![]() |
Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe Ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU wa Mbinguni.
Leo namzungumzia kazi ya kila Mteule wa KRISTO.
Sijui kama unajua kazi Yako ni nini baada ya Bwana YESU KRISTO Mwokozi kukuokoa.
◼️Kazi ya wateule wa KRISTO ni kumtumikia MUNGU.
1 Wakorintho 15:58" Basi, ndugu zangu wapendwa, mwimarike, msitikisike, mkazidi sana kutenda kazi ya BWANA sikuzote, kwa kuwa mwajua ya kwamba taabu yenu siyo bure katika BWANA."
✓✓Kiini cha utumishi wetu kwa MUNGU ni kuwafanya watu wote wawe wateule wa KRISTO kama tulivyo sisi.
Mathayo 28:19 "Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la BABA, na MWANA, na ROHO MTAKATIFU; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari."
◼️Katika utumishi wetu kwa MUNGU kila mmoja amepewa kituo chake cha kazi.
Je kituo chake cha utumishi ni kipi ulichowekwa na ROHO MTAKATIFU?
✓✓Utumishi wako kwa KRISTO lazima uwe Katika moja ya nguvu hizi 4 ambazo ROHO MTAKATIFU hutoa kwa watumishi wote wa MUNGU.
Waefeso 4:11-12 " Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu; kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa KRISTO ujengwe;"
✓✓Tatizo wa watu wa MUNGU wengi ni kutoroka vituo vyao vya kazi kiutumishi.
✓✓Watu wengi huhama kwa kujihamisha katika vituo vyao vya kazi kiutumishi walivyoitwa Katika utumishi.
✓✓Cha kujua ni kwamba vituo vya utumishi sio dhehebu wala Kanisa.
Vituo vya kazi ki utumishi sio mji wala mtaa fulani.
◼️Vituo vya kazi ki utumishi sio jengo la Kanisa fulani wala sio kwa Mchungaji fulani.
◼️Kituo chako ki utumishi ni karama yako Katika kusudi la MUNGU.
✓✓Narudia tena kusema kwamba watu wengi hukimbia vituo vyao vya kazi ki utumishi, vituo vya kazi ki utumishi ni karama.
Karama ni nini?
✓✓Karama ni zawadi za neema ambazo ROHO MTAKATIFU humpa mtu aliyempokea YESU KRISTO kama Mwokozi wake ili mtu huyo amtumikie MUNGU.
✓✓Kwa maana nyingine ya karama ni zawadi za neema ambazo MUNGU humpa mtu ili amtumikie yeye Katika KRISTO YESU kwa njia ya ROHO MTAKATIFU.
1 Petro 4:10-11 "kila mmoja kwa kadiri alivyoipokea KARAMA, itumieni kwa kuhudumiana; kama mawakili wema wa neema mbalimbali za MUNGU. Mtu akisema, na aseme kama mausia ya MUNGU; mtu akihudumu, na ahudumu kwa nguvu anazojaliwa na MUNGU; ili MUNGU atukuzwe katika mambo yote kwa YESU KRISTO. Utukufu na uweza una yeye hata milele na milele. Amina."
✓✓Inawezekana wewe kituo chako cha kazi ki utumishi ni kuhubiri na sio kufundisha.
Ukihama kituo chako cha kazi unaweza kufeli.
✓✓Inawezekana kituo chako cha kazi ki utumishi ni uinjilisti mitaani na sio kuimba, ukihama kituo chako cha kazi utatumia nguvu sana kufanikiwa ukiwa Katika kituo kipya ambacho sio chako.
Baadhi ya vituo vya kazi ki utumishi katika kazi ya MUNGU ni:-
1. Kuhubiri kwa njia ya kawaida.
2. Kuhubiri kwa uimbaji.
3. Kufundisha.
4. Kupiga vyombo vya mziki.
5. Uinjilisti mitaani, shuleni n.k
6. Kuombea kazi ya kuombea kazi ya injili kwa mzigo mkubwa rohoni.
7. Ufundi stadi wa mambo ya kihuduma.
8. Kuhubiri kwa njia ya kutoa Sadaka zinazoipeleka mbele Injili.
Hivyo ni baadhi tu ya vituo vya kiutumishi Katika kazi ya MUNGU.
Je wewe kituo chako cha kazi ni kipi?
✓✓Ndugu kaa Katika kituo chako cha kazi na mtumikie Bwana YESU KRISTO kwa upendo na furaha.
✓✓Changamoto ya Wakristo wengi ni kudhani huduma walizopewa ni vyeo ndio maana kila Mtu anajiita Mtume hata kama huo utume hana ndani yake.
✓✓Leo Kuna watu huona kuitwa Nabii ndio cheo kikubwa hivyo naye anajiita Nabii wakati MUNGU hamtumii katika Unabii Bali uchungaji.
Warumi 12:6-11 " Basi kwa kuwa tuna karama zilizo mbalimbali, kwa kadiri ya neema mliyopewa; ikiwa unabii, tutoe unabii kwa kadiri ya imani; ikiwa huduma, tuwemo katika huduma yetu; mwenye kufundisha, katika kufundisha kwake; mwenye kuonya, katika kuonya kwake; mwenye kukirimu, kwa moyo mweupe; mwenye kusimamia kwa bidii mwenye kurehemu, kwa furaha.
