![]() |
Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.
◼️MUNGU anaweza kugeuza maapizo ya maadui zako, na viapo hivyo vikawa baraka kwako.
Kumbu 23:5 "Lakini BWANA, Mungu wako, hakukubali kumsikiza huyo Balaamu; BWANA, Mungu wako, aliyageuza yale maapizo kuwa ni baraka, kwa vile alivyokupenda BWANA, Mungu wako."
✓✓Biblia inasema kwamba MUNGU aligeuza maapizo ya Baraki kwa Waisraeli, maapizo hayo yakageuzwa na kuwa baraka kwa Waisraeli.
Maapizo hayo yalikuwaje?
Biblia inayazungumzia.
Hesabu 22:6" Basi, njoo wewe, nakusihi unilaanie watu hawa; maana wana nguvu kunishinda mimi. Labda nitawaweza, tupate kuwapiga, niwafukuze watoke katika nchi yangu, kwa maana najua ya kuwa yeye umbarikiye hubarikiwa, na yeye umlaaniye hulaaniwa."
✓✓Maapizo ya Baraki yalikuwa kwamba Balaamu awalaani Waisraeli lakini badala ya Waisraeli kulaaniwa MUNGU akawabariki, yaani MUNGU aligeuza maapizo ya Baraki yakawa baraka na sio laana.
✓✓Maadui zako wanaweza kukaa kikao kukulaani lakini ukijua kufanya maombi basi MUNGU anaweza kugeuza maapizo yao hivyo badala ya kuwa laana yakawa baraka.
Yaani kama wanasema "atakufa huyu" ndio MUNGU akakupa kuishi Miaka mingi kuliko wao wote waliosema utakufa.
✓✓Hujawahi kuona au kusikia Mtu akimtakia Mtu Mwingine kufa Kisha akafa yeye kabla ya aliyemtakia kufa?
Hiyo ndio inaitwa MUNGU kugeuza maapizo mabaya kubwa baraka.
Wako wabaya wanaoweza kumwazia Mtu mwema mambo mabaya ili yampate.
Zaburi 41:5-10 " Adui zangu wananitaja kwa maneno mabaya, Atakufa lini, jina lake likapotea? Na mmoja wao akija kunitazama asema uongo, Moyo wake hujikusanyia maovu, Naye atokapo nje huyanena. Wote wanaonichukia wananinong'ona, Wananiwazia mabaya. Neno la kisirani limemgandama, Na iwapo amelala hatasimama tena. Msiri wangu tena niliyemtumaini, Aliyekula chakula changu, Ameniinulia kisigino chake.
Lakini Wewe, BWANA, unifadhili, Uniinue nipate kuwalipa."
✓✓Yusufu ndugu zake walikusudia kumuua, kisha wakakusudia kumuuza ili awe Mtumwa, kisha akawa mtumwa na kisha akawa mfungo asiye na hatia, MUNGU akageuza maapizo hayo yote na kumfanya Yusufu kuwa Rais Msaidizi wa Nchi.
MUNGU aligeuza mabaya kuwa mema.
Mwanzo 50:20 "Nanyi kweli mlinikusudia mabaya, bali MUNGU aliyakusudia kuwa mema, ........"
✓✓Omba ndugu na utamuona MUNGU wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo.
✓✓Wewe Mwanamke Inawezekana Mawakala wa shetani walipanga usiolewe, watashangaa unaolewa kwa kufunga ndoa takatifu Kanisani.
✓✓Wewe Ndugu inawezekana wachawi Waliapa usipate kazi, MUNGU anaweza kugeuza viapo vyao na wakashangaa unapata kazi nzuri.
✓✓Inawezekana unaumwa sana na wachawi waliapa kwamba hutapona, uking'ng'ana na YESU KRISTO kwa maombi hakika MUNGU atageuza viapo vyao kuwa baraka, walisema huponi lakini YESU KRISTO anakuponya na kukupa miaka mingi ya kuishi.
Zaburi 102:19-20 " Maana ametazama toka patakatifu pake pa juu, Toka mbinguni BWANA ameiangalia nchi, Ili akusikie kuugua kwake aliyefungwa, Na kuwafungua walioandikiwa kufa."
