![]() |
Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
Bwana YESU atukuzwe ndugu.
Karibu ujifunze kitu katika ujumbe huu mfupi.
Walawi 1:1-3 " BWANA akamwita Musa, na kusema naye kutoka katika hema ya kukutania, akamwambia, Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Mtu wa kwenu atakapomtolea BWANA matoleo, mtatoa matoleo yenu katika wanyama wa mifugo, katika ng'ombe na katika kondoo. Matoleo yake kwamba ni sadaka ya kuteketezwa ya ng'ombe, atatoa ng'ombe mume mkamilifu; ataleta mlangoni pa hema ya kukutania, ili akubaliwe mbele ya BWANA."
✓✓Kwa mujibu wa maandiko hapo juu ni kwamba moja ya kazi mojawapo ya sadaka ni ili kukubaliwa mbele za MUNGU.
✓✓Lakini MUNGU anasema anahitaji sadaka kamilifu na sio vinginevyo.
Sadaka za Waisraeli zamani zilikuwa wanyama, MUNGU alikataa Mtu kutoa Sadaka ambayo ni kilema.
Walawi 22: 20 “Lakini mnyama ye yote aliye na kilema msimtoe; kwa kuwa hatakubaliwa kwa ajili yenu”
◼️MUNGU wa Mbinguni anaendelea kukataza watu kutoa Sadaka kilema.
Malaki 1:13 “Tena mwasema, Tazama, jambo hili linatuchokesha namna gani! Nanyi mmelidharau, asema Bwana wa majeshi; nanyi mmeleta kitu kilichopatikana kwa udhalimu, na kilema, na kilicho kigonjwa; ndivyo mnavyoleta sadaka; je! Niikubali hii mikononi mwenu? Asema Bwana.
◼️MUNGU wa Mbinguni anataka watu watoe Sadaka ila wasitoe sadaka kilema.
◼️ MUNGU hataki utoe sadaka ambayo hiyo Sadaka ni kama mgonjwa. Toa sadaka nzima na sio kutoa Sadaka inayoumwa.
◼️Toa sadaka ambayo haitokani na udhalimu.
Ndugu, Inawezekana Kuna Mtu tangu aanze kutoa Sadaka kwa MUNGU katika KRISTO YESU Mtu huyo huwa tu anatoa sadaka kilema.
Ndugu, Inawezekana sadaka zako zote ulizotoa Mwaka huu ni sadaka kilema ndio maana huoni Matokeo, Anza kutoa Sadaka safi kuanzia Leo.
Sadaka safi ni ipo?
✓✓Ni Sadaka ambayo Mtu anaitoa kwa Moyo mkunjufu.
2 Wakorintho 9:7-8 " Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana MUNGU humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu.
Na MUNGU aweza kuwajaza kila neema kwa wingi, ili ninyi, mkiwa na riziki za kila namna siku zote, mpate kuzidi sana katika kila tendo jema;"
✓✓Ni Sadaka nzuri inayoambatana na Moyo wako mkamilifu kwa MUNGU.
✓✓Ni Sadaka ambayo haiambatani na malalamiko na masononeko moyoni mwako.
✓✓Ni sadaka kubwa na nzuri kiroho.
2 Wakorintho 9:6 "Lakini nasema neno hili, Apandaye haba atavuna haba; apandaye kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu."
✓✓Ni sadaka ya hiari sio ile Sadaka ambayo mpaka utishwe ndio utoe.
✓✓Ni Sadaka ambayo unaitoa huku ukimwangalia MUNGU wa Mbinguni na sio kumwangalia Mtumishi wa KRISTO unayempa hiyo Sadaka.
Ngoja nikupe mfano mmoja ambayo Mimi Peter Mabula katika utumishi wangu kwa KRISTO kuwa wakati nilikutana nayo kutoka kwa Ndugu wawili walioamua kutoa Sadaka.
Mtu mmoja alinitumia Sadaka ambayo MUNGU alimpa msukumo kutoa, baada ya kutoa aliniandikia meseji akisema "Mtumishi Mabula nimekutumia msaada kidogo, nimeamua tu kukusaidia "
Baada ya hapo niliingia katika Maombi nikianza na toba Kisha nikaomba kugeuza msaada wa Mtu huyu kuwa sadaka ili MUNGU aipokee Sadaka yake huku nikiambatanisha na mahitaji yake.
Kwanini nilifanya hivyo?
Ni kwa sababu katika Biblia hakuna andiko hata Moja ambalo MUNGU anahitaji msaada.
◼️Katika Biblia kwa habari za Matoleo MUNGU anahitaji Zaka, Sadaka na Dhabihu tu.