Pendo na lisiwe na unafiki lichukieni lililo ovu, mkiambatana na lililo jema. Kwa pendo la udugu, mpendane ninyi kwa ninyi; kwa heshima mkiwatanguliza wenzenu;
kwa bidii, si walegevu; mkiwa na juhudi katika roho zenu; mkimtumikia BWANA;"
Nawafahamu baadhi ya Watumishi ambao Mwanzo Mwanzo alijiita Mchungaji Kisha akajibadili Jina na kujiita Nabii Kisha baadae akajiita Mtume na baadae akajiita Mtume na Nabii, swali MUNGU alimuita kama nani? Naamini alimuita kwa huduma Moja na sio 3, unaweza ukafanya kazi kubwa sana ukiwa tu na Jina la Mchungaji mfano mbona akina Pastor Benny Hinn ni Wachungaji lakini kazi ni kubwa kuliko maelfu ya Mitume na Manabii.
Ndugu Fanya kazi katika kituo chako na kazi alichokuweka Bwana YESU KRISTO na utafanya kazi kubwa kuliko kukimbilia kituo kisicho chako.
Mbona akina Mwalimu Christopher Mwakasege wanafanya kazi kubwa kuliko maelfu na maelfu ya Mitume na Manabii?
Kwa Nini nasema hayo siku Moja nilimsikia Mtumishi mmoja wa MUNGU maarufu sana akifundisha kwamba Mwalimu ni Mdogo kuliko wote kiutumishi hivyo akipanda cheo atakuwa Mwinjilisti na akipanda cheo atakuwa Mchungaji na baada ya hapo akipanda cheo atakuwa Nabii Kisha cheo kikubwa zaidi ni Mtume.
Labda ndio maana Leo unaweza kukuta Mtu hajawahi kumshuhudia Injili hata Mtu mmoja lakini anajiita Mtume. Mtu hajawahi kupanda Makanisa hata 10 anajiita Mtume, hapana majina hayo sio vyeo Bali ni huduma hivyo ni vyema kila Mtu abaki kwenye huduma yake.
Huduma kugeuza vyeo sio Kibiblia ila ni mitazamo tu maana wapo Waalimu wanafanya kazi kubwa kuliko Mitume.
MUNGU anashughulika sana na majina pia, kwanini nasema hivyo?
Mimi Peter Mabula nilipoanza utumishi sikujiita Jina lolote nikibaki kujiita Peter Mabula, baadae nikaona nijiite Mwinjilisti baada ya kujifunza "Mwinjilisti ni nani" nikajua Mwinjilisti ni mpeleka Injili na Kwa sababu na Mimi ni mpeleka Injili wa kudumu basi Mimi ni Mwinjilisti lakini katika mazingira Yale Yale ROHO MTAKATIFU tarehe 20 April 2017 akaniambia kwa sauti kwamba "Nimekuita kuwa Mwalimu, Kufundisha Neno langu" nikajigundua Mimi ni Nani na nikajua MUNGU anashughulika sana na majina pia, hivyo Inawezekana anawashangaa Watumishi wanaojiita Nabii wakati yeye MUNGU amewaita kama Wainjilisti.
Baadae MUNGU alisema na Mimi juu ya ualimu wa aina gani alioniitia?
Mara 2 nikajiona katika ulimwengu wa roho nikiwa kama Musa alivyokuwa anawatoa Waisraeli utumwani nikasikia sauti ikisema "Kazi Yako ni Mwalimu katika kuwatoa watu kwenye utumwa wa Shetani"
Nikiwa natafakari jukumu hilo ambalo ROHO MTAKATIFU alinipa nilishangaa Mchungaji mmoja kutoka Kenya akaniandikia ujumbe namna ambavyo Bwana YESU KRISTO alimfunulia kuhusu Mimi akisema kama vile nilivyoona Mimi.
Baadae rafiki yangu mmoja kutoka Congo naye akaniambia kitu kile kile kuhusu jukumu langu katika ualimu.
Hivyo pia nikagundua hata huduma ya Ualimu Ina maagizo binafsi kwa kila Mteule wa KRISTO aliyeitwa kwenye huduma hiyo.
Ndugu nakuambia ushuhuda wangu huu ili na Wewe ujue katika kituo Cha kiutumishi ulichoitiwa, ujue umeitiwa Nini katika mwili wa KRISTO ili maelfu ya watu wafike uzima wa milele kwa Wewe kuwaeleza habari za YESU KRISTO anayeokoa.
Mche MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi na utaitwa heri.
Kama pia unatumia Facebook ni follow maana itafika kipindi nitakuwa napost tu katika page yangu na profile yangu.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292(Ni namba hii kupiga, sadaka ya kuipeleka Injili,kuandika meseji na whatsapp).
Ubarikiwe sana.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292(Ni namba hii kupiga, sadaka ya kuipeleka Injili,kuandika meseji na whatsapp).
Ubarikiwe sana.
Comments