Shuhuda mbalimbali.

Shuhuda mbalimbali.
1. Bwana Yesu asifiwe Mtumishi.
Mungu azidi kukubariki maana mkono wake kupitia kwako kila ukiniombea nafunguliwa. Hususani mwezi wa saba ulimwombea mke wangu akajifungua salama.( Alikuwa amepitisha wiki mbili za matarajio
)
Namshukuru Mungu sana kwa ajili yako.

2. Bwana Yesu asifiwe mtumishi, mimi ni mzima
Pia namshukuru MUNGU kwa kunijibu maombi yangu juu ya kupata mchumba namshukuru MUNGU sana.
Nakumbuka uliniombea nikiwa nimekata tamaa kabisa lakini MUNGU kanitendea muujiza huo maana nimepata mchumba safi anayenifaa.
Namshukuru MUNGU kwa muujuza huo na asante kwa maombi yako, endelea kuniombea mtumishi maana tunakaribia kufunga ndoa

3. Shalom Mtumishi.
Ngoja nikupe ushuhuda wangu mfupi.
Yaani Mtumishi kwanza Maombi yako na masomo ninayo mengi nimeprint hata kabla ya kukuona, mimi nilizaliwa katika waabudu shetani, familia baba na mama nyumba niliyozaliwa kuna madhabahu na miungu 2 nje uani halafu ndani kuna kiti cha Enzi na miungu 2 pia nikakua nikiwa nashiriki matambiko na uganga baadae nikaja kuolewa na mkristo asiye katika madhehebu ya Wokovu, nikawa kwenye dhehebu hilo Zaidi ya miaka 10 nikiwa sasa sishiriki chochote cha asili yangu ya kuzaliwa mana kwenye ukristo hakuna hivyo vitu
Sasa mdogo wangu alikuwa na matatizo na akataka kuombewa nikamwambia kanisani kwetu sisi hatuombei labda niulize kwa Rafiki yangu wapi tunaweza kwenda basi akatuelekeza Kanisa Kimara ambako mdogo wake anasali hapo basi tukapelekwa pale ila mchungaji alipokuja kutusalimia akaniuliza mimi nina matatizo gani? nikamwambia mimi sina matatizo nimemleta huyu ndugu yangu ndiye mwenye matatizo, mchungaji akasisitiza kuwa mimi ndiye mwenye matatizo akasema nisimame ile anataka kunigusa tuu nikamkamata mkono na sikujua kilichoendelea tena
maana nilikuwa na mapepo hatari, baada ya kuzinduka akaniambia niende nikaongozwe sala ya toba kisha nianze maombi haraka kuna nguvu za mizimu na za wachawi tena zimeshaanza kuniharibia mambo yangu, katika Maisha yangu nilikuwa siwapendi walokole wala maombi spendi kabisa. basi ikabidi nitii nifuate maelekezo hivyo, so nikaongozwa sala ya toba na straight nikaanza maombi.
HAPO SASA NDO NIKAANZA KUSOMA BIBLIA NA KUJUA DAMU YA YESU NA JINA LAKE VINAVYOFANYA KAZI. KUMBE KWA MIAKA MINGI NILIKUWA NAMILIKIWA NA NGUVU ZA GIZA, KUMBE BADO MIZIMU ILIKUWA IMENIKAMATA MAANA KUMBE KIROHO NILIKUWA MALKIA SASA NATAKIWA KUIOMBEA FAMILIA NZIMA YA BABA NA MAMA BADO WANASHIRIKI HAYO MAMBO NDIO MAANA NAULIZA JE NITAZIDI KUPATA MASHAMBULIZI ZAIDI AU NIENDELEE AU NISUBIRI HADI NISIMAME VIZURI, NINA CHANGAMOTO SANA NIMEAMINI KRISTO YESU NI UFALME MWINGINE KABISA, NDUGU WAMENITENGA HATA MAJIRANI AMBAO NI WACHAWI NINAOWAONA KWA SASA WOTE HATUONGEI YANI NI VITA KIMWILI NA KIROHO
HATA HIVYO ASANTE SANA KWA USHAURI NA MAOMBI YAKO YANATUSAIDIA SANA SISI AMBAO WENGINE ASILI ZETU ZA KUZALIWA NI MATATIZO UBARIKIWE SANA MUNGU AKUINUE KATIKA HUDUMA YAKO
Ninaomba pia maelekezo ya kuombea ukoo mzima ambao sio wakristo na wanaoshiriki matambiko na uganga wa kienyeji ila mimi ndie mkristo peke yangu sasa natakiwa niwaombee wote je si kwamba nitaanza vita na miungu ya familia kama ambavyo bado wananifuatilia? au nafanyaje?
yaani hapo nimeandika kwa kifupi ngoja nitakuandikia kwa kirefu kisha uta-amend miungu ya familia ni mibaya sana heri ya pepo au uchawi hivyo vitu kwa damu na jina la Yesu vinasambaratika mara moja ila miungu ina uhalali nimejifunza vitu vingi sana vya kiroho tangu kuokoka June 2018 tangu nimjue Kristo mimi ni kuomba tu na kusali hata walionipeleka kanisani sasa nawafundisha mimi. nikiwa nyumbani free pia nitakutafuta uniombee pia sijui jinsi ya kuanza kuiombea familia yote.
Hakika ubarikiwe sana.

