![]() |
Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.
◼️Kuna mambo saba ya kiroho ambayo kwa pamoja ukiyazingatia utalindwa na MUNGU siku zote.
1. Kuokoka.
Wakolosai 1:13-14 " Naye(MUNGU) alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake; ambaye katika yeye(YESU) tuna ukombozi, yaani, msamaha wa dhambi;"
✓✓Kuokoka kunakufanya uwe Mali ya MUNGU, hivyo ukiwa unatembea kwenye kanuni za MUNGU ujue utalindwa.
◼️Kuokoka ni kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako kisha unaanza kuishi maisha matakatifu katika yeye.
YESU KRISTO anasema " Nami nawapa uzima wa milele; wala hawatapotea kamwe; wala hakuna mtu atakayewapokonya katika mkono wangu.-Yohana 10:28
2. Maombi katika KRISTO YESU.
Mathayo 7:8 "kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa."
✓✓Ukiomba MUNGU akulinde hakika atakulinda hata kama adui zako ni wengi sana.
Habu Leo MUNGU katika KRISTO YESU akulinde mwaka huu wote, hakika atakulinda.
Maombi pia yako ya namna nyingi kulingana na ufunuo wa ROHO MTAKATIFU, lakini pia usisahau maombi ya kufunga nayo ni muhimu sana.
Mathayo 17:21 [Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga.]
3. Kumwendea MUNGU kwa imani thabiti katika KRISTO.
Waebrania 11:6" Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye MUNGU lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao."
✓✓Usimwendee MUNGU kwa kujaribu utakosa unachokihitaji Bali mwendee ukiwa umeamua Toka moyoni.
◼️Hata kulindwa na MUNGU unalindwa kwa imani, hivyo ukikosa imani thabiti katika KRISTO utakosa hata ulinzi wa MUNGU.
Ndugu tanguliza Imani kwa MUNGU kama Unahitaji ulinzi wake.
1 Petro 1:5 "Nanyi mnalindwa na nguvu za MUNGU kwa njia ya imani hata mpate wokovu ulio tayari kufunuliwa wakati wa mwisho."
4. Kutoa zaka na dhabihu.
Malaki 3:10-12 "Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema BWANA wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la. Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema BWANA wa majeshi. Na mataifa yote watawaiteni heri; maana mtakuwa nchi ya kupendeza sana, asema BWANA wa majeshi."
✓✓Hii ni muhimu sana kwa mtu anayehitaji kulindwa na MUNGU na kuepuka nguvu za giza kukushinda.
✓✓MUNGU ameahidi ulinzi kwa watoaji wa Zaka na Sadaka hivyo ukihitaji ulinzi wake juu ya familia Yako, Ndoa Yako, Biashara Yako, Afya Yako n.k basi zingatia sana utoaji kwa MUNGU.
5. Kumtegemea MUNGU katika KRISTO YESU.
Yeremia 17:7-8 " Amebarikiwa mtu yule anayemtegemea BWANA, Ambaye BWANA ni tumaini lake. Maana atakuwa kama mti uliopandwa kando ya maji, Uenezao mizizi yake karibu na mto; Hautaona hofu wakati wa hari ujapo, Bali jani lake litakuwa bichi; Wala hautahangaika mwaka wa uchache wa mvua, Wala hautaacha kuzaa matunda."
✓✓Ukitaka MUNGU wa Mbinguni akulinde basi mtegemee.
Watu wengi leo wanategemea Wanadamu, majini, mizimu n.k ndio maana MUNGU hawezi kuwalinda na watu hao wameishia tu kuonewa na nguvu za giza.
✓✓Ndugu Amua kuanzia Leo Kumtegemea MUNGU wa Mbinguni aliyejifunua pekee Katika KRISTO YESU Mwokozi.
6. Kumtumaini MUNGU.
Isaya 26:3-4 " Utamlinda yeye ambaye moyo wake umekutegemea Katika amani kamilifu, kwa kuwa anakutumaini. Mtumainini BWANA siku zote Maana Bwana YEHOVA ni mwamba wa milele."
Kumtumaini MUNGU ni nini?
✓✓Kumtumaini MUNGU ni kuwa na Imani ya kupata au kufanikiwa katika MUNGU.
✓✓Kumtumaini MUNGU nikuamini kuwa atafanya yale ambayo ameahidi kwako au katika Neno lake Biblia.
7. Kuwa na ROHO MTAKATIFU.
1 Yohana 4:4 "Ninyi, watoto wadogo, mwatokana na MUNGU nanyi mmewashinda, kwa sababu yeye(ROHO MTAKATIFU) aliye ndani yenu ni mkuu kuliko yeye(shetani) aliye katika dunia."
✓✓ROHO MTAKATIFU ni wa muhimu sana na ana kazi nyingi sana kwako mteule wa KRISTO.
✓✓Moja ya kazi ya ROHO MTAKATIFU ni kwamba atakujulisha mambo yajayo, hata mipango mibaya ya adui zako atakujulisha na kukufundisha jinsi ya kuwashinda mawakala wa shetani.
Yohana 16:13 "Lakini yeye atakapokuja, huyo ROHO wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake."
Mche MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi na utaitwa heri.
Kama pia unatumia Facebook ni follow maana itafika kipindi nitakuwa napost tu katika page yangu na profile yangu.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292(Ni namba hii kupiga, sadaka ya kuipeleka Injili,kuandika meseji na whatsapp).
Ubarikiwe sana.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292(Ni namba hii kupiga, sadaka ya kuipeleka Injili,kuandika meseji na whatsapp).
Ubarikiwe sana.
Comments