![]() |
| Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu zangu wote.
◼️Namshukuru ROHO MTAKATIFU maana amenipa ujumbe huu ili Mtu aliyekusudiwa apokee na azishinde nguvu za giza zilizopanga mipango mibaya kwake wakati huu au mwaka huu.
Shetani na Mawakala zake nao Wana fikira zao juu ya Watu wema, fikira hizo ndio mipango yao mibaya.
2 Wakorintho 2:11" Shetani asije akapata kutushinda; kwa maana hatukosi kuzijua FIKIRA ZAKE."
Je mipango/fikira za shetani juu Yako ni nini?
Ndugu jambo la kujua ni kwamba shetani na walio upande wake wote hawajawahi kukupangia jambo jema hata Moja,ndio maana Unamhitaji sana YESU KRISTO ili umshinde shetani na Mawakala zake wote.
◼️Katika KRISTO YESU mawakala wa shetani wanaweza kushindana na Wewe katika jambo lolote lakini hawatakushinda ukiomba.
Yeremia 1:19 "Nao watapigana nawe; lakini hawatakushinda; maana mimi nipo pamoja nawe, asema BWANA, ili nikuokoe."
◾Jambo lingine Mimi Peter Mabula nataka ujue Wewe Rafiki yangu ni kwamba kuna Ulimwengu wa roho na kuna Ulimwengu wa mwili.
✓✓Kuna aina mbili za ulimwengu wa roho ambazo ni Ulimwengu wa roho wa nuru na Ulimwengu wa roho wa giza.
✓✓Mwanadamu yeye anaishi katika ulimwengu wa mwili.
◼️Ulimwengu wa roho wa nuru uko chini ya MUNGU mwenyewe na Biblia inasema kwamba MUNGU anatuwazia mema sisi wanadamu, na ametupa Neema katika KRISTO YESU ili tuombe atatupa au tumtafute ataonekana kwetu.
Yeremia 29:11-13 " Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema BWANA, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho. Nanyi mtaniita, mtakwenda na kuniomba, nami nitawasikiliza. Nanyi mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote."
◾Ulimwengu wa roho wa giza uko uko chini ya shetani ambapo Biblia inasema kazi ya ulimwengu wa roho wa giza kwa wanadamu ni kuiba kiroho, kuharibu kiroho na kuua kiroho.
Yohana 10:10 "Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; ......"
◼️Sasa mwanadamu anaishi katika ulimwengu wa mwili na kila jambo hadi litokee katika ulimwengu wa mwili lazima kwanza liwe limeanzia ulimwengu wa roho.
✓✓Jambo la kujua ni kwamba matatizo mengi yanayowatokea wanadamu chanzo chake ni ulimwengu wa roho wa giza na sio ulimwengu wa roho wa nuru.
Biblia iko wazi sana katika Maombolezo 3:33 kwamba " Maana moyo wake(MUNGU) hapendi kuwatesa wanadamu. Wala kuwahuzunisha."
✓✓Kumbe MUNGU hapendi kuwatesa wanadamu wala kuwahuzunisha, ukiona vifungo, mateso na uonevu kwako ujue chanzo ama ni wewe au ni nguvu za giza.
✓✓Watu wengi wakijikuta kwenye matatizo husingizia MUNGU amewaacha au MUNGU ameruhusu na kumbe tatizo ni wao au nguvu za giza walizoziruhusu wao.
✓✓Sasa najua kabisa wewe umepanga mipango yako ya wakati huu au mwaka huu, umefanya vyema sana lakini kumbuka pia ulimwengu wa roho wa giza unaweza kumpangia Mtu mambo mabaya ya kutokea wakati huu au mwaka huu kwake, wewe utakayezijua siri hizi katika somo hili nina hakika ukiomba utazuia kila mipango kutokea ulimwengu wa roho wa giza kwa ajili yako.
◼️Ashukuriwe MUNGU maana ROHO MTAKATIFU hutupa kuzijua fikra za shetani hivyo tukiomba tunamshinda shetani
na mawakala zake wote.
2 Wakorintho 2:11" Shetani asije akapata kutushinda; kwa maana hatukosi kuzijua FIKIRA ZAKE."
◾Nini wanaweza kukupangia mawakala wa shetani katika mwaka wako huu?
