USIOGOPE KUFANYA KAZI YA MUNGU

Na Mwl Peter Mabula 
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi 



Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe Ndugu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU wa Mbinguni.

◾Mtu mmoja aliniambia kwamba ananichukia sana kwa sababu ya mafundisho yangu. Mtu huyo hadi alisema mambo mabaya kuhusu mimi ila wala sikushtuka kwa sababu yake kwa sababu Injili ilianza kupingwa tangu ilipoletwa na Bwana YESU lakini sijawahi kumuona hata mtu mmoja aliyeipinga injili ya KRISTO na akaishinda.

◼️Wote walioipinga Injili ya KRISTO ni wao walikuja kuondoka na kuiacha Injili ikiendelea mbele zaidi na zaidi.

Kwangu mimi niliposikia hivyo kutoka kwa mtu huyo nilijua kabisa inawezekana wako wengi sana wa aina yake, sikuwajali bali niliendelea kufundisha Neno la MUNGU.

✓✓Kazi ya Injili lazima iendelee mbele Haijalishi nani na wa wapi hataki.

Isaya 58:1 "Piga kelele, usiache, Paza sauti yako kama tarumbeta; Uwahubiri watu wangu kosa lao, Na nyumba ya Yakobo dhambi zao."

Ndugu, inawezekana wewe ni Mtumishi Mwaminifu wa Bwana YESU na unashindana na watu wengi kwa sababu tu unawahubiria injili safi ya Wokovu wa KRISTO,
Ndugu, napenda kukuambia kwamba wewe sio Mtumishi wa kwanza kupingwa, bali wapo watumishi pia walipingwa lakini kwa sababu kuhubiri kwao kulikuwa kulitimiza kusudi la MUNGU basi Bwana YESU alitokea kwao na kuwaambia hivi '' Usiogope, bali nena, wala usinyamaze,kwa kuwa mimi ni pamoja nawe, wala hapana mtu atakayekushambulia ili kukudhuru; kwa maana mimi nina watu wengi katika mji huu. -Matendo 18:9-10 ''

◼️Hata wewe leo Bwana YESU anakuambia kwamba usiogope bali nena Neno la MUNGU wala usinyamaze.

1 Wakorintho 15:58 "Basi, ndugu zangu wapendwa, mwimarike, msitikisike, mkazidi sana kutenda kazi ya BWANA sikuzote, kwa kuwa mwajua ya kwamba taabu yenu siyo bure katika BWANA."

✓✓Jambo la kujua ni kwamba kuna watu wanakupinga kwa sababu wewe uko katika nuru na wao wako katika giza, inawezekana wanakupinga kwa sababu maombi yako yanaharibu nguvu zao za giza walizozitegemea.

✓✓Ndugu hakikisha unaendelea kuwaambia watu kweli ya MUNGU ya Wokovu wa YESU KRISTO ili waokoke na kuachana na dhambi zao.


◼️Neno la MUNGU litasimama, wala halitayumbisha.

Ndugu mmoja aliniandikia ujumbe huu hapa chini na nikabaki nashangaa.
Ujumbe huo uko hivi;

"Mtumishi Mabula asante sana kwa maombi yako na masomo yako mbalimbali. Mimi nimeokoka na nampenda YESU. Nimehamia Mkoani kwa sasa ila zamani nilikuwa Wilayani na huko ndiko nilikookokea na baadae nikawa kiongozi Kanisani.
Kabla ya hapo nilikuwa na kazi nzuri Wilayani nikaondolewa, nilikuwa na kiwanja chenye hati nikakatazwa kujenga, na aliyenikataza ni yule Kiongozi wa Wilaya ambaye alinipa hati, yaani uchumi wangu ukapigwa hadi nikabaki nashangaa.
Baadae nikawa najifunza masomo yako na nikawa nayaandika na kuyatumia kufundisha Kanisani, hasa masomo ya Maombi maana Mimi nilikuwa kiongozi wa Maombi Kanisani.