✓✓Watu wengi hutoa msaada na zawadi, MUNGU huwa hapokei msaada na zawadi ambazo ni sadaka.
✓✓Sasa wengi hujikuta wanatoa Sadaka kilema bila kujua na MUNGU hapokei Sadaka kilema, ndio maana nimesema Inawezekana Kuna Mtu mwaka mzima hutoa sadaka kilema bila yeye kujua.
✓✓Lakini kwa sababu sadaka ina kazi nyingi kwenye ulimwengu wa roho na husababisha matokeo katika ulimwengu wa mwili basi wateule wa KRISTO inawapasa kuwa watoaji.
✓✓Hulazimishwi kutoa sadaka mbele za MUNGU lakini kuna baraka unaweza usiambatane nazo kamwe maishani mwako kama hutakuwa na maombi yanayoambatana na sadaka.
✓✓Yaani kama hitajio la ulimwengu wa roho kuhusu suala lako ni sadaka basi bila sadaka hutaona mpenyo wa jambo hilo.
Niliwahi kusikia sauti juu ya kutoa sadaka kwa ajili ya ujenzi wa Kanisani wakati naishi Zanzibar, msukumo ulikuwa ni mkubwa rohoni hadi nikawashirikisha watu ili wanisaidie ili nifanikiwe jambo hilo lakini kwa sababu wao hawakuwa na mzigo huo rohoni hawakunijali na wengine walikataa.
Hata hiyo Sadaka Mimi sikuwa nayo, baadae nikapata nafasi ya kukopa benki Tsh milioni 2, nikatoa zaidi ya nusu kwa ujenzi wa Kanisa ndipo nikawa na amani.
Lakini kabla nilikuwa najiuliza " kwani maombi tu hayatoshi hadi sadaka hiyo kubwa?"
Lakini bado rohoni msukumo ulikuwa mkubwa, nilipotii vitu vingi vilifunguliwa maishani mwangu.
Mchungaji wa pale Kanisani aliona mambo kutoka ulimwengu wa roho kuhusu Mimi na alinitamkia baraka za ajabu sana. Yake mambo aliyoyaona ni makubwa kiasi nilibaki nimeduwaa kwa furaha, MUNGU wa Mbinguni ameendelea kuyakamilisha kwa hatua.
✓✓Sio kila hitaji lazima maombi yake yaampatane na sadaka lakini Ukisikia msukumo rohoni mwako juu ya sadaka ujue hitajio la ulimwengu wa roho ni sadaka hivyo timiza.
Mhubiri mmoja wa Marekani alianzisha huduma na mambo yakawa mazuri, baadae alisikia sauti rohoni ikimwambia kwamba auze vitu vyake akatoe sadaka kwa Mtumishi mwingine mkubwa sana na tajiri sana, mtumishi huyo ilimsumbua sana yaani yeye anavyo kidogo na hivyo hivyo kidogo ampeleke Mtumishi tajiri sana, ilimsumbua sana lakini alipotii leo hii yeye Kanisa lake ni kama uwanja wa mpira, watu ni maelfu.
✓✓Ndugu, MUNGU anahitaji sadaka kamilifu na sio sadaka dhaifu au sadaka ziada.
Na sadaka usitoe tu kama ushahidi na utarajie matokeo.
2 Wakorintho 9:6-8 " Lakini nasema neno hili, Apandaye haba atavuna haba; apandaye kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu. Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana MUNGU humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu. Na MUNGU aweza kuwajaza kila neema kwa wingi, ili ninyi, mkiwa na riziki za kila namna siku zote, mpate kuzidi sana katika kila tendo jema;"
✓✓MUNGU anahitaji sadaka kamilifu na sio ziada wala dhaifu.
✓✓Inawezekana wewe hudhani watumishi ndio wanaagiza watu kutoa sadaka, lakini Ukichunguza Biblia unagundua ni MUNGU ndio anaagiza tuwe tunatoa sadaka.
Sadaka ni hitajio la kiroho kwa ajili ya mtu mwenyewe anayetoa sadaka hiyo, ndio maana MUNGU anawaagiza wateule wake katika KRISTO YESU kuwa watoaji wa sadaka.
Zingatia mteule wa KRISTO na MUNGU atakubariki sana.
Mche MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi na utaitwa heri.
Kama pia unatumia Facebook ni follow maana itafika kipindi nitakuwa napost tu katika page yangu na profile yangu.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292(Ni namba hii kupiga, sadaka ya kuipeleka Injili,kuandika meseji na whatsapp).
Ubarikiwe sana.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292(Ni namba hii kupiga, sadaka ya kuipeleka Injili,kuandika meseji na whatsapp).
Ubarikiwe sana.
Comments