![]() |
Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu zangu wote.
Karibu ujifunze kitu kupitia ujumbe huu ambao yalikuwa ni majibu yangu kwa Mama mmoja aliyeniandikia.
◾Mama huyo aliniandikia ujumbe akisema "Mtumishi nilikuwa katika maombi nikipambana na roho za nyoka zinazonifuata kila siku, pia usiku huwa hatulali maana kuna vitu hutua kila siku juu ya paa la nyumba yetu na kutembea juu ya bati hadi asubuhi. Namshukuru sana MUNGU maana nimeokoka miezi kama 10 iliyopita kupitia masomo yako, na tumekuwa tukiomba nguvu za giza zinapungua au kuondoka kwa muda tu, sasa leo nikiwa katika maombi nimesikia sauti ikiniambia kwamba kuna laana ndio maana bado vita ni vikubwa, nisaidie Mtumishi Mabula na nifundishe ili nifute hizo laana, niliambiwa kwa sauti pia kwamba laana mojawapo ni kutokutoa fungu la kumi, kiukweli sijawahi kutoa fungu la kumi, mwezi huu naanza kutoa ila kwa miaka yote ambayo sijawahi kutoa nahitaji ulielekeze jinsi ya kutubu. Pia nimewahi kutoa mimba na wakati mwingine nahisi kuna laana kwenye ukoo wetu na ardhi yetu. Pia nizalishwa na mwanaume kisha akaniacha na huyo mwanaume nilikuja kugundua baadae kwamba alikuwa katika mikataba ya kishetani inayotutesa hadi leo. Nisaidie Mtumishi wa MUNGU katika hili ili nijue jinsi ya kuomba. Kuna siku nimefunuliwa juu ya laana ya kutokutoa zaka ili nilishupaza shingo, nahitaji sana msaada wa kujua kuomba ili kufuta laana."
Baada ya ujumbe huo nilimjibu kama ifuatavyo.
Ubarikiwe sana.
Mshukuru MUNGU amekufunulia juu ya hilo maana amekupa nafasi ya kupona katika hilo la laana, sasa nini ufanye?
1. Tubu kwa ajili ya laana ya MUNGU inayotokana na makosa ya wazazi wako, babu zako na mume wako ambaye alikuzalisha na kukuacha, tubu kwa ajili ya makosa yao yaliyotengeneza laana.
Kumb 28:20 ''BWANA atakuletea laana na mashaka, na kukemewa, katika yote utakayotia mkono wako kuyafanya, hata uangamie na kupotea kwa upesi; kwa ule uovu wa matendo yako, uliyoniacha kwayo.''
✓✓Kuna uovu unaweza kutengeneza laana, uovu huo unaweza kuwa wako binafsi, uovu wa wazazi wako unaokuhusisha wewe, uovu wa familia au ukoo unaokuhusisha wewe na hata uovu wa mwenzi wako ulioiingiza familia katika maagano ya kishetani.
2. Kama kuna laana ya kutokutoa zaka tubu pia tubu kwa ajili ya hiyo.
Malaki 3:9 "Ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana mnaniibia mimi, naam, taifa hili lote."
3. Baada ya hapo futa laana inayokufuatilia mjini.
✓✓Inakupasa ubarikiwe baa sio ulaaniwe.
Kumbu 28:6 "Utabarikiwa uingiapo, utabarikiwa na utokapo."
4. Futa laana inayofuatilia mtoto wako kutokana na makosa ya baba yake.
Kumbu 28:18 "Utalaaniwa uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, maongeo ya ng'ombe wako, na wadogo wa kondoo zako."
5. Futa kila laana za vinywa vya watu kuhusu wewe na watoto wako.
Yakobo 3:9-10 " Kwa huo twamhimidi MUNGU Baba yetu, na kwa huo twawalaani wanadamu waliofanywa kwa mfano wa MUNGU. Katika kinywa kile kile hutoka baraka na laana. Ndugu zangu, haifai mambo hayo kuwa hivyo."
✓✓Baada ya kutubu maombi yote kuhusu laana hufutwa kwa jina la YESU KRISTO huku ukitumia damu ya YESU KRISTO kufuta.
tumia
1 Yohana 1:7" bali tukienenda nuruni, kama yeye alivyo katika nuru, twashirikiana sisi kwa sisi, na damu yake YESU, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote."
na Ufunuo 12:11 "Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa."
Naamini kuna kitu kizuri umejifunza.
Zingatia mteule wa KRISTO na MUNGU atakubariki sana.
Mche MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi na utaitwa heri.
Kama pia unatumia Facebook ni follow maana itafika kipindi nitakuwa napost tu katika page yangu na profile yangu.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292(Ni namba hii kupiga, sadaka ya kuipeleka Injili,kuandika meseji na whatsapp).
Ubarikiwe sana.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292(Ni namba hii kupiga, sadaka ya kuipeleka Injili,kuandika meseji na whatsapp).
Ubarikiwe sana.
Comments