UTAKASO NI NINI?

Na Mwl Peter Mabula 
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi 



Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe Ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU wa Mbinguni.

◾Utakaso ni nini?

✓✓Utakaso ni hali ya kupata kibali cha MUNGU cha kusafishwa dhambi.

Kibali cha MUNGU cha kufutwa kwa dhambi za mwanadamu yeyote kipo katika KRISTO YESU kwa njia ya kumpokea kama Mwokozi kisha kutubu katika yeye.

1 Yohana 2:12 '' Nawaandikia ninyi, watoto wadogo, kwa sababu mmesamehewa dhambi zenu, kwa ajili ya jina lake. ''

✓✓Utakaso ni hali ya kusamehewa dhambi na kusafishwa dhambi kwa damu ya YESU KRISTO.

◼️Kazi ya kusamehe dhambi ni ya MUNGU, kazi ya kufuta dhambi ni ya Damu ya MUNGU, kazi ya kusafisha dhambi ni ya Damu ya YESU KRISTO.

1 Yohana 1:7 '' bali tukienenda nuruni, kama yeye(MUNGU) alivyo katika nuru, twashirikiana sisi kwa sisi, na damu yake YESU, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote. ''

◼️Sasa ndani ya mtu aliyepata utakaso wa damu ya YESU KRISTO, ndani ya mtu huyo kuna kibali cha ROHO MTAKATIFU kuingia kwa mtu huyo na kumuongoza katika kusudi la MUNGU.

◼️Njia ya kwanza ya kumpokea ROHO MTAKATIFU ni kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako kisha ukatubu na kuacha dhambi.

✓✓Ndani ya Mtu aliyetakaswa kwa damu ya YESU KRISTO kuna ROHO MTAKATIFU.

Lakini ndani ya mtu ambaye hajatakaswa kwa damu ya YESU KRISTO, ndani ya mtu huyo kuna maroho ya giza, hivyo ni muhimu sana kila mtu kuuhitaji utakaso wa damu ya YESU KRISTO ndani yake, kwa kuokoka, kutubu na kuacha dhambi ili ROHO MTAKATIFU aingie kwa mtu huyo na kufanya makazi.

✓✓Utakaso wa damu ya YESU KRISTO unaambatana na nguvu za ROHO MTAKATIFU ndani ya mtu husika, hivyo ndugu hakikisha umetakaswa kwa damu ya YESU KRISTO.

◼️Katika maombi yako tubu kisha omba kwa MUNGU ili damu ya YESU KRISTO ikutakase yaani ikufutie hatia, adhabu na dhambi zote zilizotokana na dhambi na tena damu ya YESU KRISTO itakufanya usiwe mchafu.

✓✓Ukiona Mkristo ameokoka na bado ana mapepo au ana nguvu za giza maana yake huyo ameuruhusu MUNGU amfutie dhambi ila hajairuhusu Utakaso.

Ndugu, unapoomba maombi ya toba ukitumia damu ya YESU KRISTO kumbuka kwamba damu ya YESU KRISTO ina kazi mbili katika kipengele hicho cha kutubu.
✓✓Damu ya YESU inafuta dhambi na inatakasa, hivyo usiishie tu kuomba kwamba damu ya YESU ikufutie dhambi bali ihitaji pia ili ikutakase na kukutenga mbali na nguvu za giza.

1 Yohana 1:9 '' Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote. ''

◼️Hakikisha umetubu na kuacha dhambi na kutakaswa kwa damu ya YESU KRISTO.
Zingatia  na MUNGU atakubariki sana.
Mche MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi na utaitwa heri.
Kama pia unatumia Facebook ni follow maana itafika kipindi nitakuwa napost tu katika page yangu na profile yangu.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter  Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292(Ushauri, Maombezi, Whatsapp n.k)
Share ujumbe huu kwenye magroup ya Whatsapp uliyopo.
Ubarikiwe

Comments