![]() |
Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu zangu wote.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU wa Mbinguni.
Katika ibada ya mkesha wa Pasaka mwaka fulani nilipewa nafasi ya kuwa kiongozi wa kipindi cha maombi Kanisani kwetu, rohoni nilipewa ufunuo huu wa maombi ambao niliufundisha kwa muda mchache kisha tukaomba maombi ya ushindi sana.
✓✓Neno la MUNGU ni jipya kila siku hivyo unaweza kutumia ufunuo huu kuomba na damu ya YESU KRISTO ya Pasaka ambayo ni ya agano jipya itakufanya uwe mshindi ajabu.
✓✓Kumbuka wateule wa KRISTO tumenunuliwa kwa damu ya YESU KRISTO ili tusiwe watumwa tena.
1 Wakorintho 7:23 "Mlinunuliwa kwa thamani; msiwe watumwa wa wanadamu."
Maombi hayo ni haya.
1. Omba maombi ya toba ukitumia damu ya YESU KRISTO kukuweka huru mbali na dhambi.
1 Yohana 1:7 "bali tukienenda nuruni, kama yeye alivyo katika nuru, twashirikiana sisi kwa sisi, na damu yake YESU, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote."
2. Omba damu ya YESU KRISTO ya agano ikutakase.
✓✓Ahadi ya MUNGU ni kwamba atatakasa hata eneo lako ambalo halijawahi kutakaswa.
Yoeli 3:21 "Nami nitaitakasa damu yao ambayo sijaitakasa; kwa maana BWANA ndiye akaaye Sayuni."
✓✓Neno la MUNGU pia linataka kila mtu atakaswe kwa damu ya YESU KRISTO ya Agano.
Warumi 6:22 "Lakini sasa mkiisha kuwekwa huru, na kuwa mbali na dhambi, na kufanywa watumwa wa MUNGU, mnayo faida yenu, ndiyo kutakaswa, na mwisho wake ni uzima wa milele."
✓✓Kutakaswa maana yake ni kuondolewa uchafu wa kiroho uliokuwa kizuizi.
✓✓Unapoomba maombi ya kutakaswa kumbuka sana kutaja eneo unalotaka litakaswe kwa damu ya YESU KRISTO.
Watu wengi husema tu "Eee MUNGU Baba nitakase" ila hawasemi wanataka watakaswe nini, hakikisha unataja eneo ambalo unataka litakaswe na damu ya YESU KRISTO.
✓✓Omba damu ya YESU KRISTO itakase mwili wako kiroho.
✓✓Omba damu ya YESU KRISTO itakase nafsi yako kiroho.
✓✓Omba damu ya YESU KRISTO itakase roho yako kiroho.
✓✓Omba damu ya YESU KRISTO itakase ndoa yako, inawezekana ndoa yako ina uchafu wa kiroho unaoifanya isiwe katika hali nzuri siku zote, inawezekana ndoa yako haikuanza katika misingi ya utakatifu n. K
✓✓Omba damu ya YESU KRISTO itakase uchumba wako.
✓✓Omba damu ya YESU KRISTO itakase kibali chako kwenye ulimwengu wa roho.
✓✓Omba damu ya YESU KRISTO ya agano itakase afya yako ili magonjwa yauachie mwili wako.
✓✓Omba damu ya YESU KRISTO ya agano itakase kazi yako na uchumi wako.
✓✓Omba damu ya YESU KRISTO ya agano jipya itakase familia yako na ukoo wako n. k.
3. Omba damu ya YESU KRISTO ya agano jipya ikupatanishe na baraka zako ulizofarakana nazo kwenye ulimwengu wa roho.
Wakolosai 1:20 "na kwa yeye kuvipatanisha vitu vyote na nafsi yake akiisha kufanya amani kwa damu ya msalaba wake; kwa yeye, ikiwa ni vitu vilivyo juu ya nchi, au vilivyo mbinguni."
✓✓Inawezekana wewe nguvu za giza zimekufarakanisha na uchumba, yaani huwezi kuchumbiwa au huwezi kuchumbia, huwezi kutulia katika uchumba, kumbe nguvu za giza zimekufarakanisha na kitu kinaitwa uchumba, ukiingia tu kwenye uchumba hujisikii kuendelea na uchumba au unaachwa tu bila kosa wala dhambi, leo ita damu ya YESU KRISTO ya agano jipya ili ikupatanishe na uchumba na mchumba hata mfunge ndoa takatifu yenye ushuhuda.
✓✓Inawezekana mawakala wa shetani walishaizika ndoa yako, ndio maana kila siku mnatishiana kuachana na mwenzi wako, ndoa yenu ina mgogoro na imeshatenganishwa kwenye ulimwengu wa roho na mawakala wa shetani, leo ita damu ya YESU KRISTO ili ikupatanishe na ndoa yako na ikupatanishe na mwenzi wako wa ndoa na ndipo ndoa yenu itakuwa na amani na furaha na baraka za MUNGU.
✓✓Inawezekana nguvu za giza zimekutenganisha na afya njema ndio maana kila siku unaumwa, leo jipatanishe na afya njema kwa damu ya YESU KRISTO ya agano jipya.
Biblia inasema hapo juu kwamba "yeye(YESU) kuvipatanisha vitu vyote na nafsi yake akiisha kufanya amani kwa damu ya msalaba wake;"
Kumbe damu ya YESU KRISTO ni ya upatanisho pia.
✓✓Inawezekana maadui wamekufarakanisha na uchumi mzuri ndio maana japokuwa unafanya kazi halali kwa bidii sana lakini mafanikio hakuna, leo ita damu ya YESU KRISTO ya agano ili ikupatanishe na uchumi mzuri unaotakana na kazi yako njema.
✓✓Inawezekana mawakala wa shetani wamekufarakanisha na uzao ndio maana uko kwenye ndoa na muda mrefu hujapata mtoto, leo jipatanishe na uzao wako na utaupata.
✓✓Jipatanishe na kibali chako, kwa maombi jipatanishe na watu wazuri na waliobeba kusudi la MUNGU kwa ajili yako.
✓✓Inawezekana pia familia au ukoo mnaishi kama maadui wakubwa sana, ita damu ya YESU KRISTO ya agano jipya ili ikupatanishe na ndugu zako hata muishi kwa upendo, furaha na amani ya MUNGU.
Hata wanaokuchukia unaweza kuomba maombi ya toba kisha ukaita damu ya YESU KRISTO ya agano ya upatanisho na utashangaa hawakuchukii tena, utashangaa wanakupa ushirikiano tena.
Mambo mengi sana yanahitaji upatanisho kwenye ulimwengu wa roho, wewe ndio unajua katika maisha yako ni wako panahitaji upatanisho wa damu ya YESU KRISTO ndipo mambo yatakuwa sawa, ndugu omba.
4. Omba damu ya YESU KRISTO ya agano ikupe ushindi dhidi ya nguvu za giza.
Ufunuo 12:11 "Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa."
Naamini kuna kitu kizuri umejifunza.
Zingatia mteule wa KRISTO na MUNGU atakubariki sana.
Mche MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi na utaitwa heri.
Kama pia unatumia Facebook ni follow maana itafika kipindi nitakuwa napost tu katika page yangu na profile yangu.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292(Ni namba hii kupiga, sadaka ya kuipeleka Injili,kuandika meseji na whatsapp).
Ubarikiwe sana.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292(Ni namba hii kupiga, sadaka ya kuipeleka Injili,kuandika meseji na whatsapp).
Ubarikiwe sana.
Comments