◼️Ndugu, kazi yako ni kuishi Maisha matakatifu katika KRISTO YESU, kufanya maombi ya kumsihi MUNGU ageuze maapizo ya wakuu wa giza waliyoyapanga kuhusu wewe na inakuwa kwa Jina la YESU KRISTO Mwokozi wetu aliye hai milele.
Inawezekana wabaya wako walisema ndoa yako inakufa, MUNGU anaweza kugeuza maapizo yao hivyo ndoa yako inakuwa ni ndoa ya amani na furaha huku ndoa zao ndizo zinaanza migogoro.
Inawezekana kuna mganga wa kienyeji alikuroga usizae, MUNGU anaweza kugeuza maapizo yao hao mawakala wa shetani na sasa kwa maombi ukapata uzao bora, huku wao wakiteswa na watoto wao.
Zaburi 113:9 "Huweka nyumbani mwanamke aliye tasa, Awe mama ya watoto mwenye furaha."
Mawakala wa shetani waliapa kwa viapo kwamba hutapata kibali popote kamwe, MUNGU anaweza kukupa kibali kikuu sana, unaweza kupata kibali hadi ikulu au Bungeni au Wizarani au Ofisi kubwa nyingine yeyote na ukafanya kazi yako vyema na kwa mafanikio huku ukisifiwa na wakuu wako wa kazi, kibali cha MUNGU kina nguvu sana.
Zaburi 113:7-8 "Humwinua mnyonge kutoka mavumbini, Na kumpandisha maskini kutoka jaani. Amketishe pamoja na wakuu, Pamoja na wakuu wa watu wake."
✓✓Ni furaha kwako kama MUNGU akigeuza viapo vya maadui zako, kazi yako ni kuishi maisha matakatifu ya haki katika KRISTO YESU huku ukiwa Muombaji.
Inawezekana mawakala wa shetani wameapiana kwamba mtoto wako au ndugu yako au mzazi wako au mwenzi wako hatapona bali atakufa, Bwana YESU anaweza kugeuza kwa kumponya na kumpa maisha marefu sana.
Kutoka 23:26 "Hapatakuwa na mwenye kuharibu mimba, wala aliye tasa, katika nchi yako; na hesabu ya siku zako nitaitimiza."
✓✓Omba tu ndugu ili MUNGU ageuze viapo vya maadui zako, viapo hivyo vigeuke baraka.
✓✓Omba ndugu na ishi maisha matakatifu ya Wokovu wa Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
◼️Mwamini MUNGU na mtegemee zaidi, omba ukitumia maandiko, omba katika jina la YESU KRISTO huku ukitumia damu ya YESU KRISTO na Neno la MUNGU.
✓✓Maadui zako wanaweza kujikuta kila baya walilokutamkia linageuka kinyume chake na maana MUNGU amegeuza maapizo yao yote yawe baraka kwako huku wao ndio wakifikwa na mabaya waliyokusudia.
Zaburi 71:13 "Waaibishwe, watoweshwe, adui za nafsi yangu. Wavikwe laumu na aibu wanaonitakia mabaya."
Nani alisema hutafanikiwa?
✓✓Anaweza asifanikiwe yeye Ila sio wewe.
✓✓Wapo hadi watu kazi zao ni kulaani watu na kuwafunga kwa maneno mabaya, ndugu kama wewe umeokoka na ni muombaji basi ukiomba maombi ya kugeuza uteka basi MUNGU anaweza kugeuza viapo vya maadui zako na uteka wao na sasa ukafanikiwa na kuzidi.
Mkumbuke Ayubu ambaye alipoteza Mali zake zote, lakini alivyosimama na MUNGU siku zote MUNGU akampa baraka Mara mbili ya Mali za kwanza.
Ayubu 42:10" Kisha BWANA akaugeuza uteka wa Ayubu, hapo alipowaombea rafiki zake; BWANA naye akampa Ayubu mara mbili kuliko hayo aliyokuwa nayo kwanza."
Omba ndugu na MUNGU akubariki sana.
Zingatia mteule wa KRISTO na MUNGU atakubariki sana.
Mche MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi na utaitwa heri.
Kama pia unatumia Facebook ni follow maana itafika kipindi nitakuwa napost tu katika page yangu na profile yangu.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292(Ni namba hii kupiga, sadaka ya kuipeleka Injili,kuandika meseji na whatsapp).
Ubarikiwe sana.
Comments