SHUHUDA

Namshukuru sana Bwana YESU anayewapa shuhuda baadhi ya watu na shuhuda hizo wananijulisha na Mimi niliyewaombea au niliyewafundisha Neno la MUNGU alilonipa ROHO MTAKATIFU.
Utukufu wote kwa MUNGU juu mbinguni.
Baadhi ya shuhuda walizoniandikia watu ni hizi.
1. Bwana Yesu apewe sifa mtumishi Mabula, nakushukuru sana maana baada ya wewe kumwombea mke wangu sasa ni mjamzito.
Sifa, heshima na utukufu ni kwa Bwana Yesu.
2. Shalom mtumishi Mabula.
Heri ya mwaka mpya.
Mwaka ulioisha wewe ulifanyika darasa la kiroho kwangu na kunitoa kutoka hatua moja na kunipeleka hatua nyingine
Ninaposema umenivusha kutoka mbali huwa naamaanisha kweli kweli, kwa muda mrefu wa miaka 9 sasa nilikua naishi na mwanamke bila ndoa takatifu hivo kupitia masomo yako hasa lile la UTHAMANI WA MTU. 1kor 6:20 nilifunga ndoa jana ili na mimi niongeze thamani yangu kwa mwaka 2019.
Asanteeeee mtumishi na Mungu akubariki sana.
3. Ushuhuda wa mwanafunzi anayechukua digrii ya pili.
"Bwana Yesu Asifiwe mtumishi, Namshukuru Mungu maana akili yangu imeanza kufunguka. Darasani mwalimu akifundisha naanza kuelewa, course nne zilizopita nilikua nikiingia darasani sielewi kabisa, nilikua nasubiri wenzangu waje kunielewasha napo nilikua naelewa kwa shida, kiasi ambacho tukiwa tunasoma ikatokea hata najua kitu kidogo kuhusiana na hilo soma walikua hawanisikilizi mpaka mtu mwingine akielezee. Ilifikia mahali hata tukipangwa group na mtu kwa ajili ya kufanya kazi za darasani wananikimbia kwa sababu wanajua sina mchango wowote. Hapa namshukuru Mungu sana ingawa bado wanafunzi wenzangu wananiona sina msaada kwao ila najua ipo siku Mungu ataniheshimisha. Namuomba Mungu hayo masomo mannne niliyoyafanyia mtihani yaani neema yake tu ndo inihurumie. Nakumbuka kuna siku nilikupigia simu na ukaniuliza kwamba "mara ya mwisho ulilia lini?", na mimi nikakujibu "wiki iliyopita" ,ukaniuliza ulikua unalia kuhusu nini? na mimi nikakujibu nilikua namlilia Mungu afungue akili yangu na wewe ukanijibu Mungu atafungua akili yako nikajua tu kulikua na connencton ya mimi, wewe na Roho Mtakatifu, nilimshukuru Mungu na ndio matokeo nimeanza kuona sasa. Mungu akubariki mtumishi wa Mungu na azidi kukuinua kwa viwango vya juu kiroho na kiuchumi.
Amina."
4. Huu nao kwangu ni ushuhuda, rafiki yangu mmoja kutokea nchi jirani aliyekuwa anasumbuliwa sana na majini mahaba kiasi kwamba hadi yazini naye ndipo anaingia katika siku zake(Period) aliniandikia hivi:
SIYO KAMA NAKUSUMBUA MTUMISHI .
WAKATI NAPITIA HAYA MAGUMU NILIKUWA NAMWAMBIA MUNGU NIPE MTU WA KUNISAIDIA .
SIKU MOJA NIKASIKIA SAUTI INANIAMBIA PETER MABULA.
NIKADHARAU SIKULICHUKULIA MAANANI NIKAJUA MAWAZO YANGU.
SIKU INGINE NIKASUKUMWA KUITAFUTA NAMBA YAKO KWENYE MASOMO YAKO.
NIKACHUKUA NAMBA NIKAKAA NAYO MIEZI 4 BILA KUKUTAFUTA.
ILA NILIKUWA NAKUCHUNGULIA KAMA UPO HEWANI KILA WAKATI.
SIKU MOJA NILIWAZA ATA KUFA' NILICHOKA SANA. NIKAMFWATA MCHUNGAJI WANGU NIKAMSIMULIA KIDOGO NIKAMWAMBIA NAHITAJI MAOMBI NIMEINGILIWA JANA NA JINI MAHABA SINA AMANI. PIA KAMA INATOKEA KILA MWEZI.
MCHUNGAJI WANGU AKANIAMBIA NITAKUTAFUTA. NA SIKU HIYO NILIWAHI KANISANI NIKIJUA ATANIFANYIA MAOMBI. NILIMKUTA OFISINI.
NA HII KWA MCHUNGAJI NI MARA YA PILI ;MARA YA KWANZA NILIMUOMBA ANIFANYIE MAOMBI YA UKOMBOZI. AKANIKWEPA.
KWA KWELI NILIUMIA SANA.NILIWAZA MENGI SANA.
ILA ILE SIKU NIKASUKUMWA NIKUTAFUTE WEWE; NIKAAMBIWA HUYU MTU ATAKUSAIDIA.
HAYA MAMBO YALINICHOSHA NIKAENDA KWA MMAMA MMOJA KANISANI KWETU NAE NI MUOMBAJI MZURI. NILISIMULIA TATIZO LANGU(AKACHEKA SANA AKASEMA NEEMA SIJUI TUTACHOMOKA VIPI MIMI MWENYEWE INANITOKEA KAMA WEWE NA WAKATI MWINGINE NAMCHUKIA MUME WANGU.
NDIO TUNAPAMBANA.
NAJUA KUNA USHINDI MBELE YANGU SASA

