![]() |
Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu yangu.
Karibu nikujuze jambo muhimu sana.
◼️Maana mojawapo ya "dhambi" ni mabaya yanayokuficha usionekane na MUNGU.
Ngoja nianzie kwenye madhara ya dhambi Kisha nitaingia katika kiini Cha somo la Leo.
✓✓Ndugu Yangu, najua wewe ni muombaji mzuri.
Najua umeshaomba mambo mengi tu kwa MUNGU ili utendewe lakini naomba ujue hili Leo kwamba dhambi zako zinaweza kukuficha ili usionekane na MUNGU hata kupokea Baraka ulizoomba kwa MUNGU.
✓✓Ndugu, dhambi imeshakuficha Mara ngapi ili usionekane na MUNGU na kupokea Baraka zako kutoka kwa MUNGU?
◼️Kuomba ni kitu kingine na utakatifu ni kitu kingine ila vinategemeana sana.
✓✓Maombi sahihi ni Yale yanayoambatana na maisha matakatifu sahihi
Wapo watu husema imekuwa vigumu wao kuiacha dhambi fulani.
Wapo watu husema "nifanyeje ili niache dhambi fulani. "
Ukweli ni kwamba watu hao wanakuwa hawajaamua tu kuiacha dhambi hiyo, wanakuwa hawajaamua kuiepuka jehanamu ya moto.
Biblia iko wazi kwamba kuna jehanamu kwa watenda dhambi ambao wamegoma kuokoka, kutubu na kuacha dhambi.
Ufunuo 20:15 "Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto."
Inawezekana yuko mtu ni Mzinzi au Mwasherati na anaomba msaada wa kiroho wa namna ya kuacha dhambi hiyo chafu na inayochafua mwili na roho.
Inawezekana yuko mtu ni msagaji au mpigaji wa punyeto na anaomba msaada wa kiroho wa namna ya kuacha dhambi hiyo chafu na inayochafua mwili na roho.
Inawezekana yuko mtu ni kahaba au malaya na anaomba msaada wa kiroho wa namna ya kuacha dhambi hiyo chafu na inayochafua mwili na roho.
Kumbuka hii
Mithali 15:3 ''Macho ya BWANA yako kila mahali; Yakimchunguza mbaya na mwema.''
Inawezekana yuko mtu ni msaliti wa ndoa yake au anatumika kipepo na anaomba msaada wa kiroho wa namna ya kuacha dhambi hiyo chafu.
Inawezekana yuko mtu ni mchawi au mwizi na anaomba msaada wa kiroho wa namna ya kuacha dhambi hiyo chafu.
Inawezekana yuko mtu ni muongo au mlevi na anaomba msaada wa kiroho wa namna ya kuacha dhambi hiyo.
Inawezekana yuko mtu ni tapeli au msaliti wa ndoa na anaomba msaada wa kiroho wa namna ya kuacha hiyo.
Inawezekana yuko mtu ni mwenda kwa waganga au anavaa kikahaba mitaani na anaomba msaada wa kiroho wa namna ya kuacha dhambi hiyo.
✓✓Kumbuka hii kwamba usipookoka na kutubu basi matendo yako ya dhambi siku ya mwisho yatakuwa pamoja na wewe.
Obadia 1:15 ''Kwa maana hiyo siku ya BWANA i karibu juu ya mataifa yote; kama ulivyotenda, ndivyo utakavyotendwa; malipo yako yatakurudia juu ya kichwa chako mwenyewe.''
Inawezekana na wewe una dhambi yako sugu ambayo unadhani huwezi kuiacha, leo nina majibu kwa ajili ya namna ya kuishinda dhambi.
Naomba zingatia ujumbe huu.
◼️Ili uishinde dhambi ni lazima ufarakane kwanza na hiyo dhambi, zingatia hilo na usije ukasahau hata siku moja.
Narudia tena "ILI UISHINDE DHAMBI FULANI NI LAZIMA KWANZA UFARAKANE NA DHAMBI HIYO"
✓✓Huwezi kuishinda dhambi ikiwa hujafarakana na dhambi hiyo.
✓✓Huwezi kujitenga na shetani kama bado una urafiki naye.
✓✓Huwezi kuishinda dhambi fulani inayokusumbua ikiwa bado una urafiki bado na dhambi hiyo.
