KUKAA KATIKA USIKIVU WA SAUTI YA MUNGU.

Na Mwl Peter Mabula 
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.



Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU wa Mbinguni.

◼️Penda kukaa katika usikivu wa sauti ya MUNGU maana ndani ya usikivu kuna majibu yako.

Usikivu ni nini?

✓✓Usikivu ni tabia ya uelekevu.

✓✓Usikivu wa sauti ya MUNGU ni tabia ya kufanya kama ilivyoamriwa kwenye hiyo sauti ya MUNGU uliposikia.

◼️Usikivu ninaouzungumzia mimi leo ni usikivu wa kumsikia MUNGU katika KRISTO YESU anasema na wewe kupitia Neno lake, ndani ya huo usikivu kuna majibu yako.

Kutoka 19:5-8 "Sasa basi ikiwa mtaitii sauti yangu kweli kweli, na kulishika agano langu, hapo ndipo mtakapokuwa tunu kwangu kuliko makabila yote ya watu; maana dunia yote pia ni mali yangu, nanyi mtakuwa kwangu ufalme wa makuhani, na taifa takatifu. Hayo ndiyo maneno utakayowaambia wana wa Israeli. Musa akaenda akawaita wazee wa watu, akawafunulia maneno hayo yote, BWANA aliyokuwa amemwagiza. Watu wote wakaitika pamoja wakisema, Hayo yote aliyoyasema BWANA tutayatenda. Naye Musa akamwambia BWANA maneno ya hao watu."

◼️Usikivu ninaouzungumzia mimi usikivu wa kumsikia ROHO MTAKATIFU na kufuata anachokitaka yeye maana usipozingatia kuna baraka hutazipata.

Zekaria 4:6 "Akajibu akaniambia, akisema, Hili ndilo neno la Bwana kwa Zerubabeli, kusema, Si kwa uwezo, wala si kwa nguvu, bali ni kwa roho yangu, asema BWANA wa majeshi."

◼️Usikivu ninaouzungumzia mimi ni kuwa makini na kuzingatia sauti ya MUNGU inayozungumza na wewe.

Mwanzo 17:1" Abramu alipokuwa mtu wa miaka tisini na kenda, BWANA akamtokea Abramu, akamwambia, Mimi ni MUNGU Mwenyezi, uende mbele yangu, ukawe mkamilifu."

✓✓Kuna namna MUNGU anaweza kusema na wewe.

◼️MUNGU anaweza akasema umtumikie.

◼️MUNGU anaweza akasema umtolee matoleo fulani, kumbe Kuna sababu ya ushindi wako.

◼️MUNGU anaweza akasema uache dhambi.

◼️MUNGU anaweza akasema mahali fulani usiende, kumbe ni kwa faida Yako.

◼️MUNGU anaweza akakuambia usishirikiane na watu fulani.

◼️MUNGU anaweza akasema "Nenda"

◼️MUNGU anaweza akasema "subiri kwanza"

✓✓Kuna namna nyingi MUNGU anaweza akasema na wewe, usipokuwa msikivu na mzingatiaji wa sauti ya MUNGU unaweza ukapishana na kusudi la MUNGU.

Kumbu 28:15-19 "Lakini itakuwa usipotaka kuisikiza sauti ya BWANA, MUNGU wako, usiyaangalie kufanya maagizo yake yote na amri zake, nikuagizazo hivi leo, ndipo zitakapokujia laana hizi zote na kukupata. Utalaaniwa mjini, utalaaniwa na mashambani. Litalaaniwa kapu lako na chombo chako cha kukandia. Utalaaniwa uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, maongeo ya ng'ombe wako, na wadogo wa kondoo zako. Utalaaniwa uingiapo, utalaaniwa na utokapo,"

✓✓Ndio maana ni jambo la muhimu sana kuwa msikivu na mzingatiaji wa sauti ya MUNGU.

✓✓Ndio maana ni muhimu sana kuwa msikivu na mzingatiaji wa sauti ya Neno la MUNGU.

◼️MUNGU anaweza kusema na wewe kwa njia mbalimbali, mfano MUNGU anaweza akasema na wewe kupitia mafundisho ya Neno lake unayofundishwa.

◼️MUNGU anaweza kusema na wewe kwa ndoto au maono.

◼️MUNGU anaweza kusema na wewe kwa ufunuo wa ROHO MTAKATIFU.

◼️MUNGU anaweza kusema na wewe kupitia watumishi wake waaminifu katika KRISTO YESU, wewe unaona watumishi tu kumbe ndani ya wanachokueleza kuna ujumbe wa MUNGU wenye sauti ya MUNGU kwa ajili yako.

◼️MUNGU anaweza akasema na wewe kupitia Malaika.

◼️MUNGU anaweza kusema na wewe kwa andiko la Biblia.

◼️MUNGU anaweza kusema na wewe kupitia utu wako wa ndani, yaani ndani yako unasikia msukumo wa kufanya jambo fulani la Ki MUNGU.

◼️MUNGU anaweza kusema na wewe kupitia macho yako ya rohoni, unashangaa unaona vitu kwenye ulimwengu wa roho, vingine ni vya MUNGU na vimebeba kusudi la MUNGU katika KRISTO YESU kwa ajili Yako au na kwa ajili ya wengine.

✓✓Jambo muhimu ni kwamba unaoisikia sauti ya MUNGU uwe msikivu na zingatia maelekezo ya sauti ya MUNGU, fanyia kazi maelekezo ya Neno la MUNGU.
Zingatia mteule wa KRISTO na MUNGU atakubariki sana.
Mche MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi na utaitwa heri.
Kama pia unatumia Facebook ni follow maana itafika kipindi nitakuwa napost tu katika page yangu na profile yangu.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter  Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292(Ni namba hii kupiga, sadaka ya kuipeleka Injili,kuandika meseji na  whatsapp).
Ubarikiwe sana.

Comments