4. Bwana asifiwe Mtumichi.
Mimi iko Congo na asante kwa msg ya vocal unatumaga.
mutumichi wa Mungu ata na mimi bado ninafatilia uchauri wako niendeleye na Yesu. na ile msg ya vocal ulitumiaga ambao inasema usimuogope aduwi yako uliomuona kwenye ndoto imesaidia mimi sana ata nikiota ndoto mbaya si iogopi tena ila nina omba tu kwa Mungu. ila Mutumichi naomba kama una mafundicho kuusu damu ya Yesu unisaidie.

Hizo ni baadhi ya shuhuda ambazo baadhi ya marafiki walinitumia baada ya kusaidika na Neno la MUNGU na wengine kusaidia kwa maombi.
Nimekuletea shuhuda hizo kama walivyonitumia.
Utukufu kwa MUNGU Baba mbinguni.
Namshukuru Bwana YESU kwa neema yake.
Namshukuru ROHO MTAKATIFU kwa kunipa Neno la MUNGU.
MUNGU akubariki uliyejifunza kitu katika shuhuda hizi.
By Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la MUNGU.


Shuhuda zinaendelea.
1. Bwana Yesu Kristo asifiwe mtumwa wa BWANA wa majeshi! Nakupa hongera kwa makala yako yenye kichwa, "KRISMAS NA KUZALIWA KWA BWANA YESU KRISTO", Iliyotolewa kwenye gazeti la Nyakati toleo Na. 941 la disemba 9-15,2018. Mungu aliye hai akutunze.
2. Bwana YESU asifiwe Mtumishi wa MUNGU.
Ninayo furaha kubwa kwa matendo makuu sana YESU KRISTO wa Nazareti aliyonitendea. Napenda nikushirikishe furaha hiyo kuwa YESU amemrudisha binti yangu Neema jana akiwa mzima. Sifa, Heshima, Utukufu na Enzi yote ni kwa MUNGU.
MUNGU wa mbinguni akutunze na kukubariki Mtumishi wa MUNGU kwa upendo wako wa kuomba kwa mzigo juu ya binti yangu. Masomo na maombi yako yalinisaidia sana katika hiyo vita kupata mbinu na maarifa ya kupigana katika ulimwengu wa roho bila kuchoka mpaka shetani aachie.
Sina maneno ya kusema kwako ya thamani zaidi ya kumshukuru MUNGU kwa ajili yako na kusema Asante. Ushuhuda wangu utakapokamilika nitauandika kadri Roho Mtakatifu atakavyoniongoza nitakutumia.
Ilikuwa mwezi wa kumi (Oktoba) tarehe 16 binti yangu alipopotea na miezi miwili kamili ndipo alipopatikana.
Miezi miwili kamili alikuwa hajulikani aliko.
Asante kwa maombi yako na MUNGU akubariki sana.

