![]() |
Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.
1 Wafalme 5:1 ''Basi Naamani, jemadari wa jeshi la mfalme wa Shamu, alikuwa mtu mkubwa mbele ya bwana wake, na mwenye kuheshimiwa, kwa sababu kwa mkono wake BWANA alikuwa amewapa Washami kushinda; tena alikuwa mtu hodari wa vita; lakini alikuwa mwenye ukoma.''
Biblia inasema Naamani alikuwa mtu wa cheo kikubwa , aliyeinuliwa na kubarikiwa lakini alikuwa na ukoma.
✓✓Ukoma wa Naamani ulikuwa ni kifungo kwake.
Inawezekana na wewe uko kwenye vifungo vya giza kama Naamani.
✓✓Naamani ilibidi afuate maombezi ili afunguliwe kutoka vifungo vya giza vilivyomtesa.
◼️Maombi ya kufunguliwa Naamani kwenye kifungo chake yalihitaji ajichovye mara saba kwenye maji ndipo atafunguliwa.
Naamani alipojichovya mara ya kwanza hakufunguliwa kifungo chake.
Inawezekana na wewe umeshajichovya mara moja au mara mbili lakini bado hujafunguliwa kifungo chako.
✓✓Inawezekana umeshajichovya mara 3 au mara 4 lakini bado hujafunguliwa, yaani inawezekana umeshaombewa mara moja au mara mbili au mara kadhaa lakini hujafunguliwa kifungo chako vizuri.
✓✓Inawezekana wewe ni Kama Naamani umejichovya mtoni mara tano au mara sita na sasa umekata tamaa hivyo huhitaji tena kujichovya mara ya saba, na kumbe hiyo mara ya saba ndio ushuhuda wako wa ajabu utatokea.
Inawezekana baada ya kuombewa mara moja au mara mbili au mara sita umekata tamaa ya kupona au kufunguliwa, inawezekana kwa sababu hiyo umeanza hadi kuwaona watumishi kwamba wameshindwa kukuombea ukafunguliwa, umeanza hata kuwatukana maana hata zaka na sadaka zako ulitoa vyema ila bado hujafunguliwa, kumbe inasubiriwa mara ya saba ili ufunguliwe.
✓✓Ndugu, Naamani kulingana na kifungo chake na kulingana na ufunuo uliotoka juu yake kutoka ulimwengu wa roho ilibidi ajichovye mara saba na sio mara tano au mara nne tu.
✓✓Kulingana na mahitajio ya kiroho ya kufunguliwa Naamani ilikuwa ni lazima ajichovye mara saba ndipo atafunguliwa.
✓✓Inawezekana umetoa sadaka mara 5 au mara 6 na kuiambatanisha na maombi, inawezekana umeombewa mara 5 au mara 6 ila tatizo lilipungua tu bila kuisha, ndugu, wakati mwingine unaihitaji mara ya saba kama Naamani ndipo utafunguliwa.
◼️Biblia inasema kwamba Naamani alipotii na kujichovya mara ya saba hakika alifunguliwa vifungo vyake.
2 Wafalme 5:14 ''Ndipo akashuka, akajichovya mara saba katika Yordani, sawasawa na neno lake yule mtu wa MUNGU; nayo nyama ya mwili wake ikarudi ikawa kama nyama ya mwili wa mtoto mchanga, akawa safi. ''
Mara saba ya Naamani ilileta ushindi wa ajabu kwake, alikuwa mwenye ukoma sugu na aliyeharibika ngozi lakini kwa kitendo cha kujichovya mara ya saba basi ngozi ya mwili wake ikawa kama ngozi ya mtoto Mchanga, yaani ngozi yake ikawa haina mabaka, haina ukilema wala haina makunyanzi, ikawa safi.
✓✓Ilitakiwa Naamani ajichovye mara saba ndipo atafunguliwa vifungo.
Unajifunza Nini?