Wanaweza kukupangia ratiba ya kipepo ili yaliyo ndani ya ratiba hiyo yakupate.
wanaweza kukuandalia kalenda za kichawi, wanaweza kukuandalia matukio ya kipepo na wanaweza kukucholea ramani ya kipepo na wakahakikisha mwaka mzima unatembea kwenye ramani hiyo ya giza.
✓✓Kuna watu kila mwaka anaandika mipango labda mitano au yeyote ili itimie mwaka huo kwake lakini kila mwaka haitimii, tatizo ni hayo mambo manne niliyokutajia hivyo ukishughulika kimaombi hakika utashangaa mipango ya shetani inakufa na mipango yako iliyo katika MUNGU inatimia yote.
✓✓Kama kila mwaka unafuatiliwa na nguvu za giza mwaka huu kimaombi jikomboe kutoka hizo nguvu za giza.
✓✓Kumbuka unao maadui unaowajua na usiowajua na wakati mwingine adui zako wanaweza kuwa wengi kuliko idadi ya nywele za kichwa chako.
Zaburi 69:4 "Wanaonichukia bure ni wengi Kuliko nywele za kichwa changu. Watakao kunikatilia mbali wamekuwa hodari, Adui zangu kwa sababu isiyo kweli. Hata mimi nalilipishwa kwa nguvu Vitu nisivyovichukua."
◾Kuna maadui wengi wanaoweza kukupangia mipango na usipojua namna ya kuwashinda kiroho wanaweza kukushinda kila wakati na kila mwaka.
✓✓Kuna maadui wachawi, majini, wakuu wa giza, kuzimu, waganga wa kienyeji ulikopelekwa na mtu anayekuchukia, washirikina na wanadamu wanaotumika kishetani dhidi yako, hao wote ni maadui wanaoweza kukupangia ratiba, ramani, matukio au kalenda ili tu uendelee kuteseka katika hicho walichokusudia.
◾Mawakala wa shetani wanaweza kukupangia ratiba au matukio katika huu mwaka , wanaoweza kukupangia kalenda ya miaka hata mitatu yaani yaliyokufunga tangu mwaka juzi hata mwaka huu yanaendelea.
◼️Ndugu kuna kutoka ukizingatia mbinu za maombi nitakazokuletea katika somo hili, Neno halisi la MUNGU huwa haliji bure, waliokusudiwa naamini mwisho wa mwaka huu watanipa shuhuda kwa jina la YESU KRISTO.
✓✓Kuna watu hudhani ni kwema tu hivyo hamna haja ya kuomba.
Ndugu, ni Biblia ndio inasema kwamba kila Mkristo anao maadui, yuko vitani na inampasa kushinda.
Waefeso 6:12 " Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho."
✓✓Kwa maombi leo unaweza kuzuia matukio yote ya kichawi yaliyoandaliwa mwaka huu mwezi wowote kwako.
✓✓Kazi yako kama muombaji ni kudhibiti kazi zote za kipepo zilizopangwa kwa ajili ya wakati huu kwako.
✓✓Unaweza kuichana leo ratiba ya kishetani iliyopangwa kuhakikisha mwaka huu hufungi ndoa, hupati kazi, ndoa yako haipati amani n.k
✓✓Inawezekana unakusudia mwaka huu ununue kiwanja, ufunge ndoa, upate uzao, upate kazi n.k
Mipango yako inaweza kufutwa na wakuu wa giza usipoomba, kama kalenda yao ya vifungo kwako inaendelea basi basi usipoifuta ujue wanaweza kukuzuia na mwaka huu.
Ngoja nikupe mfao hai mmoja.
Zaburi 102:20 " Ili akusikie kuugua kwake aliyefungwa, Na kuwafungua walioandikiwa kufa."
◼️Biblia inasema kwamba MUNGU atawafungua walioandikiwa kufa.
✓✓Atawafungu wakati gani?
Ni pale utakapoomba ili kuharibu roho ya mauti iliyokusudiwa kwako.
✓✓Sasa kwa sababu Biblia inaonyesha kwamba wapo walioandikiwa kufa ila MUNGU akawaokoa na kifo hiyo ina maana kwamba MUNGU hakuwaandikia kufa wakati huo.
Mawakala wa shetani ndio wanaweza kumwandikia mtu kufa katika majira waliyokusudia katika mwaka.
Inawezekana yuko mtu anasoma somo hili muda huu na wakuu wa giza wamepanga mwaka huu huu ndoa yake ife, uchumba ufe, biashara ife, watu wake muhimu wafe n.k
Nini ufanye katika Maombi?
