![]() |
Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu zangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.
◼️Kila jambo jema lina kanuni zake ili kulipata.
◼️Kila kitu kizuri kuna kanuni zake ili kukipata.
✓✓Mfano elimu nzuri ili uipate inakupasa kwenda shule, kwenda shule na kusoma kwa bidii ndio kanuni ya kupata elimu nzuri.
◼️Hata baraka za MUNGU nazo ili kuzipata zina kanuni zake ndipo utazipata.
✓✓Zipo Kanuni nyingi za Kibiblia na kuzifuata zote ndipo zinaleta baraka kwako.
Mimi Peter Mabula najua Wewe rafiki yangu unapenda baraka za MUNGU na Mimi pia nazipenda baraka za MUNGU, basi ni Muhimu sana kufuata kanuni hizi zote na MUNGU aliyesema katika Neno lake kwamba atakubariki hakika atakubariki.
Mwanzo 12:2" nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako; nawe uwe baraka;"
◾Kwanini ufuate kanuni zote kwa pamoja na sio kufuata kanuni moja tu?
◼️Ni kwa sababu kanuni zote hizi zinategemeana.
Kanuni za MUNGU za kuzifuata ili Zilete baraka kwako.
1. Kufanya kazi njema na halali.
Kwanini ufanye kazi?
✓✓Ni kwasababu MUNGU hubariki kazi za mikono, hivyo kama hufanyi kazi yeyote utakuwa unazuia hizo baraka hata kama una sifa za kubarikiwa zingine zote.
Kumb 28:8 "BWANA ataiamuru baraka ije juu yako katika ghala zako, na mambo yote utakayotia mkono wako; naye atakubarikia katika nchi akupayo BWANA, Mungu wako."
✓✓Baraka sio kufanya kazi lakini kufanya kazi ni mlango wa kubarikiwa.
✓✓Wapo pia wanaofanya kazi sana ila hawajabarikiwa na MUNGU kwa sababu hawafuati kanuni zingine za MUNGU za kubarikiwa.
✓✓Ndugu ukitaka baraka za MUNGU fanya kazi au tafuta kazi maana kinachobarikiwa na MUNGU ni kazi uifanyayo.
◼️Hata ndani ya Biblia waliobarikiwa ni waliokuwa wanafanya kazi.
✔️✔️Nuhu kazi yake ilikuwa ukulima.
Mwanzo 9:20 "Nuhu akaanza kuwa mkulima, akapanda mizabibu;"
✔️✔️Ibrahimu na Lutu kazi zao zilikuwa ufugaji sana.
Mwanzo 13:7 "Kukawako ugomvi kati ya wachunga wanyama wa Abramu, na wachunga wanyama wa Lutu; na siku zile Wakanaani na Waperizi walikuwa wakikaa katika nchi."
✔️✔️Kuna watu kazi zao zilikuwa fundi ujenzi,wengine kazi zao zilikuwa useremala.
2 Wafalme 12:11" Na fedha iliyopimwa wakawapa mikononi wale waliofanya kazi, walioisimamia nyumba ya BWANA; na hao wakawatolea maseremala na wajenzi walioifanya kazi katika nyumba ya BWANA,"
✔️✔️Hata wewe inakupasa kuwa na kazi iwe ya kuajiriwa au kujiajiri, hata wewe inakupasa kutafuta kazi.
2. Utoaji wa zaka na sadaka.
2 Wakorintho 9:6 "Lakini nasema neno hili, Apandaye haba atavuna haba; apandaye kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu."
✓✓Kutoa matoleo ni kupanda kwenye ufalme wa MUNGU na ni lazima upokee.
◼️Kutoa fungu la kumi na sadaka ni agizo la MUNGU la tangu kizazi cha kwanza cha wanadamu, agizo la MUNGU hili liliendelea kipindi cha mababa wa imani, agizo hilo liliendelea kipindi cha torati na agizo hilo linaendelea kipindi hiki cha Kanisa, ni agizo la muda wote kwa wanadamu wampendao MUNGU.
✓✓Utoaji una matokeo mengi sana kiroho lakini pia utoaji matoleo ndio ufunguo mkubwa wa kupokea baraka za MUNGU.
✓✓Bila utoaji huwezi kubarikiwa na MUNGU hata kama unafanya kazi.
Malaki 3:10 "Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema BWANA wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la."
3. Kuwa mtu wa maombi.
✓✓Maombi ni kanuni muhimu sana ya kupokea baraka za MUNGU maana MUNGU ameruhusu tukiomba kwake katika KRISTO YESU tutapewa.
