![]() |
By Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe ndugu zangu wote.
◼️Leo omba maombi ya kung'oa, kubomoa, kuharibu na kuangamiza.
Yeremia 1:10 "angalia, nimekuweka leo juu ya mataifa na juu ya falme, ili kung'oa, na kubomoa, na kuharibu, na kuangamiza; ili kujenga na kupanda."
1. Maombi ya kung'oa.
Unang'oa nini?
◼️Unang'oa mapando yote ya shetani.
Maana kila asilolipanda MUNGU basi hilo ni pando la shetani na inatakiwa tuling'oe pando hilo.
Mathayo 15:13 "Akajibu, akasema, Kila pando asilolipanda BABA yangu wa mbinguni LITANG'OLEWA."
Magonjwa na vifungo ni mapando ya shetani, leo ng'oa mapando yote ya shetani kwa Jina la YESU KRISTO.
Kama mnaishi maisha matakatifu lakini kuna mafarakano ndani ya Ndoa au uchumba ni mapando ya shetani, leo ng'oa mapando yote ya shetani kwa Jina la YESU KRISTO.
✓✓Tumia nafasi yako kiroho katika KRISTO YESU kwa maombi ili kung'oa mapando yote ya shetani yaliyopandwa kazini kwako,nyumbani kwako, kwenye biashara yako, kwenye familia au ukoo, kwenye mwili wako, kwenye uzao wako na kwenye kibali chako.
Imeandikwa kila pando asilolipanda MUNGU litang'olewa hivyo leo wewe Mteule wa KRISTO yang'oe mapando yote ya shetani.
2. Maombi ya kubomoa.
Unabomoa nini?
◼️Unabomoa madhabahu za giza zote zinazoshindana na wewe.
Kumbu 7:5 "Lakini watendeni hivi; zivunjeni madhabahu zao zibomosheni nguzo zao, yakateni maashera yao, ziteketezeni kwa moto sanamu zao za kuchonga."
Inawezekana unapambana madhabahu ya uchawi, uganga, mizimu, madhabahu ya ulevi, madhabahu ya kidini iliyo kinyume na KRISTO YESU Mwokozi, madhabahu ya ukoo au madhabahu ya kipepo ya kifamilia n. K
Inawezekana inapambana na madhabahu za majoka ndio maana kila siku inapambana na nyoka ndotoni, leo bomoa madhabahu hizo za giza.
Katika kubomoa madhabahu za giza kanuni mojawapo ya kimaombi ni kujua hizo madhabahu ziko sehemu gani ili uzibomoe na kulifuta hapo jina la hiyo miungu hapo.
Kumbu 12:2-3 " Vunjeni kabisa mahali pote walipokuwa wakiitumikia miungu yao mataifa mtakayoyamiliki, juu ya milima mirefu, na juu ya vilima, na chini ya kila mti wenye majani mabichi; nanyi zivunjeni madhabahu zao, zibomoeni nguzo zao, na maashera yao yateketezeni kwa moto, na sanamu za kuchonga za miungu yao zikateni; na jina lao lifutilieni mbali na mahali hapo."
3. Maombi ya kuharibu.
Unaharibu nini?
◼️Unaharibu kazi zote za shetani katika maeneo yako, familia yako, kazini kwake au kwenye nyumba unayokaa.
✓✓Ashukuriwe MUNGU maana Bwana YESU KRISTO alikuja duniani ili kuzivunja na kuziharibu kazi zote za shetani, sasa kwa sababu wewe ni mteule wa KRISTO basi leo kwa maombi haribu kazi zote za shetani huku ukizitaja kazi hizo.
1 Yohana 3:8 "atendaye dhambi ni wa Ibilisi; kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa MUNGU alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi."
Haribu tabia mbaya ndani yako au ndani ya ndugu zako, haribu nguvu za giza ndani ya mwenzi wako ili asiwe mkali au msaliti n. K
Nani anataka kufungua kituo cha uganga wa kienyeji katika mtaa wako, leo haribu hiyo kazi ya shetani na hawatamjengea madhabahu shetani katika mtaa wako au kijiji chako.