1. Kwa Maombi hiyo ratiba ya kishetani kukuhusu ichane kwa jina la YESU KRISTO na kuichoma moto kwa Damu ya YESU KRISTO.
Matendo 19:19 "Na watu wengi katika wale waliotumia MAMBO YA UGANGA wakakusanya vitabu vyao, WAKAVICHIMA MOTO ....."
✓✓Vitabu vya wachawi na waganga wa kienyeji vinaweza hata kuandikwa Nini kimpate Mtu mwema.
◼️Hiyo ratiba ya kipepo iliyoandikwa iwe ni kuzimu, kwa mganga au kwenye Madhabahu za giza ifute kwa Jina la YESU KRISTO.
2. Kwa Maombi futa matukio ya kichawi kwako yaliyopangwa kukuhusu Wewe wakati huu au mwaka huu.
✓✓Je wamekupangia mwaka huu?
✓✓Je wamepanga uumwe, ufe, ufukuzwe kazi, ufilisike, uache au wamekupangia Nini?
Ndugu, Isaya 7:7 inasema jambo hilo halitakuwa Wala halitasimama ukimkimbilia MUNGU kwa Jina YESU KRISTO Mwokozi kwa Maombi.
Isaya 7:7 "Bwana MUNGU asema hivi, Neno hili halitasimama wala halitakuwa."
✓✓Ukisema ugonjwa huu hautakuwa Wala hautasimama ujue ni kweli ugonjwa huo hautakuwa kwako.
✓✓Ukisema kwa Jina la YESU KRISTO zuio la kunizuia kupata kazi, kufungua Biashara na kufunga Ndoa hilo zuia halitakuwa Wala halitasimama uwe na uhakika itakuwa hivyo, omba katika Jina la YESU KRISTO utamuona MUNGU wa Miujiza.
3. Kwa Maombi haribu ramani yote ya kichawi waliokupangia mawakala wa shetani wakati huu au mwaka huu.
◼️Una mamlaka katika Jina la YESU KRISTO ya Kufunga kila ramani ya kichawi ulilopangiwa na Mawakala wa shetani wote.
Mathayo 16:19 "Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lo lote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni."
Ramani ya kichawi maana yake wamekupangia utaanzia hapa mwaka huu Kisha utaishia hapa, yaani kama utaanza mwaka huna kazi pia utamaliza mwaka huna kazi, utaanza mwaka unaumwa umalize mwaka umekufa, Leo katika Jina la YESU KRISTO kataa na Funga ramani za kuzimu zote kuhusu Wewe, una Mamlaka katika Jina la YESU KRISTO hivyo Omba.
4. Futa kalenda za kichawi zote kuhusu Wewe.
Kama unavyojua kalenda za kawaida zilivyo Kuna siku zimewekewa alama kwamba siku fulani ni sikukuu fulani, siku fulani hakutakuwa na kazi n.k
Sasa kwenye ulimwengu wa roho wa giza wanaweza kutengeneza kalenda yao kwamba siku fulani mwezi fulani huyu apate ajali, aachwe, aibiwe, duka lake liwake moto n.k
Leo Wewe kwa Mamlaka ya Jina la YESU KRISTO katika Maombi futa kalenda zote za kichawi na zitafutika.
Ukifuta kalenda hizo ujue Nguvu za giza zilizopewa tarehe hiyo ili kuja kukutesa hawatakuja, kwanza hawatajua hata kama Kuna ratiba hiyo kuhusu Wewe.
Ndugu ukiomba katika Jina la YESU KRISTO utatendewa hakika.
Yohana 14:14 "Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya."
5. Mshukuru MUNGU kwa Maombi.
Zaburi 9:1 "Nitamshukuru BWANA kwa moyo wangu wote; Nitayasimulia matendo yako yote ya ajabu;"
✓✓Unaweza pia kumshukuru MUNGU kwa sadaka ya shukrani na Maombi.
Zaburi 50:23 "Atoaye dhabihu za kushukuru, Ndiye anayenitukuza. Naye autengenezaye mwenendo wake, Nitamwonyesha wokovu wa MUNGU."
Zingatia na MUNGU atakubariki sana.
Mche MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi na utaitwa heri.
Kama pia unatumia Facebook ni follow maana itafika kipindi nitakuwa napost tu katika page yangu na profile yangu.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292.
Ubarikiwe sana.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292.
Ubarikiwe sana.

Comments