✓✓Huwezi kuushinda uzinzi na uasherati ikiwa bado una urafiki na uzinzi na uasherati na bado una urafiki na wazinzi na waasherati.
✓✓Huwezi kuushinda uongo na wizi kama bado una urafiki na uongo na wizi.
✓✓Huwezi kuishinda dhambi yeyote kama bado hajaamua kufarakana na dhambi hiyo.
Sasa naamini umeelewa na utaishinda na kuiacha dhambi yako sugu, utaiacha kirahisi sana maana utaichukia hiyo dhambi na kufarakana nayo.
✓✓Ukiichukia dhambi fulani huwezi kuwa na ukaribu nayo tena.
✓✓Ukifarakana na dhambi fulani hutaweza kuitenda tena.
◼️Sasa wewe farakana na dhambi zote kuanzia Leo na hutazitenda.
Kumbuka atendaye dhambi ni wa shetani.
1 Yohana 3:8a "atendaye dhambi ni wa Ibilisi; kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. "
✓✓Ni suala la maamuzi tu ya kuichukia dhambi na kufarakana nayo na hutaifanya tena.
✓✓Ukiona mtu anafanya dhambi fulani kila mara ujue mtu huyo hajaamua kufarakana na dhambi hiyo hata aiache, yaani bado ana urafiki au undugu na dhambi hiyo.
Ngoja nikupe mifano miwili.
◾Binti akifarakana na dhambi ya uasherati basi binti huyo hataruhusu kamwe mahusiano ya kimapenzi, hatavaa kikahaba, hatakubali kukaa gizani na mwanaume yeyote wakiwa wawili tu, atavunja urafiki na marafiki wabaya wanaowaza dhambi hiyo, atatumia muda wake mwingi katika mambo ya MUNGU maana hana urafiki tena na dhambi.
◾Mwanaume akifarakana na ulevi ujue hataenda bar, atavunja urafiki na walevi, hatanunua pombe kwa sababu ameshafarakana na ulevi.
✓✓Naamini umeelewa namna ya kuiacha dhambi sugu inaayokusumbua, wasaidie hata watu wako wa karibu mbinu hii ili wasiende jehanamu kwa sababu ya dhambi zao sugu.
Ndugu, Neno la MUNGU linamtaka kila mtu ajitenge na dhambi za kila namna.
1 Wathesalonike 5:22 "jitengeni na ubaya wa kila namna."
Ili uishinde dhambi daima fanyia kazi mambo haya pia.
1. Uwe na akili ya kiroho ya kukusaidia kuutumia muda wako katika MUNGU.
✓✓Mfano ni kuutumia muda wako katika ibada na maombi badala ya muda huo kutenda dhambi.
1 Petro 4:7 " Lakini mwisho wa mambo yote umekaribia; basi, iweni na akili, mkeshe katika sala."
2. Ishi maisha matakatifu ya Wokovu wa KRISTO YESU.
1 Petro 1:15 '' bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote;''
3. Mtegemea MUNGU daima.
Isaya 26:3-4 "Utamlinda yeye ambaye moyo wake umekutegemea Katika amani kamilifu, kwa kuwa anakutumaini. Mtumainini BWANA siku zote Maana Bwana YEHOVA ni mwamba wa milele."
4. Pambana kiroho ili ushinde hila za shetani, amua kuambatana na MUNGU.
Yakobo 4:7-10 "Basi mtiini MUNGU. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia. Mkaribieni MUNGU, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu, enyi wenye nia mbili. Huzunikeni na kuomboleza na kulia. Kucheka kwenu na kugeuzwe kuwa kuomboleza, na furaha yenu kuwa hamu. Jidhilini mbele za BWANA, naye atawakuza."
Naamini kuna kitu kizuri umejifunza.
Zingatia mteule wa KRISTO na MUNGU atakubariki sana.
Mche MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi na utaitwa heri.
Kama pia unatumia Facebook ni follow maana itafika kipindi nitakuwa napost tu katika page yangu na profile yangu.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292(Ni namba hii kupiga, sadaka ya kuipeleka Injili,kuandika meseji na whatsapp).
Ubarikiwe sana.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292(Ni namba hii kupiga, sadaka ya kuipeleka Injili,kuandika meseji na whatsapp).
Ubarikiwe sana.
Comments