Baadhi ya shuhuda.
Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu zangu wote.
Nakuletea baadhi ya shuhuda kama nilivyotumiwa na baadhi ya marafiki zangu.

1. Asifiwe Yesu.
Napenda nikushukuru sana mtumishi Wa Mungu.
Mimi ni yule kijana wa Kenya uliyenishauri kumueleza Mchungaji wangu uovu niliomtenda Mungu yaani dhambi ya (uasherati) nilikuwa nimeshindwa nitaanzaje niliwaza kujiua, nikaacha kanisa hata nikahama nyumbani.
Lakini Kwa kukumbuka alikonitoa Mungu na ulivyonishsuri nilitii nikamweleza Mchungaji wangu.
Aliniombea Sala ya toba upya.
Na kuniagiza kutubu.
Ilikuwa ni aibu lakini nikatoka kwake nikiwa huru.
Ahsante sana.

2. Habari za uzima Mtumishi ,namshukuru Mungu Sana pamoja na kutuombea mtoto wangu amefanya vizuri Sana matokeo ya darasa la nne unakumbuka nilikua nakuambia marks zake alizokua anapata? Lakini huu mtihani waTaifa Kuna masomo Amepata A tupu mpaka baba yake ameuliza "Ni wewe kweli au mwingine?"
amefanya vizuri kwa kweli Amepata A -4 ,B-1 na C-1 na wastani B ,utakumbuka nilivyokuwa naumia mtumishi juu ya mwanangu, alikuwa analeta mtihani mpaka wa hesabu 20 kiswahili 47 lakini leo hii hayo masomo yote Amepata A ni SoMo la uraia na maadili ndio kapata C na lenyewe angepata hata B tu angekua na wastani wa A kwa masomo yote ,Mungu ananipigania Sana na kunitetea anajua ninayopitia, Jina lake lihidimiwe Nina furaha na Amani na asante kwa maombi.

3. Mtumishi Mabula Nakushukuru sana kwa ushuhuda wako wa ajabu kuhusu jinsi ulivyosamehe
jambo ambalo uliapa kutolisamehe ambao ushuhuda huo uliutoa kwa Maisha ya ushindi
blog. Mimi ni mwanadada kutoka nchini Kenya na ushuhuda wako ulinivutia sana.
sababu kuu ya kukuandikia ujumbe huu ni kukujulisha kuwa ningependa
kuokoka sana na kuacha dhambi lakini sijui pa kuanzia.
Ningependa uniongoze wokovuni.
Asante.

4. Shalom.
Namtukuza Bwana anaendelea kunipigania.
Nashukuru sana Maombi yako mengi yamefungua ufahamu wangu hasa yale ya kuvunja maneno mabaya ambayo tumewahi kujitamkia au kutamkiwa, na yale ya kuvunja Laana. Kuna maeneo mengi tumejikwamisha wenyewe bila kujua. Ashukuriwe Mungu wetu kwaajili ya utumishi wako.