3. Bwana YESU asifiwe mchungaji.
Kweli kwa % nyingi sana mchungaji
masomo na mafundsho yako kwakweli naona yananipigisha hatua flani katika MUNGU, Sasa tatizo kubwa tena lililosalia linalo ufanya moyo wang hauna amani ndo hili la ndoto za kufanya mapenzi,
Nahisi kuna nguvu na roho za kipepo zinanifatilia ndizo nahitaj zikaniachie na maagano yaliyofanyika huko kuzimu ya kpepo yakaharibike, kwa jina la YESU Kristo aliye hai, maana mimi staki na mimi si mahala pao kuzimu, nakusihi mtumishi, nipatie muda nikupgie ukanisaidie pia kukemea na kuharibu hizi roho za kpepo zinazo nifuata hadi ndotoni.
"NINAZIKATAA KWA MOYO WANGU WOTE NA KUZICHUKIA MCHUNGAJI.

4. Shalom Mtumishi. Ninamshukuru Mungu kwa ajili yako maana mafundisho unayoyatoa facebook hakika yamekuwa msaada sana kwangu. Kupitia hayo nikizingatia nakuwa safi kiroho.
Ila pia ninahtaji msaada wa kiroho kuna mahali nimekwama ,tatizo la tamaa mbaya linanisumbua sana nimekuwa wa kuokoka na kurudi nyuma kila mara kwa sababu ya jambo hili.,naomba msaada kwa hilo mtumishi.

5. Mtumishi Wa Mungu Wa Mbinguni Ubarikiwe Bwana Akulinde Na Azidi Kukutumia Nakutakia Krismas Njema Na Mwaka Mpya Mwema Naendelea Kufuatilia Somo La Kumshukuru Mungu Namshukuru Mungu Kwa Ushauri Wako Na Maombi Kwaajili Ya Mwanangu Maana Siku Ya Kwanza Kukupigia Nilikuwa Nimekata Tamaa Kabisa, Sasa Ni Mwaka Na Miezi Tangu Tuwe Ndugu Katika Kristo Mume Wangu Anaendelea Vizuri Kiimani Najua Na Mtoto Wangu Atapona Kabisa Kifafa. Ubarikiwe Sana.
Penye Mafanikio Huwa Kuna Ushauri Na Maombi Ya Mama Msalimie Na Mama Mabula Mbarikiwe

6. Mungu Baba wa mbinguni akubariki
mtumishi Peter, mpendwa jamani
aibariki na kazi yake katika wewe. Amen.
hakika Bwana ni mwema kanitembelea na mimi hakika nina furaha na amani katika yeye YESU Mwokozi mfalme.
Hitaji langu kama ulivyoniombea nimejibiwa.
Mungu akubariki sana Mtumishi.
Pia Mtumishi peter naomba ukiomba usisahau kuniombea na mimi Roho wa Bwana azidi kuniongoza.
Nakupenda mno katika Bwana Yesu.
Ubarikiwe.

Hizo ni baadhi ya shuhuda ambazo baadhi ya marafiki walinitumia baada ya kusaidika na Neno la MUNGU na wengine kusaidia kwa maombi.
Nimekuletea shuhuda hizo kama walivyonitumia.
Utukufu kwa MUNGU Baba mbinguni.
Namshukuru Bwana YESU kwa neema yake.
Namshukuru ROHO MTAKATIFU kwa kunipa Neno la MUNGU.
MUNGU akubariki uliyejifunza kitu katika shuhuda hizi.
By Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la MUNGU.