Mathayo 7:8 "kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa."
✓✓Maombi yana kazi nyingi sana ndio maana lazima maombi yaampatane na wewe ili ubarikiwe.
✓✓Maombi yanaweza kuzuia adui kuiba uchumi wako au mali zako, maombi yanaweza kufungua milango ya mbinguni ya baraka kwako.
✓✓Maombi katika jina la YESU KRISTO ni kanuni muhimu sana ya baraka.
Fanya kazi huku ukiwa muombaji na utakuwa mtu wa shuhuda njema kila mara maana MUNGU atakubariki.
4. Kuwa mtu wa shukrani kwa MUNGU.
✓✓Hii ni kanuni muhimu sana ukitaka uwe na baraka za MUNGU zinazodumu.
1 Wathesalonike 5:18 "shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya MUNGU kwenu katika KRISTO YESU."
✓✓Kwanza kumshukuru huruhusu ongezeko kwako.
Zaburi 50:23 '' Atoaye dhabihu za kushukuru, Ndiye anayenitukuza. Naye autengenezaye mwenendo wake, Nitamwonyesha wokovu wa MUNGU. ''
✓✓Ni muhimu sana kumshukuru MUNGU maana hata vitu vyote ni vyake, hivyo amekubariki tu wewe kwa sehemu kutoka katika vitu vyake, usipokuwa mtu wa shukrani kwa MUNGU ujue hata ulivyonavyo vinaweza kuondolewa kwako maana sio mali yako.
Zaburi 24:1 "Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya BWANA, Dunia na wote wakaao ndani yake."
✓✓Hivyo ni mlango wa baraka unapomshukuru MUNGU.
✓✓Mshukuru MUNGU kwa sadaka na kwa maombi.
Zaburi 100:3-5 '' Jueni kwamba BWANA ndiye Mungu; Ndiye aliyetuumba na sisi tu watu wake; Tu watu wake, na kondoo wa malisho yake. Ingieni malangoni mwake kwa kushukuru; Nyuani mwake kwa kusifu; Mshukuruni, lihimidini jina lake; Kwa kuwa BWANA ndiye mwema; Rehema zake ni za milele; Na uaminifu wake vizazi na vizazi.''
✓✓Kumshukuru MUNGU ni kuonyesha unamtegemea MUNGU.
✓✓kumshukuru MUNGU ni kuonyesha unamtumaini MUNGU.
✓✓Na siku zote watu wanaomtegemea MUNGU na kumtumaini hubarikiwa.
Yeremia 17:7" Amebarikiwa mtu yule anayemtegemea BWANA, Ambaye BWANA ni tumaini lake."
5. Kutii maelekezo ya MUNGU kupitia ROHO MTAKATIFU.
✓✓Wakati mwingine ROHO MTAKATIFU anaweza kukupa maelekezo fulani binafsi ambayo unatakiwa kuyafuata na kumbe ndani ya maelekezo hayo na baraka zako ziko humo.
Mfano ni huu.
Mwanzo 12:1-3 " BWANA akamwambia Abramu, Toka wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi nitakayokuonyesha; nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako; nawe uwe baraka; nami nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani; na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa."
✓✓Maelekezo ya MUNGU kwa Ibrahimu yalikuwa atoke kwao aende kule MUNGU amempangia, na huko MUNGU alimbariki sana.
✓✓Maelekezo binafsi ya MUNGU yanaweza kuja hata kwako na ukitii utabarikiwa hadi utashangaa.
✓✓Unaweza kuambiwa kwa ufunuo wa ROHO MTAKATIFU umtumikie Bwana YESU KRISTO na kumbe na baraka zako zimeambatanishwa na huduma yako hiyo, unaweza kuambiwa fanya kitu fulani na kumbe ndani ya hicho kitu ulichoagizwa na MUNGU kuna baraka zako.
Zingatia mteule wa KRISTO na MUNGU atakubariki sana.
Mche MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi na utaitwa heri.
Kama pia unatumia Facebook ni follow maana itafika kipindi nitakuwa napost tu katika page yangu na profile yangu.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292(Ni namba hii kupiga, sadaka ya kuipeleka Injili,kuandika meseji na whatsapp).
Ubarikiwe sana.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292(Ni namba hii kupiga, sadaka ya kuipeleka Injili,kuandika meseji na whatsapp).
Ubarikiwe sana.
Comments