![]() |
Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.
Wakolosai 3:16 "Neno la KRISTO na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia MUNGU kwa neema mioyoni mwenu."
◼️Mambo 10 ya kujua kuhusu Neno la KRISTO.
1. Neno la KRISTO YESU ndilo Neno la MUNGU mwenyewe.
Yohana 14:24" Mtu asiyenipenda, yeye hayashiki maneno yangu; nalo neno mnalolisikia silo langu(YESU), ila ni lake Baba(MUNGU) aliyenipeleka."
2. Asiyelishika Neno la KRISTO Neno hilo ndilo litamhukumu siku ya mwisho.
Yohana 12:48 "Yeye anikataaye mimi(YESU), asiyeyakubali maneno yangu, anaye amhukumuye; neno hilo nililolinena ndilo litakalomhukumu siku ya mwisho."
3. Neno la KRISTO halitapita kamwe.
Mathayo 24:35" Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe."
4. Anayemuonea aibu YESU KRISTO na Neno lake mtu huyo ataonewa aibu siku ya mwisho.
Marko 8:38 "Maana kila mtu atakayenionea haya mimi, na maneno yangu, katika kizazi hiki cha uzinzi na dhambi, Mwana wa Adamu atamwonea haya mtu huyo, atakapokuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika watakatifu."
5. Ukilifanyia kazi Neno la KRISTO utafananishwa na mtu mwenye akili aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba.
Mathayo 7:24" Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba;"
6. Mtu ajaye kwa YESU KRISTO na kulifanyia kazi Neno la KRISTO mtu huyo anakuwa ameweka msingi wake juu ya kwamba usiotikisika wala kuharibiwa.
Luka 6:47-48 "Kila mtu ajaye kwangu, na kuyasikia maneno yangu na kuyatenda, nitawaonyesha mfano wake. Mfano wake ni mtu ajengaye nyumba, na kuchimba chini sana, na kuweka msingi juu ya mwamba; na kulipokuja gharika, mto uliishukia nyumba ile kwa nguvu, usiweze kuitikisa; kwa kuwa imejengwa vizuri."
7. Mtu alisikiaye Neno la KRISTO na asilifanyie kazi mtu huyo atafananishwa na mpumbavu.
Mathayo 7:26" Na kila asikiaye hayo maneno yangu asiyafanye, atafananishwa na mtu mpumbavu, aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga;"
8. Neno la KRISTO huonyesha pia kutimia yote aliyoandikiwa KRISTO Katika Torati, Manabii na Zaburi.
Luka 24:44 "Kisha akawaambia, Hayo ndiyo maneno yangu niliyowaambia nilipokuwa nikali pamoja nanyi, ya kwamba ni lazima yatimizwe yote niliyoandikiwa katika Torati ya Musa, na katika Manabii na Zaburi."
9. Mtu akikaa ndani ya KRISTO na akaliishi Neno la KRISTO anapata kibali cha kuomba kwa MUNGU na kupokea.
Yohana 15:7 "Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa."
10. Imani ya waenda uzima wa milele chanzo cha imani hiyo ni kulisikia Neno la KRISTO.
Warumi 10:17 "Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la KRISTO."
◼️Nimekuandikia ujumbe huu ndugu ili kukujulisha kwamba Neno la KRISTO ndilo Neno la MUNGU na huna sababu hata moja ya kujitenga na Neno la KRISTO.
✓✓Kuna manabii wa uongo wengi siku hizi, uwe makini ili wasikutoe kwa YESU KRISTO Mwokozi.
✓✓Kuna mitume wa uongo wengi siku hizi, uwe makini ili wasikutoe kwa YESU KRISTO kwenye uzima.
✓✓Kuna wachungaji wa uongo wengi siku hizi, uwe makini ili wasikutoe kwa YESU KRISTO anayeokoa.
✓✓Kuna wainjilisti matapeli wengi siku hizi, uwe makini ili wasikutoe kwa YESU KRISTO Mwokozi.
✓✓Kuna walimu wa uongo wengi siku hizi, uwe makini ili wasikuondoe kwenye Wokovu wa Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
✓✓Kuna watu sasa hata hawaombi tena katika Nina la YESU KRISTO, hao ni matapeli, wakimbie haraka sana.
Ndugu nawiwa rohoni mwangu pia nikushauri Mambo haya yafuatayo.
◼️Haijalishi unaishi katikati ya mazingira magumu sana, ishi maisha matakatifu.
◼️Ndugu, haijalishi huna kazi au huna pesa, ishi maisha matakatifu ya Wokovu wa KRISTO YESU.
✓✓Wakati wa shida au wakati wa tabu bado inakupasa uishi maisha matakatifu ya Wokovu wa KRISTO.
2 Timotheo 2:19" Lakini msingi wa MUNGU ulio imara umesimama, wenye muhuri hii, BWANA awajua walio wake. Na tena, Kila alitajaye jina la BWANA na auache uovu."
✓✓Ndugu, haijalishi umeoa au hujaoa ishi maisha matakatifu ya Wokovu wa KRISTO.
✓✓Haijalishi umeolewa au hujaolewa hakikisha unaishi maisha matakatifu ya Wokovu wa Bwana YESU KRISTO.
✓✓Haijalishi una kazi au huna hakikisha unaishi maisha matakatifu ya Wokovu.
✓✓Haijalishi uko Kanisani au uko shuleni, hakikisha unaishi maisha matakatifu ya Wokovu.
◼️Katika hali zako zote za maisha yako yote hakikisha YESU KRISTO ni Mwokozi wako na unaishi maisha matakatifu katika Wokovu wake.
Hali yako yeyote usikubali ikakufanya uishi maisha ya dhambi.
✓✓Ndugu jilinde sana usianguke dhambini.
✓✓Waliookoka hujilinda mbali na dhambi, ndugu naomba uwe wewe.
1 Yohana 5:18" Twajua ya kuwa kila mtu aliyezaliwa na MUNGU hatendi dhambi; bali yeye aliyezaliwa na MUNGU hujilinda, wala yule mwovu hamgusi."
Mche MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi na utaitwa heri.
Kama pia unatumia Facebook ni follow maana itafika kipindi nitakuwa napost tu katika page yangu na profile yangu.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292(Ni namba hii kupiga, sadaka ya kuipeleka Injili,kuandika meseji na whatsapp).
Ubarikiwe sana.
Comments