![]() |
Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu zangu.
Natamani kila Mtu ausome ujumbe huu hadi mwisho.
Karibuni tujifunze mambo kadhaa kuhusu baraka.
Karibuni tujifunze mambo kadhaa kuhusu baraka.
Zaburi 3:8 "Wokovu una BWANA; Baraka yako na iwe juu ya watu wako.'
Baraka ni nini?
✓✓Baraka ni Nguvu ya MUNGU iletayo mafanikio katika Maisha ya Mtu husika.
Mwanzo 24:1 "Basi Ibrahimu alikuwa mzee mwenye miaka mingi, na BWANA alikuwa amembariki Ibrahimu katika vitu vyote."
✓✓Baraka ni roho ya MUNGU inayomsaidia Mtu kufanikiwa katika Yale mema anayoyafanya.
Ni Muhimu uwe na kazi njema ya kufanya ili roho ya MUNGU ya baraka ifanye kazi kwako.
Waamuzi 5:24 "Atabarikiwa Yaeli kuliko wanawake wote; Mkewe Heberi, Mkeni, Atabarikiwa kuliko wanawake wote hemani."
✓✓Baraka ni Nguvu ya MUNGU inayofanikisha mambo mema na makubwa yanayoleta usitawi kwa Mtu.
Mwanzo 25:11 "Ikawa, baada ya kufa kwake Ibrahimu, MUNGU akambariki Isaka mwanawe. Naye Isaka akakaa karibu ya Beer-lahai-roi."
◼️Baraka huanzia kwanza katika ulimwengu wa roho ndipo huja kutimia katika ulimwengu wa mwili.
Waefeso 1:3 "Atukuzwe MUNGU, Baba wa Bwana wetu YESU KRISTO, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake KRISTO;"
◼️Hivyo ni Muhimu sana kuwa mtii wa mambo ya rohoni ambayo ROHO MTAKATIFU anakuambia katika ulimwengu wa roho.
Kumbu 11:27 "baraka ni hapo mtakapoyasikiza maagizo ya BWANA, Mungu wenu, niwaagizayo leo;"
◼️Uwe Mtu wa kupambana kiroho kwa Maombi katika Jina la YESU KRISTO dhidi ya wezi wa baraka maana kiroho baraka inaweza kuibiwa na usiipate kabisa hata kama ilikuwa Yako.
Mfano hai ni kwenye hili andiko ambapo baraka ya Esau ilichukuliwa na Yakobo.
Mwanzo 27:35 "Akasema, Nduguyo amekuja kwa hila, akauchukua mbaraka wako."
Kuna vyanzo vingi vya baraka lakini Mimi Peter Mabula kwa Ufunuo nakuletea vyanzo 4 Muhimu sana vya baraka za MUNGU.
1. Mtu kutii maagizo ya MUNGU na kanuni za MUNGU za namna ya kubarikiwa.
Zaburi 128:4-6 "Tazama, atabarikiwa hivyo, yule amchaye BWANA. BWANA akubariki toka Sayuni; Uone uheri wa Yerusalemu siku zote za maisha yako;
Naam, ukawaone wana wa wanao. Amani ikae na Israeli."
✓✓Kumcha MUNGU kunaweza kuwa chanzo kikuu cha baraka za mtu.
✓✓Kumcha MUNGU kunaweza kuhusisha mtu kuwa mtoaji Sadaka, Zaka na Dhabihu, mtu kuwa muombaji, mtu huyo kuwa anatii maelekezo ya ROHO MTAKATIFU n.k
Kumbukumbu la Torati 28:2 na baraka hizi zote zitakujilia na kukupata usikiapo sauti ya Bwana, Mungu wako.
◼️Ni vyema sana kumtii MUNGU na kutembea kwenye kanuni zake mbalimbali za namna ya kubarikiwa.
2. Mtu kuwa na mahusiano mema mema na aliyebarikiwa tayari.
✓✓Kuwa na mahusiano mema na mtu aliyebarikiwa kunaweza kuwa chanzo cha baraka kwa mtu husika.