Nani anakuchongea kazini ili ufukuzwe,nani anamshawishi mchumba wako vibaya, haribu kila kazi ya shetani na itaharibika leo kwa jina la YESU KRISTO Mwokozi aliye hai.
Haribu roho ya hofu na woga ndani yako n.k
4. Maombi ya kuangamiza.
Kuangamiza nini?
◼️Kuangamiza falme za giza na majeshi ya pepo wabaya.
Waefeso 6:12 "Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho."
✓✓Ukiwa unapambana na ufalme wa giza ujue unapambana vitu viwili.
Unapambana na mfalme wa giza na unapambana na watenda kazi wa huo ufalme wa giza.
Kuna wafalme wa giza wengi ambao chini yao wana watendakazi ambao ni majini, kwa hiyo hakikisha unaangamiza ufalme wa giza kwa kumpiga mfalme wa huo ufalme na pambana pia na nguvu za giza zinazotumwa kutoka ufalme huo.
Ufalme wa giza ukiuruhusu ukatawala huwa unafanya uharibifu mkubwa sana na utashangaa familia yako au wewe unakuwa na vita kwenye kila eneo.
Kazi nyingine ya ufalme wa giza ni kuteka watu wa MUNGU na kuteka uchumi wa watu wa MUNGU.
Mfano hai ni wafalme waliomteka Lutu na hawakuishia kumteka Lutu tu bali waliteka na mali zake yaani uchumi wake. Ibrahimu mtumishi wa MUNGU alipambana na falme hizo hadi Lutu akaachiliwa.
Mwanzo 14:12-17 " Wakamtwaa Lutu, mwana wa nduguye Abramu, aliyekaa huko Sodoma, na mali yake, wakaenda zao. Mtu mmoja aliyeponyoka akaenda, akampasha habari Abramu Mwebrania; naye amekaa panapo mialoni ya Mamre, yule Mwamori, ndugu ya Eshkoli, na ndugu ya Aneri, na hao walikuwa wamepatana na Abramu. Abramu aliposikia ya kwamba nduguye ametekwa mateka, akawapa silaha vijana wake, waliozaliwa katika nyumba yake, watu mia tatu na kumi na wanane, akawafuata mpaka Dani. Akajipanga apigane nao usiku, yeye na watumwa wake, akawapiga, akawafukuza mpaka Hoba, ulioko upande wa kushoto wa Dameski. Naye akarudisha mali zote, akamrudisha na Lutu nduguye na mali zake, na wanawake pia, na watu. Abramu aliporudi kutoka kumpiga Kedorlaoma na wale wafalme waliokuwa pamoja naye, mfalme wa Sodoma akatoka amlaki katika bonde la Shawe, nalo ni Bonde la Mfalme."
Hapo ndipo tunajua uvamizi wa ufalme ni ili kuteka watu na uchumi.
Lakini ni jambo la ajabu familia moja ya Ibrahimu mtumishi wa MUNGU iliweza kuwashinda falme zaidi ya mbili za maadui, hiyo inatufundisha na kutupa ujasiri kwamba wewe muombaji mmoja katika KRISTO YESU unaweza kupambana na ufalme fulani wa giza na ukaushinda, tunashinda kwa maombi tu huku tukijua namna ya kupambana na tunajua tunapambana na nini.
◼️MUNGU Baba ametupa mamlaka kubwa sana katika KRISTO YESU na tukijitambua hakuna ufalme wa giza utatushinda.
Luka 10:19 "Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru."
Inatosha kwa leo maarifa haya ya kukusaidia kujua ili uombe.
Zingatia mteule wa KRISTO na MUNGU atakubariki sana.
Mche MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi na utaitwa heri.
Kama pia unatumia Facebook ni follow maana itafika kipindi nitakuwa napost tu katika page yangu na profile yangu.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292(Ni namba hii kupiga, sadaka ya kuipeleka Injili,kuandika meseji na whatsapp).
Ubarikiwe sana.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292(Ni namba hii kupiga, sadaka ya kuipeleka Injili,kuandika meseji na whatsapp).
Ubarikiwe sana.
Comments