◼️Ulimwengu wa roho una Kanuni nyingi hivyo zingatia sana Kufuata maelekezo ya ROHO MTAKATIFU siku zote ili uwe mshindi.
Kwa Naamani Mara moja tu haikutosha, mara mbili haikukidhi mahitajio ya ulimwengu wa roho.
Hata wewe inawezekana umeombewa mara moja lakini bado hujafunguliwa, usikate tamaa bali endelea na kuomba au kuombewa maana mara saba yako ikifika utamshangaa Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
Mahali pengine Biblia inakutaka uombe hadi upokee, ndio maana ya kuomba bila kukoma.
1 Wathesalonike 5:17 " ombeni bila kukoma; shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya MUNGU kwenu katika KRISTO YESU."
✓✓Kwa Naamani kuomba mara nne au mara tano bado haikukidhi mahitajio ya ulimwengu wa roho hata ukoma wake utoke.
✓✓Hata kuombewa mara sita bado haikukidhi mahitajio ya ulimwengu wa roho ili afunguliwe vifungo vya magonjwa.
✓✓Lakini mara ya saba ikabadilisha maisha yake kuanzia siku
hiyo.
◼️Inawezekana na wewe unaisubiri mara saba yako, inawezekana umeomba kwa miaka kumi lakini mara Saba yako siku ikitokea hautabaki kama ulivyo.
Siku Moja mimi Peter Mabula nikiwa maeneo fulani ya mkoa wa Pwani Karibu na Tanga Dada mmoja mwimbaji Kanisani kwao mwenye umri wa miaka 30 aliniambia kitu Cha ajabu sana, alisema ameshaomba sana kwa habari ya Mume hadi amekata tamaa na hataomba tena hata siku Moja Maisha yake yote yaliyobaki. Nikamwambia "ukiacha kuomba unsmkomesha nani?" Akasema "Hakuna" nikamwambia "Basi endelea kuomba na kuishi maisha matakatifu nami nitakuombea pia na utaingia kwenye Ndoa yenye ushuhuda"
Sasa kwanini inakuwa hivyo?
Ni kwa sababu hajui utaratibu wa ulimwengu wa roho wakati Mwingine.
✓✓Ndugu, inawezekana umetoa au umeomba mara 20 au 30 lakini mara saba yako ya kiroho ikifika hakika utamuona MUNGU.
◼️Wako ambao waliomba na kuombewa muda mrefu lakini siku moja ya maombi ilikuja na ushindi wao.
Mfano hai ni Hana aliyekuwa hana mtoto.
1 Samweli 1:5 '' lakini Hana humpa sehemu mara mbili; maana alimpenda Hana, ingawa BWANA alikuwa amemfunga tumbo. ''
✓✓Hana alikuwa anapewa na Mume wake sadaka mara mbili zaidi ili akamtolee MUNGU, na hii ilikuwa mwaka kwa mwaka lakini bado tumbo lake la uzao lilikuwa halijafunguliwa.
Hana alikuwa na uchungu rohoni na aliomba kwa kulia sana hadi akaweka nadhiri kwa MUNGU ikiwa atabarikiwa mtoto, licha na uchungu na maumivu ya rohoni lakini hakuacha kuomba, aliingojea mara saba yake.
1 Samweli 1:10-11 ''Naye huyo mwanamke alikuwa na uchungu rohoni mwake, akamwomba BWANA akalia sana. Akaweka nadhiri, akasema, Ee BWANA wa majeshi, ikiwa wewe utaliangalia teso la mjakazi wako, na kunikumbuka, wala usinisahau mimi mjakazi wako, na kunipa mimi mjakazi wako mtoto mume, ndipo mimi nitakapompa BWANA huyo mtoto siku zote za maisha yake, wala wembe hautamfikilia kichwani kamwe. ''
✓✓Hana aliweka nadhiri, alitoa matoleo tena aliyokuwa anapewa mara mbili kuliko wenzake, alikuwa anaomba na siku moja ya ajabu, naweza kuiita siku yake ya saba ilipofika alipata sio tu bora uzao bali uzao bora.