◾Mfano hai ni Potifa aliyebarikiwa kwa sababu alikuwa na uhusiano mzuri na Yusufu ambaye kwenye ulimwengu wa roho alikuwa mbarikiwa tayari.
Mwanzo 39:5 "Ikawa tokea wakati alipomweka awe msimamizi juu ya nyumba yake, na vyote vilivyomo, BWANA akabariki nyumba ya yule Mmisri kwa ajili ya Yusufu. Mbaraka wa BWANA ukawa juu ya vyote alivyokuwa navyo katika nyumba, na katika shamba."
◾Mfano hai Mwingine ni Labani alibarikiwa kwa sababu alikuwa na uhusiano mzuri na Yakobo mbarikiwa.
Mwanzo 30:27 "Labani akamwambia, Iwapo nimeona fadhili machoni pako, kaa, maana nimetambua ya kwamba BWANA amenibariki kwa ajili yako."
Sasa ukiangalia habari za Yusufu na Yakobo sio kwamba wakati huu walikuwa matajiri wa kimwili Bali walikuwa matajiri wa kiroho ndio maana Labani na Potifa walipojihusisha nao walibarikiwa.
Hiyo ikufundishe kwamba Kuna Mtu sio tajiri Sasa ila ukiwa na uhusiano naye mzuri unakuwa tajiri Wewe hata kabla yake.
Hivyo baada ya somo hili sio kwamba uwafuate matajiri wa kimwili ili uwe na urafiki nao ndipo utajirike, usifanye hivyo maana Kuna matajiri wa kimwili utajiri wao chanzo chake ni shetani hivyo ukijihusisha nao ndio unakuwa maskini zaidi maana Nguvu ya MUNGU ya baraka ndani Yako ndio itaondoka kabisa.
Ndio maana ni Muhimu sana kumsikiliza ROHO MTAKATIFU.
Ila ukiwa na uhusiano mzuri na Mtu aliyebarikiwa kiroho hakika na Wewe utabarikiwa.
◼️Biblia inasema kwamba YESU KRISTO ni mbarikiwa.
Mathayo 21:9 "Na makutano waliotangulia, na wale waliofuata, wakapaza sauti, wakisema, Hosana, Mwana wa Daudi; ndiye mbarikiwa, yeye ajaye kwa jina la BWANA; Hosana juu mbinguni."
◼️kwa sababu YESU KRISTO ni mbarikiwa, basi kuwa na uhusiano na YESU KRISTO ni chanzo pia cha baraka hivyo wapo watu wengi waliobariki kwa sababu wana mahusiano na YESU KRISTO yaani wamekubali kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wao na wanafuata Neno lake.
◼️Kuwa na uhusiano na YESU KRISTO mbarikiwa kutakufanya na wewe ubarikiwe kuanzia ulimwengu wa roho hadi ulimwengu wa mwili.
✓✓Tatizo tu la watu wengi ni namna ya kutunza mahusiano yao na YESU KRISTO Mwokozi.
Yeye Bwana YESU KRISTO anasema " Mkinipenda, mtazishika amri zangu.-Yohana 14:15"
3. Mtu kutokea familia iliyobarikiwa.
◼️Chanzo kingine cha baraka za mtu ni mtu huyo kutoka katika familia iliyobarikiwa kwenye ulimwengu wa roho.
✓✓Mfano ukiwa wa kutokea familia ya Ibrahimu lazima ubarikiwe maana unatokea familia iliyobarikiwa kuanzia kwenye ulimwengu wa roho hadi kwenye ulimwengu wa mwili.
Mwanzo 22:15-18 "Malaika wa BWANA akamwita Ibrahimu mara ya pili kutoka mbinguni akasema, Nimeapa kwa nafsi yangu asema BWANA, kwa kuwa umetenda neno hili, wala hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee, katika kubariki nitakubariki, na katika kuzidisha nitauzidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, na kama mchanga ulioko pwani; na uzao wako utamiliki mlango wa adui zao; na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia; kwa sababu umetii sauti yangu."