Nilipokuwa kiongozi wa maombi Kanisani, kuna mama alikuwa mzee wa Kanisa akaanza kutukataza kuomba maombi ya vita, mimi niliendelea kutafuta mafundisho yako, nafanya maombi ya vita,kwa kuwaongoza watu, yeye akawa na baadhi ya watu, hawapendi hayo maombi, yaani alishawishi watu kuyakataa maombi ya vita. MUNGU alionekana sana kupitia Maombi hayo. 
Baada ya siku chache kuna siku Mchungaji alikuwa anawaombea watu Kanisani kwenye Ibada ya Jumapili. Mtoto mmoja akaanguka mapepo na mapepo yale kusema kwamba yule mama ambaye ni mzee wa Kanisa ni mchawi na aliwatuma hao mapepo kupitia chakula aina ya nyama. Ni kweli mama yule kuna kipindi alitugawia nyama na hata Mimi na mke wangu tulipewa nyama hizo tukala, kumbe zilikuwa zimeambatanishwa na nguvu za giza.
Mapepo Yale yakaweza wazi na ndipo ikajulikana kwamba yule mzee wa Kanisa ni mchawi. Baada ya pale yule mama akawa anaonyesha chuki live, alijua nimemgundua uchawi wake.
Maisha yaliendelea ila baadae Nikaamua nihamie hapa Mkoani mjini. Siku moja tunamuombea mtoto mmoja mapepo yakalipuka na kusema uchawi wa yule mama na yakasema yakinitaja Mimi kwa jina yakisema kwamba "
tumembana huyu kiuchumi,ila bado mpaka tumpate, anajifanya anatupiga kweli kimaombi. Nikiwa hapa mkoayni mwanangu wa kike wa kwanza yuko sekondari. Siku moja akaingia darasani akadondoka, akaombewa,mapepo yakasema hatutaki asome, tunataka babaake asifanikiwe. yanasema yale mapepo kwamba yametoka kule wilayani nilikokuwa mwanzo. Na Yale mapepo yakasema tumeweka agano huyu asifanikiwe.
Ndo hayo mapambano Mtumishi, Ila muda mwingi nafanya maombi ya kufunga na maombi ya vita.
Nakushukuru sana kwa maombi yako maana sasa nimeshinda.
Naamini mchawi yule na wenzake wamepigwa.
Juzi juzi kampigia simu mke wangu akitaka ajue kuhusu huku ila najua ameipatapata.
Mtumishi nashukuru uliniombea na nimeomba kazi na na kati ya wote tumeitwa 30 na najua Mimi ni mshindi kwa jina la YESU KRISTO. Endelea tu kuniombea Mtumishi."

Ninachotaka kusema kuhusu ushuhuda huu ambao rafiki huyu alinitumia ni kwamba;.
✓✓Ndugu huyu alichukiwa na Kiongozi wake kwa ajili ya Injili, ila Injili ya KRISTO ilishinda.

✓✓Injili ilitumika kufichua uovu wa aliyeipinga. Hiyo ndio kazi ya Neno la MUNGU.

Waebrania 4:12 "Maana Neno la MUNGU li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo."

✓✓Ndugu kuchukiwa kwa ajili ya kazi ya MUNGU kupo na kutaendelea kuwepo hivyo usiogope, endelea kuhubiri habari za KRISTO kwa watu wote.
Kumbuka Wateule wa KRISTO waaminifu ni kama Kondoo katikati ya mbwa mwitu wakali maana mbwa mwitu hawataki Injili ya KRISTO iliyo hai iokoayo.

Mathayo 10:16-18 " Angalieni, mimi nawatuma kama kondoo kati ya mbwa-mwitu; basi iweni na busara kama nyoka, na kuwa watu wapole kama hua.  Jihadharini na wanadamu; kwa maana watawapeleka mabarazani, na katika masinagogi yao watawapiga; nanyi mtachukuliwa mbele ya maliwali na wafalme kwa ajili yangu, kuwa ushuhuda kwao na kwa mataifa."

◼️Wewe usiogope Bali endelea kuhubiri Injili ya Bwana YESU KRISTO Mwokozi.


Zingatia  na MUNGU atakubariki sana.
Mche MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi na utaitwa heri.
Kama pia unatumia Facebook ni follow maana itafika kipindi nitakuwa napost tu katika page yangu na profile yangu.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter  Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292.
Ubarikiwe sana 

Comments