Siku ya saba ya Hana ilipofika Biblia inasema usiku huo huo alipata mimba ya Mtoto wa kiume ambaye ni Nabii Samweli.
1 Samweli 1:19-20 ''Wakaondoka asubuhi na mapema, wakasali mbele za BWANA, kisha wakarejea na kufika nyumbani kwao huko Rama; Elkana akamjua mkewe Hana; naye BWANA akamkumbuka. Ikawa, wakati ulipowadia, Hana akachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; akamwita jina lake Samweli, akisema, Kwa kuwa nimemwomba kwa BWANA. ''
✓✓Kwa sababu Hana katika siku ya saba yake alipata uzao na akaongeza na tendo la Imani na kutimiza nadhiri, ndipo kwake yalitimia maneno yanayosema ''Eeeh My God is good oh, Everything is double double oh (Is double double) ''
Maana yeye aliomba apewe mtoto mmoja wa kiume lakini MUNGU akambariki jumla watoto sita, hiyo ndio double double from JESUS CHRIST.
Biblia inasema '' Naye BWANA akamwangalia Hana, naye akachukua mimba, akazaa watoto, wa kiume watatu na wa kike wawili. Naye huyo mtoto Samweli akakua mbele za BWANA.-1 Samwel 2:21''
✓✓Ndugu inawezekana wewe uko sasa katika mara sita yako lakini umechoka na kukataa tamaa.
✓✓Inawezekana wewe ulifika mara sita yako lakini ukaanguka dhambini hivyo ukafuta hata hizo 6 hivyo inakupasa kuanza moja kwa utakatifu na adabu mbele za MUNGU.
✓✓Inawezekana wewe ulifika mara sita yako lakini manung'uniko, kujihesabia haki, kuwasema vibaya watumishi wa MUNGU, Kuacha ibada na maombi, kulalamika, kujitamkia maneno mabaya ndivyo vinavyokupunguzia kuifikia mara saba yako maana vitu hivyo vinafuta au kupunguza hivyo unajikuta uko katika mara 3 yako tu ukifika mara sita vitu hivyo vinakurudisha nyuma unajikuta unaanza mara ya kwanza.
✓✓Ndugu Unahitaji kuomba hadi mara saba yako maana ikifika hiyo utamuona MUNGU.
◼️Waisraeli walizunguka Yeriko kwa siku sita na katika hizo siku 6 kila siku walizunguka ngome ya Yeriko mara moja, lakini ilipofika siku ya saba walizunguka Yereko mara saba na katika mara ya saba kuta za Yeriko zilizokuwa kizuizi chao zilianguka.
Yoshua 6:3-4 '' Nanyi mtauzunguka mji huu, watu wote wa vita, mkiuzunguka mji mara moja. Fanya hivi siku sita.
Na makuhani saba watachukua tarumbeta saba za pembe za kondoo waume, mbele ya hilo sanduku; na siku ya saba mtauzunguka mji mara saba, nao makuhani watapiga tarumbeta zao.''
✓✓Kwa siku sita walikuwa wanafanya maombi na kuendelea na maisha ila bado ukuta wa Yeriko ulikuwa haujadondoka.
Yoshua 6:14 ''Siku ya pili wakauzunguka mji mara moja, wakarejea kambini; ndivyo walivyofanya siku sita. ''
✓✓Ungekuwa wewe umeombewa mara sita harafu tatizo bado lipo nadhani ungemwacha hata YESU na kuzifuata miungo hivyo kujipoteza.
✓✓Ungekuwa wewe umetoa zaka mara sita na umetoa sadaka na nadhiri na dhabihu mara 5 nadhani inawezekana ungeanzisha vita na Mtumishi wa MUNGU.
◼️Mimi Peter Mabula Niko hapa leo kukuambia rafiki yangu kwamba wakati mwingine unatakiwa uingoje mara saba yako maana ndipo ukuta wa Yeriko kwako utadondoka na kutoweka, tatizo litaisha, kibali chako kitarudi, uchumi wako utafunguliwa, uzao wako utafunguliwa, ndoa yako itafunguliwa, kazi yako itakupa majibu mazuri.
