YESU KRISTO ANATAKIWA KUINULIWA JUU SANA.

Na Mwl Peter Mabula 
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi 



Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu zangu wote.
Karibuni tujifunze Neno la MUNGU.

◼️YESU KRISTO anatakiwa kuinuliwa juu sana.

✓✓Wahuhiri wengi kosa kubwa sana wanalolifanya kujiinua wao, kuinua huduma zao, kuinua madhehebu yao na kuinua mambo mengine, ni jambo baya sana.

◼️Ukisoma Biblia nzima katika mahubiri ya injili utaona anayeinuliwa ni YESU KRISTO kwa utukufu wa MUNGU Baba.

◼️Ndugu, unayemtumikia MUNGU hakikisha unamwinua YESU KRISTO maana hakuna Mwokozi mwingine wa uzima ila ni huyo pekee.

Yohana 12:32 "Nami nikiinuliwa juu ya nchi, nitawavuta wote kwangu."

✓✓Kila Mkristo au Mtumishi ana wajibu wa kumwinua YESU KRISTO.

✓✓Ndugu, mwinue YESU KRISTO mbele za marafiki zako ili wampokee kama Mwokozi.

✓✓Mwinue YESU KRISTO mbele ya Kanisa ili kila aliye Kanisa aambatane na YESU KRISTO daima.

✓✓Mwinue YESU KRISTO mbele za watu wote ili wamkimbilie kama Mwokozi.

◼️Kumbuka hakuna Mwokozi mwingine yeyote kwa ajili ya uzima wa milele.

Matendo 4:12 "Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo."

◾Changamoto ya baadhi ya makanisa leo ni kuwafanya waumini wajione wao ndio muhimu hivyo mtaani na popote walipo utawasikia wakisema "sisi ni watoto wa nabii Fulani au Mchungaji Fulani au mtume Fulani"
Yaani watu utambulisho wao sio YESU KRISTO tena ila ni dhehebu au kiongozi wao wa kiroho.

✓✓Wanainua dhehebu na mtu wakati anayepaswa kuinuliwa ni YESU KRISTO.

✓✓ROHO MTAKATIFU kazi yake mojawapo ni kumtukuza Bwana YESU, na ROHO MTAKATIFU akiwa ndani ya mtu atamfanya Mteule kumtukuza YESU KRISTO kwa utukufu wa MUNGU Baba.

Yohana 16:14 " Yeye(ROHO MTAKATIFU) atanitukuza mimi(YESU KRISTO), kwa kuwa atatwaa katika yaliyo yangu na kuwapasha habari."

◼️Kumbuka kumtukuza YESU KRISTO ndio pia kumtukuza MUNGU Baba wa mbinguni.

Yohana 8:54 "YESU akajibu, Nikijitukuza mwenyewe, utukufu wangu si kitu; anitukuzaye ni Baba yangu, ambaye ninyi mwanena kuwa ni MUNGU wenu."

◼️Mkristo usipokuwa na tabia ya kumwinua Bwana YESU KRISTO utakuwa unakosea sana sana.

◼️Biblia inasema Bwana YESU KRISTO anatakiwa kuinuliwa juu.

Yohana 3:14-15 "Na kama vile Musa alivyomwinua yule nyoka jangwani, vivyo hivyo Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa; ili kila mtu aaminiye awe na uzima wa milele katika yeye."

✓✓Wewe mkristo usipomwinua YESU KRISTO utamwinua nani?

✓✓Ni makosa makubwa kama humwinui Bwana YESU KRISTO.

Wako watu wako busy usiku na mchana kuwainua wachungaji wao, wainjilisti wao, walimu wao, manabii wao na mitume wao na sio kumwinua YESU KRISTO, hayo ni makosa.

✓✓Kumbuka hakuna Mtumishi anayeweza kumpeleka mtu uzima wa milele, hivyo kumwinua huyo mtu ni kuonyesha hujui ukifanyacho maana hakika faida hata moja.

◼️Ndugu, jifunze kwa Mtume Petro ambaye katika mahubiri yake alimtaja Paulo mara moja sehemu moja tu( 2 Petro 3:15 ) ila alimtaja Bwana YESU KRISTO mara nyingi sana maana ni YESU pekee ndio anapaswa kuinuliwa.

1 Petro 4:14 "Mkilaumiwa kwa ajili ya jina la KRISTO ni heri yenu; kwa kuwa ROHO wa utukufu na wa MUNGU anawakalia."

◼️Jifunze kwa Mtume Yohana ambaye alimtaja Mtume Petro mara chache sana katika vitabu vyake mfano ( Yohana 21:21) lakini alimtaja YESU KRISTO mara nyingi sana.

2 Yohana 1:9 "Kila apitaye cheo, wala asidumu katika mafundisho ya KRISTO, yeye hana MUNGU. Yeye adumuye katika mafundisho hayo, huyo ana Baba(MUNGU) na Mwana(YESU) pia."

Leo Mimi nakutana kila siku na Wakristo ambao katika maongezi yao yote ni mara chache sana kuwasikia wakimtaja Bwana YESU KRISTO lakini viongozi wao wa kiroho huwataja mara nyingi sana, ni vibaya sana.

✓✓Ndugu kama ulikuwa hujui ni kwamba  shetani anaweza kuwafanya watu wasimwinue YESU KRISTO ili kupunguza kundi la kuufuata Wokovu wa KRISTO.

◼️Ndugu, wewe mwinue YESU KRISTO na sio kuwainua wanadamu.

◼️Anayetakiwa kuinuliwa juu ni YESU KRISTO na sio wanadamu.

✓✓Mwinue YESU KRISTO na mtukuze MUNGU.

◼️Mwinue YESU KRISTO ili watu wamtukuze MUNGU.

◼️Anayetakiwa kuinuliwa ni YESU KRISTO na sio nabii, Mchungaji wala Mtume wala Mtumishi yeyote hatakiwi kuinuliwa.

◼️Wewe mwinue YESU KRISTO kila uliko maana ni yeye ndiye anayepaswa kuinuliwa, kwa utukufu wa MUNGU Baba.

Wafalisayo hawakujua kwamba KRISTO YESU anatakiwa kuinuliwa.

Yohana 12:34 " Basi mkutano wakamjibu, Sisi tumesikia katika torati ya kwamba KRISTO adumu hata milele; nawe wasemaje ya kwamba imempasa Mwana wa Adamu kuinuliwa? Huyu Mwana wa Adamu ni nani?"

Hawa hawakuwa wanajua kwa usahihi maana Bwana YESU alikuwa hajatukuzwa, kwa sasa ameshatukuzwa hivyo wewe huna haja ya kuacha kumwinua, mwinue Bwana YESU KRISTO na kwa njia hiyo utakuwa unahubiri injili ya uzima wa milele.

2 Wakorintho 4:5-6 "Kwa maana hatujihubiri wenyewe, bali KRISTO YESU ya kuwa ni Bwana; na sisi wenyewe kuwa tu watumishi wenu kwa ajili ya Yesu. Kwa kuwa MUNGU, aliyesema, Nuru itang'aa toka gizani, ndiye aliyeng'aa mioyoni mwetu, atupe nuru ya elimu ya utukufu wa MUNGU katika uso wa YESU KRISTO."

Zingatia  na MUNGU atakubariki sana.
Mche MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi na utaitwa heri.
Kama pia unatumia Facebook ni follow maana itafika kipindi nitakuwa napost tu katika page yangu na profile yangu.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter  Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292.
Ubarikiwe sana

Comments