5. Shalom mtumishi.
Nimebarikiwa saana na soma lako "Jinsi ya kuwashinda mawakala wa shetani"
Mtumishi hili soma nahisi usiku wa jana nimefunguliwa mie. Nimekuja kugundua naishi kwenye Ramani zao wakuu wa giza tangu 2016, Amani kwenye ndoa yangu haipo hali ya hewa imebadilika tunaishi kwa chuki nilijua sijui sababu leo nimejua.
Asante sana na nitafanyia kazi maelekezo yako ya maombi na najua nitafunguliwa.

6. Shalom Mtumishi wa Mungu aliye hai, Leo napenda kusema maneno haya, " Mungu huwezi kumlinganisha na chochote hapa duniani wala mbinguni" kuna siku nilikwambie unisaidie kuomba juu ya uhamisho wa mdogo wangu ukaniombea, maana nilikuwa nimehangaika sana hadi siku za kuzuia uhamisho zikafika sijafanikiwa maana yeye yupo form two, kwa hiyo barua zilisainiwa kote sasa ilipofika kwa afisa elimu mkoa ikashindikana maana tayari walishazuia form two kuhama, nilichokifanya ni kumwambia Yesu kuwa " ulisema kuwa hakuna lisilowezekana kwako, naomba nipate uhamisho" gafla nikapata ujasiri wa kutafuta kuongea afisa elimu akanielewa na hatimaye akapitisha uhamisho! Watu wengi wemerudi bila saini yake lakini Yesu ameweka saini kwangu, sifa na utukufu ni kwa Mungu aliye hai.

Shuhuda zinaendelea.
1. Bwana Yesu apewe sifa mtumishi.
Nashukulu kwa maombi yako Yesu ameniponya, maumivu yameisha . Jana nilikuwa naumwa sana yaani kichwa nilifikia mpaka kumwangia kila baada ya muda.
Baada ya maombi uliyoniombea ugonjwa uliyeyuka na mpaka sasa Mimi ni mzima.

2. Mchungaji Mabula ninakushukuru kwa maombi yako nimemuona Mungu.
Hali ya kiuchumi imekua bora kuliko hapo awali.
Nilikua na hali mbaya sana kiuchumi lakini sasa hivi namshukuru Mungu milango imefunguka.
Mungu aendelee kukutumia kwa viwango vya juu zaidi kwa ajili ya utukufu wake.
Amina

3. Mungu Mkubwa,nimeona Mabadiliko Kwa Kipindi Hiki Kifupi Cha Siku Chache baada ya maombi yako.
Baadhi Ya Ndugu zangu Wameanza Kunikumbuka,lakini Pia Watu Wanaonizunguka Wanaonekana kuanza Kunipenda Hata Wale Waliokua Wananichukia.
Ubarikiwe Mtumishi Kwa Kunisaidia Kwa Maombi, Mungu Akukumbuke

4. Shalom mtumishi nakusalimu katka jina la Bwana YESU, mimiy nipo mbeya, kiukwel napenda kumshukuru sana MUNGU kwa mambo makuu anayo nitendea pia napenda kutoa shukurani zangu za dhati kupitia wewe nimekuwa nikibalikiwa sana na mafundisho yako kupitia facebook nimebalikiwa sana MUNGU akubaliki sana mtumishi maana mafundisho yako yamenisaidia sana.

Bwana YESU asifiwe!
Ninao marafiki wengi sana ila wewe ni mojawapo wa marafiki wa kipekee sana Kwangu.
MUNGU akukumbuke na akubariki, mwaka 2019 uwe ni mwaka wako wa kukumbukwa na MUNGU.
Kama alivyokumbuka nadhiri ya Hana(1 Samweli 1:9) akumbuke na nadhiri zako.

Kama alivyo alivyolikumbuka Neno lake(Zaburi 105:42) akumbuke Neno alilokuambia.
Akumbuke agano lako na yeye(Zaburi 111:5).
Ubarikiwe sana.
Nakutakia mwaka wa baraka na ushindi.

Comments