✓✓Kwa Waisraeli siku ya saba yao ilipofika Biblia inasema
Yoshua 6:20 '' Basi watu wakapiga kelele, na makuhani wakazipiga tarumbeta; hata ikawa, hapo watu waliposikia sauti ya tarumbeta hao watu wakapiga kelele kwa sauti kuu sana, na ule ukuta wa mji ukaanguka nchi kabisa, hata watu wakapanda juu, wakaingia katika mji, kila mtu akiendelea kukabili mbele; wakautwaa huo mji. ''
Unajifunza nini?
◼️Mara saba yako ya kuzunguka yeriko yako kimaombi itafika na ugonjwa utaondoka, kukataliwa kutaondoka, kifungo kitaondoa, tatizo litafutika kwa jina la YESU KRISTO Mwokozi aliye hai.
✓✓Ndugu ingoje mara saba yako huku ukiendelea na maombi na utoaji n.k kulingana na maelekezo ya MUNGU juu yako.
Naamani angejichovya kwenye maji mara 5 au mara 6 asingefunguliwa kifungo chake maana maelekezo ya rohoni ilitakiwa mara 7 ndio ukoma utaondoka.
Waisraeli wangezunguka Yeriko mara 5 au mara 6 ukuta wa Yeriko usingedondoka maana mahitajio ya ulimwengu wa roho juu ya kuungusha ukuta huo ulikuwa mara saba katika siku ya saba.
◼️Inawezekana wewe unakosea maelekezo ya ROHO MTAKATIFU juu ya kufunguliwa kwako na juu ya kufanikiwa kwako ndio maana umebaki pale pale bila baraka yako unayoihitaji sana.
◼️Kuna mambo mengi mahitajio ya ulimwengu wa roho ni kuombwa mara moja tu lakini yapo mahitajio mengine unahitaji kufunga na kuomba, yako mahitajio mengine unatakiwa kuomba kwa imani na sio kuomba billa imani ya kupokea.
yako mahitajio mengine unatakiwa kuomba au kuombewa ukiambatananisha na sadaka nzuri, yako mahitajio mengine unatakiwa kushirikisha waombaji wengine huku na wewe ukiomba.
◼️Ndugu kama unamtegemea YESU KRISTO na yeye ndiye Mwokozi wako basi endelea kuomba na fuata msukumo wa ROHO MTAKATIFU ndani yako juu ya kushinda kwako.
Ndugu, mbona unataka kuishia njiani wakati Biblia inakutaka kuomba bila kukoma?
1 Thesalonike 5:17 '' ombeni bila kukoma;''
Ndugu mbona hata umeacha kumtolea MUNGU zaka, sadaka na dhabihu kwa sababu tu amechelewa kukujibu wakati sauti ya MUNGU iliyo katika Neno lake inakutaka usiache kumtolea MUNGU?
Kumb 14:22 '' Usiache kutoa zaka ya fungu la kumi katika maongeo yote ya mbegu zako, yatokayo shamba mwaka baada ya mwaka. ''
Inawekekana kwa sasa umeshasahau kwamba ''Lakini nasema neno hili, Apandaye haba atavuna haba; apandaye kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu. Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana MUNGU humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu.-2 Kor 9:6-7 ''
✓✓Ndugu, nakuomba ingoje mara saba yako huku ukiishi maisha matakatifu usiku na mchana, huku ukiomba na kusonga mbele na Wokovu wa Bwana YESU ulio wa thamani sana.
Mche MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi na utaitwa heri.
Kama pia unatumia Facebook ni follow maana itafika kipindi nitakuwa napost tu katika page yangu na profile yangu.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292(Ni namba hii kupiga, sadaka ya kuipeleka Injili,kuandika meseji na whatsapp).
Ubarikiwe sana.
Comments