✓✓Kuna watu wanatokea familia zilizobarikiwa hivyo na wao wamebarikiwa.
Mfano nimesema kwamba mtu kutokea familia ya Ibrahimu lazima mtu huyo alikuwa amebarikiwa ona mfano wa kina Isaka, Yakobo na Esau.
Mwanzo 28:4 "Akupe mbaraka wa Ibrahimu, wewe na uzao wako pamoja nawe, upate kuirithi nchi ya kusafiri kwako, MUNGU aliyompa Ibrahimu."
✓✓Ndugu, inawezekana hujatokea familia iliyobarikiwa lakini unaweza kufuata kanuni za MUNGU za baraka ndani ya KRISTO na ukabarikiwa.
4. Mtu aliyetengwa na MUNGU ili akutamkie Baraka Wewe.
Kumbu 33:1 "Hii ndiyo baraka ya Musa, huyo mtu wa MUNGU, aliyowabarikia wana wa Israeli kabla ya kufa kwake."
✓✓Huu ni mfano hai wa Mtu aliyeandaliwa na MUNGU ili amtamkie baraka Mtu Mwingine na atabarikiwa sana Mtu huyo.
Watu hawa wa kutamka Baraka hasa ni Watumishi wa MUNGU waaminifu Katika KRISTO YESU, Watumishi hawa wamewekwa ili kuachilia baraka kwa baadhi ya Watu na Mtu yule anabarikiwa sana.
Unaweza ukashangaa rohoni mwako unasukumwa uwe Karibu na Mtumishi wa MUNGU fulani, Inawezekana huyo Mtumishi kwa wakati huu Wewe unamzidi uchumi na MUNGU anataka Wewe ndio umsaidie kwa pesa zako nyingi na kumbe MUNGU amepitisha baraka zako kwa Mtumishi huyo, ukizingatia Kuna siku atakutamkia baraka ambazo zitakuwa hivyo hivyo hakuna atakayezuia.
Kuna Watumishi wa KRISTO waaminifu ni wa kawaida sana lakini wakikutamkia baraka itakuwa kama wanavyotamka kwa sababu tu wamebebeshwa baraka Yako.
Changamoto inakuwa hao Watumishi watakutamkia baraka Yako wakati gani?
Mara nyingi ni baada ya Wewe kutoa Sadaka hasa sadaka kubwa kiroho na umeitoa kwa Moyo wa kumpenda MUNGU bila kushawishiwa na Mtu yeyote.
Sadaka hizo nyingi hutengeneza matamko ya kiroho ambayo hutokea bila kizuizi chochote.
Jifunze kwa Isaka baada ya sadaka nzuri ya chakula ya Yakobo, Isaka baada ya kupewa sadaka hiyo alitamka baraka ambayo sio ya kufanya kazi mwaka mmoja Bali ya Miaka mingi sana sana.
Mwanzo 27:25-29 " Akasema, Niletee karibu nami nipate kula mawindo ya mwanangu, ili roho yangu ikubariki. Akamsogezea karibu, naye akala; ............................
MUNGU na akupe ya umande wa mbingu, Na ya manono ya nchi, Na wingi wa nafaka na mvinyo. Mataifa na wakutumikie Na makabila wakusujudie, Uwe bwana wa ndugu zako, Na wana wa mama yako na wakusujudie. Atakayekulaani alaaniwe, Na atakayekubariki abarikiwe."
Baraka hizi zilitamkwa baada tu ya sadaka kutolewa, Naamini Umejifunza.
Zingatia mteule wa KRISTO na MUNGU atakubariki sana.
Mche MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi na utaitwa heri.
Kama pia unatumia Facebook ni follow maana itafika kipindi nitakuwa napost tu katika page yangu na profile yangu.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292(Ni namba hii kupiga, sadaka ya kuipeleka Injili,kuandika meseji na whatsapp).
Ubarikiwe sana.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292(Ni namba hii kupiga, sadaka ya kuipeleka Injili,kuandika meseji na whatsapp).
Ubarikiwe sana.
Comments