![]() |
Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu zangu wote.
Karibuni sana tujifunze Neno la MUNGU aliyeziumba mbingu na nchi.
◼️Kanisa lenye nguvu ni lile ambalo ROHO MTAKATIFU anatawala.
✓✓ROHO MTAKATIFU ndiye hulipa Kanisa la MUNGU uhai, uzima na nguvu.
Zekaria 4:6 "............ Si kwa uwezo, wala si kwa nguvu, bali ni kwa roho yangu, asema Bwana wa majeshi."
✓✓Kanisa ni Mkristo aliyeokolewa na YESU KRISTO Mwokozi, hivyo Mkristo huyo akiwa na ROHO MTAKATIFU atakuwa na uhai wa kiroho na kimwili, atakuwa salama maana ROHO MTAKATIFU atamjulisha na kumfundisha.
✓✓Kanisa ni kundi la watu ambao YESU KRISTO ni Mwokozi wao na wanaishi maisha matakatifu ya Wokovu na kumwabudu MUNGU Baba katika roho na kweli, Kanisa hili likiambatana na ROHO MTAKATIFU lazima liwe Kanisa hai lenye uzima na mamlaka ya kiroho yenye nguvu.
◼️Ndio maana Biblia inataka kila Mtu duniani awe na KRISTO huku akimtumikia MUNGU katika ROHO MTAKATIFU.
Mathayo 28:19" Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;"
✓✓Kama Kanisa hai la KRISTO duniani hakikisha wewe Kanisa una ROHO MTAKATIFU na unamtii ili akusaidie kuishi maisha ya ushindi duniani.
1 Yohana 4:2-6 " Katika hili mwamjua ROHO wa MUNGU; kila roho ikiriyo kwamba YESU KRISTO amekuja katika mwili yatokana na MUNGU. Na kila roho isiyomkiri YESU haitokani na MUNGU. Na hii ndiyo roho ya mpinga Kristo ambayo mmesikia kwamba yaja; na sasa imekwisha kuwako duniani. Ninyi, watoto wadogo, mwatokana na MUNGU nanyi mmewashinda, kwa sababu yeye aliye ndani yenu ni mkuu kuliko yeye aliye katika dunia. Hao ni wa dunia; kwa hiyo wanena ya dunia na dunia huwasikia Sisi twatokana na MUNGU. Yeye amjuaye MUNGU atusikia; yeye asiyetokana na MUNGU hatusikii. Katika hili twamjua ROHO wa kweli, na roho ya upotevu."
◼️ROHO MTAKATIFU akiwa kwenu atawafunulia mambo mengi sana ya kuwasaidia na kuwafundisha.
◼️Kwenye Kanisa lenu mkiambatana na ROHO MTAKATIFU atawafunulia mambo mengi sana ili kuwasaidia.
1 Kor 2:10-11 '' Lakini MUNGU ametufunulia sisi kwa ROHO. Maana ROHO huchunguza yote, hata mafumbo ya MUNGU. Maana ni nani katika binadamu ayajuaye mambo ya binadamu ila roho ya binadamu iliyo ndani yake? Vivyo hivyo na mambo ya MUNGU hakuna ayafahamuye ila ROHO wa MUNGU.''
◼️Kwenye kundi lenu la maombi au kwaya yenu mkiwa na ROHO MTAKATIFU atawafunulia mambo mengi sana sana ya kuwasaidia.
Yohana 14:26 '' Lakini huyo Msaidizi, huyo ROHO MTAKATIFU, ambaye Baba(MUNGU) atampeleka kwa jina langu(YESU KRISTO), atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia.''
◼️Kwenye idara yenu ya Wamama au Vijana au Wababa mkiambatana na ROHO MTAKATIFU atawafunulia mambo mengi sana ya kuwasaidia na kusaidia kazi yenu na kiroho cha kila mmoja wenu.
Zaburi 32:8 '' Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea; Nitakushauri, jicho langu likikutazama.''
◼️Kwenye familia yenu au kwenye ndoa yenu mliookoka mkiambatana na ROHO MTAKATIFU hakika atawafunulia mambo mengi sana na kuwasaidia katika mambo mengi sana.
Yohana 16:13 '' Lakini yeye atakapokuja, huyo ROHO wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake. ''
◼️Roho mtakatifu ni wa muhimu sana katika maisha binafsi ya Mkristo aliyeokoka, kwa Kanisa, kwa Ndoa, kwenye Familia, kwenye kundi, kwenye idara Kanisani n.k
✓✓Mhitaji sana ROHO MTAKATIFU katika maisha yako yote.
✓✓Mhitajini sana ROHO MTAKATIFU katika Kanisa lenu, Ndoa yemu, familia au kundi lenu.
Kumbuka Warumi 8:14-16 inasema '' Kwa kuwa wote wanaoongozwa na ROHO wa MUNGU, hao ndio wana wa MUNGU. Kwa kuwa hamkupokea tena roho wa utumwa iletayo hofu; bali mlipokea roho ya kufanywa wana, ambayo kwa hiyo twalia, Aba, yaani, Baba. ROHO mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa MUNGU;''
Zingatia na MUNGU atakubariki sana.
Mche MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi na utaitwa heri.
Kama pia unatumia Facebook ni follow maana itafika kipindi nitakuwa napost tu katika page yangu na profile yangu.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292(Ni namba hii kupiga, sadaka ya kuipeleka Injili,kuandika meseji na whatsapp).
Ubarikiwe sana.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292(Ni namba hii kupiga, sadaka ya kuipeleka Injili,kuandika meseji na whatsapp).
Ubarikiwe sana.
Comments