![]() |
Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu, jifunze ufahamu huu ili uwe mshindi daima.
✓✓Silaha nyepesi ambayo shetani huitumia ili kuwapata watu wengi ni majaribu, ndio maana anaitwa "mjaribu"
1 Wathesalonike 3:5 "Kwa hiyo mimi nami nilipokuwa siwezi kuvumilia tena, nalituma mtu ili niijue imani yenu, asije yule mjaribu akawajaribu, na taabu yetu ikawa haina faida."
✓✓Silaha hii ya majaribu shetani huitumia kwa watu wengi ili kuwatisha.
✓✓Shetani hutumia silaha ya majaribu pia ili kuwafanya watu wamtii yeye na kukosa uzima wa milele.
✓✓Shetani hutumia pia silaha ya majaribu ili kuwafanya watu wakose tumaini, hata kama tumaini lipo.
◼️Ndugu yangu unayesoma ujumbe huu, hata kama shetani ametumia silaha ya majaribu kwako usikubali kumpa nafasi hata moja maishani mwako.
Waefeso 4:27 "wala msimpe Ibilisi nafasi.'
Nini ufanye kama shetani amekuletea silaha yake ya majaribu ?
1. Hakikisha unakuwa muombaji ili usiingie katika majaribu hayo.
Marko 14:38 "Kesheni mwombe, msije mkaingia majaribuni, roho i radhi ila mwili ni dhaifu."
2. Kama uko katika majaribu tayari muombe MUNGU ili akutoe katika majaribu hayo.
2 Petro 2:9 "basi, BWANA ajua kuwaokoa watauwa na majaribu, na kuwaweka wasio haki katika hali ya adhabu hata siku ya hukumu;"
3. Mpinge shetani naye atakukimbia haraka.
Yakobo 4:7 "Basi mtiini MUNGU. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia."
4. Pambana kiroho dhidi ya nguvu za giza ambazo hizo zote hutokana na shetani, pambana kimaombi maana unayo mamlaka katika KRISTO YESU Mwokozi.
Yoshua 23:10 "Mtu mmoja miongoni mwenu atafukuza watu elfu; maana BWANA, Mungu wenu, ndiye anayewapigania, kama alivyowaambia."
5. Hakikisha hakuna kinachokutenga na KRISTO.
Warumi 8:35-39 " Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? Je! Ni dhiki au shida, au adha, au njaa, au uchi, au hatari, au upanga? .................... Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo, wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa MUNGU ulio katika KRISTO YESU Bwana wetu."
Zingatia mteule wa KRISTO na MUNGU atakubariki sana.
Mche MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi na utaitwa heri.
Kama pia unatumia Facebook ni follow maana itafika kipindi nitakuwa napost tu katika page yangu na profile yangu.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292(Ni namba hii kupiga, sadaka ya kuipeleka Injili,kuandika meseji na whatsapp).
Ubarikiwe sana.

Comments