakemea washirika wao maana wanadhani wakiwakemea watahama Kanisa.
✓✓Ndugu zangu, jitahidi sana watu wasikuone kama kahaba kwa sababu ya mavazi yako.
✓✓Jitahidi sana watu wasikuone kama Malaya asie na akili kwa sababu ya mavazi ya kikahaba.
Biblia inajulisha juu ya makahaba na mavazi yao ya kikahaba ila Biblia haijawahi kumwelekeza mtu yeyote popote kuvaa kikahaba.
Mithali 7:10" Na tazama, mwanamke akamkuta, Ana mavazi ya kikahaba, mwerevu wa moyo;"
Je ni wewe huvaa mavazi ya kikahaba?
Kama ni wewe acha kuanzia Leo.
Kumbuka kama wewe ni mtu wa Kanisani na unavaa kikahaba utakufanya Kanisa kutukanwa na wewe utaambulia laana.
Ndugu uliye mtu wa Kanisa usikubali kamwe kuvaa kikahaba.
MUNGU akubariki sana.
By Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la MUNGU
3. Swali la tatu
Mtumishi Mabula naomba nikuulize kitu. Nimekutana na masomo Yako mengi sana tangu mwaka 2013 je Hujawahi kujikuta Kuna sehemu kwenye somo lako ukagundua baadae kwamba hukuandika kitu kimoja kwa usahihi?
◾Majibu ya Mtumishi Peter Mabula.
Ubarikiwe sana.
Niliwahi kuandika katika somo langu Moja kwamba Neno suruali katika Biblia linapatikana katika maandiko mawili tu.
Ni kwamba kuna Mtumishi wa MUNGU mmoja alinifundisha miaka 17 iliyopita kwa njia ya redio kwamba neno Suruali ndani ya Biblia linapatikana mara mbili tu na ni katika kitabu cha Danieli tu.
Kwa sababu ndio nilikuwa nimeokoka basi nilikariri hivyo na hata kuwaambia watu hivyo.
Kwa kutokuchunguza vyema hata Mimi niliwahi kumwambia watu hivyo kwamba Biblia nzima neno Suruali lipo sehemu mbili tu.
Pia nimewahi kukutana na masomo ya baadhi ya watumishi wakifundisha huku mtandaoni wakisema kwamba neno hilo Suruali ndani ya Biblia lipo katika maandiko mawili tu, hivyo nikajua iko hivyo.
Baadae nikaamua kufanya uchunguzi nikagundua nilikosea kuwaambia watu kwamba Neno suruali katika Biblia lipo sehemu 2 tu nikarekebisha.
Sasa kwa sababu huwa nataka kuchunguza ndani ya Biblia kile ninachofundishwa basi nikagundua jambo hilo kwamba ni maandiko saba yaliyoandikwa neno Suruali.
Neno "SURUALI" kwenye Biblia linapatikana Mara 7 tu?
Hiyo ni kwa mujibu wa Mimi yaani kwa uchunguzi wangu.
✓✓Nimechunguza maandiko na neno Suruali nimelikuta katika maandiko 7 tu na Mara zote saba wanaozungumziwa kuvaa Suruali ni wanaume tu.

Comments