Shuhuda zinaendelea.
1. Za ibada mtumishi
Asante kwa maombi yako Mungu mwema kila siku.
Nashukuru sana kwa maombi nimeona Mungu akinishangaza kwa matendo yake makubwa .
Nimeanza kuingia MP yaani kwenye siku zangu bila kuingiliwa na majini mahaba Na nimemaliza MP Bila kubakwa na majini mahaba.
Nilikuwa siwezi kuingia period mpaka niingiliwe na majini mahaba. Na nikimaliza tu ile siku ya mwisho inakuwa hivyo hivyo
Namshukuru Mungu;ni furaha ya Ajabu sana.
Sifa kwa Mungu.
Mungu mwema
Nikija Tz nitakutafuta Mtumishi.
Naamini pia kwa maombi na Harusi nitafunga. Hakuna wa kuingilia Tena mahusiano Yangu.
Mungu akubariki sana.

2. Mungu akubariki Mtumishi, umekuwa ukinipa moyo wa kusonga mbele niking'ang'ana na Yesu bila kukata tamaa, nisomapo jumbe zako nabarikiwa sana, Mungu aendelee kukuinua zaidi na zaidi, maisha ya ushindi watu wengi wafuatilie. Na mimi nimeshawaambia watu 4 waliokuwa wamekata tamaa na Bwana kisa ni majaribu lakini toka waanze kufuatilia masomo yako wamejawa na furaha na wanasonga mbele, mimi bila mume wangu nisingefahamu kama kuna maisha ya ushindi.
Mungu akubariki sana Mtumishi.

3. SHALOM SHALOM SHALOM AMEN mtumishi wa MUNGU hakika yeye MUNGU ni mwaminifu hakawii wala hachelewi and his time is the best through your verses and prayers now the father of my children has paid fees for the whole semester for my daughter who is in university. pastor Glory to GOD. thanks so much.
GOD bless u

4. Bwana Yesu asifiwe ndugu Mtumishi heri ya sikukuu. Nimesoma gazeti la Nyakati tena kwa mara yangu ya kwanza kulinunua hili gazeti pengine ni njia ya mimi kuokolewa, ndipo nikakutana na mafundisho yako yamenigusa sana, Mungu akubariki na akuzidishie. ila pia samahani kwa hili ndugu Mtumishi, Nina shida mimi yaani nasoma Biblia sana lakini maandiko nashindwa kuyashika, sijui kwanini au sisomi ipasavyo kusoma?
5. Bwana asifiwe mtumishi! Namshukuru anaekutumia kuandika masomo mtandaoni hakika yamekuwa msaada kwangu,ilikuwa ni mwaka jana mwezi wa 9 mimba yangu niliyoihangaikia kwa miaka 2 ilitoka na hapo ugomvi katika familia ulianza nikakosa msaada kwani hata Mme wangu aligeuka nikawa mtu wakulia tu,lakini sijui ilikuwaje nikawa naona tu masomo yako kwenye simu yangu kuhusu magumu niliyokuwa napitia,Mungu ni mwema mwezi ule ulikuwa unatoa masomo kuhusu shida nilizokuwa napitia yani utafikiri nilikwambia,hakika kupitia masomo yako nilianza kupata faraja,na roho yakukata tamaa ikaanza kutoweka taratibu,mpaka leo masomo yako yameleta msaada kwangu, nilikupigia simj pia ukaniombea na sasa niko mimba inayoendelea vizuri, endelea kuniombea Mungu anijalie nipate mtoto! Na mwakani Mungu azidi kukutumia kwa viwango vingine vya juu zaidi.
Hizo ni baadhi ya shuhuda ambazo baadhi ya marafiki zangu wamenitumia.
Nimekuletea shuhuda kama zilivyo.
MUNGU akubariki sana.
By Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la MUNGU.




Comments